Category Archives: Alpha being Alpha!

Nawatakieni kheri katika kufunga mwaka na neema za mwaka mpya!

Wapendwa wasomaji wangu, ndugu jamaa, na marafiki, katika haya masaa machache yaliyobakia kumaliza mwaka huu wa 2017 napenda kuwatakia kheri katika kufunga mwaka na pia nawaombea neema na baraka zote za mwaka mpya ziwashukie na kukaa nanyi siku zote!   Blog hii nili register rasmi tarehe 15th Dec, 2015 hivyo mpaka sasa ninakuwa nimetimiza miaka miwili na wiki kama mbili hivi! Mwaka wa kwanza nilifanya vizuri sana tena sana! I was very proud of myself! Mwaka wa pili niliyumba kidogo kwasababu "vidudu mtu" wale mafundi wa majungu na fitina wakaingilia kati! Hivyo kimaendeleo ya blog sikufanya vizuri japo wasomaji wangu wameongezeka kwa zaidi ya 300%++ ukilinganisha na mwaka wa kwanza  Wanasemaga 'adui' ukimjua hakusumbui kichwa! Basi nami nashukuru kwa nafasi waliyonipa kwani nimewajua! Hawaniumizi kichwa, kwanza hata nguvu ya kusimama mbele yangu hawana! Wanajua sentence yangu moja inawatosha kuwapa "heart attack" 🤣🤣  hawana uwezo wa kuniangusha mimi wamebakia kupiga majungu behind my back, and definitely that is where they belong "behind my back" I hope I "smell"  good enough to make them stay there forever 🤣🤣 Siwapi nafasi tena! Yani huwezi amini wengine mpaka nacheka nao lakini akili kwa kichwa ati!!  2018 narudi kwenye mstari! Nawahaidi mambo mazuri kama yale ya mwaka wa kwanza! Tutajifunza na kucheka sana! Life is too short embu tujifurahie siye!.....Malengo yangu ni kwamba kila miaka 5 na make major move, lakini kama nitaweza kufanya hizo major move kabla ya miaka 5 nitashukuru sana! Just pray for me as I pray for you na sote tubarikiwe! Ukiona mapungufu yangu chukulia kama "fursa" kwako, kwani hata mimi niliona mapungufu ya wengine nikaona ni "fursa" yangu! Hivyo siku zote jifunze kutokana na makosa ya wengine siyo lazima yakukute wewe! Safari yangu ya kupunguza uzito! 🙈🙈 Japo siwataharifu kila wiki kama nilivyo haidi lakini bado iko pale pale. Na ninepungua, sema lile tumbo la chini ndio bado😭😭 Niliacha kuwapa progress kila wiki kwani ilikuwa inanikatisha tamaa kuona wiki nzima napungua 1Lb😜😜 nikaona bora nifanye mazoezi na diet kimya kimya ikifika mwezi wa 5 mwakani nawapa report iliyo kamilika!   Nimepungua toka size 16 na 18 mpaka 12 na kuna nguo moja ndio 14, nafikiri inategemea na deaigner na material iliyotumika! Namshukuru Mungu kwa mambo mengi sana, na moja ya jambo ambalo ameweza kunibariki nalo mwaka huu ni kuonana na ndugu zangu. Miezi minne ya mwanzo mwaka huu nilikuwa Tanzania, nashukuru nimeweza kuonana na ndugu zangu wote! Mara nyingi nikiwa likizo kutoka na sababu za shule baadhi yao walikuwa nje ya Tanzania hivyo tulikuwa hatuwezi kukutana pamoja kwani ratiba zilikuwa tofauti sana. Mimi huwa siendi nyumbani mara kwa mara unless kuna kitu cha lazima ndio maana huwa nikienda nakaa miezi 3+! Mara nyingi kila baada ya miaka 2 ndio nakwenda. Kama kuna kitu nilifurahiya nilipo kuwa nyumbani ni kuwepo wakati wa birthday ya baba yangu! Miaka yote huwa na miss hii siku! Lakini safari hii Mungu alinibariki nilikuwa nyumbani na mimi ndio nilikuwa "master mind" behind hiyo surprise 😍👌 Mimi hapa ndo huyo nimeshika camera 😍😍 Kama kuna kitu namshukuru Mungu siku zote na nitamshukuru mpaka nakwenda kaburini ni zawadi ya hichi 👆 kiumbe! Sijui na wala sitaki kujua maisha yangu yangekuaje bila mwanangu! Mungu zidi kunilindia na kumbariki mtoto wangu! Jamani, nisiwachoshe na maneno mengi 🙈🙈 Namshukuru Mungu kwa yote! Nawatakieni kheri ya kufunga mwaka na baraka na neema zote za mwaka mpya ziwashukie na kukaa nanyi! Happy New Year everybody! Love you all!

