Category Archives: Elimu juu ya maisha

Maisha…….!

 "Wapendeni watu wote kama mnavyojipenda nafsi zenu. Mzee Igogo asubuhi hii kakutana na rafiki yake waliyopoteana kwa siku nyingi, Bw. Mwaipuge, ni mlemavu wa fikra, anaishi popote porini ama kwenye majumba chakavu. Aliwahi kuwa mtumishi wa serikali idara ya Magereza. Watoto wangu nawasihi, muwe wapenzi na furaha kwa hao wasiyothaminika machoni kwa watu wengi, kwa kuwa kwake yeye Muumba wetu, tuko sawa.">>>> Life experience from Sir O.O Igogo     Hujafa hujaumbika! Hii dunia ya Musa  tembea pole pole eeh! Usimdharau mtu yeyote mwenye pumzi ya uhai maana hujui ya kesho ya Mungu mengi!

Una Akiba ya kuishi wiki moja bila kufanya kazi??

Regrann from @joycekiriasuperwoman – Leo tuna Nguvu za kufanya kazi, na tunaishi kwa kutokana na kipato tunachopata baada ya kutumia Nguvu zetu… Ebu fikiria ukiumwa wiki bila kupiga kazi utaishije?? Una Akiba ya kuishi wiki moja bila kufanya kazi??? (Kitaalamu unatakiwa uwe na Akiba za kukuwezesha kuishi miezi Sita bila kufanya kazi endapo utapata tatizo lolote) Mimi nakuuliza wiki moja tuu 😂😂😂😂  Okay… Tujiulize Kesho tutakapokuwa tumepoteza Nguvu za kufanya kazi tutaishi kwa kipato gani???

Kama watu tunaobinuka kutafuta mafanikio tukae tutafakari juu ya hatma zetu, tujiulize kwa Sasa tunaingiza kiasi gani, na Miaka 20 baadae tutakuwa tunaingiza kiasi gani….

Wanawake wengi hapa sisi ni wahanga… Kuishi bila budget na mikakati tunaongoza 🙌🙌🙌 tunaishi bila kuwa na mkakati wa kifedha madhubuti, Tunaishi kwa matumaini ya kufanikiwa kupitia waume zetu 🙈🙈 na Matokeo Yake tunakumbwa na Changamoto kubwa sana ya umaskini …. .

Semina by @joel_nanauka

Nywele by @rosebrazilian .

Kwa udhamini wa @hc_sanitary_pads – #regrann

Maisha……!

Kuna dada alikaa miaka kumi na zaidi akimsubiria mwanaume ambaye alimuahidi kua atamuoa. Dada wa watu akajitunza na kumcha Mungu kwa bidii akimsubiria mchumba wake. Wanaume wengi walimtaka wengine kwa nia njema kabisa ya kutaka kufunga naye pingu za maisha  lakini aliwakataa wote.

Baada ya miaka kama kumi na mbili hivi yule mchumba akarudi Tanzania, akafuata taratibu zote za kimila na kidini na kufunga naye ndoa. Miaka mitatu ndani ya ndoa mwanamke akaanza kuugua alipokwenda kupima damu akifikiria ni marelia sugu akaambiwa ameathirika na HIV! Dada yule hakuamini, akaenda   hospitali kadhaa kupima na vipimo vyote vilisema hivyo!!  Ikabidi amuulize mumewe kulikoni? Baada ya mazungumzo mazito mume akakubali kuwa hakuwa muaminifu na nikweli yeye ndio ameleta ugonjwa huo na amekuwa akitumia dawa takribani mwaka mmoja!!

Dada yule alipatwa na mshtuko mkubwa sana. Hivyo baada ya mwaka mmoja akafariki akaacha mtoto wake wakiume bila mama. Yule baba yeye bado yupo anakula maisha Bongoland kwasababu anatumia dawa!!

Nachosema ni hivi there's a lot of fish in the ocean why going for Jellyfish?? Unamsubiria mtu zaidi ya miaka kumi only to end up with HIV+?? No! kama hawezi kubadili mipango yake kwa ajili yako sasa kwanini wewe unasimamisha na kubadilisha mipango yake kwaajili yake?!! Kuna vitu vya kusubiria lakini siyo mwanaume ambaye hajakuoa! Live your life now!

