Category Archives: Congratulations /Pongezi

Hongera sana aaaaa LB!……ACCOLADE 2017 Creative Designer and Fashion Icon Of The Year!


O’Lord! Nashindwa hata lakusema maneno yameniishia kwani hizi picha na video zote zinaeleza kwa kina na vizuri kuliko ambavyo ningeleeza mimi! Nafuraha kwakweli super happy for Linda na LB coutureย  brand in general! Ombi langu na faraja yangu ni lele like la siku zote LB izidi kwenda mbele, idumu milele na hii familia ibarikiwe milele zote!……. Najua bado sijawahi waungisha mkono, lakini msihofu nitawaungisha tu! Subira yavuta kheri ๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆ Mbarikiwe sana.

Ms LB: The ACCOLADE 2017 Creative Designer and Fashion Icon Of The Year

Beautiful! Lovely picture of mama na mwanae! Pendeza sana.

Better late than never!……Hongera sana Diamond!

ย Japo karibia wiki inafika tangu ushindi huu upatikane -AFRIMMA 2017 Best Male East Africa hakuna ubaya kwa mimi kutoa pongezi kwa kuchelewa kwani wenzetu wanasema “better late than never”!……..Hongera sana Diamond hakika umeitangaza๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ Tanzania katika nafasi ya kipekee sana. Ubarikiwe zaidi ya hapa! We are all proud of you the former ” Tandale” boy!ย  #Viva Diamond #Viva Wasafi ๐Ÿ™Œ๐Ÿ™

Idriss Sultan: Unaweza ukawa loyal lakini usiwe blind!

Hii interview naona ilinipita ndio nimeiona leo!

Kwanza nianze kwa kusema hongera sana Idriss Sultan kwa kupata mkataba mzuri wa kuigiza nchini Marekani. Nakutakia mafanikio mema najua utatutoa kimaso maso!.......Unajua mimi nilionaga zile picha za jeshini nikajua kuwa ni mambo yako ya comedy! Kumbe ulienda JKT ๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆ

TRUST: Interview yako nimeipenda sana. Hasa somo la kuwa "Loyal but not blind"!! Nafikiri wengi inatuchukua muda kuelewa hilo mpaka yatakapo kutokea zaidi ya mara moja ndio somo linaanza kuingia. Mimi nasema ukiona rafiki yako hapendi maendeleo ya wengine kaa naye mbali! Ukiona rafiki yako haguswi na upotevu au huaribifu wa mali zako au pesa zako hata kama ni Shilingi mojaย  achana naye kabisa! Ukiona rafiki ambaye siku zote anataka utumie njia ambayo itakughalimu zaidi achana naye! Ukiona rafiki yako ni rafiki wa karibu sana na watu wanaopinga maendeleo yako (mwenye tabia ya kuuma na kupuliza) muogope huyo rafiki! Ukiona rafiki ambaye pesa ni muhimu kwake kuliko UTU mkimbie haraka sana! Watu wanamna hiyo siku zote siyo waungwana, na wala hawana utu! BE LOYAL BUT NOT BLIND!! Somo zuri sana! BETRAYAL: Asikudanye mtu, betrayal hurts! Inauma sana kwani betrayal involves emotions which are your feelings! Hisia zako ndizo zinakufanya wewe jinsi ulivyo, hivyo mtu anapo kugeuka kwa kusudi la kukuangamiza au kusudi lolote haina tofauti na mtu anayekuchoma kisu bila ganzi! Ndio maana wenzetu wanasema "you stab me in my back"........ Naona wewe upo kama mimi ni ngumu sana kwangu kuwa na rafiki ambaye ameni betray! Don't get me wrong, nitakusamehe, tutasalimiana tukionana, hata kucheka naweza cheka nawe lakini urafiki na wewe ni MWIKO!ย  "When people show you who they are believe them" ~~~ Maya Angelou

KUTHUBUTU: Pole sana kwa changamoto ulizo pitia, na pia hongera sana kwa kuto kukata tamaa. Naamini wengi tutajifunza kutoka kwako japo wengine tu wakubwa zako. Maisha ni somo endelefu ambalo unaweza lipata toka kwa mtu yoyote bila kujali umri! You have inspired me!

