Category Archives: Awareness!

The first locally owned Call Centre in Tanzania, Utel Global Co. Ltd is about to be opened!

“We are blessed to set up the first locally owned Call Centre in Tanzania. Utel Global Co. Ltd to be launched on 01st Nov, 2017 Is your business at stake because of insufficient customer support? We can bridge the gap between you and your customers with our 24×7 call center phone answering services. Start experiencing increased sales and better conversion rates along with the satisfied customers. Please Find us at PPF Tower 3rd Floor.”~~~~Utel Global team Mrs Janeth Igogo-Nyagilo Utel Global representative 

 

Hili halikubaliki! Mh. Paul Makonda tafadhali fuatilia hili!

 Nimesha sema mara nyingi na siku zote nitasema kuwa mimi si mwanasiasa nawala sitegemei kuingia kwenye siasa, na wala hata siku moja sitamtetea mwanasiasa yoyote yule! Mambo ya siasa nawaachia mwanasiasa wenyewe wateteane! Lakini naomba ieleweke kuna mambo ambayo yataniwia vigumu kunyamaza kama hill la kwenye video! Nahapa nitaongea kama Mtanzania, na kama mama! ……….Kwakweli hili swala limenihuzunisha sana! Hii hali siyo yakukubalika haswa katika karne hii ya 21! Nikiwa kama Mtanzania niliyezaliwa katika mazingira duni na wengi wa ndugu zangu bado wanaishi kwenye mazingira duni  hivyo, hawa watoto licha ya kwamba ni Watanzania yawezekana pia wakawa ni watoto wa ndugu zangu!! Hivyo siwezi kunyamaza kwa hili! Lazima jambo kama hill linalo hatarisha maisha ya watoto zetu likemewe na lipigwe marufuku mara moja!! Ni juzi tu tumepoteza watoto 32 wa LuckyVincent sec school (somahapa) halafu bado tu mambo kama haya ambayo yanahatarisha uhai wa watoto wetu hayajakemewa na kuweka sheria kali!?! Ni lini tutajifunza kuzuia majanga na siyo kutibu!! Watoto wanatakiwa kwenda shule kusoma siyo kutafuta na kubeba maji visimani!! Huu ni unyanyasaji wa watoto na kuwakatisha tamaa ya kusoma!! My brother Paul Makonda nimesikia hii ni Kinyerezi ambapo ipo ndani ya Mkoa wako, tafadhali naomba ufatilie hili swala!

#Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Africa!

Imbumba Yamadoda: What I am doing for myself I am actually doing it for you! And what you are doing for yourself you also doing for me!

A must watch to all African men!! Hii video niliiona almost two months ago, but nikawa nasubiria a “proper” day kuiweka. Sasa kwakuwa bado tupo kwenye furaha ya maadhimisho ya mtoto wa kike duniani basi nimeona ni vyema kuiweka! Kwakweli huu ni ukweli kabisa! Watoto wa Africa haswa wakike wamewekwa kwenye “pressure” of how to become a good citizens, great mothers, wives, sisters, and aunties bila kujua kuwa it always takes two to tangle!! Unakuta mtoto wa kike very well organized mentally, spiritually,  physically, na hata financially lakini anaangukia kwenye mikono ya mwanume asiye jielewa kabisa!! Mnyanyasaji na mambo mengi ambayo yanafanya maisha yao kutokuwa na furaha! A totally unprepared man for familyhood!! Na ukijaribu kuuliza hawa wadada utasikia ma’am! “All men are the same”!! Hivyo hakuwa na chaguo zaidi ya ku settle down for less!! ………Wazazi, waleeni vijana wenu ukijua kuwa kesho atakuwa mume wa mtu, mmoja ya wana jumuiya hivyo lazima awe teyari kuwa good citizen! Kuwa na hela doesn’t make someone a good citizen or good husband tabia yake na malezi ndio vitaeleza huyo kijana wako ni mtu wa namna gani! Nimeona vijana wenye pesa na ni wanyanyasaji wa wanawake mpaka inaogopesha! Wengine ni rapists and molesters! Tuwalee watoto katika njia ipasayo ili wasiwe mzigo kwa wengine na taifa analo ishi ni jukumu lako wewe kama mzazi!