*** Hii story imetokana na kisa cha kweli kabisa siyo yakutunga. Picha yangu haina huusiano wowote na story***

Baba Keagan: Lakini yote ni MUNGU anawapima imani ili aweze kuonesha UKUU WAKE

Regrann from @paulmakonda - Mara nyingine unapopewa mtihani haupimwi wewe ila wale wanaokuzunguka, kupitia mtihani wako watatokea watabiri, wazungumzaji na watu wa kila aina hadi watakaojivisha U-Mungu kiasi cha kufikia kukufukuru mara nyingine, lakini yote ni MUNGU anawapima imani ili aweze kuonesha UKUU WAKE, na anawakusanya kwa wingi ili atakapotenda NENO LAKE lisambae, hivyo sio kila mtihani ni wa kwako. Na naomba nikiri Kupitia Keagan nimeuona UKUU WA MUNGU, tena MUNGU yule yule asieacha neno lake likaanguka, na kwa unyenyekevu mkubwa kwa hii furaha yote aliyoniletea narudisha sifa na utukufu kwake yeye alie juu'  Lakini pia kwa moyo mkunjufu kabisa nitoe shukran kwa kila mmoja aliejitoa kufurahi na kushukuru pamoja nami kupitia message, simu, post na hata maombi ya chini, tunasema asante sana sana na kupitia nyinyi nimeshuhudia Baraka nyingine ya WATU, kikubwa mtambue nathamini sana sana na kwa niaba ya mke wangu na familia kwa ujumla tunawashuru kutoka moyoni na MUNGU AWABARIKI SANA. #babaKeagan - #regrann

Monalisa kaua, kamaliza kabisa!

  Regrann from @monalisatz - Happy fathers day kwa mibaba yote iliyotelekeza wanawake wajawazito,wakatelekeza na watoto wao au kuwakana kabisa watoto wao kwa sababu wanazozijua wao,siku ya Leo iwakumbushe kwamba wao ni viumbe wajinga kuliko yeyote yule kwenye dunia hii Hata yule Nguruwe aliyetabiri Nigeria kufika nusu fainali za World Cup ana akili kuliko wao.Siku ya Leo kila watakachokula wakaharishe mfyuuu.Watakachoongea wawe wanakohoa kohoa tu ovyo wajinga kabisa nyie...hamuoni haya siku ya Leo wababa wenzenu wako so proud na watoto wao,nyie mmetumbua mimacho tu na wengine MNA vitambi kama wajawazito. Haya Happy father's day kwenu wehu nyie - #regrann

“Hata Kama Mambo Yanakwenda Vibaya, Fanya Hivi”

Hata Kama Mambo Yanakwenda Vibaya, Fanya Hivi

Ni rahisi sana kuwa na hasira, kukatishwa tamaa na hata msongo wa mawazo. Hiki ni kiu ambacho kila mtu anaweza akawa nacho kwenye maisha yake.

Nikiwa na maana kila mtu akikasirishwa, anaweza akakasirika sana au mtu akikatishwa tamaa anaweza akakata tamaa pia sana.

Lakini yote hiyo haiwezi kusaidia kitu. Busara na ukomavu wako wa kimaisha unakuja pale hasa unapokwenda kinyume na mambo hayo.

Ni kweli unaweza ukawa umekasirishwa na ukatamani upige mtu sana, sasa je, kwani ni lazima ifike mahali ukakakasirika kwa kiasi hicho?

Ni kweli unaweza ukawa umekatishwa tamaa, lakini kwa wewe haina haja kuendelea kufanya mambo ambayo yanakukatisha tamaa zaidi.

Unachotakiwa kufanya au kujifunza ni kuweza kugeuza mambo ya hovyo na yakawa bora zaidi hata kama imetokea hali ya kukasirishwa au kukatishwa tamaa.

Kufanya hali mbaya ambayo tayari naweza kusema umeshapewa na ikawa ni nzuri, huo ni ukomavu wa hali ya juu utakaokufanya uishi vizuri sana duniani.

Mtu amekuuzi sana na wewe huhitaji kuendelea kufoka au kuumia zaidi. Unatakiwa kutuliza akili yako na kufanya mambo ili yawe mazuri.

Kufanya mambo yawe mazuri hasa pale yanapokuwa yameharibika ni kitu ambacho unatakiwa ujifunze nacho sana karibu kila siku.

Kila siku na kila wakati endelea kuweka juhudi za kuwa mtu chanya, mpaka maisha yako yalete utofauti mkubwa na kwa wengine.

