Mahojiano Maalum: Tabu Obago

“Ujane siyo ulemavu wala Huyatima siyo kufungwa”  image-1-1-1Wapendwa wasomaji, wiki iliyopita niliwaletea mahojiano maalum kutoka kwa dada Zawadi Kakoschke. Katika mahojiahano hayo moja ya maswali ambayo nili muuliza ni kama kuna huusiano kati ya majina ambayo wazazi wanawapa watoto wao na mafanikio au tabia ya watoto hao. Sehemu ya mahojiano hayo yalikuwa kama ifuatavyo:-

Wewe binasfi unaamini majina ambayo wazazi wana wapa watoto wao yanachangia katika mafanikio yao kiuchumi, kielimu, na tabia zingine? Kwa mfano majina kama Amani anaweza akawa mtu wa kupenda amani siku zote, au majina kama Tabu, Sikujua yanaweza yaka changia mototo kuwa na matatizo katika maisha yake? Majina yanachangia sana katika maisha ya watoto wetu. Ndio maana mimi nilijitahidi sana kukaa na kufikiria majina ya kuwapa watoto wangu. Nimekua naamini hili kwa miaka mingi sana kuwa majina yana nguvu sana katika kujenga au kubomoa maisha ya muhusika. Huwa nashukuru sana kwa wazazi wangu kuamua kunipa jina la Zawadi nina imani kubwa hili jina limenisaidia kwa namna moja ua nyingine.

Kwakweli majibu ya dada Zawadi yalinikumbusha binamu yangu mmoja aitwaye Tabu Obago. Nika muomba nifanye mahojiano naye mafupi haswa kutaka kujua kama jina lake limekuwa nuru kwakwe au la! Na hivi ndivyo ilivyo……

Tabu naomba utuelezee, je jina la Tabu libekuwa “tabu” kweli au nuru kwako, tupe historia yako kwanza? Mimi ni dada niliye zaliwa kutoka katika mkowa wa Mara, lakini kwa sasa makazi yangu yapo katika kitongoji cha Mbagala. Mimi ni mama wa watoto wawili Jack na Julieth. Mmh! Tabu, kama jina lenyewe linavyotamkwa au maana halisi ya ili jina hakika limeambatana na mimi katika maisha yangu yote. Nimekuwa na taabu nyingi sana kama mjomba XX alivyo kuwa akipenda kusema mara kwa mara “Tabu, unatabu kama jina lako.”

Kuhusu kuzaliwa kwangu mimi ni mtoto wa pekee kwa mama yangu, marehemu Rosebela Igogo. Kusema ukweli swala hili la kuwa mototo pekee kwa mama yangu huko nyuma lilikuwa linanisononesha hasa nilipowaona wenzangu na ndugu zao wa kuzaliwa tumbo moja. Lakini nilipopata watoto wangu nahisi wameziba hiyo hali ya upweke na sasa nina furaha na amani moyoni mwamgu.

Japo katika maisha yangu nime ambatana na matukio ya kusitisha, lakini kwa kweli siwezi na wala sitamani kufuta kitu chochote kwenye historia yangu. Historia (past) ni historia iwe mbaya au nzuri ndo inaleta “leo” ya mtu. Labda niseme hivi, kwa upande wangu kitu ambacho najutia sana ambacho ningependa kufuta (edit) kwenye historia yangu ni maisha yangu ya shule. Kwani NAJUTA SANA TENA SANA nilivyochezea pesa za mama yangu shuleni na kupoteza muda. Leo hii jinsi ninavyo angaika kuwasomesha binti zangu ndo nahisi uchungu aliokuwa anaupata mama yangu.

Tabu, Wewe si tuu yatima bali pia ni mjane; niwapi huwa unapata nguvu ya kuendelea na maisha bila kukata tama?
Ni kweli mimi ni yatima na pia mjane tena mara mbili namaanisha kwa ndoa mbili!! Kinachonipa nguvu na msukumo wa kuendesha maisha yangu bila kukata tamaa ni wanangu Jack na Julieth. Natamani sana kurekebisha nilipo haribu japo ni ngumu mno. Lakini ugumu wa maisha na changamoto nilizopitia zimekuwa shule iliyonipa elimu kubwa sana.

Nikitu gani unajivunia sana? Najivunia kusimama imara katika maisha na hasa kuamua kuishi katika Leo yangu na siyo kujutia ya nyuma. Naweza kusema mpaka hapa nimeweza kujiweka sawa kama siyo ku(edit) lifestyle yangu.

Ujumbe kwa watu wote watakao soma hii story yako?(1) Kwa watoto zangu hakuna jipya chini ya jua. Mkipelekwa shule someni sana.
(2) Kwa wenzangu namaanisha wa umri wangu (42) msikate tamaa unaweza ukiamua iwe (3) Kwa yatima na wajane wenzangu naomba niwausie ujane siyo ulemavu wala huyatima siyo kufungwa tujifunze kusimama wenyewe na Mungu anakusaidia. Mwisho, haijalishi uko chini au una udhaifu gani muujiza pia hipo ila naamini mpaka uitafute siyo ikutafute.

Asante sana Tabu Obago. Nakutakia mafanikio mema na makubwa zaidi ya hayo.

Ref: Mahojiano haya yamefanywa na Alpha Igogo

 

One thought on “Mahojiano Maalum: Tabu Obago”

Leave a Reply