WEMA: Masikini, ninesikitika sana kumbe Wema alikuwa mjamzito? Tena twins!! Dah! Pole yake sana. Mungu atampa wengine muda ukifika. Nimependa the way you talk about her you didn't trash her at all!ย 

LIFESTYLE: Jamani wanawake 30รทรท eeh! Hivi huu UKIMWI unachagua ama?! Gosh!! What about magonjwa yazinaa yasiotibika hamyaogopi?! I hope you will well behave huko Hollywood maana huko ndiko kuna jehanam ya magonjwa ya zinaa!!ย ...........Otherwise, Congratulations!ย 

 

Hongera sana Zamaradi Mketema!

ย Alhamdulillah! Alhamdulillah! Alhamdulillah! Ndoa yenu idumu milele zote! Furaha amani na baraka zote za Mwenyezi Mungu zifuatane nanyi! Ubarikiwe uzao wenu vizazi na vizazi! Alhamdulillah! Though bado nashangaa what happened from ๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰ “Umeniweza, Nimekuweza, Tumewezana” to the New “Sheriff” in town? What a difference 4 months can make!!Mkague mpenzi, kwa raha zako bibi! Hujaiba ni wako, privately owned by You! I mean you only siyo kama yule “shirika la UMMA”ย  Ugawaji, linagawa chakula kila mtaa ๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€…………… Hongera sana!

Yvonne Chaka Chaka ndani ya LB!

“What an honor to have a Music legend from South Africa ๐Ÿ‡ฟ๐Ÿ‡ฆ at our store Yvonne Chaka Chaka. She is one of the best singers in Africa also known as African Princess. She is visiting Atlanta for Mutombo Dikembe’s Foundation Gala which was held at the Ritz Carlton on Saturday. @yvonne_chakachaka” ~~~~~ Linda Bezuidenhoutย 
Hongera sanaaaaaa LB for that historical moment! Wow! I’m super happy and very proud of you! Awwih! Love it!! Mbarikiwe wote! So nice!ย  Continue reading Yvonne Chaka Chaka ndani ya LB!

The baby got blue eyes!!!

Kwanza nianze kwa kusema hongera sana Diamond na Hamisa Mabetto kwa kujaliwa mtoto wa kiume. Kwakweli Mungu kawajalia mtoto mzuri mno and he got ‘blue’ eyes?! Wow! Hongereni sana……… Diamond umefanya uwamuzi bora wa kumkubali mwanao mtoto hakustahili drama hizi zote ili wewe ukubali hadharani. But nothing worth of respect like a personal who accept and take accountability of his mistake! Own your mistake no matter how bad they are!! And for that, I salute you!!ย Mungu awatunzie mwanenu I can see another super star in the making!! Congratulations to both of you!

Hongera sana Bertha na mumeo mtarajiwa!

Napenda kuchukua nafasi hii kwa kumpa pongezi na hongera nyingi sana Bertha kwa kutolewa mahali, kuvikwa pete ya uchumba, na kufanyiwa send-off party ya nguvu sana. Mungu awalinde awaweke salama mpaka siku ya harusi yenu. Mkawe na ndoa yenye furaha, amani, na upendo mwingi, Mungu atawale maisha yenu, awe ndio kimbilio lenu, na ngao yenu wakati wote. Hongera sana.ย Wapendwa Bertha ni ndugu yake na Foster Mbuna-Mkapa. Hivyo hizi picha zote kwa hisani ya Foster. ๐Ÿ™๐Ÿ™ ย  ย ย Foster katika ubora wake! I love everything on her!ย Beautiful ladies! Na hizo shape, mashallah ๐Ÿ™

“Naombeni your support and love kama mlivyoniweka hapa nilipo leo” ~~~~ Idriss Sultan

Nimetoka katika maisha ya kupewa sh 500 kwa wiki, nimetoka katika maisha ya kupigana kujifunza kiingereza kupitia vitabu na movie na kuongea na watu mpaka naonekana labda nimetoka maisha mazuri ila nilikua shule ya serikali kama wengine, nimeambiwa siwezi mengi nimeshushwa nimetukanwa nimekatishwa tamaa nimepigwa nimefungiwa milango ila naomba niseme maumivu yote nimeyaelekeza kwenye kuonyesha upendo tu na kunyamaza kwa mda mrefu miaka miwili sasa nikishughulikia hiki nnachowaonyesha leo. Naombeni your support and love kama mlivyoniweka hapa nilipo leo. Its out of love that we get to do these amazing and great things. Kwa kasi mliyonayo naona tarehe 20 imekua 19 ๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜... Launch event will be 24th and I am super excited mvione live. Let me officially introduce you to SULTAN SHOES ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ.. SultanXforemen walk like a king ๐Ÿ‘‘.. @sultanbyforemen @sultanbyforemen @sultanbyforemen #sultanXforemen

Hongera sana mwanangu Daniel na wenzako!

