Category Archives: Awareness!

Sijawahi sema, usiamini mtu!

Wapendwa kuna mtu kani email kuniomba nimuajiri yeye kama msemaji wangu wa public  (PR)! Nikamuuliza kwanini anafikiria mimi nahitaji kuwa na msemaji wa public? Akasema mbona watu wanasema unatafuta??? Nimecheka sana!! Jamani, usiamini kila kitu unachokisikia midomoni mwa watu! Mimi kama ningekuwa nahitaji PR ningeweka tangazo hapa kwa blog! Halafu PR anifanyie kazi gani Wallah! Hii hii ya ku-blog ambayo hata Cent moja sipati au kuna nyingine?! ?? shocking! ………Yani siku hizi watu wamekuwa waongo mpaka inaogopesha! Watu ambao ukiwaona uwezi amini!! Halafu wengine ndio utakuta kila Sabato asubuhi au JumaPili wao ndio wakwanza kufungua mlango wa kanisa ?? Tuombeane jamani, siku za mwisho hizi wanasema upendo wa watu utapoa, nikweli kabisa. Watu wamekua na roho za kishetani hazielezeki! Mungu atusaidie!………..Hii blog yangu imenifanya nimejua mengi sana kuhusu Watanzania. Scary!

HealthyMaisha (health coaching hub) is coming soon! 4 more days to go!

Your Health is your Wealth. We’re excited that it’s only a few days from the launch of HealthyMaisha (health coaching hub). The gateway to the new you. Follow @healthymaisha and stay tuned for all they have in store for you. Tell a friend to tell a friend, we’re going Green! ? #healthymaishalifestyle #hmcomingsoon #aug26 #healthygoodlife #healthymaisha

Show mpya inakuja: The Untold show by Sunday Shomari

*The Show | UNTOLD*

The main purpose of UNTOLD is to Educate, Inspire and Entertain. The show features Tanzania’s from different walks of life, in and outside of Tanzania. With a large diaspora community in the US and other parts of the world, we believe that we all have a contribution to where our great nation is going.

The show will explore these individual’s lives; their moments of triumph and failure , decision patterns, their motivation and inspiration, beliefs, leadership style, family, relationships etc.

With these candid conversations we hope that others will be able to relate, be inspired and take something away that they can apply to their personal lives. We hope to remove the barriers that most of us create in ourselves –
redefining possibilities, expose patterns and remove the notation that success only belongs to a select few. In life your response to events is what determines the outcome.

*Untold Season 1 premieres 8.26.17. Like, subscribe and make sure you don’t miss our premiere on the 26th!*

ADD Friends Campaign – Epsd 013: Mchango wa Imani kueneza fikra potofu juu ya Ulemavu.~~~~Peter Sarungi

ADD Frriends Campaign - Epsd 013
Mchango wa Imani kueneza fikra potofu juu ya Ulemavu.
Peter Sarungi (The Next Speaker)
Habari marafiki zetu, leo ni moja kati ya siku za kuabudu kwa baadhi ya imani tulizo nazo nchini. Nami naomba nitumie siku hii kutoa ujumbe unao endana na siku hii lakini ukigusa kampeni yetu ya kuondoa fikra potofu juu ya watu wenye ulemavu.

Tabia, desturi na utamaduni ni moja ya vitu vinavyo tengeneza mitindo ya kuishi kwa jamii. Hata hivyo Imani ndio chanzo kikuu cha kutengeneza tabia, desturi, mila na utamaduni kwa jamii. Leo hii katika jamii zetu kuna mitindo mingi ya kuishi inayo akisi imani tulizo nazo. Imani ya mtu huonekana kupitia fikra zake, kwani kile mtu anacho kiamini ndicho atakacho kitenda.

