All posts by Alpha Igogo

Chuki, ubaguzi, na upendo mtoto ufundishwa na wazazi wake!

Chuki na ubaguzi mtoto ufunzwa na wazazi wake kama ilivyo upendo! Mtoto anazaliwa na kichwa che ubongo mtupu na safi! Sasa wazazi na walezi was hawa watoto ndio inategemea watajaza huo ubongo was huyo mtoto na vitu gani! ........Nisawa na elimu kuhusu Mungu, mtoto hawezi jua umuhimu was kuabudu na kumcha Mungu kama wazazi na walezi wake hawakumfundisha na kumuonyesha kwa vitendo kuwa kuna Mungu anaye stahili kuheshimiwa na kuabudiwa! Au utakuta Mzazi anamwambia mtoto wake hiyo nguo mbaya mpe fulani (ana taja jina la mtoto mwingine) hivyo mtoto anakua akijua kuwa kama kitu kibaya au kimezeeka ndio unagawa kwa wengine! Ambapo ni makosa makubwa sana! Mzazi mfunze mtoto wako kuoenda watu wote wa rangi zote bila kujali kipato chao cha kiuchumi!

Tamera amenifanya nijisikie kuolewa na mzungu 😂😂😂 I’m curious to see how my baby will look like 🙈🙈

Hongera viongozi wapya wa THC!

Wiki iliyopita Watanzania waishio katika jiji la Houston, Texas walichagua viongozi wapya wa jumuiya yao ambao wataanza kuongoza kuanzia mwezi wa kwanza mwakani kwa kipindi cha miaka miwili. Nikiwa kama mmoja wa Watanzania ambao tunaishi ndani ya jumuiya hii naomba niwape pongezi viongozi wote waliochaguliwa kutuongoza kwa kipindi kijacho. Japo sijakaa sana hapa Houston lakini naweza shuudia kuwa nimeona mambo mazuri toka kwa wanajumuiya ambayo naamini ni matunda ya uwongozi bora. Hivyo Kama ilivyo kwa wengine nami nategemea kuona mambo mazuri zaidi katika jumuiya yetu! Hongereni Sana! Vile vile pongezi kwa viongozi mliomaliza muda wenu kwa kutuongoza vyema.  Pichani katikati ndio Rais / Mwenyekiti mpya Mr Lambert Tibaigana. Kulia ni dada Anasa Kambi yeye ni Katibu wa jumuiya. Na Kushoto ni dada Aneti Asenga yeye ni Muweka Hazina........... Kwa  picha na maelezo zaidi bonyeza 👉👉 THC

Crush diets vs Healthy eating

@Regranned from @open_kitchen2014 – Naomba leo kutoa ka elimu kidogo hizo picha mbili zote ni za mwaka huu hiyo ya kushoto ilikuwa mwezi wa nne na hiyo ya kulia ni december ila utaona kuwa kuna tofauti kubwa sasa hapo ndio uelewe tofauti ya bad crush diets na healthy eating with lots of muscle buiding kipindi cha mwezi wa tatu mpaka wa nne nilijaribu kila mbinu ili nipungue kilo 10 za mwisho zilikuwa zinanitesa sana sasa nikaanza crush diets na mazoezi yaani kwanza nilipozitoa zile kilo 10 ndani ya mwezi mmoja mwezi unao fuata zilirudi zote na zaidi nikawa very upset ndio nikaanza kusoma na kujifunza kuhusu crush diets vs healthy eating na pia nikaamua kuaza weight lifting vs cardio maana with cardio nilikuwa nanyooka tu sitengenezi shape at all nilikuwa kama mti wa fenesi 😂😂😂😂😂😂 lakini sasa hivi kidogo Alhamdulillah hata kijingu cha kukorogea uji kinaonekana japo sio cha kusimamisha chupa ila maji yanatuama kidogo 😂😂😂😂😂😂😂 .
So naomba ujue kuwa crush diets are not healthy kabisa kwasababu kwanza sukari yangu ilikuwa inashuka sana because nilikuwa nakula kidogo nafanya mazoezi zaidi and that was very dangerous nakumbuka kuna siku nimetoka kukimbia 10k nikahisi kuzimia nakuja kupima sukari ipo 3 yaani i was so scared so ni muhimu kuelewa madhara ya crush diets na pia ngozi yangu ilikuwa mbaya sana yaani nilikuwa najitahidi sana ku moisturise lakini bado ilikuwa haina mvuto mda mwingi ilikuwa inabebwa na make up 😂😂😂😂 na pia nilikuwa so weak mda mwingi nina fatigue sana so i stopped huo ujinga kabis a .
..
Sasa hivi navaaa size 14/16 mwili wangu upo shaped vizuri na ninaendelea kila siku kuutengeneza sitaki kupungua zaidi ya hapo nimeridhika kabisa mimi sina skinny body frame so mwili wangu hauwezi kuwa kama beyonce never ever 😂😂😂😂 lazima uwe na target inayoendana na body frame usije ukawa kama a walking zombie maana kila nguo ukivaaa unaoneka kama imetundikwa , uso mpaka unakosa nuru mtu akikuangalia sura inakuwa kama inamzomea 😂😂😂😂mambo gani sasa hayo ..
. . So sasa hivi yes mwili wangu unaoneka thicker na abit more masculine and i love it AMKA TWENDE HATA WEWE UNAWEZA –