Ni watu wachache sana ambao wako tayari kubadilisha hali mbaya ya msongo wa mawazo walionayo, kukatishwa tamaa na kukasirishwa kuwa nzuri.

Wengi wakikasirishwa na wengine hukasirika na kukasirisha zaidi. Hivyo, unatakiwa usiwe miongoni mwao. Unatakiwa uwe mtu wa kubadilisha hali.

Kufanya hali yoyote iwe bora ni zoezi ambalo unaweza ukalifanya karibu kila siku kwenye maisha yako pale ambapo unakuwa unaona mambo hayajakwenda sawa.

Unatakiwa uelewe hili, pale mambo yako yanapokwenda hovyo, fanya mambo hayo yawe bora. Jitahidi kubadili hali hiyo kwa busara na ikawa bora.

**By Mapigano**

“Mwanaume ambaye hawaheshimu Wazazi wake jua hatakuheshimu wewe kama mke wake na hatawaheshimu Wazazi wako pia”

Regrann from @lemutuz_superbrand - FACT: To you all my dear Sisters.......Mwanaume ambaye hawaheshimu Wazazi wake jua hatakuheshimu wewe kama mke wake na hatawaheshimu Wazazi wako pia ....Mwanaume asiyejua kuheshimu Traffic Signs anapoendesha gari lake barabarani ujue hatakuheshimu hata wewe...yaani Mwanaume asiyejua Stop Sign...asiyejua Red Light....asiyejua Zebra yaani kusubiri watembea kwa miguu wapite .....atakufanyia hayo hayo kwenye Ndoa au Relationship ....Ukiumwa hatasubiri upone ataku Cheat ...Ukisafiri kikazi hatasubiri urudi ataku Cheat! ..Ukifiwa ukaenda Msibani hatakusubiri urudi ataku Cheat tu! ....Kama Mwanaume wako anagombana sana na madereva wengine barabarani ujue ATAKUDUNDA TU kama Mpenzi au mke wake ....kama anakaripia karipia watu kwenye simu ujue atakukaripia na wewe ....I mean kama vipi MUWACHE CAUSE ATAKUSUMBUA MBELE YA SAFARI I mean ni Ushauri wangu wa bure Uchukue au Niachie ...ila usije kulia lia kuwa hukujua au hukuambiwa! - @lemutuz_superbrand - #regrann

Zamaradi Mketema: Karibu tarehe 15th April ukumbi wa MAKUMBUSHO YA TAIFA

Regrann from @zamaradimketema -

Tumejikuta tunatambua wanawake wengi ambao wamefanikiwa leo hii na kuwaangalia kama watu waliozaliwa wakawa tu hivyo walivyo kutokana na picha yao ya leo bila kujua struggles zao, machozi yao, mapito yao, kusota kwao, kushindwa kwao, kufeli kwao, kukataliwa kwao na hata mateso na changamoto nyingi zilizofunikwa na HALI ZAO ZA SASA.

Katika safari ya maisha na utafutaji wengi huangalia CAPITAL kama ufumbuzi ama kitu pekee kinachotukwamisha kusonga kwenye NDOTO tulizonazo bila kujua kuna vingi huwa vinaturudisha nyuma wanawake na huenda ni matatizo makubwa kuliko kukosekana kwa capital ama vianzio, na hivyo vitu ndio vinafanya hata uwe na kazi ushindwe kuifanya ipasavyo ama hata kuichukia mara nyingine, ama kuna muda ujione huna tu thamani na kukufanya uogope na kunyong'onyea hata pale unapotakiwa kujitokeza na kutoa ulicho nacho, ama ushindwe kusimama vizuri kwenye biashara yako au kushindwa kabisa kuanzisha chochote kutokana na mengi yaliyokuelemea.

Huenda kwasasa uko kwenye hii STAGE, na kuhisi mbele hamna maisha, jambo moja unalopaswa kujua ni kwamba HAWA WANAWAKE UNAOWAANGALIA KAMA MIFANO wengi wao wamepitia kwenye hatua ambazo upo sasa, kuna ambao waliwaza hata kujiua, kuna ambao waliwahi kukosa kabisa, kuna wale waliopoteza dira kiasi cha kutokujua cha kushika, na kuna kipindi walijiona hawana thamani kama ambavyo UNAJIONA SASA, lakini hawakukubali, WALIAMKA, na wakagoma kupelekwa na upepo huo, wakasimama imara na mpaka leo hii tunawapongeza na wengine kuwaita ROLE MODELS. 