Fikra potofu za jamii juu ya ulemavu ni moja ya zao linalo tokana na imani zetu katika jamii. Sipo kwaajili ya kupinga imani za watu lakini ni wajibu wangu kukataa imani kandamizi kwa walemavu. Imani zetu zimekuwa ziki tuaminisha kwamba moja ya makundi yenye kuhitaji misaada na huruma kutoka kwa jamii ni watu wenye ulemavu. Waumini wengi wamekuwa wakiamini kwamba ukimsaidia mlemavu basi unapata baraka na thwawabu kwa Mungu. Wanaamini walemavu wameumbwa ili kuwa chanzo chao cha baraka na mafanikio iwapo wata saidia kundi hilo.

Imani hii imejenga fikra ya kuwaona walemavu kama sehemu ya mtihani wa imani kwa jamii, imeleta fikra ya kuwaona walemavu kama viumbe walsio weza na hata ikitokea mlemavu huyo ameweza basi wataamini sio yeye wala jitihada zake bali ni Mungu. Yaani ni kama kobe unapo mkuta amepanda juu ya mti, lazima utasema kapandishwa.

Hizi ni fikra potofu zinazo tokana na mafundisho ya imani zetu. Kuna haja ya viongozi wa dini kubadilika haraka maana wakati ni huu ambao ADD Friends Campaign imefunguliwa maono yaliyo jificha kwa muda mrefu.
Ikiwa wewe unapata thwawabu kwa kunipa msaada wa siku moja, je mimi napata wapi hiyo thwawabu??? Au mimi si wa Mungu?? Au mimi naingia mbinguni bure??

Karibu ADD Friends tufikiri tofauti kwa pamoja ili kutibu jamii juu ya fikra potofu kwa watu wenye ulemavu.

MPIGIE KURA KARIM MICHUZI ASHINDE TUZO YA FILAMU FUPI ZA UMOJA WA ULAYA

MPIGIE KURA KARIM MICHUZI ASHINDE TUZO YA FILAMU FUPI ZA UMOJA WA ULAYA

Tupige kura wapendwa tulete huu ushindi nyumbani! Kijana anakipaji kizuri sana. Embu tuungane pamoja! Asante

Mchele bandia (wa plastic) ndani ya Houston, Texas!

Juzi liliwaletea habari ya Samaki bandia huko London! Sasa leo nawaletea habari ya Mchele bandia ndani ya jiji la Houston, Texas. Inaogopesha kwakweli. Huyu dada anasema alinunua chakula kwa restaurant  (sina huwakika kama ni restaurant ya Waafrica au la) lakini alipoenda kuuliza baada ya tukio akaambiwa kuwa Mchele walinunua kwenye Africa store moja ambayo  ni mharufu hapa Houston (binafsi siijui hiyo store). Kitu ambacho naweza sema nikuwa kama hawa wauwaji wamefanikiwa kuingiza mchele huu Marekani basi lazima Tanzania utakuwepo wa kumwaga! Kuweni wadadisi na hivi vyakula! ………… Embu tazama hiyo video ?

Mungu atusaidie, atuhepushe na huyu shetani anayetaka kutumaliza!

Umesikia kuhusu Samaki bandia (wa plastic)?!