Vita vizuri mmevipiga na kazi mmemaliza. Pumzikeni kwa amani ya Bwana!

Mungu awape nguvu wanafamilia na wafiwa wote kuweza kukabiliana na maisha bila wapendwa wao! Poleni sana Watanzania wote. Wapumzike katika amani ya Bwana! Mungu ibariki 🇹🇿🙏

Hakuna ubaya kumkumbusha mtu kitu au kumpa mtu tahadhari. Tatizo ni jinsi unavyo sema na mahala unapo semea ndiyo huleta shida!

Kwanini unamkatisha mwenzio tamaa? Wewe Kama haukubaliani na ndoto za mtu mwingine, basi pale anapo amua ku share na wewe badala ya kumkatisha tamaa ni vyema ukanyamaza’  If you don’t have any positive thing to say to someone just “shut your front door!” Tujifunze kupenda kubariki wengine  nasi tutabarikiwa tena zaidi. Mtu anapo share na wewe  mawazo  yake au  mipango yake inamaana amekuamini, kama upendi aendelee kukuamini basi nyamaza! Hivyo itakuwa umetumia busara zaidi kuliko kuanza kumtolea maneno ya kukatisha tamaa kama vile; “sidhani kama utafanikiwa”, au “mh! Jitahidi mwanzo  mugumu.”

Okay, mtu kufuata  ndoto zake sio lazima afanikiwe kama wewe unavyotaka au unavyo fikiria kwani kitendo cha mtu kujaribu teyari ni mafanikio tosha! na wewe ni nani haswa mpaka ujue what the future holds of your fella?  Unajua aliye tengeneza bulb alijaribu mara ngapi kabla ya kufanikiwa? Bill Gate alishawahi kusema kuwa yeye huwa haajiri mtu ambaye hajawahi ku fail! Na hawa ni watu ambao leo hii dunia inawatazama kama baadhi ya watu ambao ni the most achievers in the world!  “Mmh! Mwanzo mugumu” oh! well, who doesn’t know that?! Nani asiejua kua katika kujaribu kufanya kitu chochote kile unaweza usifanikiwe? Why uone umuhimu wa kumguna mtu ili umwambie mwanzo mugumu? Au Wenzetu wanasema “talking / saying with attitude” hivi unajua Billoner Mr. Trump amewahi ku file bankruptcies mara ngapi? na ni nani asiye jua kuwa Rome haikujengwa ndani ya masaa 24?!

Hakuna ubaya kumkumbusha mtu kitu au kumpa mtu tahadhari. Tatizo ni jinsi unavyo sema na mahala unapo semea ndiyo huleta shida! Pia tabia ya kurudia rudia kitu kimoja kila wakati it becomes annoying! Namwishoe mtu anaanza kulichukulia hilo neno in a negative way hata kama ulilisema kwa nia nzuri. Kwanza nimegundua  ukiona mtu anakukatisha tamaa kwenye juhudi zako jua huyo mtu anatamani sana kuwa wewe ila hawezi! Hivyo kupooza maumivu  anaona akuvunje wewe nguvu ya kusonga mbele! Siku zote jaribu kuwa mbaraka kwa mwingine hata kama mambo yako unaona hayapo sawa. Kwa kufanya hivyo utajenga tabia ya kupenda maendelo ya wengine nahapo ndipo utakapo barikiwa nawewe. Be a blessing! Kataa kuwa na roho ya kichawi!