 

Siku ya mtoto wa kike duniani: Tokomeza mimba za utotoni kufikia uchumi wa viwanda

“Kinachoendelea muda huu hapa Tarime, kongamano linalohusisha Wazee wa Mila, watoto wa kike, na wadau wa Maendeleo – Siku ya mtoto wa kike 2017 ni 🔥🔥… Unapitwaje jamani.. kauli mbiu ni “Tokomeza Mimba za Utotoni kufikia uchumi wa viwanda.. Wewe unawalinda vipi watoto ???? Ni jukumu letu sote 💪” Joyce Kiria

Where is my Jojo?! What happened to her?!

 Nawauliza walimwengu wa Dar es salaam na Tanzania kwa ujumla, yuko wapi Jokate wangu???? Mimi sitaki matani ya hivyo!!! Siku zaidi ya kumi hajaonekana yuko wapi?? Na nini mbaya imemkuta?!! Kamanda Sirro, please check on my baby sister please!! Kaka yangu Paul Makonda nakuomba unitafutie Jojo wangu, tafadhali hii siyo powa kabisa!! Jojo, I miss you beautiful where are you  my babysister? Please, I want to see your beautiful face and cute smile please!! I hope you’re well wherever you’re! Let me know baby girl! Love you 😘😘

Sale ya nguvu @Molocaho furniture by Amorette, kuanzia Sept. 1-8!

Haya sale ya nguvu kwa wale wanaopenda vitu vizuri vya kupendezasha nyumba na vyumba vya kulala! Nikutoka kwa Molocaho furniture by Amorette! Sale inaanza kesho asubuhi September Mosi (Sept.1st) masaa ya Africa Mashariki na kumalizika September 8th. Wahi kesho ujipatie furniture zenye ubora wa kimataifa kwa bei karibu na bure! Halafu siunajua asilimia fulani ya mauzo inakwenda kwenye ule mfuko wa kusaidia jamii wa Dr.Ntuyabaliwe Foundation! Basi nenda kaunge mkono tusaidie jamii yetu!

ADD Friends Campaign – Epsd 017 Tutakuwa Mubasha Azam Two Alhamisi asubuhi.

ADD Friends Campaign – Epsd 017
Tutakuwa Mubasha Azam Two Alhamisi asubuhi. 

Peter Sarungi (The Next Speaker)

Tunaendelea kutoa elimu mpya kwa jamii inayo zunguka watu wenye ulemavu ili kuondokana na fikra potofu.
Alhamisi 24/8/2017 Asubuhi ya saa mbili tutakuwa mubashara Azam Two tukijadili mada isemayo;

“Je nini kifanyike ili kuendeleza ustawi wa jamii ya watu wenye ulemavu nchini??”

Karibu tujadili na kujifunza wote. Kama una maoni, maswali na hata ushauri kuhusiana na mada hii una ruhusiwa kushiriki katika ukurasa wangu wa fb na tutazisoma hewani mubashara.

Karibu #ADDfriends tujenge ustawi mzuri kwa jamii ya walemavu.

Zari please watch this (Iyanla fix my life with Evelyn Lozada)!

Zari, this is all for you. I want you to take a moment and watch these clips or you can watch the whole episode on YouTube and see if you can relate yourself to Evelyn Lozada or learn something worthy to apply in your life! I see the “bling bling ” is off again! Not sure for how long will it be this time!!

Wishing you the best. Love you always!!

Road To Heaven Sent premiere: zimebaki siku 3, jiunge na WemaApp kuiona!

Nilipoanza na 10 days wallahy sikujua kama zitaenda fast kiasi hichi… Zimebaki 3 days yaani in other words tuna masaa 72 tu yamebaki… Wow…!!! Wow…!!! Wow…!!! Najua kuna walio mbali na wanajiuliza watapataje pataje kuona hii Kazi ya mikono yangu… Jibu kamili ni WemaApp tu… Will make sure unafanikiwa kujionea kazi hii kiganjani mwako… Ama nene… Lakini Pia, pale Mlimani City Tunaenda kwa Slogan moja tu ambayo ni, “Are you invited..???” Kama hutopata chance siku hio basi kutakuwa na After party …. Details zote ntawaletea Baadae…. 😉😉😉 #RoadToHeavensentPremiere

Sijawahi sema, usiamini mtu!