Hivyo hata kwako, kwa hali yoyote unayopitia sasa, nataka nikwambie INAWEZEKANA!! nakuahidi utavuka na utaipita hiyo hali na kuwa mpya kabisa, na hakuna ajabu kesho tukakutolea reference kama mmoja wa mifano bora ya wanawake waliofanya maajabu.

Amka kwenye huo usingizi, sio wewe peke yako unaeteseka, na hata kama unapitia manyanyaso, vikwazo, kutokuwa na Dira ya maisha ama changamoto yoyote iwe ya Kijamii, kihisia ama KIUCHUMI nakuhakikishia una nafasi kubwa ya kutoka huko na KUSIMAMA IMARA.

Karibu tarehe 15th April ukumbi wa MAKUMBUSHO YA TAIFA POSTA opposite na IFM kwa mengi zaidi, 

The GOAL is to change LIFE. Na hii siku itakuwa mwanzo wa safari ya mafanikio kwa WENGI. NI BURE!!! - #regrann

Faraja Nyalandu: Huu ni uhitaji ambao kila binadamu ana

Regrann from @farajanyalandu - Oprah Winfrey amefanya interview na marais, waimbaji, wanamichezo na mashujaa wa matukio mbalimbali. Kila mmoja akiwa ni mtu aliyefanikiwa katika eneo fulani. Hawa ni watu walioenda mbele zaidi na kujitofautisha na wengi. Lakini wote wakimaliza mahojiano, camera zikizimwa, huwa wana swali moja kwa Oprah. How did I do? Sina tafsiri ya moja kwa moja lakini ni swali ambalo wanataka kujua iwapo walipatia au walikosea. Sana sana wakitamani kusikia walifanya vizuri na interview yao ilikuwa bora. Huu ni uhitaji ambao kila binadamu anao. Si udhaifu kwasababu ni katika harakati za kujitambua. Ni vile tunataka kufanya vizuri na tungependa kupewa feedback na wakati mwingine kupewa moyo kuwa tunaenda sawa. Ni muhimu kuwa na neno la upendo kwa wengine. Tusione watu wanatembea ni wazima kumbe ndani wana vidonda. Pengine wewe ndio utakuwa wa kwanza na pengine utamuwahi kabla hajakata tamaa na kudhani hana thamani. Tutibiane vidonda. Tuthaminishane. Tukubaliane tofauti zetu. Tukosoane kwa upendo. Sisi ni watoto wa Mungu na Mungu ni pendo. Let's validate each other! #WeekendWisdom 😘 - #regrann

Mo Dewji: safari ya mtu mwingine HAIWEZI KUKUZUIA WEWE kufanikiwa kwenye safari yako

Regrann from @moodewji - Kila wakati kumbuka kuwa, safari ya mtu mwingine HAIWEZI KUKUZUIA WEWE kufanikiwa kwenye safari yako. Usipoteze muda kwenye mawazo yasiyo kuwa na umuhimu. — Mo // Always remember that, someone else's journey WILL NOT STOP YOU from succeeding in yours. Don't waste time on unnecessary thoughts. — Mo - #regrann

Zamaradi Mketema: Simama kwenye sehemu ambayo hata mtu aamue kujiongeza kwa namna gani asiweze kusimama kwenye sehemu yako

Regrann from @zamaradimketema - Wanaofanikiwa kuonekana haraka mara nyingi ni wale walio kwenye makundi ya peke yao, na zaidi kuonekana kwao kunadumu. Hakikisha unakuwa wa tofauti kiasi akose wa kulinganishwa na wewe, usiende na crowd. Usifanye kama wanavyofanya wote, usiige njia za wengine, wala usilazimishe identity zilizokuwa zimeshafanikishwa na wengine (zisizokuwa zako). Simama kwenye sehemu ambayo hata mtu aamue kujiongeza kwa namna gani asiweze kusimama kwenye sehemu yako. Iwe inaangaliwa kwa jicho lolote mtu atakaloamua kuiangalia lakini ibaki kuwa yako, ikizungumziwa hiyo sehemu wakuwaze wewe kwanza, na si kuwa NYONGEZA baada ya wenye kuaminiwa nayo kutajwa kwanza, na hakikisha unaifanya iwe sehemu ambayo SIO kila mmoja anaweza kuifika kwa KIWANGO CHAKO pale anapoamua, kusaidiwa au kuoneshwa. Na kwa bahati nzuri kila binaadamu anayo sehemu hii ila kwakuwa wengi wamejawa na hamu za kufanya kama wengine wanajikuta wanachelewa kwenye njia zao, achana na njia zitakazokuchelewesha na kukufanya uonekane mdandiaji, tafuta yako kisha uivae inavyostahili.