Me, myself, and I #TBS

  Mimi hapa nilikuwa likizo home-KekoJuu in 2010. Hapa nilikuwa navaa size 12 na hilo ndio lengo langu nishuke mpaka size 12 but never chini ya 10! Sasa hivi bado nacheza na 12 na 14 inategemea na designer.

Utegi street!

Nimetumiwa picha hii  leo ikionyesha kibao cha mtaa wa kuingia nyumbani kwa mama yangu ikiwa na jina la kijiji alipozaliwa baba yangu ambacho kinaitwa UTEGI.

  Sina huwakika ni serikali za mitaa au wilaya / mkoa ndio unatoa majina ya mitaa ila mimi nimefurahi kwani huku Marekani  vitu kama hivi huwa ni big deal sana! Nimefurahije sasa 😍😍 kijiji chetu kinajulikana kimataifa ati! Simnajua kuna UTEGI International Ltd 🤣🤣🤣 Natamani ile bara bara inayokatiza toka NSSF kupitia kwetu watu wa Tanroad nao  wangeipa jina la “Otieno Igogo road” aaaah! Sasa hapo lazima nyumba yetu ingekuwa kati kati ya makutano ya Otieno Igogo road na Utegi  street itapendeza zaidi in Dr Shika’s voice 😍😍😍 (tazama picha hii 👇👇 kwa mfano tu)   kama nawaona wenye roho za kichawi! Watu wa Kansas city hakikisheni Robert Otto anaona hii picha maana anajifanya asomi hii blog 🙄🙄 mwambie soon Utegi inatinga USA  yani kama anaweza akimbie apande juu azibe au anywe sumu ya panya afie mbali!!! Na mtandao wote wa majungu najua mnasomaga hapa kama nawaona. Tatizo NYOTA AAA  🤣🤣🤣🤣🤣 nyota zenu zimefubaa hazingai 😂😂😂😂🙈🙈 anyway, hicho kilikuwa kibwagizo tu! Nimefurahi na namshukuru Mungu kwa yote!

Kama wewe ni mpangaji usimdharau mmiliki wa nyumba ya udongo!

Kama wewe unaishi kwenye nyumba ya kupanga usimdharau yule anayemiliki nyumba ya udongo! Hauna haki ya kufanya hivyo! Kwani wewe unayeishi nyumba ya kupanga hauna uwezo au nguvu ya kutosha kumiliki hata ardhi ya kujenga nyumba ya udongo. Nasiku ikatokea hauna kazi au ajali ya ulemavu ikakukuta ukashindwa kufanya shughuli za kuzalisha pesa inamaana utashindwa kulipa kodi ya pango na mwenye nyumba yake atakufukuza! Lakini yule mwenye nyumba ya udongo maisha yataendelea tu! Nyumba ya udongo inaweza isiwe na mvuto sana kwenye macho ya watu lakini inatoa matumizi sawa na nyumba ya matofali! Wakiitwa majina ya watu na mali zao mwenye nyumba ya udongo jina lake litakuwepo lakini jina la yule anaeishi nyumba ya kupanga itakuwa shida kwake! Usimdharau mwenye chake! Kama wewe ni mpangaji usimdharau mmiliki wa nyumba ya udongo!……..Anyway, hayo ni mawazo yangu asubuhi hii siku ya JumaTatu! Nawatakieni wiki njema na uzalishaji mwema!

Repost: women over 40!

