Binadamu kama Nyani!

Kuna binadamu wenye tabia za kama huyu Nyani anaye mvuta mwenzie mkia. Yani mtu anatumia nguvu za ziada kutaka kumuangusha fulani kwasababu tu anamzidi mahala fulani.

Ukweli usiopingika ni kwamba nguvu anyopoteza kumvuta mwenzake chini ni kubwa sana kuliko nguvu ambayo angetumia kufikiria apandaje juu ya mti! Kama angeweza kujitathimini na kujua wapi anakosea halafu angeamua kutumia nguvu hiyo hiyo kupanda juu nafikiri huwenda angekuwa mbali zaidi ya huyo anaye mvuta chini.

Hivi ndivyo baadhi ya watu walivyo. Wanachukua nguvu nyingi kimchukia mtu au watu ambao hawana uhusiano wowote katika kushindwa kwao au kutokufanikiwa kwao. Badala ya kujitathimini wao wanajenga chuki. Kwamfano, embu fikiria kama huyu Nyani anaye mvuta mwenzake kama angeamua kuzunguka upande wa pili wa mti akatumia hiyo nguvu kupanda unafikiri angekuwa wapi? Huwenda angekuwa amefika juu ya mti akapunga na upepo mwanana huku akimchora mwenzie!

#TafakariJuuYaMaishaYako #AchaChukiHaijengi

Leave a Reply