Umesikia au kuona hii?! Naamini wengi mmesikia nankuona mchele bandia sina huwakika kama wengi wameona kituko hiki! Juzi nilitumiwa video inayo onyesha mtu amenunua Samaki bandia katika moja ya maduka / supermarket ya Waafrica huko London. Kwakweli inaogopesha sanaaaaaa! Shetani ameamua kutuangamiza kwa njia ya vyakula baada ya kuona watu wanahimizwa kula vyakula bora haswa kuachana na nyama nyekundu! Embu tazama hii video ?
Kama wewe ni mmoja wa watu ambao hawachunguzi nini wanakula basi anza sasa kwani itakusaidia sana! Kama unaweza kushika na kukagua fanya tu kama huyo kaka kwenye video Nakumbuka mwanzoni mwa mwaka huu nilipokuwa nyumbani nilimfundisha sana mama yangu kuacha tabia ya kununua kitu kwa kupewa recommendation na rafiki au mwanafamilia. Kunasiku tulikuwa Supermarket, sasa kwakuwa anajua mimi huwa situmii white-bread (ile ya ngano iliyo kobolewa), sasa akabiambia hizi biscuits ni nzuri sana ni "whole wheat" tena Sugar-free  nilishawahi kuzitumia ngoja nikununulie. Sasa kabla hajanunua nikachukua package moja nakusoma maelezo yake ?? Nilipigwa na butwaa! Nikamuuliza, mama nani alikwambia hizi biscuits ni Sugar free?! Akasema dada yangu mkubwa (ninaye mfuata) ndio alimwambia. Halafu akakoleza; "tena anazipenda kweli"! ??  Nikamwambia mama mara ngapi nakwambia usome ingredients ya kitu kabla ya kununua? ?? Hizi biscuits wameandika Sugar free lakini inaaina nyingine ya Sukari ndani yake ambayo ni mbaya zaidi! Yani bora kula Sukari yakawaida ni salama zaidi ya hiyo! Mama yangu yeye miaka mingi sana hatumii Sukari, lakini hakuna kitu kibaya kama High Fructose Corn Syrup! Hii ni aina ya Sukari ambayo wengi wasiojua wanatumia lakini ni hatari sana. Ni sukari inayotengenezwa kwa mahindi na mihunzi yake. Inatumiwa sana kwenye artificial juices, and food! Baadhi ya watu wenye Diabetes wanatumia kama "surpliment" lakini ni hatari bora kuacha kutumia Sukari kabisa. Au tumia coconut syrup, honey, au maple syrup. Lakini hii Fructose Corn Syrup kaa nayo mbali!

New Song: Umoja ni nguvu by Leyla Bezuidenhout

 Princess Lelya katuletea wimbo wa kutuunganisha Watanzania wote. Msikilize  ☝ akijielezea katika radio 106 huko Atlanta, Georgia. Wimbo mzuri sana unakwenda kwa jina la “Umoja Ni Nguvu”!……… Nimeupenda sana kwani ameona mbali na kutokukubali kuingiza vyama vya siasa katika wimbo huu kwani isingekuwa na mvuto na nguvu ya wimbo ingepotea! …….Watu wa diaspora ni vizuri kuachana na mambo ya siasa ya “uchama”! Maendeleo hayana chama, kabila, wala dini! Hivyo nivizuri watu wakaungana kwa “U-Tanzania” wetu na kupigania haki na maendeleo ya Watanzania na sio chama fulani! ………Anyway, binafsi nimeupenda, chukua muda wako kuusikiliza na tafakari! …….. Hongera sana Lelya, well done!

“We need to be able to tell our own story…….we need to rebrand Africa”~~~~Akon

 

Jamani msinicheke, yani mie my brain ipo very “selective” inapokuja kwenye vitu vya kusikiliza, kutazama, au kukaa…….. Ubongo wangu ukigoma kuwa that’s not for you, basi inatuma msg kwa  hisia / feelings zangu nazo zinagoma kabisaaaa! Ndio maana nasema msinicheke nikiwaambia kuwa leo hii ndio kwa mara ya kwanza namsikia huyu mwanamuziki maharufu aitwaye Akon  kwasababu ni nadra sana utanikuta nikisiliza  hiyo aina ya music anayo imba! Hivi unajua sijui hata wimbo mmoja wa Kanye West ?? at least Jaz najua ule wa “All I need in this life of sin its me and my girlfriend” ?? Sasa kama na wewe ni kama mimi ngoja nikwambie kwa kifupi tu kuwa Akon ni mwanamuziki Mmarekani ambaye asili yake anatoka Senegal. Alizaliwa Marekani, wakarudi Senegal na wazazi wake mpaka alipofika umri wa miaka 7 akaridu U.S.A tena. Lakini pamoja na kuwa maisha yake yamekuwa hapa U.S.A roho yake bado ipo Africa na anataka tuitengeneze Africa yetu iwe kama mataifa hayo makubwa kwani inawezekana. Na jambo kuu la kwanza ni kuanza ku “rebrand” Africa kwa kutumia Waafrica, kulingana na maadili yetu, matamanio yetu, na mtazamo wetu! ………..tafadhali msikilize vizuri kwenye hii video ? kama lugha ni changamoto basi tafuta mtu akusaidie kukueleza…………. kusoma zaidi juu yake na malengo yake nenda ?? (Akon_Africa)

Jubilee ya miaka 25 ya Kowak Girls Secondary school. August 26th, 2017!