Nimeipata hii article kwenye Facebook nikaona siyo mbaya ku share nanyi hapa. Mtaniwia radhi kwa wale msioelewa lugha hii ……..Picha zangu hazihusiani na hii story lakini mwakani itakuwa 41 so get your life 🤣🤣  #TBT “Ladies and gentleman, this is a must read!!! THIS HAS BEEN WRITTEN BY A MAN……….This is for all you girls 40 years and over….. and for those who are turning 40, and for those who are scared of moving into their 40’s…AND for guys who are scared of girls over 40!!!!…. This was written by Andy Rooney from CBS 60 Minutes.  

Andy Rooney says: As I grow in age, I value women who are over 40 most of all. Here are just a few reasons why: A woman over 40 will never wake you in the middle of the night to ask, “What are you thinking?” She doesn’t care what you think. If a woman over 40 doesn’t want to watch the game, she doesn’t sit around whining about it. She does something she wants to do. And, it’s usually something more interesting.

A woman over 40 knows herself well enough to be assured in who she is, what she is, what she wants and from whom. Few women past the age of 40 don’t give a damn about what you might think about her or what she’s doing. Women over 40 are dignified. They seldom have a screaming match with you at the opera or in the middle of an expensive restaurant. Of course, if you deserve it, they won’t hesitate to shoot you, if they think they can get away with it. Older women are generous with praise, often undeserved. They know what it’s like to be unappreciated.

A woman over 40 has the self-assurance to introduce you to her women friends. A younger woman with a man will often ignore even her best friend because she doesn’t trust the guy with other women. Women over 40 couldn’t care less if you’re attracted to her friends because she knows her friends won’t betray her.

Women get psychic as they age. You never have to confess your sins to a woman over 40. They Always Know.  A woman over 40 looks good wearing bright red lipstick. This is not true of younger women. Once you get past a wrinkle or two, a woman over 40 is far sexier than her younger counterpart. Older women are forthright and honest. They’ll tell you right off if you are a Jerk if you are acting like one! You don’t ever have to wonder where you stand with her.

Yes, we praise women over 40 for a multitude of reasons. Unfortunately, it’s not reciprocal. For every stunning, smart, well-coiffed hot woman of 40+, there is a bald, paunchy relic in yellow pants making a fool of himself with some 22-year-old waitress. Ladies, I apologize. For all those men who say, “Why buy the cow when you can get the milk for free”. Here’s an update for you. Nowadays 80% of women are against marriage, why? Because women realize it’s not worth buying an entire Pig, just to get a little sausage!

Embu tucheke kidogo! Eti wewe waonaje kwa hili?

Juzi kati niliweka tangazo la msiba wa ndugu yangu  kwa hii blog , nikaambatanisha na picha ambazo tulipiga akiwa hai ambapo ilikuwa mara ya mwisho kuonana naye Tazama hapa 👉👉  (Tanzia). Sasa kuna mtu ameweka comment akishangazwa na picha niliyotumia kwani tulikuwa tuna tabasamu. Anasema tunatangazaje kifo kwa furaha hivyo? Soma 👇👇  Nimecheka kwani kwangu imekuwa kichekesho,nikahisi huyu dada lazima atakuwa Muhaya maana Wahaya akili zao wanazijua wenyewe, na hilo pozi wala uulizi katoka mkoa gani 😅😅 …… Hivi kuna kanuni ya picha ipi itumike kutangaza msiba? Ukishaweka picha ya marehemu akiwa mwenyewe zile zingine sizinakua ni kumbukumbu mlizopiga!! Jamani, mimi ni Msabato na Mjaluo vile vile hivyo kuna vitu vingine haswa kwenye swala la misiba mtanisamehe. Kwani kuomboleza kupo tu lakini huwezi kuomboleza kama mpagani! Halafu, tujenge tamaduni za kuonyesha upendo wa dhati kwa wale ambao wanagusa maisha yetu wakati bado wako hai! Mambo ya kumlilia mtu na maneno mazuri akisha kufa ni upuuzi mtupu! Yani mimi kama umeshindwa kunipenda nikiwa hai, hata salamu hutujuliani gafla nikisha kufa eti wewe ndo unakuja na makelele yako kunililia?! No! Sitaki! Kaa kwako nitashukuru zaidi, kuliko kuja kunililia kinafiki! Kwanza kuliliwa na wanafiki inaweza ikawa kikwazo cha kuingia Mbinguni 😅😅 just saying! Sipendi wanafiki haswa nikisha kufa nawaomba msije! Nionyeshe unanipenda na kunijali nikiwa hai! Nami nitafanya vivyo hivyo!