Wapendwa kuna mtu kani email kuniomba nimuajiri yeye kama msemaji wangu wa public  (PR)! Nikamuuliza kwanini anafikiria mimi nahitaji kuwa na msemaji wa public? Akasema mbona watu wanasema unatafuta?😅😅 Nimecheka sana!! Jamani, usiamini kila kitu unachokisikia midomoni mwa watu! Mimi kama ningekuwa nahitaji PR ningeweka tangazo hapa kwa blog! Halafu PR anifanyie kazi gani Wallah! Hii hii ya ku-blog ambayo hata Cent moja sipati au kuna nyingine?! 🙉🙉 shocking! ………Yani siku hizi watu wamekuwa waongo mpaka inaogopesha! Watu ambao ukiwaona uwezi amini!! Halafu wengine ndio utakuta kila Sabato asubuhi au JumaPili wao ndio wakwanza kufungua mlango wa kanisa 🙆🙆 Tuombeane jamani, siku za mwisho hizi wanasema upendo wa watu utapoa, nikweli kabisa. Watu wamekua na roho za kishetani hazielezeki! Mungu atusaidie!………..Hii blog yangu imenifanya nimejua mengi sana kuhusu Watanzania. Scary!

HealthyMaisha (health coaching hub) is coming soon! 4 more days to go!

Your Health is your Wealth. We’re excited that it’s only a few days from the launch of HealthyMaisha (health coaching hub). The gateway to the new you. Follow @healthymaisha and stay tuned for all they have in store for you. Tell a friend to tell a friend, we’re going Green! 😊 #healthymaishalifestyle #hmcomingsoon #aug26 #healthygoodlife #healthymaisha

Show mpya inakuja: The Untold show by Sunday Shomari

*The Show | UNTOLD*

The main purpose of UNTOLD is to Educate, Inspire and Entertain. The show features Tanzania’s from different walks of life, in and outside of Tanzania. With a large diaspora community in the US and other parts of the world, we believe that we all have a contribution to where our great nation is going.

The show will explore these individual’s lives; their moments of triumph and failure , decision patterns, their motivation and inspiration, beliefs, leadership style, family, relationships etc.

With these candid conversations we hope that others will be able to relate, be inspired and take something away that they can apply to their personal lives. We hope to remove the barriers that most of us create in ourselves –
redefining possibilities, expose patterns and remove the notation that success only belongs to a select few. In life your response to events is what determines the outcome.

*Untold Season 1 premieres 8.26.17. Like, subscribe and make sure you don’t miss our premiere on the 26th!*

ADD Friends Campaign – Epsd 013: Mchango wa Imani kueneza fikra potofu juu ya Ulemavu.~~~~Peter Sarungi

ADD Frriends Campaign - Epsd 013
Mchango wa Imani kueneza fikra potofu juu ya Ulemavu.
Peter Sarungi (The Next Speaker)
Habari marafiki zetu, leo ni moja kati ya siku za kuabudu kwa baadhi ya imani tulizo nazo nchini. Nami naomba nitumie siku hii kutoa ujumbe unao endana na siku hii lakini ukigusa kampeni yetu ya kuondoa fikra potofu juu ya watu wenye ulemavu.

Tabia, desturi na utamaduni ni moja ya vitu vinavyo tengeneza mitindo ya kuishi kwa jamii. Hata hivyo Imani ndio chanzo kikuu cha kutengeneza tabia, desturi, mila na utamaduni kwa jamii. Leo hii katika jamii zetu kuna mitindo mingi ya kuishi inayo akisi imani tulizo nazo. Imani ya mtu huonekana kupitia fikra zake, kwani kile mtu anacho kiamini ndicho atakacho kitenda.

