(audio): “Muumbaji wa ndoa ni Mungu peke yake…..Hakuna mwalimu wa ndoa hapa duniani” – Tumaini Kilangwa

2015-08-22 12.59.00

Tumaini Kilangwa au da Tuma, yeye ni mama wa watoto wawili, mke, na mfanyabiashara. Katika mahojiano haya ambayo yote amerekodi na unaweza sikiliza ameongelea mambo mabali mbali kuanzia alipotokea, maisha yake ya elimu, maisha kama mama, maisha kama mke, na maisha kama mfanyabiashara. Ni mahojiano mazuri sana ambayo yanafundisha na kutia moyo kuwa hakuna lisilo wezekana kwa Mungu (kama unaamini kuna Mungu). Tafadhali chukua muda wako umsikilize wala hutojutia kamwe!2015-03-25 05.57.39Elimu na kazi alizofanya

2015-08-22 17.42.52Dada Tuma kwa sasa ameamua kuachana na kazi za kuajiri hivyo yeye ni mfanya biashara anaye miliki mgahawa ujulikanao kama Eastern Cuisine. Uliopo Wichita Kansas.

2015-08-22 17.38.15Pichani ☝ ni watoto wa da Tuma wakiwa wamevalia Tshirt za mgahawa huo….

FB_IMG_1431827984235Katika swala la uzazi na malezi ya watoto wake mpaka hapa walipofika japo safari bado inaendelea Tumaini anashuhudia kwa kusema “tumeuona  mkono wa Mungu na tunaendelea kuuona ukuu wake siku hadi siku.” Ni ushuhuda wa kusisimua na unatoa faraja kwa wale ambao wanapitia changamoto kama hizi katika malezi au jambo lolote lile. Embu msikilize wewe wenyewe…….

FB_IMG_1431828022321 Kuna changamoto nyingi katika malezi haswa ukizingatia tupo katika inchi ya ugenini ambapo mila na desturi zetu nitofauti na tulizo lelewa ameeleza da Tuma……

2015-04-22 21.29.44Dada Tuma ametoa ushauri au ujumbe kwa Watanzania wote waishio nje ya Tanzania na hata wale waliopo nyumbani kwamba  wawe na moyo wa kupenda kujaribu vitu na wasikate tamaa, kuwa na plan na mipango kwenye maisha. Utambuwe karama yako ili uweze kuweka mipango yako vizuri. Pia ameshauri watu kumtegemea Mungu sana kwani Mungu wetu ni Mungu wa upendo na anasikia sala za watu wote!

2015-08-23 17.58.59Maisha ya ndoa yanahitaji uvumilivu na maombi ya kila siku. Da Tuma amewasihi wanandoa haswa wadada kuacha tabia ya kuiga iga mambo ambayo wanayaona au kusikia kutoka kwa watu wengine hususani kwenye “kitchen parties” kwani kitu ambacho kimewezekana kwenye ndoa ya mwenzako siyo lazima kifae kwenye ndoa yako! Hakuna Mwalimu wa ndoa hapa duniani ni Mungu peke yake……!

Napenda kutoa shukran zangu za dhati kabisa kwa dada Tumaini, pamoja na kubanwa sana na kazi na misha ya familia lakini kwa upendo kabisa ameweza kuchukua muda wake wa pekee na kukubali kufanya mahojiano haya na mimi. Ubarikiwe sana da Tuma.

Pia shukran kwa wote ambao wamejitolea kwa njia ya pekee kabisa kuweza kushare picha zao, mawazo yao, na pia ku-share maisha yao kwa njia ya mahojiano na hii blog. Wote naomba Mwenyezi Mungu awabariki sana kwani mimi binafsi sina cha kuwalipa!

N.B: Kama unataka ku-share nasi kitu chochote au unaswali wasiliana nami kwa [email protected] Pia naomba nikumbushie kuwa huitaji kuweka email wala jina lako unapotaka ku-comment japo fomu ya comment inaonyesha hivyo lakini si lazima. Asanteni wote!

Mahojiano haya yameandaliwa na Alpha Igogo

 

8 thoughts on “(audio): “Muumbaji wa ndoa ni Mungu peke yake…..Hakuna mwalimu wa ndoa hapa duniani” – Tumaini Kilangwa”

  1. Wonderful interview! This is the kind of info that are meant to bee shared around with bloggers. Shame on the attention seekers who use blogs to destroy other people’s lives!

    You be blessed!

Leave a Reply