Category Archives: Congratulations /Pongezi

Hongera viongozi wapya wa THC!

Wiki iliyopita Watanzania waishio katika jiji la Houston, Texas walichagua viongozi wapya wa jumuiya yao ambao wataanza kuongoza kuanzia mwezi wa kwanza mwakani kwa kipindi cha miaka miwili. Nikiwa kama mmoja wa Watanzania ambao tunaishi ndani ya jumuiya hii naomba niwape pongezi viongozi wote waliochaguliwa kutuongoza kwa kipindi kijacho. Japo sijakaa sana hapa Houston lakini naweza shuudia kuwa nimeona mambo mazuri toka kwa wanajumuiya ambayo naamini ni matunda ya uwongozi bora. Hivyo Kama ilivyo kwa wengine nami nategemea kuona mambo mazuri zaidi katika jumuiya yetu! Hongereni Sana! Vile vile pongezi kwa viongozi mliomaliza muda wenu kwa kutuongoza vyema.  Pichani katikati ndio Rais / Mwenyekiti mpya Mr Lambert Tibaigana. Kulia ni dada Anasa Kambi yeye ni Katibu wa jumuiya. Na Kushoto ni dada Aneti Asenga yeye ni Muweka Hazina........... Kwa  picha na maelezo zaidi bonyeza ?? THC

Is baby number 2 on the way?!….if so; hongera sana Madam Rita!

Haya kuna huu ubuyu nawaletea wapenda ubuyu wenzangu ??? Niliona hii picha wiki imepita sasa, kimoyo moyo nikasema “she looks like pregnant” lakini nikadharau! Sasa juzi kinaenda kuchungulia tena Instagram page yake nikaona no update! Nikasema mbona siku hizi anapotea sana kwa social media!! basi nikaamua kusoma comments chini ya hiyo picha si ndio naona watu wengi wakimpongeza na kumsifia kuwa mimba imempendeza! 

Honestly, nimefurahi utafikiri mie ndio Madam Rita ?? huyo atakuwa mtoto wake wa pili baada ya miaka zaidi ya 20 kama ni kweli mjamzito! Isijekuwa mtu amevimbiwa maharagwe ya Mbeya sisi tunampa pongezi ?? …………anyway, Madame, please rusha basi picha nyingine tukuone mpenzi ?? Hongera sana, Mungu awe nawe ?

Harusi hii watu walipendeza lakini…..!

Mr and Mrs Jons

Hii harusi ya Romy Jons mdogo wake na Diamond walipendeza sana kwenye mavazi!  

Japo kwenye nywele za bibi harusi na Zari sijaapenda sana. Hazikutengenezwa vizuri kivile!   Halafu mimi sipendi hizi suruali za kubana kwa wanaume ?? lakini sindio mambo ya fashion zao hao wa kwenye entertainment industry! Otherwise, ingeneral walipendeza.

Kitu ambacho sikukipenda ni jinsi Diamond na Zari alivyopata attention zaidi kuliko maharusi!  

It seems to me Diamond and Zari over-did themselves ambapo naona watu wakawa hawana jinsi ila kuwatizama na kuwashangilia!  

Naelewa kwanini bwana harusi alimtaka kaka yake awe msimamizi wa harusi lakini kumbuka harusi ni siku yako moja tu ambayo unatakiwa kupata all the attention na siyo mtu  mwingine! Hivyo kuwa na “mastar” wawili ndio wasimamizi wake I think was a bit too much! Especially mastar wenyewe ndio wale ambao wako “hyper” 24/7 lazima wata overshadow your day! Harusi huwa haijurudii ni kitu cha mara moja  labda uwe na “nyota” kama ya Irene Uwoya ndio utafanya harusi mbii hivyo usifanye makosa ambayo utajutia baadaye! Otherwise Hongera zao!  

Esma (wifi mtu) alipendeza zaidi kuanzia kichwa mpaka nguo! 

Nasikia mama Diamond katangaza kuwa anamimba? ??? Naona hii familia imeamua kuwa kama the Kadashians wa hapa Marekani ?? Who am I to judge?! Just wishing her well, twamsubiria huyo mziwanda!

Shout-out to my cousin Sophia Makoyo! New lawyer in town!

