Category Archives: Birthday wishes

Kama ulipitwa: Mali’s 50th birthday bash!

Wapendwa kama ulipitwa na hii event basi ngoja leo ni TBS right! Angalia hii video ime summarize the whole birthday bash kwa muda mfupi lakini inapendeza sana. ❀ It!

Btw, narudia kumpongeza sana Linda Bezuidenhout Β (LB) kwa kufungua duka la kisasa kabisa kwenye mazingira mazuri ya kuvutia ndani ya Phipps Plaza hapo Georgia! Hongera sanaaaaaa 😍πŸ’ͺ

Birthday wishes

Leo ilikuwa ni siku ya kuzaliwa our Iron Lady, nikisema kuwa she is the Β pillar of our family itakuwa nimemkosea heshima sanaaaaaa! She's one of the Very few pillars tulio jaliwa nao na Mwenyezi Mungu  katika ukoo wa Chief Sarungi Igogo!
Janeth alipokuwa amekwenda kumpa mama salamu zake za shukran ya siku ya kuzaliwa kwake katika office za HoleyPharm, Upanga, Dar es salaam
 Nguzo imara ambayo tunamuomba Mungu amzidishie maisha marefu yenye afya njema sana kwani tuna muhitaji kuliko maelezo! Hii nguzo ikitetereka basi jua ukoo huu utaanguka na kugawanyika vipande vidogo vidogo ambavyo kuungwa kwake will be Another Miracle! Eeh Mwenyezi Mungu tunakuomba usikie sala na dua zetu katika jina lake Yesu! πŸ™ ........Happy birthday Nyawiti we love you!

Happy belated birthday muke ya Michuzi

Happy belated birthday muke ya uncle Michuzi! Asante sana kwa kumtunza uncle wetu anatupatia habari za huwakika. Mungu akuzidishie uhai ukaishi maisha marefu yenye afya njema. Happy birthday auntie ake! Btw, uncle Michuzi hivi unajua mkeo ni aunt yake mwanangu? πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… mtaalamu wa kujikomba nimeanza πŸ™ˆπŸ™ˆ Honestly, Ainde ni shangazi kabisa wa mtoto wangu, mama Ainde a.k a mama Ai ni bibi wa mwanangu Β muulize aunt Teddy wa Atlanta. Plus tulikuwa neighbors Β (kwa Mai) na wakina Ainde before they moved to Botswana.........haya mkikutana na mimi msinikatae kuwa hamnijui πŸ˜…πŸ˜…

Kheri ya siku ya kuzaliwa mdogo wangu!

Kheri ya siku ya kuzaliwa mdogo wangu / jirani yetu Janet  a.k.a Mrs Samora! Mungu akuzidishie neema na baraka zake. Furaha na amani vikadumu ndani ya nyumba yenu, upendo ukaimarike zaidi ndani yako na familia yako. ......Asante sana kwa kuwa jirani mwema. Tumekuwa wote, nyumba zetu upande mmoja tuna share ukuta na geti moja, ufunguo wa geti mmoja unakaa kwenu mwingine ulikuwa unakaa kwetu kwa miaka mingi sanaaaaaa! Wewe na wadogo zako mmesoma shule moja na wadogo zangu toka #Vidudu pale Chang'ombe Nursery na primary school! Lakini cha ajabu mpaka dakika hii naandika huu ujumbe, sikumbuki hata siku moja sisi kama watoto kugombana, wala wazazi wetu sijawahi ona wakigombana!! Wala kukasirikiana! Tumeishi kwa upendo wa hali ya juu kiasi kwamba najivunia kusema wewe sio tu jirani bali ni ndugu yangu! Shida yetu ilikuwa yenu na shida yenu ilikuwa shida yakwetu!......Asante sana mdogo wangu kwa upendo na amani mliyo tupatia. Mungu akuongoze uzidi kuwa baraka kwa wengine wengi! Happy birthday! I ❀ you!

Kheri ya kutimiza miaka Khamsini ya kuzaliwa kwako mama Diamond!

Miaka Khamsini mama bado unadai kabisaaaa πŸ‘ŒπŸ‘Œ Furaha ya kuzaliwa kwako. Mungu akupe maisha marefu zaidi! Nafurahi kuona siku hizi umejiweka pembeni na mambo ya makelele ya mitandaoni! Safi sana! Kaa kimya hivyo hivyo! Happy Golden birthday mama Nasib! But where is “step dad” at? 50 bado kabisa πŸ˜…πŸ˜…

Happy golden birthday Mr. Mali Kimesera

Kheri ya kutimiza miaka Khamsini ya kuzaliwa kwako! Mie bado nakumbuka ukarimu wenu na upendo mlionionyesha! Daima nitawashukuru na kuwatakia mema siku zote! Β πŸŽ‚πŸΎπŸ» Happy Golden birthday baba wa ma-private Jet 😍………. Please tembelea Instagram na Facebook za Linda Bezuidenhout / Linda Bezuidenhout personal page ujionee “ThrowBack” za nguvu!

Happy 40th birthday to me!