 

Joyce Kiria: Haya MACHOZI yangu namlilia Mungu wangu aliye juu, yeye ndo ataamua

@Regranned from @joycekiriasuperwoman - Changamoto kubwa 2018 #Kipigo
Sikutegemea kama ipo siku kwa mkono wako ungeunyanya KUNIPIGA @kilewo2020mwanga 😭😭😭😭 * Ukasahau kabisa! Ukasahau yooooote.. nimeharibu career yangu kupigania ndoto yako kwa kugawa watu wangu kwenye biashara zangu, nimepoteza ndugu jamaa na marafiki, umeniachia nimebeba mzigo wa familia kwa muda wote... Malipo yako ni KUNIPIGA/ KUNIDHALILISHA/ KUNITOA MACHOZI😭😭😭
Umenipiga kwa sababu Mimi Ni MNYONGE siyo! SINA NGUVU, kwa sababu ni MWANAMKE Sina nguvu za kupigana na MWANAUME ... Umeniumiza mwili wangu unauma kila mahali umefiria damu na kichwa ukanigongesha kwenye gari, ili iweje? Nia yako ilikuwa ninini? kuniua??? Mungu amenipigania.

 Haya MACHOZI yangu namlilia Mungu wangu aliye juu, yeye ndo ataamua...😭😭😭😭😭😭 Kama NI Mimi niliandamana na watoto, nikakufanyia kampeni na deni kubwa nikaingia mpaka nikafungiwa Kipindi hewami, ninakutunza wewe na Watoto wako kwa miaka yote, MUNGU YUPO.... LEO UMENIPIGA @kilewo2020mwanga ??? Sawa watakusifia hao wanaokusifu ujinga, wanaokuambiaga Mimi sikuheshimu, badala wakwambie ufanye kazi utunze familia, Leo watakuona wewe ni MWANAUME kwa KUNIPIGA... - #regrann

Dina Marios: Nilifanya kazi kama miezi minne bila kulipwa mshahara wala chochote.

Nakumbuka wakati naanza kazi 2005 nilifanya kazi kama miezi minne bila kulipwa mshahara wala chochote. Nilikuwa natembea umbali mrefu sana wakati mwingine sababu ya kukosa nauli ili kwenda kazini. Na hata nilipoanza kulipwa nakumbuka mshahara wangu ulikuwa 45,000 ulikuwa mdogo sana na hautoshi.Ila niliridhika kwa sababu nilikuwa najua ni mwanzo wa safari yangu na bado sina ujuzi kivile wala uwezo mkubwa.

Leo hii vijana wengi ninaokutana nao kutafuta ajira swala la kujitolea ni gumu kwao?kusubiri ni ngumu kwao kwanza wengi wavivu na bado wanataka kufanikiwa na kupata pesa.Mtu hafanyi kitu bila kuuliza nitapata nini???

Katika kutafuta kufanikiwa wakati mwingine fanya kazi hata za kujitolea usitangulize malipo.Hili litakupa nafasi ya kujijengea uwezo na kukupa wasifu utakaokusaidia kujipanga vizuri na pengine ukawa mwanga wa ajira ya malipo hapo baadae.

Mdogo wangu Mimi alonifatia alipomaliza chuo sehemu alikuwa anafanyia field waliona uwezo wake wakampa ajira lakini sababu alikuwa bado mdogo wakawa wanamlipa kidogo sana akawafanyia kazi miaka 4 bila mshahara kupanda. Kila siku ananiambia sister mshahara mdogo sana mie nataka kuacha kazi.

Nikamwambia usijihisi upo kazini fanya kazi kama vile upo chuoni chukua ujuzi na mafunzo. Fanya kazi kwa bidii am sure siku ukitoka hapo basi uwe umepata sehemu yenye kukulipa vyema na waseme wamepata jembe haswaaa. Mwaka mmoja baadae akapata kazi tena kwa kufuatwa sio yeye kuomba ambayo wanamlipa vizuri sanaaa na ameweza kutimiza malengo yake mengi sana.

