“Asante mume wangu kwa kunipenda na kunijali….!” Mrs. Maria Makonda

Wiki iliyopita niliwaelezea sakata la mke wa  TV icon and comedian Mrs Bill Cosby a.k.a Camille Cosby jinsi alivyojitokeza saa za mwisho bega kwa bega na mumewe huku aki-smile kwa raha zake! Kama ulipitwa basi soma ?? MrsBillCosby

Basi leo tena na waletea maneno aliyo andika Mke wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mrs Maria Makonda au kwa jina maharufu ni “Mrs Daudi Bashite” ?? hizi social media ni shidaaa! Btw, kabla sijaendelea naomba ieleweke kuwa sina chuki na Makonda wala familia yake japo simuungi mkono kwa mambo aliyo yafanya kama kiongozi! Hata hivyo mimi sio mwana siasa wala sio mwanaharakati wa siasa hivyo hayo ninawaachia wataalamu wa mambo hayo ku-deal nayo! Hii blog is all about love, spirituality, family, friendship, relationships, sisterhood, brotherhood, parenthood, empowerment, na mambo mengine kama hayo ambayo yana inspire jamii! Kama kuna mtu anataka siasa tafadhali usisite kwenda  kwa Mange Kimambi, Peter Sarungi,  na Lemutuz! Haya back to our topic! ……….. Juzi kati kwa kupitia account yake ya Instagram Mrs Makonda aliandika maneno haya “Asante sana mume wangu kwa kunipenda na kunijali. Mungu akutunze”! ?? Haya maneno anayaandika baada ya scandals zote ambazo zimemuandama mumewe kuanzia sakata la vyeti feki, vita feki ya madawa ya kulevya, na mengine mengi bila kusahau kuhusishwa na scandal za kuwa na mahusiano ya kimapenzi na muigizaji Kajala Masanja pamoja na Agnes Masogange! …….. Mimi nasema waacheni watu na ndoa zao kwani hakuna mtu anaejua sababu haswa zinazowafanya wanawake wengi wasimame na waume zao hata pale ambapo watu wengi wanaona ni wakati wa kumuacha “high and dry”! Sijui ni kwasababu ya kiapo #Kitakatifu. au mapenzi au ni huruma tu ambayo mwanamke ameumbwa nayo! Simnaona hata mimi hapa bado nimesimama kidedea na my Muhaya yani hapa ni Kigoma mwisho wa reli  ???  kama nawaona wapika majungu sura zao zinavyo pooza ?? Haachwi mtu hapa poleni sana mtahachika nyie na ndoa zenu fake za Facebook ?? #StandByYourMan #GodHelpUs

Leave a Reply