Haya wana Kowak Girls Secondary school mpo!! Nimetumiwa ujumbe huu na Mkuu wa shule  (soma ?) kuhusu Jubilee ya miaka 25 ya Kowak Girls, itakayofanyika tarehe August 26th, 2017.  Tafadhali ukipata ujumbe huu mjulishe na mwenzako ili kuwezesha sherehe hii kufanikiwa........... Hongera sana Kowak Girls Secondary  walimu, wahitimu, na wanafunzi wote! ?
Soma ? (AboutKowakGirlsSec)

Bang magazine kulikoni? …….. Mmerudi sokoni ama?

 Wapendwa wa team ya Bang magazine vipi? Mmerudi sokoni au mnampango wa kurudi? Tuelezeni basi tujue, maana twaona picha lakini hamtupi maelezo vizuri! .............Ushauri wangu kwa Emelda Mwamanga, kama bado hujafanya mie nakuomba ufanye hili mpendwa; jishushe ukamuombe Jacqueline msamaha pia na Dr. Mengi ili Bang irudi;  You can't fight a Billionaire's wife!! Woman what's wrong with you (in Madea's voice ??)  . ...........Mama wawili, unajua jinsi ninavyo kupenda na pia nampenda Emelda sasa unanipa wakati mgumu mpendwa. Please, Mrs Billionaire (I love it when I  call you that ?) just forgive her and drop the case! ............Ok, najua soon tutamuona mama wawili kwa Bang akitangaza. Molocaho furniture ?

TAUS retreat, July 12 – 16, 2017

Nawasalimu wote katika jina la Bwana! ……. Naomba uweke hii event kwa calendar yako ya mwaka huu! Never  too late for spiritual revival so please add it! Ni TAUS retreat itakayofanyika tarehe July 12 -16, 2017 huko Wisconsin, U.S.A! Hii ni retreat ambayo inafanyika kila mwaka na huwa inaandaliwa na umoja wa Tanzania wa dhehebu la Wasabato hapa Marekani  (TAUS) lakini huwa wanakaribisha watu wote wa madhehebu yote kwa dini zote na hata wale ambao hawana dini wanakaribishwa! …….kusoma zaidi na uweze kujiandikisha basi  fungua hii link ? Emailing DOC-20170531-WA0005

                      WOTE MNAKARIBISHWA!

 

Mama Salma Kikwete umekosea sana! Hiyo inaitwa institutionalized discrimination!

Mama yangu, ninacho jaribu kukwambia ni kwamba fungua macho yako utazame hii hoja yenu kwa macho mapana utaona jinsi gani imejaa ubaguzi na unyanyapaaji wa hali ya juu kwa mabinti wanao pata mimba wakiwa shuleni! Kama mmeamua kufukuza shule wanafunzi basi mfukuze wote wanaofanya ngono wakike na wakiume kwa ujumla wao na siyo kubagua wanaopata mimba tu! Hivi mama Salma, kweli unataka kusimama hapa na kuiambia dunia, mbele za Mungu kuwa huyu binti yako mwenye gauni jeusi bado ni bikira?! Au kwasababu hajapata mimba kwahiyo unamuona mtakatifu?!! Kumbuka kabla ya kutunyooshea kidole sisi hakikisha kucha zako ni safi! Maana lazima tutazikagua!! Hizi sheria mnazoziweka bila kutafakari madhara yake katika jamii ipo siku damu zenu zitazilipa tu! Yawezekana leo hii haitamkuta binti yako lakini huenda kesho yakamkuta mjukuu wako! Oh! Nimekumbuka nyie ni “high profile” people, you do “high profile crimes” bila sisi walalahoi kujua, mama kumbuka Mungu anawaona!!