When I say beauty and brain, trust me I know it, seen it cause it runs in our family bloodstream ?? wenye wivu pandeni juu mkazibe ??……Hey lemme shout-out to my sweet, charming, smart cousin Sophia Makoyo for attaining her bachelor in law from University of Dodoma a.k.a UDOM! Hongera sana binamu yangu najua huu ni mwanzo tu, mazuri mengi yanakuja! Have faith and keep it up! Sky is just another platform! Hongera sana ???❤

Hongera sana Rose M. Awiti na mumeo!

Hongera sana binamu yangu Rose M. Awiti kwa kufunga ndoa takatifu. Mwenyezi Mungu akujalie furaha, amani, afya njema, na akawe kiongozi wenu siku zote ili ndoa yenu idumu milele. Hongera sana. Kwafaida ya wasomaji wangu, Rose ni mtoto wa mjomba wangu. Baba yake ni mdogo wake mama yangu mzazi ambaye anamfuata mara ya 5 kuzaliwa. Wiki iliyopita siku ya Ijumaa alifunga ndoa na mpemba wake ??? na mimi sasa nina shemeji mpemba ?? safari hii nikienda Bongoland itabidi nifike Pemba ?? Mwenye shati la drafti ndio baba mzazi wa bibi harusi. Bibi harusi na shangazi yake mlezi-mama Igogo ambaye ni kama mama mlezi kwani yeye ndiye aliyesimama kama mama tangu mama yake mzazi bibi harusi afariki.

Bibi harusi na shangazi zake upande wa baba  Kwa mara nyingine, hongera sana binamu yangu. Mbarikiwe wote.

King Kiba: Thank you Africa

"Thank you Africa! You made it possible to win two awards @afrimawards. Fans across the world Asanteni sana!
Photo credit @joho_001 #KingKiba" Nami naomba nichukue muda huu kumpongeza Mfalme wetu Ali Kiba kwa kututoa kimaso maso! Honestly, Mimi hivi vitu huwa sifatilii kabisa unless nineona kwa mtu ndio maana nimechelewa kupost. Thanks to LeMutuz!...... Hongera sana King Kiba ?

Hongera sana aaaaa LB!……ACCOLADE 2017 Creative Designer and Fashion Icon Of The Year!


O’Lord! Nashindwa hata lakusema maneno yameniishia kwani hizi picha na video zote zinaeleza kwa kina na vizuri kuliko ambavyo ningeleeza mimi! Nafuraha kwakweli super happy for Linda na LB couture  brand in general! Ombi langu na faraja yangu ni lele like la siku zote LB izidi kwenda mbele, idumu milele na hii familia ibarikiwe milele zote!……. Najua bado sijawahi waungisha mkono, lakini msihofu nitawaungisha tu! Subira yavuta kheri ?? Mbarikiwe sana.

Ms LB: The ACCOLADE 2017 Creative Designer and Fashion Icon Of The Year

Beautiful! Lovely picture of mama na mwanae! Pendeza sana.

Better late than never!……Hongera sana Diamond!

 Japo karibia wiki inafika tangu ushindi huu upatikane -AFRIMMA 2017 Best Male East Africa hakuna ubaya kwa mimi kutoa pongezi kwa kuchelewa kwani wenzetu wanasema “better late than never”!……..Hongera sana Diamond hakika umeitangaza?? Tanzania katika nafasi ya kipekee sana. Ubarikiwe zaidi ya hapa! We are all proud of you the former ” Tandale” boy!  #Viva Diamond #Viva Wasafi ??

Idriss Sultan: Unaweza ukawa loyal lakini usiwe blind!

Hii interview naona ilinipita ndio nimeiona leo!

Kwanza nianze kwa kusema hongera sana Idriss Sultan kwa kupata mkataba mzuri wa kuigiza nchini Marekani. Nakutakia mafanikio mema najua utatutoa kimaso maso!.......Unajua mimi nilionaga zile picha za jeshini nikajua kuwa ni mambo yako ya comedy! Kumbe ulienda JKT ??