Ukichoka unaruhusiwa kupumzika…….!

Wapendwa wasomaji wangu, I am taking a break! Nitarudi mwishoni mwa mwezi wa 11 au wiki ya kwanza ya December.  Mambo mengi kwa sasa nahitaji kupumzika sina muda wa ku blog! Hata wewe ukichoka ni ruhusa kupumzika lakini usilale fofofo 😍😍 …..Asanteni.

Usiumize kichwa chako na mipango ya mtu! Fanya yako!

Nafikiri kuna ugonjwa mpya wa umeingia  nashindwa kuelewa niupe jina gani. Sijui ndio ugonjwa wa “kuwashwa washwa” in Dr. Magufuli’s voice 🙈🙈 baadhi ya watu wanapenda kufatilia mambo ya watu mpaka huruma! Sikujua mambo yangu yanaumiza watu kichwa namna hiyo! Am I such a big deal?! Sikujua asanteni, na hapo ni haka ka blog tu watu hamlali 🤣🤣🤣 ee Mungu endelea kumimina hizo baraka zako, mtumishi wako nipo teyari kuzipokea Baba, mimina Baba 🙏🙏  Eti mtu unaangaika kutaka kujua kwanini amehamia Houston? Jamani kwani kuna dhambi gani mie kuhamia Houston!! Oh, nasikia unataka kuhamia? Nihamie wapi tena??? Mie hapa ndio Kigoma mwisho wa reli!! Yani mnakera nyie watu!!  …….watu wangejua kuna raha sana kufanya yako wasinge angaika na maisha ya mtu! Wewe mbaba / mama mzima mwanaume loser fulani anakutumia kufatilia mambo ya Alpha halafu na wewe unajiona mjanja eti unakubali 🙉🙉 hivi unalipwa kiasi gani? Maisha yangu yanakuvutia eeh!? Basi wewe endelea kutembelea hii blog majibu yako yote utayapata hapa wala usiumize kichwa kumuuliza mtu! ……..Embu acha kuumiza kichwa na mipango ya maisha ya mtu mwingine fanya yako! 😠😠

“I’m Charles McCater. I’m going to die Charles McCater”

“I’m Charles McCarter. I’m going to die Charles McCarter. I don’t even know why you’re here. Call Brenda and get my kids. where are my kids?! I asked you to do one little thing and you can’t even do that after 18 years get out……”

Kuna watu hata uwe mwema kwao kiasi gani they will never ever appreciate you or respect what you did / doing to them! …..Sasa ndio kama huyu “Charles McCarter” mtu ambaye ameokoa maisha yake tena wakati akiwa na kila sababu ya kumuacha afe yeye ndio kwanza anamdharau na kumuongezea hasira!! ……..Eti “I’m Charles McCarter. I’m going to die Charles McCarter”!! Jamani, lazima tukubali kuwa kuna watu hawawezi kubadilika isipokuwa kwa uwezo wa roho mtakatifu pake yake!! Na wengine hawawezi badilika kwani roho wa Mungu alisha hama ndani yao! Watu wa namna hii hata kama unawaombea waombee tu lakini kaanao mbali kwani wanaweza wakakufanya ufanye maamuzi ya hasira bila kutegemea kama huyo mama!! …….huu usemi wa Maya Angelou “when people show you who they are believe them” kwakweli nimejikuta siku hizi nautumia sana katika kuangalia ni watu wa namna gani I want around me! Mtu akisha kuonyesha dalili zote za kuwa yeye labda ni mchonganishi, mmbea, tapeli, tafadhali wala usisite kuamini kuwa she / he is less than what your  instinct is telling you!! Some people are “Charles McCarter” and they will die “Charles McCarter”! Just leave them alone!  ***Picha yangu haina huusiano wowote na story nimeitumia tu****

Hello there…….!