Kumnyima mtoto yoyote haki ya ku-access education ni kinyume na haki za binadamu. Kwani kupata elimu ni haki ya msingi ya binadamu wote! Wanafunzi wanaopata mimba wanatakiwa waachwe waendelee na masomo yao kama kawaida bila kubaguliwa na mtu yoyote yule. Kama hiyo ni ngumu basi wapewe “sick leave” wakisha jifungua waendelee na masomo yao.  Au kama hizo mimba zinawakera sana basi wafungulieni Abortion clinics ili wawe wanakwenda kuzi-abort huko, labda roho zenu zitafurahia!!

Kumbuka kuwa unapomnyima mama moja  haki ya kuelimika inamaana unatengeneza jamii / community ya watu wasio na muelekeo wa maisha na kuendeleza mila ambazo hazina tija kwa taifa! Mama ndio nguzo za familia nyingi haswa Africa. Hakuna njia mbadala katika hili swala zaidi ya kuwaacha waendelee na masomo yao bila ubaguzi wowote ule kwa faida zao binafsi, vizazi vyao, na taifa kwa ujumla!

Ngoja nimalizie kwa kusema kuwa, tatizo wazazi wengi wa Africa wanataka waonekane kuwa wao ni malaika hawajawahi fanya mistakes yoyote ile maishani mwao! Ndio maana wako guilty na busy kuwahukumu watoto kwa kuwapa adhabu za ajabu ajabu badala ya kuwaelekeza juu ya maisha. Unajua yale mambo ya kila mzazi anajifanya alipata ‘A’ darasani, alikuwa wakwanza siku zote, na kila mwanamke aliolewa akiwa bikira! Just a bunch of nonsense (Excuse my language)!. Uongo mwingi kwa watoto zenu bila sababu yoyote ya msingi!  Btw, hii ni karne ya 21, mama yangu where have you been?! Unaona statistics za dunia zinavyo kwambia yani karne hii wazazi nmnatakiwa kuongea na watoto / wajukuu zenu juu ya sex / elimu ya kujamiiana kabla ya miaka 10! Kwani watoto wa miaka 10 siku hizi wako sexually active na wengine wanabeba mimba! How? I don’t know usiniulize mimi lakini hiyo ndio hali halisi ya sasa, just get with the program mama!!

Mama Salma Kikwete umekosea sana! Hiyo inaitwa institutionalized discrimination!

Hivi ule usemi wako wa “mtoto wa mwenzio ni wako” uliufuta baada ya kuvua kofia ya u-FirstLady!! Bado najaribu kukutafakari nia yako haswa ni nini?! Wahenga walisema “uchungu wa mwana aujuae ni mzazi” lakini mimi saa nyingine napingana na huu usemi kwani kuna watu hawajawahi onja machungu ya uzazi wala malezi lakini wanaumizwa na kuguswa na watoto wa wengine kuliko baadhi ya wanawake walio zaa! Hapa simuongelei  mwingine bali ni aliyekuwa mkuu wangu ya shule ya Kowak Girls Secondary school Sister Magdalena (R.I.P). 

Miaka 23 iliyopita, nilipopata ujauzito nilikuwa form 2 pale Kowak Girls Secondary school Wilaya ya Rorya, mkoa wa Mara. Shule ilikuwa inaongozwa na wamishonari wa Catholic na huyu Sister Magdalena ndio alikuwa Headmistress (yeye alikuwa Mmarekani) na msaidizi wake alikuwa Sister Nyambosa  ambaye alikuwa Mtanzania. Sasa Sister Nyambosa kulingana na the so called “mila na desturi, sheria za Tanzania na dini” alitaka nifukuzwe shule!! Eti hiyo ndio adhabu yangu nikajifunze! But guess what?!! Sister Magdalena akasema NO! Hato hidhinisha hiyo barua ya mimi kufukuzwa shule kwani haoni logic ya hizo mila na desturi, pamoja na sheria za Tanzania. Yeye aliamini kuwa kitendo cha mimi kuwa mama kwa umri ule ni adhabu tosha! Pia nilikuwa mmoja ya wanafunzi wazuri pale shuleni hivyo hakuona kwanini aniharibie future yangu kwa kunifukuza shule ambayo technically angekuwa anaharibu future ya watoto wawili (mimi na kiumbe kilichokuwa tumboni mwanangu wakati ule).