Fikra potofu za jamii juu ya ulemavu ni moja ya zao linalo tokana na imani zetu katika jamii. Sipo kwaajili ya kupinga imani za watu lakini ni wajibu wangu kukataa imani kandamizi kwa walemavu. Imani zetu zimekuwa ziki tuaminisha kwamba moja ya makundi yenye kuhitaji misaada na huruma kutoka kwa jamii ni watu wenye ulemavu. Waumini wengi wamekuwa wakiamini kwamba ukimsaidia mlemavu basi unapata baraka na thwawabu kwa Mungu. Wanaamini walemavu wameumbwa ili kuwa chanzo chao cha baraka na mafanikio iwapo wata saidia kundi hilo.

Imani hii imejenga fikra ya kuwaona walemavu kama sehemu ya mtihani wa imani kwa jamii, imeleta fikra ya kuwaona walemavu kama viumbe walsio weza na hata ikitokea mlemavu huyo ameweza basi wataamini sio yeye wala jitihada zake bali ni Mungu. Yaani ni kama kobe unapo mkuta amepanda juu ya mti, lazima utasema kapandishwa.

Hizi ni fikra potofu zinazo tokana na mafundisho ya imani zetu. Kuna haja ya viongozi wa dini kubadilika haraka maana wakati ni huu ambao ADD Friends Campaign imefunguliwa maono yaliyo jificha kwa muda mrefu.
Ikiwa wewe unapata thwawabu kwa kunipa msaada wa siku moja, je mimi napata wapi hiyo thwawabu??? Au mimi si wa Mungu?? Au mimi naingia mbinguni bure??

Karibu ADD Friends tufikiri tofauti kwa pamoja ili kutibu jamii juu ya fikra potofu kwa watu wenye ulemavu.

Mchele bandia (wa plastic) ndani ya Houston, Texas!

Juzi liliwaletea habari ya Samaki bandia huko London! Sasa leo nawaletea habari ya Mchele bandia ndani ya jiji la Houston, Texas. Inaogopesha kwakweli. Huyu dada anasema alinunua chakula kwa restaurant  (sina huwakika kama ni restaurant ya Waafrica au la) lakini alipoenda kuuliza baada ya tukio akaambiwa kuwa Mchele walinunua kwenye Africa store moja ambayo  ni mharufu hapa Houston (binafsi siijui hiyo store). Kitu ambacho naweza sema nikuwa kama hawa wauwaji wamefanikiwa kuingiza mchele huu Marekani basi lazima Tanzania utakuwepo wa kumwaga! Kuweni wadadisi na hivi vyakula! ………… Embu tazama hiyo video 👇

Mungu atusaidie, atuhepushe na huyu shetani anayetaka kutumaliza!

Umesikia kuhusu Samaki bandia (wa plastic)?!

Umesikia au kuona hii?! Naamini wengi mmesikia nankuona mchele bandia sina huwakika kama wengi wameona kituko hiki! Juzi nilitumiwa video inayo onyesha mtu amenunua Samaki bandia katika moja ya maduka / supermarket ya Waafrica huko London. Kwakweli inaogopesha sanaaaaaa! Shetani ameamua kutuangamiza kwa njia ya vyakula baada ya kuona watu wanahimizwa kula vyakula bora haswa kuachana na nyama nyekundu! Embu tazama hii video 👇
Kama wewe ni mmoja wa watu ambao hawachunguzi nini wanakula basi anza sasa kwani itakusaidia sana! Kama unaweza kushika na kukagua fanya tu kama huyo kaka kwenye video Nakumbuka mwanzoni mwa mwaka huu nilipokuwa nyumbani nilimfundisha sana mama yangu kuacha tabia ya kununua kitu kwa kupewa recommendation na rafiki au mwanafamilia. Kunasiku tulikuwa Supermarket, sasa kwakuwa anajua mimi huwa situmii white-bread (ile ya ngano iliyo kobolewa), sasa akabiambia hizi biscuits ni nzuri sana ni "whole wheat" tena Sugar-free  nilishawahi kuzitumia ngoja nikununulie. Sasa kabla hajanunua nikachukua package moja nakusoma maelezo yake 🙊🙊 Nilipigwa na butwaa! Nikamuuliza, mama nani alikwambia hizi biscuits ni Sugar free?! Akasema dada yangu mkubwa (ninaye mfuata) ndio alimwambia. Halafu akakoleza; "tena anazipenda kweli"! 😂😂  Nikamwambia mama mara ngapi nakwambia usome ingredients ya kitu kabla ya kununua? 🙉🙉 Hizi biscuits wameandika Sugar free lakini inaaina nyingine ya Sukari ndani yake ambayo ni mbaya zaidi! Yani bora kula Sukari yakawaida ni salama zaidi ya hiyo! Mama yangu yeye miaka mingi sana hatumii Sukari, lakini hakuna kitu kibaya kama High Fructose Corn Syrup! Hii ni aina ya Sukari ambayo wengi wasiojua wanatumia lakini ni hatari sana. Ni sukari inayotengenezwa kwa mahindi na mihunzi yake. Inatumiwa sana kwenye artificial juices, and food! Baadhi ya watu wenye Diabetes wanatumia kama "surpliment" lakini ni hatari bora kuacha kutumia Sukari kabisa. Au tumia coconut syrup, honey, au maple syrup. Lakini hii Fructose Corn Syrup kaa nayo mbali!