Alpha Igogo- blogger

Hello wapendwa! Natumaini wote wazima wa afya njema. Ni muda sasa tangu niiweke sura yangu humu, imebidi leo “nijirushe”  bila kupenda maana wengine hamkawii kusahau sura yangu 😁😁 Nawageni ndio wanazidi kuongezeka siku hadi siku, karibuni sana! ……Mimi naitwa Alpha Igogo ndio mmiliki wa hii blog! Wenyewe na lugha zao wanasema “Owner and C.E.O” aha! Mie niite Alpha inatosha kabisa! C.E.O bila pesa hainogi hata kidogo 😆😆 Huyu mrembo niliyepiganae picha ni binti yangu, mwanangu wa pekee kwasasa! Nimesema “kwasasa” lakini pia usisahu nimesema wa “pekee” hivyo hakuna ajuaye ya kesho huwenda hayo maneno yote yakabadilika au yakabaki jinsi yalivyo! Well, I’m a woman I am allowed to change my mind (in Wendy Williams voice) 😁😁 ……..though niko very curious kuona kama nikizaa na “Mzungu” mtoto wangu atafananaje 🤣🤣🤣 Yani niliwaza tu, je atatokea mweusi kama mimi au atakuwa wa light chocolate? Au atakuwa mzungu kama baba yake? Nywele zake je zitakuwa kama mzungu au kipili pili kama zangu? Atachukua shepu ya “Kibantu” au atakuwa kama mzungu? Honestly, nipo so curious 😁😁 Nilimwambia mwanangu hili wazo langu, akasema “something must be seriously wrong with your brain” 🙈🙈 …….Je! watakajua kama nikiongeza mtoto mwingine atakuwa na baba mzungu au muafrica?! Basi endelea kutembelea blog hii bila kuchoka na jibu lako utalipata hapa hapa 😍😍 Haya jamani kibonge mie, nawatakieni siku njema. Tuonane wakati mwingine!

“I realized that they don’t know what grace is, they can’t identify serenity,”

"It's definitely difficult being a woman and growing up a girl. When you're graceful, people say you lack personality; when you're serene, people say you're boring; when you're confident, people say you're arrogant; when you're feminine, people say you're too girly; and when you climb trees, people say you're too much of a tomboy! As a woman, you really need to develop a very strong sense of self and the earlier you can do that, the better! You have to be all the things that you are, without allowing other people's ignorance change you! I realized that they don't know what grace is, they can't identify serenity, they have inferiority complexes, they are incapable of being feminine, and they don't know how to climb trees!" ~~~~~~~~~ C. JoyBell C.

Hakuna dhambi kuwa wa tofauti na wengine. Dhambi nikulazimisha kuwa kama wengine!

Hakuna dhambi kuwa wa tofauti na wengine. Dhambi nikulazimisha kuwa kama wengine! Kuna watu ambao maisha yao binafsi yanawapita au wanajikuta kwenye matatizo kila siku iyendayo kwa Mungu kisa na mkasa ni kulazimisha kukubalika kuwa mmoja wa “nyumbu” wa kundi fulani! Nimewaita “Nyumbu” kwasababu Nyumbu ndio wanatabia ya kufata mkumbo wa wengine ili akubalike! Trying so hard to “fit in”! Na saa nyingine hata kama una fit-in kwenye group fulani haimaanishi kuwa hapo ni mahali pako stahiki! Kuna watu wanashindwa kupata mibaraka yao mikubwa ambayo Mungu amewaandalia kwasababu ya kulazimisha kuwa kwenye group fulani!

Mibaraka ya Mungu ni mitakatifu hawezi kupa kama hauko teyari! Hivyo nilazima uwe umeandaa sehemu au umejiandaa kwa kujisafisha / fanya matengenezo ya njia zako ndipo anakumiminia!

