Dondoo 10 muhimu sana kwa wazazi na wazazi watarajiwa wote

Habari za jioni wapendwa… Nadhani wengi watu humu ndani ni wazazi au Wazazi watarajiwa.. So si vibaya kama tutasoma hapa na kuzingatia dondoo 10 muhimu sana kwa wazazi na wazazi watarajiwa wote

1. Mkanye mtoto wako wa kike na hata wa kiume kuhusu kukubali kupakatwa hovyo, bila kujali ni nani anampakata, hata kama ni mjomba wake.

2. Usivue nguo mbele ya mwanao pindi akifikisha miaka 2 au zaidi. Jifunze kumwomba akupishe.

3. Usiruhusu mtu yoyote amwite mwanao “Mchumba”, “Mke wangu” au “Mme wangu.”

4. Kila wakati mwanao anapoenda kucheza na wenzake, hakikisha unafuatilia kujua wanacheza nini, siku hizi hata watoto wanafundishana michezo michafu na wengine wana maambukizi.

5. Kama mwanao ameonyesha kutopenda kwenda kwa mtu fulani usimlazimishe, pia chunguza kwa ukaribu ili kujua sababu.

6. Inashauriwa kupitia kwanza mwenyewe movie yoyote kabla ya kuruhusu mwanao waiangalie.

7. Mwanao anapofikisha umri wa miaka 3 anza kumfundisha jinsi ya kusafisha sehemu zake za siri mwenyewe, na umuonye asiruhusu mtu yoyote kumshika sehemu hizo.

8. Mfundishe mwanao thamani ya kuishi bila kufuata mkumbo.

9. Mwanao akilalamika kuhusu mtu fulani, usikae kimya.

10. Usipende kumruhusu mwanao kulala na housegirl au houseboy au mgeni. Huwezi jua tabia za watu na wanayomtendea usiku!!!

Mwandishi wa Mada hii
Mwandishi Wa Mada Hii

One thought on “Dondoo 10 muhimu sana kwa wazazi na wazazi watarajiwa wote”

Leave a Reply