New Song: Umoja ni nguvu by Leyla Bezuidenhout

 Princess Lelya katuletea wimbo wa kutuunganisha Watanzania wote. Msikilize  ☝ akijielezea katika radio 106 huko Atlanta, Georgia. Wimbo mzuri sana unakwenda kwa jina la “Umoja Ni Nguvu”!……… Nimeupenda sana kwani ameona mbali na kutokukubali kuingiza vyama vya siasa katika wimbo huu kwani isingekuwa na mvuto na nguvu ya wimbo ingepotea! …….Watu wa diaspora ni vizuri kuachana na mambo ya siasa ya “uchama”! Maendeleo hayana chama, kabila, wala dini! Hivyo nivizuri watu wakaungana kwa “U-Tanzania” wetu na kupigania haki na maendeleo ya Watanzania na sio chama fulani! ………Anyway, binafsi nimeupenda, chukua muda wako kuusikiliza na tafakari! …….. Hongera sana Lelya, well done!

“We need to be able to tell our own story…….we need to rebrand Africa”~~~~Akon

 

Jamani msinicheke, yani mie my brain ipo very “selective” inapokuja kwenye vitu vya kusikiliza, kutazama, au kukaa…….. Ubongo wangu ukigoma kuwa that’s not for you, basi inatuma msg kwa  hisia / feelings zangu nazo zinagoma kabisaaaa! Ndio maana nasema msinicheke nikiwaambia kuwa leo hii ndio kwa mara ya kwanza namsikia huyu mwanamuziki maharufu aitwaye Akon  kwasababu ni nadra sana utanikuta nikisiliza  hiyo aina ya music anayo imba! Hivi unajua sijui hata wimbo mmoja wa Kanye West 🙈🙈 at least Jaz najua ule wa “All I need in this life of sin its me and my girlfriend” 😅😅 Sasa kama na wewe ni kama mimi ngoja nikwambie kwa kifupi tu kuwa Akon ni mwanamuziki Mmarekani ambaye asili yake anatoka Senegal. Alizaliwa Marekani, wakarudi Senegal na wazazi wake mpaka alipofika umri wa miaka 7 akaridu U.S.A tena. Lakini pamoja na kuwa maisha yake yamekuwa hapa U.S.A roho yake bado ipo Africa na anataka tuitengeneze Africa yetu iwe kama mataifa hayo makubwa kwani inawezekana. Na jambo kuu la kwanza ni kuanza ku “rebrand” Africa kwa kutumia Waafrica, kulingana na maadili yetu, matamanio yetu, na mtazamo wetu! ………..tafadhali msikilize vizuri kwenye hii video 👇 kama lugha ni changamoto basi tafuta mtu akusaidie kukueleza…………. kusoma zaidi juu yake na malengo yake nenda 👉👉 (Akon_Africa)