Vijana wengi wa kike hata wanawake wazima wasiku hizi wanapenda sana maisha ya kuiga na kufata mkumbo kwasababu hawajui thamani yakuwa mtu ‘Huru’! Mtu mwenye mtazamo na maamuzi yako binafsi ambayo hayavunji sheria wala kuingilia haki na uhuru wa mtu mwingine! Why trying so hard to fit in when you were born to stand out! #BeYou


Kama picha zinavyo onekana, mimi naamini ni mtu huru! Basi weekend hii na week hii yote nimejisikia na nimeamua ku-rock mabutu hair style! Kwani kuna dhambi gani mtu kusuka mabutu? Yani kuna joto kiasi kwamba sitaki kusuka rasta, na mawigi yananiwasha kwa hili joto!  Nasema hivi, hakuna dhambi kuwa wa tofauti, dhambi nikulazimisha kufanana na kila mtu! In a world full of Kardashians be Princess Diana!………..Btw, Sijajichubua, ni makeup na reflection ya miyonzi ya jua! #AlphaBeingAlpha Hii picha ☝ nilipiga Summer 2015, one week baada ya kuhamia Texas! Hapa sikupaka makeup 😍

 

“Save your sorry”!

Embu tuongee kidogo wapendwa, hivi nawewe umechoka na hawa watu ambao wanakutenda tena kwa makusudi halafu akitegemea kuwa atakuja kukuomba msamaha and everything will go back to normal 🙉🙉 Najua hakuna mkamilifu lakini kuna vitu fulani mtu akikutamkia au kukutendea kama ni mtu unaye jithamini lazima useme No! You have crossed the line, "save your sorry" to someone else! Kama Janet Jackson kwenye hii movie  😅😅  (tazama clip 👇)........... Yani mimi sijui nimekuaje siku hizi nafikiri watu wamechukua upendo na ukarimu wangu kama udhaifu hivyo kwa muda mrefu I put up with a lot of crap! But ma'am! Some must happened with my 40th birthday, I have ZERO tolerance with Unkind people, ungrateful people, wale watu ambao unakwenda above and beyond for them only to be " verbally and emotionally abuse"??? Boy!! Save your sorry! Sio at this age! Kama ni  teenager unaweza sema you are in that age trying to figure out who you are but at this age! Nope! Wewe na your sorry Okwende huko (in Luo accent) 😅😅 I will forgive you  but our friendship will never be the same again!

 

 

Make no mistake about it…..!

"Don't give anybody privileges and rights without responsibilities. The mind cannot handle being afforded privilege without purpose. Make no mistake about it, whatever is earned cannot be mistaken for free, cheap or easy. Giving a grown person free privileges is like giving a baby a razorblade. Just because somebody wants to hold you does not mean that they can handle the responsibilities that come with you."~~~Bishop Larry Boyd

Ladies!~~~~not everyone is able to go where you are going……!

"LADIES!...... not everyone is able to go where you are going & there's no reason to hold on to someone that don't want to be held. Sometimes you have to cut the ropes & sail on to deeper waters... alone! And those who are not with you will just have to paddle back to shore!" ~~~~Bishop Larry Boyd

Happy 40th birthday to me!

Asante Mungu kwa mwaka mpya! Hakika nimeona pendo lako! Jina lako libarikiwe milele! Asante sana wazazi wangu kwa kunileta katika dunia hii! Namshukuru sana mama yangu kwa kunizaa lakini pia namshukuru sana baba yangu kwa kuacha wanawake wote na kumchagua mama yangu maana kama isingekuwa hivyo nisinge kuita wewe mama! Asante sana family yangu (kaka, dada, wadogo, na wengine wote) kwa uwepo wenu kwangu ndio nguzo yangu imara nasimamia, kivuli changu wakati wa jua kali, na kimilio langu wakati wa shida!……..Asante sana mwanangu najivunia sana wewe kuwa mtoto wangu na niheshima ya pekee kutoka kwa Mungu kunipa wewe katika maisha yangu! Nakupenda sana!
Happy 40th birthday to me! #LetLoveLeads #LifeBeginsAt40 🎈🎈🍴🎂🍨❤😍

Let me be……….!