Baada ya Rais kujithibitisha kwamba hali haikuwa imetendeka, ni nini kinafuata…..!

@Regranned from @mutwiba – Wakati Rais akifanya maamuzi ya kuwaachia familia ya Nguza Viking, anafungua mjadala mpya na muhimu wa kisheria na haki Tanzania

Binafsi ningependa kujua ni kipi ambacho Mahakama ZOTE zilijithibitisha “beyond shadow of a doubt” kwamba familia hii ilitenda makosa yaliyosababisha kuhukumiwa kifungo na kunyimwa dhamana na hata msamaha walioomba, na umekuwaje sasa imejulikana kwamba hayakutendeka?Swali la ziada (ambalo siamini kama kuna atakayeuliza waziwazi 🤦🏿‍♂) ni kwamba……
Baada ya Rais kujithibitisha kwamba hali haikuwa imetendeka, ni nini kinafuata kwa waliohusika ama mfumo mzima kuhakikisha kwamba hawatokei kina Babu Seya wengine? – #regrann

Hakikisha ujumbe huu umewafikia Wahaya wote!

Mwanasheria msomi wa kimataifa mwenye asili ya Kiluo kutoka Utegi, Rorya, mkowa wa Mara, ajulikanae kama Janeth O. O Igogo.  Leo hii asubuhi masaa ya Africa Mashariki akiwa ndani ya jiji la Bukoba mara tu baada ya kutua salama katika mji huo unaosifika kwa matetemeko ya ardhi kupitia Facebook page yake alituma salamu kwa Wahaya wote wanao ng’ang’ania mjini kurudi kwako wakajenge Kagera ya viwanda vyenye kasi ya Rais  Dr. Magufuli…….. Ujumbe huu ni muhimu sana ukiupata hakikisha kila Muhaya unaye mjua ameusoma 🤣🤣🙈 #AzimioLaKagera 

Zamaradi Mketema: Kumbuka details ndio zinazotengeneza PACKAGE, na package ya ukweli unayoifahamu ni wewe

@Regranned from @zamaradimketema – Ukiona MAAMUZI yako yanaangalia sana watu ujue una hatihati ya kuharibu maisha yako, kuna watu wanategemea sana ushauri na APPROVAL za ndugu, jamaa wa karibu na marafiki katika kila kitu bila kuchuja mengine aone ni ya kwake na yanamuhusu yeye tu, tusichofahamu linapokuja swala la hisia na mahusiano hakuna ubaya wa kusikiliza lakini fata kulingana na moyo wako, wengi wanaokushauri watakushauri kulingana na interest zao juu ya huyo mtu au vile wanavyomuona nje, lakini kumbuka wewe ndio unaishi nae na ndio mwenye moyo. Na zaidi kuna vingi unavyovijua ambavyo wao hata wawe karibu kiasi gani hawatakaa wavione, na hata kama mnahadithiana mara nyingi mnaongelea matukio na sio DETAILS, na kumbuka details ndio zinazotengeneza PACKAGE, na package ya ukweli unayoifahamu ni wewe, ila kwa kutaka kuridhisha watu unaweza jikuta unaacha kufanya maamuzi sahihi kwakuwa fulani kakwambia sio sawa tena kwa kuangalia tu kile ULICHOMUAMINISHA NACHO ama kumwambia, mwisho wa siku athari za UKWELI unabaki nazo wewe. Kumbuka tu Washauri ni wengi kwenye maisha lakini hawana msaada wowote na wewe pale linapokukuta, watu wapo kila siku lakini hupaswi kuwazingatia kiasi mpaka ukasahau lenye umuhimu na wewe kwa kuwapendezesha wao, wao wanafanya ya kwao bila kujali utawahukumu vipi na ya kwako yatakapoharibika utakaekaa ndani kulia ni wewe peke yako, na zaidi hawatakuwepo muda wote kwa ajili yako. – #regrann

Is baby number 2 on the way?!….if so; hongera sana Madam Rita!