TRUST: Interview yako nimeipenda sana. Hasa somo la kuwa "Loyal but not blind"!! Nafikiri wengi inatuchukua muda kuelewa hilo mpaka yatakapo kutokea zaidi ya mara moja ndio somo linaanza kuingia. Mimi nasema ukiona rafiki yako hapendi maendeleo ya wengine kaa naye mbali! Ukiona rafiki yako haguswi na upotevu au huaribifu wa mali zako au pesa zako hata kama ni Shilingi moja  achana naye kabisa! Ukiona rafiki ambaye siku zote anataka utumie njia ambayo itakughalimu zaidi achana naye! Ukiona rafiki yako ni rafiki wa karibu sana na watu wanaopinga maendeleo yako (mwenye tabia ya kuuma na kupuliza) muogope huyo rafiki! Ukiona rafiki ambaye pesa ni muhimu kwake kuliko UTU mkimbie haraka sana! Watu wanamna hiyo siku zote siyo waungwana, na wala hawana utu! BE LOYAL BUT NOT BLIND!! Somo zuri sana! BETRAYAL: Asikudanye mtu, betrayal hurts! Inauma sana kwani betrayal involves emotions which are your feelings! Hisia zako ndizo zinakufanya wewe jinsi ulivyo, hivyo mtu anapo kugeuka kwa kusudi la kukuangamiza au kusudi lolote haina tofauti na mtu anayekuchoma kisu bila ganzi! Ndio maana wenzetu wanasema "you stab me in my back"........ Naona wewe upo kama mimi ni ngumu sana kwangu kuwa na rafiki ambaye ameni betray! Don't get me wrong, nitakusamehe, tutasalimiana tukionana, hata kucheka naweza cheka nawe lakini urafiki na wewe ni MWIKO!  "When people show you who they are believe them" ~~~ Maya Angelou

KUTHUBUTU: Pole sana kwa changamoto ulizo pitia, na pia hongera sana kwa kuto kukata tamaa. Naamini wengi tutajifunza kutoka kwako japo wengine tu wakubwa zako. Maisha ni somo endelefu ambalo unaweza lipata toka kwa mtu yoyote bila kujali umri! You have inspired me!

WEMA: Masikini, ninesikitika sana kumbe Wema alikuwa mjamzito? Tena twins!! Dah! Pole yake sana. Mungu atampa wengine muda ukifika. Nimependa the way you talk about her you didn't trash her at all! 

LIFESTYLE: Jamani wanawake 30÷÷ eeh! Hivi huu UKIMWI unachagua ama?! Gosh!! What about magonjwa yazinaa yasiotibika hamyaogopi?! I hope you will well behave huko Hollywood maana huko ndiko kuna jehanam ya magonjwa ya zinaa!! ...........Otherwise, Congratulations! 

 

Hongera sana Zamaradi Mketema!

 Alhamdulillah! Alhamdulillah! Alhamdulillah! Ndoa yenu idumu milele zote! Furaha amani na baraka zote za Mwenyezi Mungu zifuatane nanyi! Ubarikiwe uzao wenu vizazi na vizazi! Alhamdulillah! Though bado nashangaa what happened from ?? “Umeniweza, Nimekuweza, Tumewezana” to the New “Sheriff” in town? What a difference 4 months can make!!Mkague mpenzi, kwa raha zako bibi! Hujaiba ni wako, privately owned by You! I mean you only siyo kama yule “shirika la UMMA”  Ugawaji, linagawa chakula kila mtaa ???…………… Hongera sana!

Yvonne Chaka Chaka ndani ya LB!

“What an honor to have a Music legend from South Africa ?? at our store Yvonne Chaka Chaka. She is one of the best singers in Africa also known as African Princess. She is visiting Atlanta for Mutombo Dikembe’s Foundation Gala which was held at the Ritz Carlton on Saturday. @yvonne_chakachaka” ~~~~~ Linda Bezuidenhout 
Hongera sanaaaaaa LB for that historical moment! Wow! I’m super happy and very proud of you! Awwih! Love it!! Mbarikiwe wote! So nice!  Continue reading Yvonne Chaka Chaka ndani ya LB!

The baby got blue eyes!!!

Kwanza nianze kwa kusema hongera sana Diamond na Hamisa Mabetto kwa kujaliwa mtoto wa kiume. Kwakweli Mungu kawajalia mtoto mzuri mno and he got ‘blue’ eyes?! Wow! Hongereni sana……… Diamond umefanya uwamuzi bora wa kumkubali mwanao mtoto hakustahili drama hizi zote ili wewe ukubali hadharani. But nothing worth of respect like a personal who accept and take accountability of his mistake! Own your mistake no matter how bad they are!! And for that, I salute you!! Mungu awatunzie mwanenu I can see another super star in the making!! Congratulations to both of you!

Hongera sana Bertha na mumeo mtarajiwa!