Ngoja nimpongeze mwanangu kidogo, my future Pilot (nasubiria ticket za bure) ๐Ÿ˜๐Ÿ˜……… Wamefanya mashindano ya ๐Ÿ–Ž โœkuandika Insha kimkoa (mkoa wa Geita) amekuwa mshindi wa pili ๐Ÿ‘โœ‹๐Ÿ‘Œ Yeye ni mwanafunzi wa form Three (mwenye nguo nyekundu), hapo Geita Seventh Day Adventist school. Ni shule moja safi sana, inaongoza mkoa wa Mwanza na Geita kote!ย Mungu azidi wabariki, awatangulie katika masomo yenu. Msome kwa bidii. Mbarikiwe sana.ย 

New Song: Umoja ni nguvu by Leyla Bezuidenhout

ย Princess Lelya katuletea wimbo wa kutuunganisha Watanzania wote. Msikilize ย โ˜ akijielezea katika radio 106 huko Atlanta, Georgia. Wimbo mzuri sana unakwenda kwa jina la “Umoja Ni Nguvu”!……… Nimeupenda sana kwani ameona mbali na kutokukubali kuingiza vyama vya siasa katika wimbo huu kwani isingekuwa na mvuto na nguvu ya wimbo ingepotea! …….Watu wa diaspora ni vizuri kuachana na mambo ya siasa ya “uchama”! Maendeleo hayana chama, kabila, wala dini! Hivyo nivizuri watu wakaungana kwa “U-Tanzania” wetu na kupigania haki na maendeleo ya Watanzania na sio chama fulani! ………Anyway, binafsi nimeupenda, chukua muda wako kuusikiliza na tafakari! …….. Hongera sana Lelya, well done!

“May you grow to change the world and be there for others.” Millen Magese

May you bring Hope ,faith and Miracles to millions women out there who wishes to hold their children just the way I wished to hold you. May you grow to change the world and be there for others . May you believe in God and own his miracles . As much as life can be tough ,may you learn to be patient, work hard and knowing that ,everything always happens for a reason and every human being has their own path and plans from God for them. Don't ever loose hope . And no matter what happens in your life remember,you have our God Almighty and I will be here always . Father I thank you for making me A Woman and Finally A mother . Father I thank you for bringing my dad back What a gift .jina Lako Lihimidiwe ๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™ I love you my Son โค๏ธ And to you godmother @funminewyork . I believed you had a good heart you have been with me for 13 years but Gosh what you have done through out my pregnancy journey is unexplainable. God bless you sis I can't say more . ๐Ÿ˜ข๐Ÿ˜ข๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™ Prince Kairo Michael Magese was born Time :6 .58 am Weight :9 pounds 2 oz Date :July 13 th 2017 . You're my Victorious just like the meaning of your name "Kairo"#AChildWePrayedFor๐Ÿ™ Glory to God . Dansaki . Asante Mungu Many thanks to Dr Seckin @endofound , Dr Lobo,Dr Gyamfi and the whole team from Columbia Doctors . Many thanks to all my friends and family oooh you guys tried @theojinika @lebogangm @samanthajansen @jimi_mugul .Special thanks to all Endometriosis groups World wide for all you do . We will raise awareness till we find Cure ๐Ÿ’ช๐Ÿฝ.And to you all my supporters thank you , Don't stop supporting us. I believe A cure for Endometriosis is almost here . Support Us๐Ÿ‘Š๐Ÿฝ๐Ÿ™๐Ÿ™ To Everyone don't you ever forget ,If you knew who walked beside you, at all times, on the path that u have chose, you could never experience fear or doubt again,Have Faith ๐Ÿ’ช๐ŸฝStand on Your Faith ๐Ÿ’ช๐ŸฝChange Your Story ๐Ÿ’ช๐ŸฝYou Can Do It๐Ÿ’ช๐Ÿฝ Millen Magese ๐Ÿ’› #PrinceKairo๐Ÿ‘‘

“Tusiwe wepesi wa kupungukiwa na imani, tena tusichoke njiani.”~~~~ Faraja Nyalandu

