Baba kasema yamekwisha sasa tujenge taifa!

Baba kafanya maamuzi yake! Rais Dr. Magufuli siku ya jana masaa ya Africa Mashariki kama wengi mlivyo sikia ameingilia kati na kumaliza mgogoro uliokuwepo kati ya marafiki wawili kaka yangu Paul Makonda na shemeji yangu Ruge πŸ˜‚ mtaalamu wa kujikomba nimeanza πŸ™ˆπŸ™ˆ Well, kama hujui basi ndo hivyo Rais Dr. Magufuli ni my Guardian father, Paul Makonda kaka yangu, Ruge shemeji yangu, na Rais Donald Trump ni mjomba wangu, Ivanka Trump ni cousin-sister wangu, na Jared Kushner ni shemeji yangu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ "Bongo mmeshaharibu na kwa Bush msiguse" Β πŸ™Œ I'm feeling Juma Nature right now #Utajiju........  Anyway back kwa story yetu. Sasa naona Rais kaamua kutumia nafasi yake kama baba kumaliza hili zogo. Inaweza isieleweke kwa walio wengi kwanini amemaliza hili zogo kirahisi hivi kutokana na hali halisi ya tukio zima! Naomba watu mkumbuke kuwa hakukuwa na kesi yoyote mahakamani kuhusiana na zogo hili! Hakuna hata mtu mmoja kati ya wakurugenzi wa Clouds, wala wafanyakazi wao aliyefika Police na kufungua malalamiko/ mashtaka rasmi! Hivyo serikali inahaki ya kujiosha kuwa hawana taharifa. Pia shemeji yangu Ruge na kaka yangu Makonda ni mrafiki wa muda mrefu sana, hivyo kwa Makonda zile office za Clouds zilikuwa kama nyumbani! Ni rahisi kusema huu ugomvi Mh. Rais kauchukuli Β more of morals than ethical and legal Β issue na ndio maana kaumaliza the way he did! 
Lakini kumbuka kuwa hata Ruge huko nyuma kwenye ile "tell it all" interview yake na Clouds 360 alisema kuwa yeye hataki ugomvi na Paul Makonda, yakuwa amemsamehe! Sasa tatizo ni pale kaka yangu Paul Makonda alipo drag huu ugomvi na kumtolea kashfa shemeji yangu Ruge!........Ngoja nikwambie ni rahisi sana kwa mwanaume kumsamehe mwanamke anapo mvunjia heshima kuliko mwanaume mwenzie! Yani ugomvi huu unaweza ukaisha machoni pa watu lakini joto lake litabakia likiunguza chini ya carpet kwa muda mrefu sanaaaaa! Huu ugomvi kiuhalisia bado haujaisha!............ 


Mimi bado nabakia na msimamo wangu kuwa simuungi kaka yangu RC. Makonda mkono kwa aliyo yatenda. Ningefurahia zaidi kuona anaomba msamaha kwa Ruge publicly hii siyo tu kwa ajili ya Ruge bali kwa manufaaa ya amani na maendeleo ya Taifa letu! Just humble yourself my brother utaheshimika zaidi! Lakini naomba ieleweke yakwamba; sina chuki yoyote ile juu ya RC Makonda wala familia yake!........

Plus, tujifunze kuweka mipaka ya urafiki wetu! Nakumbuka kuna siku baba yetu (Sir O.O Igogo) alikuwa anatuelezea kitu akasema, hivi mmeshawahi kuniona mimi nikiwaleta wafanyabiashara wenzangu kuzungumzia hapa nyumbani? Akafafanua kuwa, mambo yangu ya kazi na biashara zangu yote yanaishia pale mlangoni mwa ofisi za Utegi Tech. Hapa nyumbani kwangu ni mahala pa familia yangu na siyo ofisi!.......Mazoea yakizidi bila kujua kwanini mmezoeana yanaleta shida! Tuweke mipaka ya urafiki wetu kulingana na mahali husika. Marafiki wa kanisani basi wabaki kuwa marafiki wa kanisani na hivyo hivyo kwa wengine............ Mungu ibariki Africa, Mungu ibariki Tanzania.

Leave a Reply