Napenda kuchukua nafasi hii kwa kumpa pongezi na hongera nyingi sana Bertha kwa kutolewa mahali, kuvikwa pete ya uchumba, na kufanyiwa send-off party ya nguvu sana. Mungu awalinde awaweke salama mpaka siku ya harusi yenu. Mkawe na ndoa yenye furaha, amani, na upendo mwingi, Mungu atawale maisha yenu, awe ndio kimbilio lenu, na ngao yenu wakati wote. Hongera sana. Wapendwa Bertha ni ndugu yake na Foster Mbuna-Mkapa. Hivyo hizi picha zote kwa hisani ya Foster. ??     Foster katika ubora wake! I love everything on her! Beautiful ladies! Na hizo shape, mashallah ?

“Naombeni your support and love kama mlivyoniweka hapa nilipo leo” ~~~~ Idriss Sultan

Nimetoka katika maisha ya kupewa sh 500 kwa wiki, nimetoka katika maisha ya kupigana kujifunza kiingereza kupitia vitabu na movie na kuongea na watu mpaka naonekana labda nimetoka maisha mazuri ila nilikua shule ya serikali kama wengine, nimeambiwa siwezi mengi nimeshushwa nimetukanwa nimekatishwa tamaa nimepigwa nimefungiwa milango ila naomba niseme maumivu yote nimeyaelekeza kwenye kuonyesha upendo tu na kunyamaza kwa mda mrefu miaka miwili sasa nikishughulikia hiki nnachowaonyesha leo. Naombeni your support and love kama mlivyoniweka hapa nilipo leo. Its out of love that we get to do these amazing and great things. Kwa kasi mliyonayo naona tarehe 20 imekua 19 ???... Launch event will be 24th and I am super excited mvione live. Let me officially introduce you to SULTAN SHOES ???.. SultanXforemen walk like a king ?.. @sultanbyforemen @sultanbyforemen @sultanbyforemen #sultanXforemen

Hongera sana mwanangu Daniel na wenzako!

Ngoja nimpongeze mwanangu kidogo, my future Pilot (nasubiria ticket za bure) ??……… Wamefanya mashindano ya ? ✍kuandika Insha kimkoa (mkoa wa Geita) amekuwa mshindi wa pili ?✋? Yeye ni mwanafunzi wa form Three (mwenye nguo nyekundu), hapo Geita Seventh Day Adventist school. Ni shule moja safi sana, inaongoza mkoa wa Mwanza na Geita kote! Mungu azidi wabariki, awatangulie katika masomo yenu. Msome kwa bidii. Mbarikiwe sana. 

New Song: Umoja ni nguvu by Leyla Bezuidenhout

 Princess Lelya katuletea wimbo wa kutuunganisha Watanzania wote. Msikilize  ☝ akijielezea katika radio 106 huko Atlanta, Georgia. Wimbo mzuri sana unakwenda kwa jina la “Umoja Ni Nguvu”!……… Nimeupenda sana kwani ameona mbali na kutokukubali kuingiza vyama vya siasa katika wimbo huu kwani isingekuwa na mvuto na nguvu ya wimbo ingepotea! …….Watu wa diaspora ni vizuri kuachana na mambo ya siasa ya “uchama”! Maendeleo hayana chama, kabila, wala dini! Hivyo nivizuri watu wakaungana kwa “U-Tanzania” wetu na kupigania haki na maendeleo ya Watanzania na sio chama fulani! ………Anyway, binafsi nimeupenda, chukua muda wako kuusikiliza na tafakari! …….. Hongera sana Lelya, well done!