Kufupisha story hii, wakafikia makubaliano yakunipa sick leave mpaka nitakapokua tayari kurudi shule basi wao walikuwa tayari kunipokea au kunipa uwamisho kwenda shule nyingine! Miezi sita baada ya kujifungua nilitafuta shule nikahamia, uhamisho wangu ulitumwa bila tatizo!! Shule niliyo hamia ilikuwa ni Nurulyakini Secondary school pale Mwembe Yanga, Temeke. Nilirudia form 2 kwani nilikuwa sijafanya mtihani wa form 2 nilipokuwa nimetoka Kowak. Wanaonijua vizuri wanaweza kushuhudia kuwa hata siku moja sijawahi kuwa ashamed kusema kuwa mimi nina mtoto. Kwani miezi mchache tu hapo shuleni nilianza kuwaambia wanafunzi wenzangu na hatimaye story zikafika hadi kwa walimu wote wa shule! Guess what?! Hakuna aliye jali wala kunifanya nijisikie vibaya kuwa mimi ni mama katika umri ule!! Walichojali ni academic records zangu! Tulipoingia form 3, nikachaguliwa kuwa Assistance HeadGirl, na nipofika form 4 wakanichagua kuwa HeadGirl na hiyo yote ni kwasababu ya jinsi nilivyo kuwa hapo shuleni walimu walipenda sana na kuniona as a blessing to their school.

Nakumbuka siku moja dada aliyekuwa ananiangalizia mtoto alikuwa anaumwa hivyo hakuweza kukaa na mtoto siku hiyo. Ilikuwa ni wiki ambayo tunafanya final exams review kwa ajili ya kuanza final exams za form 4!! Nilikuwa na 2 choices; ama nisiende shule nibaki nyumbani nimuangalie mwanangu au nimbebe mwanangu niende naye shule! Sikiliza mama, jinsi walimu wangu na wanafunzi wenzangu walivyo nifanya nijisikie wakawaida kama wao, yani wala sikufikiria mara mbili!! Nikamuogesha mwanangu nikajiandaa nikaendanae shuleni. Nipo darasani nasoma na mwanangu yupo pembeni yangu! Hakuna aliyeniona waajabu wala nini!  kila mtu alikuwa anamfurahiya mwanangu!! And for the records nilifaulu vizuri sana form 4!

Mama yangu sikiliza, tatizo lolote lile hata liwe kubwa kiasi gani ilikutafutiwa suluhisho la kudumu inategemea na attitude ya jamii husika na viongozi wake! Embu tafakari kama Sister Magdalena asingeweka msisitizo kuwa hato hidhinisha hiyo barua ya kunifukuza shule mimi ningekuwa wapi leo?!! Vipi kama walimu na wanafunzi wa Nurulyakini wangenibagua na kunitenga je mimi ningeweza endelea na masomo yangu?! Je, maisha yangu na ya mwanangu yangekuaje kama nisingepatiwa nafasi ya pili ya kufanya matengenezo?! Maana hivyo vyeti vyangu I mean my academic records ndio vilivyonileta hapa nilipo leo hii!! Labda nikwambie tu kuwa Nurulyakini ni shule ya Waislamu!

Hii tabia ya kutokutoa nafasi ya pili kwa “wakosaji” ndio inaleta matitizo mengi ndani ya Tanzania kama mambo ya vyeti feki, na forgeries nyingine! Viongozi wenye mtazamo kama wako ndio wanao changia matatizo kama hayo niliyo yataja katika jamii yetu!

