Baba Keagan: Lakini yote ni MUNGU anawapima imani ili aweze kuonesha UKUU WAKE

Regrann from @paulmakonda  - Mara nyingine unapopewa mtihani haupimwi wewe ila wale wanaokuzunguka, kupitia mtihani wako watatokea watabiri, wazungumzaji na watu wa kila aina hadi watakaojivisha U-Mungu kiasi cha  kufikia kukufukuru mara nyingine, lakini yote ni MUNGU anawapima imani ili aweze kuonesha UKUU WAKE, na anawakusanya kwa wingi ili atakapotenda NENO LAKE lisambae, hivyo sio kila mtihani ni wa kwako. Na naomba nikiri Kupitia Keagan nimeuona UKUU WA MUNGU, tena MUNGU yule yule asieacha neno lake likaanguka, na kwa unyenyekevu mkubwa kwa hii furaha yote aliyoniletea narudisha sifa na utukufu kwake yeye alie juu'  Lakini pia kwa moyo mkunjufu kabisa nitoe shukran kwa kila mmoja aliejitoa kufurahi na kushukuru pamoja nami kupitia message, simu, post na hata maombi ya chini, tunasema asante sana sana na kupitia nyinyi nimeshuhudia Baraka nyingine ya WATU, kikubwa mtambue nathamini sana sana na kwa niaba ya mke wangu na familia kwa ujumla tunawashuru kutoka moyoni na MUNGU AWABARIKI SANA. #babaKeagan  - #regrann

Leave a Reply