“May you grow to change the world and be there for others.” Millen Magese

May you bring Hope ,faith and Miracles to millions women out there who wishes to hold their children just the way I wished to hold you. May you grow to change the world and be there for others . May you believe in God and own his miracles . As much as life can be tough ,may you learn to be patient, work hard and knowing that ,everything always happens for a reason and every human being has their own path and plans from God for them. Don't ever loose hope . And no matter what happens in your life remember,you have our God Almighty and I will be here always . Father I thank you for making me A Woman and Finally A mother . Father I thank you for bringing my dad back What a gift .jina Lako Lihimidiwe ??? I love you my Son ❤️ And to you godmother @funminewyork . I believed you had a good heart you have been with me for 13 years but Gosh what you have done through out my pregnancy journey is unexplainable. God bless you sis I can't say more . ????? Prince Kairo Michael Magese was born Time :6 .58 am Weight :9 pounds 2 oz Date :July 13 th 2017 . You're my Victorious just like the meaning of your name "Kairo"#AChildWePrayedFor? Glory to God . Dansaki . Asante Mungu Many thanks to Dr Seckin @endofound , Dr Lobo,Dr Gyamfi and the whole team from Columbia Doctors . Many thanks to all my friends and family oooh you guys tried @theojinika @lebogangm @samanthajansen @jimi_mugul .Special thanks to all Endometriosis groups World wide for all you do . We will raise awareness till we find Cure ??.And to you all my supporters thank you , Don't stop supporting us. I believe A cure for Endometriosis is almost here . Support Us???? To Everyone don't you ever forget ,If you knew who walked beside you, at all times, on the path that u have chose, you could never experience fear or doubt again,Have Faith ??Stand on Your Faith ??Change Your Story ??You Can Do It?? Millen Magese ? #PrinceKairo?

“Tusiwe wepesi wa kupungukiwa na imani, tena tusichoke njiani.”~~~~ Faraja Nyalandu

Neema ya Mungu haina kipimo tena hutenda kwa wakati wake. Hakuna lililo gumu mbele za Mungu. Hakuna ajuaye kesho ila Yeye mwenye mamlaka yote. Kila aliloahidi anaenda kulifanya. Asante dada @ladivamillen, ushuhuda wako ukaseme na kila aliyekata tamaa. Tusiwe wepesi wa kupungukiwa na imani, tena tusichoke njiani. God reigns! #TearsOfJoy #BabyKairo

**ngoja nikusindikizie huu ujumbe wako na huu wimbo**
 

“Dear My little Prince Kairo Magese Michael My Miracle Son” ~~~~~~Millen Magese

It's a week since I first hold you in my arms. I'm still trying to absorb the whole thing. This will probably be the longest caption I ever written but please bare with me ?. Through my scars you brought me a Star ⭐️ Jehova you lifted me higher today . Father Lord , I'm acknowledging you for who you're and for what you've done in my life . You Must want to change your story for miracles to work. Miracles happens in such a mysterious way . I wanted my story to change so I prayed harder , I took risks ,bold steps with no fear and sympathy. I kept my faith higher than just HOPE . I believed He would hear me out. Father I thank you ,through me you showed your Power . I'm grateful . Last year around this time I lost an embryo #ZoeKhloe . June 30th 2016 . It was so painful to bare but father Lord you had a plan , you're again showing all of us that ,you're a living God and nothing is permanent. Thank you father Lord for changing my story which you let it happened on the 13th July 2017 ,the same number that have been my history but now you change it with a different story . Thank you for giving me this miracle Boy ??
I have been writing this note since two months before your arrival because I was scared and nervous that I won't have words to say today as I'm holding you in my arms . Dear My little Prince Kairo Magese Michael My Miracle Son! You mean the world to me just like your names . Today the 20th of July , you're exactly a one week old baby and mama is grateful. Without God's plan ,Faith and perseverance I wouldn't be holding you today. As rough as this journey has been , it was all worth it to fight for you ,to cry for you to pray for you ,to go through Hundreds and hundreds of injections,humiliations , pain ,emotions breakdown ,loss , Scars but you chose me to be your mother and God chose me to be your mother. You're truly A child we all prayed for . Im not sure If i deserve to be your mother but all I know it was worth for me to fight to be your mother ,so I will forever be there for you . You're my Son . Am blessed to be your Mother?..........Part1
alphaigogo.com is dedicating this song to Millen Magese, the new born king,  and all women suffering the pain of living with ENDOMETRIOSIS around the world!  Our God is awosome, He is able! Ametenda maajabu ??

Soma post ya nyuma ?? (MillenMagese)

Hongera sana Mr and Mrs Davis Kateti!

Mr and Mrs Kateti
Hongera sana mdogo wangu Davis Kateti na wifi yangu Ester Kateti kwa kula kiapo KITAKATIFU. Mungu awaongoze katika kila jambo jema mlitendalo! Akapate kuwa ngao na kimbilio lenu wakati wote siku zote katika nyakati zote za raha na tabu! Akabariki uzao wenu hata kizazi cha tatu na cha Nne! Nyumba yenu ikawe hekalu ndogo; amani, upendo, furaha vikadumu ndani yenu! Hongereni sana wapendwa!

Continue reading Hongera sana Mr and Mrs Davis Kateti!