Neema ya Mungu haina kipimo tena hutenda kwa wakati wake. Hakuna lililo gumu mbele za Mungu. Hakuna ajuaye kesho ila Yeye mwenye mamlaka yote. Kila aliloahidi anaenda kulifanya. Asante dada @ladivamillen, ushuhuda wako ukaseme na kila aliyekata tamaa. Tusiwe wepesi wa kupungukiwa na imani, tena tusichoke njiani. God reigns! #TearsOfJoy #BabyKairo

**ngoja nikusindikizie huu ujumbe wako na huu wimbo**
 

“Dear My little Prince Kairo Magese Michael My Miracle Son” ~~~~~~Millen Magese

It's a week since I first hold you in my arms. I'm still trying to absorb the whole thing. This will probably be the longest caption I ever written but please bare with me ๐Ÿ˜Š. Through my scars you brought me a Star โญ๏ธ Jehova you lifted me higher today . Father Lord , I'm acknowledging you for who you're and for what you've done in my life . You Must want to change your story for miracles to work. Miracles happens in such a mysterious way . I wanted my story to change so I prayed harder , I took risks ,bold steps with no fear and sympathy. I kept my faith higher than just HOPE . I believed He would hear me out. Father I thank you ,through me you showed your Power . I'm grateful . Last year around this time I lost an embryo #ZoeKhloe . June 30th 2016 . It was so painful to bare but father Lord you had a plan , you're again showing all of us that ,you're a living God and nothing is permanent. Thank you father Lord for changing my story which you let it happened on the 13th July 2017 ,the same number that have been my history but now you change it with a different story . Thank you for giving me this miracle Boy ๐Ÿ™๐Ÿ™
I have been writing this note since two months before your arrival because I was scared and nervous that I won't have words to say today as I'm holding you in my arms . Dear My little Prince Kairo Magese Michael My Miracle Son! You mean the world to me just like your names . Today the 20th of July , you're exactly a one week old baby and mama is grateful. Without God's plan ,Faith and perseverance I wouldn't be holding you today. As rough as this journey has been , it was all worth it to fight for you ,to cry for you to pray for you ,to go through Hundreds and hundreds of injections,humiliations , pain ,emotions breakdown ,loss , Scars but you chose me to be your mother and God chose me to be your mother. You're truly A child we all prayed for . Im not sure If i deserve to be your mother but all I know it was worth for me to fight to be your mother ,so I will forever be there for you . You're my Son . Am blessed to be your Mother๐Ÿ™..........Part1
alphaigogo.com is dedicating this song to Millen Magese, the new born king, ย and all women suffering the pain of living with ENDOMETRIOSIS around the world! ย Our God is awosome, He is able!ย Ametenda maajabu ๐Ÿ’ช๐Ÿ™

Soma post ya nyuma ๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰ (MillenMagese)

Hongera sana Mr and Mrs Davis Kateti!

Mr and Mrs Kateti
Hongera sana mdogo wangu Davis Kateti na wifi yangu Ester Kateti kwa kula kiapo KITAKATIFU. Mungu awaongoze katika kila jambo jema mlitendalo! Akapate kuwa ngao na kimbilio lenu wakati wote siku zote katika nyakati zote za raha na tabu! Akabariki uzao wenu hata kizazi cha tatu na cha Nne! Nyumba yenu ikawe hekalu ndogo; amani, upendo, furaha vikadumu ndani yenu! Hongereni sana wapendwa!

Continue reading Hongera sana Mr and Mrs Davis Kateti!

Kheri ya kutimiza miaka 8 ya ndoa yenu!

 Kheri ya kutimiza miaka nane ya ndoa yenu Mr and Mrs Rweikiza! Nawatakieni furaha na amani tele katika maisha yenu na upendo mwingi ndani ya familia yenu na watu wote wanao wazunguka. Happy belated Wedding Anniversary ย (06/20)!.. .... Mbarikiwe sana.

Btw, naomba leo kwa mara nyingine nimshukuru sana mtani wangu ย (Mr. Rweikiza) for a kind act that he did to me way back then in Wichita! Sema this time nitasema hapa kwa blog!ย Napenda kukushukuru sana kwa ukarimu wako uliyonifanyia wakunipeleka kufanya Road Driving Test ili nipate Leseni ya kuendesha gari hapa Marekani! Ubarikiwe sanaaaaaa na familia yako!  Haya ngoja niwape story ilivyokuwa; mara ya kwanza nilipelekwa na my brother Mwiga Kapya (where is he?) lakini sikupita mtihani, yule mtu aliyenifanyia road test alisema sikufanya "completely stop" ย kwenye stop sign ๐Ÿ™Š๐Ÿ™Š hivyo hakunipa! Sasa ikabidi nipange siku nyingine, nafikiri ilikuwa baada ya wiki hivi! My brother Mwiga akawa amebanwa na ratiba hivyo akamuomba Mr. Rweikiza anipeleke!Kuja kumbe alikuwa ni mtani wangu! Wahaya oyeeeeeeeee! Lol! Sijui ni kwanini lakini nimejikuta most of my sincere, kind friends ni Wahaya! I think I will never get away from them ย ๐Ÿ˜…๐Ÿ˜… Mtani wangu, asante sana. And Happy 8th Anniversary!