Haya kuna huu ubuyu nawaletea wapenda ubuyu wenzangu 😀😀😀 Niliona hii picha wiki imepita sasa, kimoyo moyo nikasema “she looks like pregnant” lakini nikadharau! Sasa juzi kinaenda kuchungulia tena Instagram page yake nikaona no update! Nikasema mbona siku hizi anapotea sana kwa social media!! basi nikaamua kusoma comments chini ya hiyo picha si ndio naona watu wengi wakimpongeza na kumsifia kuwa mimba imempendeza! 

Honestly, nimefurahi utafikiri mie ndio Madam Rita 🙈🙈 huyo atakuwa mtoto wake wa pili baada ya miaka zaidi ya 20 kama ni kweli mjamzito! Isijekuwa mtu amevimbiwa maharagwe ya Mbeya sisi tunampa pongezi 🙊🙊 …………anyway, Madame, please rusha basi picha nyingine tukuone mpenzi 😍😍 Hongera sana, Mungu awe nawe 🙏

Vaa vizuri mpenzi wangu upendeze donge liwashike mabusu moto moto….!

“……. 🎶🎶🎶🎼🎤 Vaa vizuri mpenzi wangu upendeze donge liwashike mabusu moto Moto mimi na wewe mpaka kufa 🎶🎶 uuusiwasikilize hao wanaotaka kuharibu mapenzi yetu …..🎶🎶

Watanzania wengi wamefurahishwa na huu msamaha! Sasa imenibidi niwaze je, hukumu yao ilikuwa ya uonevu hivyo wanastahi msamaha huo? au nikosa lingine linafanywa kwa pressure ya  jamii nakwa mara nyingine siasa inachembe chembe zake humo?! Mimi binasfi, kulingana na kesi hii ilivyokuwa na maswala yote ya ushaihidi nimeshindwa kujua ni wapi nisimamie!  

Maswala ya kulawiti na ubakaji ni maswala nyeti sana, ambapo jamii inatakiwa kuwa makini sana lasivyo watu wazima na watoto wengi wataendelea kufanyiwa huu unyanyasaji bila kupata msaada wowote ule kutoka kwa jamii pamoja na kwenye vyombo vya haki! Stigmazation kwenye maswala haya bado nikubwa sana kwenye jamii yetu; hivyo watu hawapo huru kutoka hadharani na kuripoti mambo kama haya,  familia nyingi bado wanaficha mambo kama haya yakitokea kwenye familia zao! Jamii tuwe waangalifu sana kwa hili. Lakini wakati huo huo tusije hukumu watu kwa kuwapa adhabu nzito wakati hawakutenda kosa lolote! Kumbua kesi ya marehemu Michael Jackson wa hapa Marekani! Saa nyingine chuki binfsi huwa zinafanya watu wanasingizia wengine mambo kama haya ili kuwafedhehesha na kuataka kupata pesa!

Vile vile mtu akiwa amekutwa na hatia ya makosa kama hayo ni vizuri jamii na serikali ikawa na utaratibu wa kuwaangalia hawa watu na nyenendo zao zote kwa kipindi fulani. Wasiruhusiwe kukaa na watoto sehemu yoyote ile bila uangalizi wa watu wengine! Nawala wasiruhusiwe kuwa sehemu ambayo kuna watoto kama kwenye shule, sehemu za michezo n.k! Once a convicted rapist always will be! Maybe they were able to get away with it this time, lakini kama kweli hiyo ni tabia yao basi amini watafanya tena! Jamii kuweni macho! Parents beware!…….. Otherwise, hongereni kwa kupata msamaha wa Rais! Mungu ibariki 🇹🇿 🙏

Embu tucheke kidogo!