By no means, siungi mkono maswala ya wanafunzi wa kike kupata mimba wakiwa mashuleni. Hata mwanangu analijua hilo kwani niliongenae mapema mno nilipo ona anaakili za kutosha kuelewa kile nitakacho mueleza. Lakini naomba uwelewe kuwa tatizo si kupata mimba, tatizo ni familia, jamii, na serikali imeshindwa kuelewa kuwa kuna uhitaji mkubwa wa kuelimisha familia pamoja na jamii nzima kuhusu swala la kujamiiana na changamoto zake haswa kwa watoto wakike! Leo hii unasema waliopata mimba wasiruhusiwe kuendelea na shule, ok! Fine! Vipi wanao adhirika na magonjwa Kama HIV, gonorrhea, genital herpes, syphilis, n.k  hao mnawafanyaje?! Kwani hayo pia siyanatokana na ngono??! Hauoni kama kuna haja ya kuwataka madaktari wawataharifu shule mara tu wampatapo mwanafunzi anaugonjwa wowote wa zinaa ili nao wafukuzwe shule?? Mbona mnawaonea wanaopata mimba peke yao?! Ooh! Au mnaonaje muanzishe sheria ya watoto wakike kukagualiwa kama wako sexually active au bado kabla ya kuingia shule katika kila muhula?! Labda hiyo ingetoa fursa sawa kwa mabinti wote! Na wanaume je mgewafanyaje?!!! Acha ubaguzi na unyanyapaaji mama yangu?!

***ITAENDELEA……… ***

Get inspired by dada Tuma!

Get inspired by dada Tuma weight loss journey! Fanya mwaka 2017 kuwa mwaka wako wa kufanya matengenezo kwa afya ya mwili wako na roho! Leo nawaonyesha picha ya dada yangu kipenzi dada Tuma ambaye alianza safari yake ya matengenezo ya afya yake mwishoni mwa mwaka jana, na sasa hivi she looks amazing! Yeye anafanya mazoezi na kuzingatia zaidi vyakula anavyo kula. Naona kuna watu wanatumia dawa ili wapungue lakini mimi naona ni bora mtu upungue kidogo kidogo hata kama ni kwa muda mrefu kuliko kutumia dawa! Lakini mwenye maamuzi ya mwisho juu ya mwili wako ni wewe mwenyewe!………..Happy birthday dada Tuma na hongera sana ?❤❤

Mama Salma Kikwete umekosea sana! Hiyo inaitwa institutionalized discrimination!!

Sipendi kuongelea maswala ya siasa tena kwa hii blog ila kuna mambo ambayo nikiona kuna umuhimu wa kutoa maoni yangu basi nitafanya hivyo. Mama yangu mama Salma Kikwete unajua nakupenda sana. Jambo kuu katika sheria za upendo ni kumwambia mtu ukweli pale anapo kosea. Basi nami naomba nikwambie kuwa  mama yangu umekosea sana!

Nimesikiliza kwa makini hoja yako juu ya wanafunzi wanaopata MIMBA wakiwa mashuleni ikanigusa kwa masikitiko makubwa sana kwani huyo mwanafunzi ambaye wewe unamuongelea LEO alikuwa ni mimi MIAKA 23 iliyopita! Siamini leo hii baada ya miongo miwili kupita hili swala bado halijatafutiwa suluhisho chanya ndani ya Tanzania na leo hii inabidi nisimame kuwatetea waathirika wote wa mimba za utotoni/ mashuleni?!

Awali ya yote naomba utambuwe kuwa hakuna binti yoyote anayependa kupata mimba akiwa shule. Lakini hiyo haimaanishi kuwa wanaopata mimba ni wanadhambi kuliko wale ambao hawajapata mimba au wanaotoa mimba. Hii stigmatization na discrimination kwa wanafunzi wanaopata mimba au mabinti wanaopata mimba kwenye umri mdogo lazima jamii ikemee kwa nguvu zote. “Structured” life style ndio tatizo kubwa sana katika familia na jamii  nyingi za Kiafrika haswa Tanzania!!

Pili nani alisema mimba ni ugonjwa unaomzuiya binti kuendelea na masomo yake?!! Mnapo mzuiya huyu binti kuendelea na masomo yake vipi kuhusu mwanaume aliye mpa huyu binti mimba?! Yeye anapewa adhabu gani?? Kwanini watoto wakike ndio wamekuwa wa kubebeshwa lawama na mizigo yote bila kuangalia both sides of the coin?? Hivi hizi mimba huwa wanajipa wenyewe au?! Na vipi wale ambao wanapata mimba kwa njia ya ubakaji nao wapo kwenye hukumu hii au?!!