Hongera sana Ravvyn! You have done us proud!!

Tanzania oye eeeeeee! Finally RayVnny ametutoa kimaso maso kwenye dunia ya #wazungu! Nasisi kwa mara ya kwanza, tumetambulika rasmi na kuwekwa kwenye Entertainment industry ya Wamarekani! #BETAwards…… Asante sana kijana wetu, asante sana Watanzania kwa ushirikiano wetu tulio uonyesha na kuleta ushindi huu nyumbani! Viva Tanzania! Viva WCB!

RayVnny, I’m so impressed kuona RayVnny anaongea good English! Safi sana! Yani mimi ni #Zezeta wa nyimbo zako ๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜˜

The journey to motherhood: Congratulations Nambua Cassandra!

Alpha Igogo -bloggerWapendwa wasomaji wangu, naomba niwaletee tukio zuri sana la safari ya kuzaliwa mtoto Prince. Ni tukio ambalo limekuwa recorded na shemu ya hiyo video imeonyeshwa na mama mzazi kwa kupitia account yake ya Instagram! ……….. Kwanza nianze kwa kusema hongera sana kwa Nambua kwa kujaliwa mtoto wa kiume! Mungu amlinde akuwe katika kimo na hekima. Akampendeze Mungu kwanza na kisha wanadamu! Karibu katika chama cha wakinamama/ wazazi! Safari hii ni ndefu, yenye changamoto nyingi lakini ni tamu mno! Nasema nitamu mno kwani kama kuna kitu nime furahia kwa 100% ย na bado naendelea kufurahia with all the pride is being a mother! Lakini kila siku namrudishia sifa na utukufu kwakwe Mungu maana bila yeye hakuna litakalo wezekana! ……..kwakweli nimependa sana hii familia ya Mr and Mrs Mlaki! Nimependa sana their spirit, wako so open and together, inapendeza sana mfano mzuri sana wa kuigwa katika jamii! Hii dunia imeshabadilika (21st century) kuna mambo mengi ya karne 19 inabidi kuyaacha maana siyo tu jamii haiipi nafasi bali pia hata technology haivitaki! Kwa mfano katika karne hii 21 n* kitu cha kawaida kabisa katika jamii zilizo ona mbele mama na kijana wake kuwa ndani ya chumba cha upasuaji wakimuangalia binti/ dada akileta kiumbe kingine duniani! Wakati jambo kama hilo bado linaweza likawa tatizo katika sehemu nyingi za Africa! ……….. Maelezo yote ambayo yameambatana na picha yameandikwa na Nambua ambaye ni mama mzazi wa Prince! ย #NaniKamaMama.ย Yesterday 4th June, 2017 was one of my big day osn earth. Nimepata experience ya ajabu sana katika maisha yangu. Mwenyenzi Mungu Muumba Mbingu na Nchi amenijalia kujifungua mtoto wa kiume 9.25am South African time. HIYO NI FIRST FOTO ALIPOTOKA TUMBONI KWANGU, ALIPOTOLEWA KAANZA KULIA. Ilikuwa sala yangu kujifungua mtoto wa kwanza DUME. I’M OFFICIALLY A MOTHER. Jana usiku sijalala kabisa nimekaa natoa macho, namshangaa huyu mtoto. Bado siamini kama ni mtoto wangu, namuona stranger, mgeni flani hivi. Na sikujua watoto wanatoka mbali hivi. Heshima kwa wamama wote waliozaa.ย ๐Ÿ˜˜๐Ÿ˜™. Napenda kuwashukuru wote waliokuwa na mimi katika hii safari yangu. Nikisema nitaje majina mengi sitamaliza. Surely it was a long trip. My brother @laumlaki huyu ni commando aliingia theatre aka record tukio zima la Cesarean operation na mama yangu @lwisemanka amempokea mjukuu wake. Lord Jesus I give you glory. In Christ I have made it to God be the Glory. Yeremia 29:11 HAKIKA MAWAZO YA BWANA NI MEMA JUU YANGU, Yeremia 33:3…… BWANA AMENIONYESHA MAMBO MAKUBWA MAGUMU NISIOYAJUA.