😂😂😂😂😂💃🏼💃🏼💃🏼💃🏼💃🏼💃🏼 O’Yes! Just give them the taste of their own medicine! I did that to  Muhaya, gave him a really good doze 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂  alifikiri mie Muhaya mwenzie 🙈🙈 Before you start the fire try to know your firefighter 🏇🏇🏇🏇

Faraja Nyalandu: Sio nyakati zote nilikuwa napendeka wala kuvumilika

@Regranned from @farajanyalandu – Siku kama ya leo miaka kumi iliyopita niliitika ndio kukutunza, kukupenda na kukuheshimu mpaka kifo kitakapotutenganisha. Nilikuwa msichana, na sasa ni mwanamke. Katika wengi uliniona mimi. Umenivumilia, umenilinda, umenitunza na kunipenda. 

Sio nyakati zote nilikuwa napendeka wala kuvumilika. Kila tulilovuka limetuimarisha zaidi na si kwa uwezo wetu, bali kwa uwezo wa Mungu. Asante kwakuwanami. Asante kwaupendowako. Asante kwa Sarah Divine na Christopher Aman. Umekuwasehemu ya maishayangu, ndivyoilivyo leo, hatakeshohatamilele. Nakupenda sana. #10YearsOfLove #10thWeddingAnniversary – #regrann

I am a woman-So what?!

           I AM A WOMAN!!! -So what?

I get into an argument with a man, he slaps me, I feel the pain, yet they tell me I provoked him. I should have been quiet, I should have been patient. I should apologize to him.

I get into an argument with a man, I slap him, they tell me I have no respect, no home training. I should have been quiet, I should have been patient. I should apologize to him.
Because I am a woman, I don’t have a right to be angry. So, the degree of my innocence is directly proportional to the degree of my silence in the face of oppression and brutality….. Because I am a woman, my husband cheats on me, I am told to tolerate it to save my marriage. The barbaric and stupid excuse is that ”it is in their nature to cheat, I should slim down, dress better, cook better, pray harder and be more pleasant to him”

I cheat, and I am called a whore, I have committed an abomination, I have no right to look elsewhere for the love and emotional support I lack at home, I am an irresponsible mother.

So I am sent packing, from the home we both built, with all my earthly possessions stuffed into a tiny box on my head. I am henceforth forbidden from seeing my two older children, I’m lucky to be allowed to go with my little one still suckling on my left breast. Three years later, the little one is tagged a bastard. Now, my new name is “after-three”, because I am a woman.

He is 28 and runs a company. He’s tagged wonderful, hardworking, focused, career oriented, successful at a very young age.

I am 28 and I run a company ” Hmmmm, she is not even married, unserious, can not order her priorities right, a hustler, loves money, let her go and get a husband oh”

And I wonder if being successful has anything to do with a person’s gender.

Because I am a woman,
I am not allowed to have wits or be a prodigy, I cannot be financially buoyant, professionally successful or be treated with respect without a man beside me.

Then I am tagged a generous leg opener, “a runs girl”. They never see the possibility that I actually had to go through ups and downs to get to where I am.

Because I am a woman.

A man looses his wife to death and remarries a year after, he did the right thing, he’s being praised and congratulated for moving on, after all life is for the living.

A woman looses her husband to death and remarries after 4yrs, “ahhh! so early? Are u sure she wasn’t sleeping with that man even when her husband was alive? That was why she killed her husband. She’s a witch! ” Because she’s a woman.

Because I am a woman, this post will be considered controversial, and everyone will try to correct me.

But don’t forget, that I am a woman and it does not make me less human!!!

Good Morning Everyone. NTV Mwasuze Mutya 9am-11am NTV/SparkTV Monday to Friday.

Wema Sepetu: Kila lenye mwamzo lazima mwisho uwepo

Nifuraha ilioje ndugu wakipatana?! Kaka yangu kipenzi Mh. Paul Makonda akiwa na MoyoMtamu wa Tanzania Wema Sepetu nyumbani kwa RC  🙌  Mungu ni mwema na amani iwe kwenu! Asante kwa wifi yangu Mrs Paul Makonda kwa kumkaribisha Wema nyumbani kwenu najua hapo lazima dinner fulani amazing ilipikwa au fresh juice fulani nzitooo zilinywewa na kushikana mikono kwa furaha  😀😀😀   kweli kuwa “shilawadu” lazima uwe na kipaji kwani si kazi ya lele mama 🙈🙈 

Embu msome Wema kwa maneno yake mwenyewe jinsi alivyo andika kupitia ukurasa wake wa Instagram 👉👉 ” wemasepetu……. Kila lenye mwanzo lazima mwisho uwepo…… cc @paulmakonda … Le RC…”

Happy 56th birthday Tanganyika!

