Let me be……….!

Life is too short let Alpha be Alpha! Yani mimi kama I could have things my ways nafikiri ningekuwa na cheka tu kama #Zezeta …….Mpendwa, Usipoteze muda wako kusikitika kwanini yamekukuta yalio kukuta! Wewe sema kama yasingenikuta mimi nani mwingine anayestahili?  Mshukuru Mungu kaamua kukutumia wewe kama chombo cha kufikisha ujumbe wake kwa watu / duniani! Mungu anajua you are strong enough to handle the stormy weather ndio maana akakupitisha njia hiyo! Maybe alijua kama kila kitu kingekuwa rahisi kwako basi usingejua kusema Asante Mungu!  Yani Mungu asingekua na nafasi katika maisha yako! Shukuru, na furahia maisha yako hata kama kuna magumu gani unapitia. Kama unataka kulia nenda sehemu ambayo upo mwenye iwe chumbani au chooni wewe nenda kajifungie ulie wee tena lia sana kwa nguvu zote kwani kulia ni dawa ya kuondoa sumu ya hasira mwilini! Ila baada ya kulia hakikisha unafuta machozi yako na kuendelea na maisha yako kwani siku zetu hapa duniani zimehesabiwa na hazipo nyingi sana! Muulize Mungu, haya, katika hili unataka nijifunze nini ambacho sikuweza kujifunza mara ya kwanza! Maana wengine huwa tuna miss the core of the lesson na kwakuwa Mungu anatupenda sana basi naye hutupatia mapigo / maonyo hata mara tatu au zaidi mpaka pale tutakapo elewa somo! Basi muulize akufungulie ili usipate pigo lingine tena………..Life is too short let me be who I’m! Alpha is all about love and love is her religion! Love me or hate me I care less about you as my birthday is just around the corner and “Life” begins at 40!……Love you!

Leave a Reply