Asante Mungu kwa mwaka mpya! Hakika nimeona pendo lako! Jina lako libarikiwe milele! Asante sana wazazi wangu kwa kunileta katika dunia hii! Namshukuru sana mama yangu kwa kunizaa lakini pia namshukuru sana baba yangu kwa kuacha wanawake wote na kumchagua mama yangu maana kama isingekuwa hivyo nisinge kuita wewe mama! Asante sana family yangu (kaka, dada, wadogo, na wengine wote) kwa uwepo wenu kwangu ndio nguzo yangu imara nasimamia, kivuli changu wakati wa jua kali, na kimilio langu wakati wa shida!……..Asante sana mwanangu najivunia sana wewe kuwa mtoto wangu na niheshima ya pekee kutoka kwa Mungu kunipa wewe katika maisha yangu! Nakupenda sana!
Happy 40th birthday to me! #LetLoveLeads #LifeBeginsAt40 πŸŽˆπŸŽˆπŸ΄πŸŽ‚πŸ¨β€πŸ˜

Happy belated birthday Dr. Mengi!

” happy birthday to the best hubby in the whole world. You have been all I could have asked for in a husband and then some. I love you” JNM

Happy belated birthday to Dr Mengi a.k.a mume ake na Jakiline a.k.a baba twins! Mungu akujalie afya njema na amani tele! Ubarikiwe sana.! ……..wamenoga eeh! Mimi penda wao sanaaa!

Get inspired by dada Tuma!

Get inspired by dada Tuma weight loss journey! Fanya mwaka 2017 kuwa mwaka wako wa kufanya matengenezo kwa afya ya mwili wako na roho! Leo nawaonyesha picha ya dada yangu kipenzi dada Tuma ambaye alianza safari yake ya matengenezo ya afya yake mwishoni mwa mwaka jana, na sasa hivi she looks amazing! Yeye anafanya mazoezi na kuzingatia zaidi vyakula anavyo kula. Naona kuna watu wanatumia dawa ili wapungue lakini mimi naona ni bora mtu upungue kidogo kidogo hata kama ni kwa muda mrefu kuliko kutumia dawa! Lakini mwenye maamuzi ya mwisho juu ya mwili wako ni wewe mwenyewe!………..Happy birthday dada Tuma na hongera sana 😍❀❀

“Nimekuweza, Umeniweza, Tumewezana”- Zamaradi Mketema

Zamaradi, I salute you mke mwenzangu! Umenena mama kama mwanamke anaye jitambua na kujithamini! Hands-off πŸ™Œ Angalau sasa nina uhakika kuwa shemeji yangu ana kwakwe sio #Yakhaya πŸ˜€πŸ˜€………. Mungu akujaliye yale yote mema ambayo roho yako inatamani! Lovely!

Happy birthday baba Juju a.k.a Ruge Mutahaba! a.k.a Shemeji yangu!

Kheri ya siku ya kuzaliwa Mkurugenzi, baba yake Juju, Shubi, na wengine ambao sijawataja. Nakutakia furaha nyingi sana katika maisha yako, afya njema, amani, na upendo mwingi kwa familia yako, ndugu, jamaa, marafiki, na jamii inayo kuzunguka! Mungu azidi kukubariki ukawe mibaraka kwa wengi! Happy birthday mume wa Zamaradi, shemiji yake na mimi hapa πŸ™ŠπŸ™Š……….. Haki kabisa, nilitamani niandike ujumbe uhu kwa Kihaya!! Tatizo mdogo wako MuhayaMmarekani basi ni shida tupu πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ Happy birthday Ruge be blessed always!

Matukio katika picha: Jesse 11th birthday

Kheri ya siku ya kuzaliwa mwanetu Jesse! Mungu azidi kukulinda, akuongoze, na azidi kukubariku katika ukuaji wako! Ukawe mtoto mwema sanaΒ Wapendwa, naomba niseme kidogo kuhusu undugu wangu Jesse……..Bibi yake Jesse mzaa baba ni mtoto wa pili kuzaliwa kwa familia ya mama yangu (familia ya marehemu mzee Cornel Awiti); hivyo Jesse ni mpwa wangu!Β Siku ya tarehe January 16, 2017 Jesse alitimiza miaka kumi na moja tangu kuzaliwa kwake! Alisherekea na wazazi wake Dr. Joseph Obure, mama yake Venny Mwita, na mdogo wake Jason! Β Jesse na wazazi wake wana ishi huko North Carolina, U.S.AΒ Mama na birthday boy! Β Lovely! Happy 11th birthday Jesse!

Happy birthday Foster Mbuna-Mkapa!

Another year, another chapter. God you have been so Good to me and you have been with me stage by stage. So many challenges that have made me stronger, disappointments that have taught me to work harder and not to depend on people 100%, I helped a few people going through complex issues which means some people think am wise and feel that they can get words of Wisdom from me.Β All these and many more my Precious God you have given me freely and I thank you for that. Apart from good, health, wealth, parents, husband, sons, friends and family you have given me inner peace, joy and happiness. Lord I give you all the Glory and Honour for taking me thus far.Β 

So, as am celebrating the gift of life and a second chance to re edit my story, I pray that you give me more Love for others, humility, joy, inner peace, patience, a heart that forgives and forget the worst, wisdom and a heart that hungers and thirst for you only. Seeking you and dwelling in your presence everyday.Β Β As am celebrating my birthday today am celebrating me. The baby/ daughter of Joe and Evalyne Mbuna, a wife, a mother, a God mother, sister to so many, a friend to many, an aunt, a cousin a sister in law and so many things that I am to different people.Β 

I celebrate the Girl that I was, Β The Lady that Β I am Now and The Classic Lady That Am Yet to Be! Thank you to all of you who have been part of my growth and progress and Thank you for your wonderful wishes. Be blessed and Highly Favoured!Happy birthday beautiful and sweet soul, woman of God, wonderful wife, amazing mother, precious daughter, and great friend! Wishing you more joy, more inner piece, good health, and more amazing life and good friendship!…..Happy birthday Foster! Ubarikiwe sana!