Idriss Sultan
"Uhuru ni kama daftari lisilo na maandishi, babu zetu walipigania daftari hilo na wakatupa tuendelee kulitunza na kuandika historia zetu, kwa ukweli uliopo ni kwamba kuna baadhi wanaojiita wazawa ila ni wasaliti na tunauza page moja moja ya daftari hilo kwa wale tuliopigana waturudishie daftari letu. Ningependa kuwapongeza wazalendo wa kweli kwa kuhakikisha wanalinda daftari letu kwa miaka 56. Mungu ibariki hii nchi nzuri sana. Hatuwezi kuwa na vyote na bado tukawa nchi yenye majonzi duniani. Tuangalie tulipotoka na tushukuru tumefika pamoja kwa amani. Naomba ibaki hivyo na kila mmoja wetu ana kipisi chake cha hii nchi basi ajue atakifanyia nini. God bless 🇹🇿 🖤 #TanganyikaIndependece @getinsta.official #picoftheday #instagood #UhuruTanganyika" ... Idriss Sultan

Mama Salma Kikwete ndani timu ya netball!

Mama yetu kipenzi mama Salma Kikwete ndani ya kivazi mwanana kabisa teyari kwa kuingia uwanjani kucheza mashindano  ya netball za timu za Wabunge wa Africa Mashariki hapo juzi kati! Inapendeza sana, inavutia, na kutia moyo wanawake wengine na mabinti unapo ona powerful figure Kama mama yetu hapo akijishusha kwa unyenyekevu na kufurahia maisha na watu wengine! Safi sana na hongera nyingi mama yetu!………… Mwaka jana naye Dr. AshaRose Migiro alituonyesha ujuzi wake wakupiga dana dana  tazama 👉👉 BigUpDrAshaRoseMigiro

Happy 10th Anniversary Mr and Mrs Nyalandu!

Wishing you happiness, good health, and everlasting love! Happy 10th wedding anniversary to you! 💝

Mhe. Anna Mghwira rasmi ndani ya Chama Cha Mapinduzi!

Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira mara baada ya kutangaza kuhamia Chama cha Mapinduzi CCM katika mkutano wa tisa wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.

Hatimaye yametimia! Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira ahamia rasmi CCM! Apokelewa kwa shamgwe na heshima zote mbele ya Mama wa Taifa mama Maria Nyerere!…….. Mimi siyo mwanachama wa chama chochote cha siasa lakini kama nikiambiwa nichague chama basi CCM kitakuwa chama changu siku zote! Yani ni kama leo hii mtu niambie nichague dini au dhehebu, jibu langu litakuwa mimi ni Mkristo wa dhehebu la Kisabato! Nitakuwa Msabato mpaka siku nakufa!  Hayo ni mawazo yangu na msimamo wangu kama yanakukwaza sorry but no sorry! …..Hivyo namtakia kheri Mhe. Anna Mghwira katika kutekeleza kazi ya ujenzi wa taifa kwa kupitia ilani ya CCM!

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira mara baada ya kuhamia rasmi katika Chama cha Mapinduzi CCM katika mkutano wa wa tisa wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.

***picha na caption zote kwa hisani ya IssaMichuziblog***

Harusi hii watu walipendeza lakini…..!

Mr and Mrs Jons

Hii harusi ya Romy Jons mdogo wake na Diamond walipendeza sana kwenye mavazi!  

Japo kwenye nywele za bibi harusi na Zari sijaapenda sana. Hazikutengenezwa vizuri kivile!   Halafu mimi sipendi hizi suruali za kubana kwa wanaume 🤣🤣 lakini sindio mambo ya fashion zao hao wa kwenye entertainment industry! Otherwise, ingeneral walipendeza.

Kitu ambacho sikukipenda ni jinsi Diamond na Zari alivyopata attention zaidi kuliko maharusi!  

