Tulinde na Kuheshimu Watoto

Kusema kweli nimesikitishwa sana na kitendo cha baadhi ya Watanzania kumdhalilisha mototo wa Flora Mbasha. Naomba niseme bie binafsi simjui Flora wa mumewe-Mr. Mbasha, na wala sijawahi kusilikiza nyimbo zake. Nilitokea kujua habari zake kipindi walipo kuwa na migogoro katika ndoa yao. Hapo ndipo nianza kusoma habari zake na kuangalia mahojiano kadhaa ambayo alikuwa amefanya huko nyuma na baadhi ya TV shows. Hivyo ninayo andika hapa si kwamba namfahamu Flora au mumewe la, hasha! Ni kwasababu ndivyo inavyo takiwa tufanye.

Kutokana na maneno ya watu kuwa huwenda huyu kichanga aliye zaliwa yawezekana asiwe mototo halali wa ndoa ya Flora na muwewe Mbasha kwa kuwa ndoa yao inamigogoro na kwa sasa wametengana. Basi wengi wamehoji nani ni baba halali wa mototo huyo. Cha kusikitisha zaidi wamenda mbali na kuweka picha yenye sura ya Flora, Mbasha (mume halali wa Flora), Gwajima (mtu inaye semekana ni Mchungaji na pia ana sadikika kuwa ni ndiyo baba wa mototo huyo), masikini piya sura ya kichanga hicho nayo imewekwa! Watu wote, wa mama kwa wababa, wakaka na kwa wasichana wote wanaandika comments za kudhihaki na kukebehi chini ya picha hiyo. Hizo comments nyingine zime walenga wazazi, zingine zime walenga washtumiwa, na zingine zina mlenga mototo huyo moja kwa moja!

Mimi binafsi, nalaani vikali kitendo hicho cha kumdhalilisha mtoto wa Flora. Nakiita ni kitendo cha kinyama na ukatili wa hali ya juu. Children should be protected, and treated in the highest respected level of humanity regardless of how they entered this world!! Si Yesu ndio aliyesema “waacheni watoto wote waje kwangu maana ufalme wa Mbingu ni wao?!” Yesu hakubagua watoto, aliwaita wote kwake, sasa kwanini sisi tunabagua watoto? Matter-of-fact, children should never be the victims of their parent’s wrong deeds! Haijalishi mimba yake ilitungwa na wababa wawili, au ilitungwa mbele ya Madhabahu, au Msikitini, au ilitungwa kwenye majani porini, it doesn’t matter, and it should never matter; watoto wote wanatakiwa kulindwa na kuheshimiwa period!

Ni jukumu letu sote kama raiya wa hii dunia kulinda na kuheshimu watoto. Nandio maana nimeamua kuliongelea swala hili kwa uwazi katika blog hii. Hapa machozi yananitoka. Ndiyo, nalia! Kwasababu kwanza mimi ni mama, hivyo mototo huyu anaweza kuwa mwanangu wa kumzaa, au mjukuu wangu. Mimi ni dada, hivyo mototo huyu angeweza kuwa my niece or nephew! Jiweke kwenye miguu ya Flora, jaribu kuvaa viatu vyake kwa dakika moja, je ungekuwa wewe ungejisikiaje kuona mototo wako ambaye ndo kwanza amezaliwa katika hii dunia, hajui hata “social media” ana dhihakiwa, na kudhalilishwa kwa namna hii?! Je, wewe ni mkamilifu? “Na asiye na dhambi awe wa kwanza kurusha jiwe!” Mungu atusamehe kwakuwa hatujuli tulitendalo. Tulinde na Kuheshimu Watoto.

Sing along with me…………….

Jesus loves the little children
All the children of the world
Red& yellow, black and white
they’re precious in his sight
Jesus loves the little children of the world
Jesus cares for all the children
All the children of the world
Black and yellow, red and white
They’re all precious in His sight
Jesus cares for the children of the world
Jesus came to save the children
All the children of the world
Black and yellow, red and white
They’re all precious in His sight
Jesus came to save the children of the world

The world will not be destroyed by those who do evil, but by those who watch them without doing anything.”-Albert Einstein

3 thoughts on “Tulinde na Kuheshimu Watoto”

  1. Nimependa maoni yako Alpha, kweli kabisa, mtoto asiwe subject ya news katika social media. By the way Flora ameeleza ya kwamba Picha iliyowekwa kwenye media si ya mtoto wake. That’s better, kwa sababu imagine mtoto akija kuwa mkubwa and then aonyeshwe such publication, ni dhahiri atajisikia so bad.

    Issue ya Mbashas na Mtumishi wa Mungu is so confusing. There are so many questions without answers. Naamini Mtumishi anatumika kuficha udhaifu au makosa ya Mwenye mke. Otherwise, yanayosemwa yangekuwa na ukweli sheria zingekuwa zimetumika, but wapi!

    Tuwaachie wenyewe wayamalize kama wataweza

  2. Nakuunga mkono Alpha. Haya ya wenyewe wayaache wamalize wenyewe. Ndoa zina challenge nyingi hivyo ni juu ya wanandoa kuzimaliza wenyewe na wengine wote shut-up na mkae pembeni. Yao yanawashinda alafu wanakuwa wepesi kusema ya wenzao.

Leave a Reply