Hapo niko theatre (operation room) najindaa nimlete mwanangu duniani. Nacheka cheka tu naona wanachelewa……๐Ÿ˜€. Niko na mama na mdogo wangu @laumlaki paparazzi. Hili tukio kwangu ni very historical considering mahala nilipotoka. Nilisema Im going to record kila kitu wakati najifungua niweke ktk dvd. Namshangaa Bwana Yesu na matendo yake makuu juu yangu. Nawashukuru sana MEDICLINIC, SANDTON. Doctors & Nurses are very friendly na makini ktk kazi. Biblia inasema katika torati: Mateso ya mwenye haki ni mengi, lakini BWANA humponya nayo yote.๐Ÿค”๐Ÿค”๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜ƒ Amen.ย 

My mother @lwisemanka, my mdogo @laumlaki and my photographer ms melody, hawa nilikuwa nao theatre. Walitaka waone ceserean section inavyokuwa, yani kila kitu na wawe wa kwanza to see my baby. Nimewaita mashilawadu wangu.๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€…….. love you all. Kweli watoto wanatoka mbali sana. Halafu hili zoezi nimelipenda sana la kuingia theatre na familya yako au photographer wako.

Hapo nimetoka kutoa mtoto tumboni naumwa sana, nimezinduka. Koo limekauka kwani niliwekewa oxygen. Yani kuitwa mama aisee ni kazi! Nafundishwa kunyonyesha naona ni adhabu halafu siamini kama nitaitwa mama. Shikamoo mwanamke. Naomba wanaume wawaheshimu wale wanawake waliozaa wakawafanya wakaitwa wababa. Hii experience ni ya ajabu. Wamama shikamooni. Kuanzia leo simgombezi tena mama yangu……. Biblia inasema ZABURI 34:19-21 MATESO YA MWENYE HAKI NI MENGI LAKINI BWANA HUPONYA NAYO YOTE.HUIHIFADHI MIFUPA YAKEย MY FIRST BORN,UZAO WANGU WA KWANZA…… BWANA MUNGU AKASEMA HAKIKA NITAKUBARIKI NAE AKANIBARIKI NA HUYU KIUMBE KATIKA JINA LA YESU …………… PRINCE THAT HIS NAME.NI PRINCE MTOTO WA MFALME WA WAFALME, JEHOVAH RAPHA. TODAY HE IS ONLY 15DAYS OLD NA AMEANZA TO POZI TAJIRI MTOTO. I LOVE YOU MY SON. I LOVE YOU. HUYU KIUMBE NIMEMJUA SIKU 15 ZILIZOPITA ILA NAMPENDA KULIKO VIUMBE VYOTE DUNIANI…….๐Ÿ˜˜๐Ÿ˜˜๐Ÿ˜˜๐Ÿ˜˜ย MY LIFE HAS CHANGED 100%. #nambuacassandra @baby.mix.baby.ย 

Me and My baby PRINCE that his name (tajiri mtoto)…… hapo yuko 12days old๐Ÿ˜€๐Ÿ˜๐Ÿ˜‡๐Ÿ˜˜. Na nilipokuwa natafakari๐Ÿค”๐Ÿค” siku zangu duniani, Nae Mungu akasema na mimi akaninong’oneza MWANANGU NEEMA YANGU YATOSHA JUU YAKO. MGHH SIKUAMINI……. ILA LEO NIMEIONA NEEMA YAKE KWA KUNIZAWADIA MTOTO WA KIUME SAWASAWA NA HAJA YA MOYO WANGU. (Heart desires) ๐Ÿ˜‡๐Ÿ˜‡๐Ÿ˜‡ Neno la Mungu linasema (Torati) Zaburi 37:4-6 Nawe utajifurahisha kwa BWANA. Naye atakupa haja za moyo wako. Umkabidhi BWANA njia yako, Pia umtumaini, naye atafanya. Ataitokeza haki yako kama nuru. Na hukumu yako kama adhuhuri……. #nambuacassandra #huumchezohauhitajihasira

***HONGERA SANA NAMBUA CASSANDRA***