Life is too short let Alpha be Alpha! Yani mimi kama I could have things my ways nafikiri ningekuwa na cheka tu kama #Zezeta …….Mpendwa, Usipoteze muda wako kusikitika kwanini yamekukuta yalio kukuta! Wewe sema kama yasingenikuta mimi nani mwingine anayestahili?  Mshukuru Mungu kaamua kukutumia wewe kama chombo cha kufikisha ujumbe wake kwa watu / duniani! Mungu anajua you are strong enough to handle the stormy weather ndio maana akakupitisha njia hiyo! Maybe alijua kama kila kitu kingekuwa rahisi kwako basi usingejua kusema Asante Mungu!  Yani Mungu asingekua na nafasi katika maisha yako! Shukuru, na furahia maisha yako hata kama kuna magumu gani unapitia. Kama unataka kulia nenda sehemu ambayo upo mwenye iwe chumbani au chooni wewe nenda kajifungie ulie wee tena lia sana kwa nguvu zote kwani kulia ni dawa ya kuondoa sumu ya hasira mwilini! Ila baada ya kulia hakikisha unafuta machozi yako na kuendelea na maisha yako kwani siku zetu hapa duniani zimehesabiwa na hazipo nyingi sana! Muulize Mungu, haya, katika hili unataka nijifunze nini ambacho sikuweza kujifunza mara ya kwanza! Maana wengine huwa tuna miss the core of the lesson na kwakuwa Mungu anatupenda sana basi naye hutupatia mapigo / maonyo hata mara tatu au zaidi mpaka pale tutakapo elewa somo! Basi muulize akufungulie ili usipate pigo lingine tena………..Life is too short let me be who I’m! Alpha is all about love and love is her religion! Love me or hate me I care less about you as my birthday is just around the corner and “Life” begins at 40!……Love you!

My weight loss journey……….!

Wapendwa wasomaji wangu, msifikirie nime bwaga “manyanga” hapana! Niliumia mguu, hivyo kwa muda wa wiki nzima nimeshindwa fanya mazoezi lakini kesho ratiba inaendelea kama kawaida!…….. hata hivyo sikuacha kuzingatia nini ninakula, hivyo mlo ulio kamilika ulikuwa unazingatiwa 😍 Haya safari inaendelea!

Niliwahi kusema hivi………!

“Ok! Lemme today address this issue to my fellow friends who think someone is less of LADY/WOMAN unless you wear something under size 10 or you have to look a certain way. First of all, we all are human being regardless of how we look-created by one person we call Him God, and to Him we all shall return one day.

Second, woman is woman whether she is fat or skinny, rich or poor, famous or not famous, tall or short, hair or hairless, black or white. We are all women and no one is obligated to be or do anything other than what they choose to be!! Third, to those people who constantly telling me “umenenepa sana, unabidi upungue” well, we all have had different life experiences and our bodies react differently, that doesn’t make any of us less woman. I do understand about health issue but who told you I’m not healthy anyway?! And where is written that skinny people are the most healthiest people in this planet?! Btw being healthy isn’t something I owe anyone except myself!! I don’t have to adhere to anyone’s specifications to be a valid woman that God has created me!! So please, save those comments “unabidi upungue” to your mama!! Yes, I said to “your mama” as I’m someone’s MAMA, she loves me, respects and adores me the way I am!!! Finally, if it’s true “we are what we eat” then I think some people need to eat BIBLE to Detoxify their evil ugly hearts!! #KeepingItReal” ******This is a Repost from my Facebook 2014**** ujumbe wangu kwa wanawake wote kuwa you are beautiful they way you are!! Don’t let idiots make you feel like you’re less of woman just simply you can’t wear size 8!! Confidence is the best outfit, keep it on everyday, and real beauty comes from within sio kwenye size ya nguo yako!! Umeshawahi ona mtu anavaa size 4 lakini anaroho ya kishetani!! Yani sura yake na matendo yake represent nothing but a devil?! I mean, am just saying!!……Wataalamu wanasema kuwa “big girls they always got big hearts”!!

Love conquers all!

Huwezi kumuonyesha KIPOFU NJIA  kwa kumtembeza gizani kwani yeye ni kipofu na haoni kama yupo gizani!! Huwezi kumfundisha mtu ambaye ni “bully” kuacha ku-bully watu just by doing the same thing wakati hicho ndicho anachokijua na ku- experience in his / her whole life!! Love! Love! Love! Kama Yesu alivyo tupenda sisi nasi tupendane vivyo hivyo!! Love conquers all!…………Kwa msionifahamu mimi naitwa Alpha Igogo na Upendo ndio Dini yangu! Nasema hivi My name is Alpha Igogo and Love is my Religion! Mbarikiwe wote.