Mama yangu, umesema vitabu vyote vya dini Qur’an na Bible eti vinakataza watoto wa kike kupata mimba kabla ya wakati?! Ni wakati gani huo unao uongelea wewe?! Mimi sijui juu ya Qur’an lakini naelewa Bible takatifu inasema “waacheni watoto wote waje kwangu maana ufalme wa Mbingu ni wao” haikusema watoto waliozaliwa na mama wa umri gani wala katika mazingira gani!! Bible imekataza UZINZI tu! Na hilo ndio swala ambalo jamii yetu bado ipo kwenye koma ya mawazo mgando halitaki kuliongelea kinaga ubaga!!

Unaongelea mila na desturi za Mtanzania halafu unachanganya na Biblia?! Unajua hapo ndipo watu wengi wanapojichanganya! Kama mnataka kuongelea mila basi msimame na mila zenu bila kuingiza vitabu vya Mungu! Halafu muache kwenda kule Ukuryani na Umasaini kuwaambia waache kukeketa watoto wakike kwani hata wao wanafuata na kutunza mila zao!! Mnaongelea mimba za watoto washule na kuwahukumu kwa kutumia neno la Mungu, vipi wababa wanao zaa nje ya ndoa hao mnawapa adhabu gani? Vipi wanaume wa Kikristu  waliofunga ndoa na wana vimada nje au wameowa wake wawili wakati Biblia hairuhusu?!

Mama Salma, dunia yote sasa hivi inaongelea jinsi ya kumnyanyua mtoto wa kike ili aweze kupambana na maisha hata kama atakuwa amepata changamoto za aina gani, sasa wewe unataka kuzidi kuwakandamiza watoto wa kike kwa sababu ipi haswa?! Je, unajuwa waathirika wakubwa  wa hii institutionalized discrimination yako ambayo unaipigia debe ni wale watoto wanaotoka kwenye familia duni?! Kwasababu ninahuwakika nyie wanenu wana uwezo wa kwenda kupata vidonge vya mpango wa uzazi wakati wowote hivyo hawa wa wenzenu ndio mnawaona wadhambi sanaaaa!!

****ITAENDELEA……****

 

Don’t miss! Its free!

Haya kwa sichana wote ambao wapo chuoni na unaojiona kuwa umebarikiwa kuwa na mawazo chanya ya jinsi ya kusaidia wasichana wengine ila haujajua ni jinsi gani uweze kuweka haya mawazo yako katika vitendo basi event si ya kukosa. Haina kiingilio ni bure kabisa tarehe 16 May, 2017 hapo COSTECH Kijitonyama kuanzia saa kumi jioni mpaka kumi na mbili.

 

Don’t miss, the Mother and Child Gala April 22, 2017!

o.k.

UN Youth Envoy

“Its time for young women to showcase by example our ability to lead and potential to deliver for all youth &that we’re not too young to lead From Tanzania I and my sister @victoria.mwanziva have declared interest to run for #UNYouthEnvoy post. Please support us. If you are a youth-led or youth organisation, you can nominate us through link in our Bio. Our win Is your win”~~~Rebecca Gyumi Wishing you all the best, najua lazima mmoja wenu atatutoa kimaso maso!

In loving memory of Ontlametse Phalatse

Ontlametse ni mtoto alikuwa ana ni-inspire sana! Nilikuwa namfatilia sana kwa Instagram, nilivutiwa sana na inspirational speech zake na jinsi wazazi wake walivyo mlea na kumjengea confidence kubwa sana ya kujikubali jinsi alivyo, kujiamini kuwa anaweza na anastahili kuishi kama wengine, na kujipenda! Nimeguswa sana na kifo chake, may her soul rest in peace! ……Ee Mungu naomba uniongezee ujasiri niweze ku-overcome all my fear and conquer them with greatness just like Ontlametse, Amen!