It seems to me Diamond and Zari over-did themselves ambapo naona watu wakawa hawana jinsi ila kuwatizama na kuwashangilia!  

Naelewa kwanini bwana harusi alimtaka kaka yake awe msimamizi wa harusi lakini kumbuka harusi ni siku yako moja tu ambayo unatakiwa kupata all the attention na siyo mtu  mwingine! Hivyo kuwa na “mastar” wawili ndio wasimamizi wake I think was a bit too much! Especially mastar wenyewe ndio wale ambao wako “hyper” 24/7 lazima wata overshadow your day! Harusi huwa haijurudii ni kitu cha mara moja  labda uwe na “nyota” kama ya Irene Uwoya ndio utafanya harusi mbii hivyo usifanye makosa ambayo utajutia baadaye! Otherwise Hongera zao!  

Esma (wifi mtu) alipendeza zaidi kuanzia kichwa mpaka nguo! 

Nasikia mama Diamond katangaza kuwa anamimba? 😀😀😀 Naona hii familia imeamua kuwa kama the Kadashians wa hapa Marekani 🤔🤔 Who am I to judge?! Just wishing her well, twamsubiria huyo mziwanda!

LeMutuz: Nilichojifunza Bongo ni hakuna anayetaka kukubali kuwa tunalo tatizo na hakuna anayetaka kuongelea solutions so we are creating a TIME BOMB.

LIVE STRAIGHT TALK:- The Art Our Lost Culture  

Sasasahivi in our Society tunatengeneza Vijana wengi Lesbians na Mashoga na hakuna anayejaribu hata kuliongelea kwa mapana au chanzo cha hili tatizo ni tatizo kwa sababu we are creating a Society of confused Youths ambao ndio Taifa la kesho! Nilichojifunza Bongo ni hakuna anayetaka kukubali kuwa tunalo tatizo na hakuna anayetaka kuongelea solutions so we are creating a TIME BOMB. Siku moja litakuja kulipuka vijana wetu kuanza kudai ndoa za Jinsia Moja tutaanza kutafutana kurundikana Rumande na Jela kumbe tuna wakati wa kutosha kulirekebisha hili tatizo now!……… As a Society tunatokea kwenye Mila na Desturi ambazo sasa hivi zinapitia a big test of kama ni kweli zilikuwa strong enough from the West Culture ambayo imekuja na sera za Wawekezaji na hasa the Television Culture ambayo Baba wa Taifa aliikataa sana. Sometimes ninajiuliza sana je kwanini Mwalimu alikuwa muoga sana na the Western Culture? Je alikuwa na wasi wasi na how fragile our Culture is?!  Maana ukienda Zanzibar hata wao wana Television pia lakini Mila na Desturi kwao hazijaharibiwa na Western Culture kama sisi huku Bara it is a FACT! ndio maana hapa mjini mitaa yetu imejaa watoto wasiokuwa na wazazi as opposed na Visiwani, wenzetu hawana hilo tatizo ……….Tanzania tumefanikiwa sana ku maintain Swahili as our Language na ni by the Fact that tulishituka mapema na kuunda Baraza la Kiswahili now nashangaa kwanini hatukuunda mapema chombo cha kusimamia Maadili na Utamaduni wetu au huenda tunavyo lakini they are toothless!………Vijana wetu wa sasa hawawezi kubeba na kuyakubali Maumivu ya Maisha ambalo ni tatizo namba moja la The West. So kule kuna Chama cha wamiliki wa Bunduki kinaitwa NRA ambacho agenda yake ni kubwa sana Dunia nzima kwa kushirkiana na NGO za Mashoga na Lesbians kule Holywood kama ulikuwa hujui wao ndio wamiliki wakubwa wa the Culture of Television ambayo unamuachia mtoto wako mdogo huku Bongo kuangalia siku nzima ………. Usichokijua kipindi cha TV cha Dakika 15 to 30 kinalazimishwa kutoa maswali na majibu ya maisha kwa matatizo ya vijana ndipo hao NRA huingiza agenda ya kutumia Bastola au kubadili jinsia kama the Kardeshians! TUKATAE HUO UTAMADUNI! – le Mutuz –