Jiwekee malengo na mikakati hata malengo makubwa huanza kwa udogo. Sawa una elimu kijana na pengine ulihisi ukimaliza chuo tu utapata kazi ya ndoto yako na mshahara mnono. Ukija kwenye ukweli mambo wakati mwingine hayaendagi hivyo. 


Ukipata sehemu hata kama wanakwambia fanya bila malipo......fanya huo ndio mwanzo wako.Jijengee maarifa na uwezo.Jamani acheni uvivu.......acheni kutaka ghafla uwe una mihela unalipwa vizuri.Jitumeni mie nawaona wengi humu makazini wavivu. Na usigelezee mwingine alianzaje ukadhani mna safari moja hapa duniani.

Good Morning!

Je ulishawahi kufanya makosa kama yangu?

 Watu wengi wanatabia ya kupenda kuhisi vitu au kumuhisia mtu badala ya kumuuliza muhusika ili wajue ukweli! Hiyo caption kwenye picha ya Dina Marios imenifanya nikumbuke makosa yangu niliyowahi kufanya huko nyuma. Dina ameweka caption 👇👇 isemayo "Msomali wa Kihaya"  kitu ambacho kimenishangaza kidogo kwani siku zote mimi nilihisi kuwa Dina ni Mchaga 🙊🙊 Sijui kwanini lakini hivyo ndivyo nilivyo muhisi!   

@Regranned from @dinamarious – Msomali wa kihaya
#VipichaPicha
 Sasa haya mambo ya kuhisi vitu kwakweli siyo mazuri hata kidogo kama unayo hiyo tabia basi kuanzia leo anza kujifinza kuuliza kwa kila jambo ambalo hujui kwani itakusaidia sana! Mimi nilipokuwa secondary mmoja wa rafiki zangu alikuwa anaitwa Msolwa Mgawe, sasa huyu Msolwa kwa muda wote tupo shule sikuwahi kumsikia akimtaja baba yake katika maongezi yake. Utasikia kamtaja mama, kaka, na dada zake lakini si baba yake hivyo kwa akili yangu yakupenda kuhisi nikahisi kuwa huwenda baba yake alikwisha fariki hivyo hataki kumuongelea 🙈🙈 ............ Sasa siku mmoja katika story sijui tulikuwa tunapanga kufanya nini ila akasema kuwa  yeye hatoweza kwani "mshua leo anarudi" akimaanisha baba yake anarudi! Nikashangaa, ikabidi nimwambie kuwa mimi nilihisi baba yake amefariki miaka mingi kwani sijawahi msikia akimuongelea baba yake! Yani group zima lilikufa kwa kicheko 😂😂😂 Msolwa akasema Alpha sidhani kama una akili timamu 😂😂😂 ..............Jamani kuuliza si ujinga bali ni kutaka kujua, na hata siku moja hakuna swali la kijinga isipokuwa wajinga ndio huwa hawaulizi maswali! Hacha kuhisi vitu au kumuhisia mtu kitu siku zote kama unaweza uliza but don't assume!! Kuhisi ni kubaya sana!

Zamaradi Mketema: Sidhani kama nikikupa Laki itakusaidia zaidi ya hiki

@Regranned from @zamaradimketema - Ninapoongelea kufanya VITU VIDOGO katika hali ya UKUBWA maana yangu huwa ni hii. @porridge_point ameniinspire hata mimi, kwanza ni degree holder, na wasomi wengi huwa tunaona mawazo yao hata ya kibiashara huwa ni makubwamakubwa tu, ila huyu baada ya kukosa kazi ameamua kuuza UJI, biashara inayoonekana sio ya hadhi yake labda kutokana na elimu yake, ila hakuangalia hilo sababu aliifikiria kwa ukubwa, huenda sio ishu kuuza uji, ila jinsi anavyouza ndio kulikonivutia, kuna wauza uji wengi mitaani kwenye machupa, lakini yeye ameona AONGEZE THAMANI, ameamua kwenda extra mile na kuwa mbunifu kwa kuwa na hizo take away cups zinazofanya yeyote ajisikie hata fahari kubeba, na hata sehemu yake ya biashara ameifanya tofauti na jinsi wauza uji wengine wanavyojiachiaga.  Sidhani kama nikikupa Laki itakusaidia zaidi ya hiki, nimeona nikupe muda wangu ili kuelezea Dunia nini unachokifanya,na zaidi kuweka contact zako hapa huenda ikafungua njia zaidi kwako, nimeona anasambaza hata kwenye mikutano ya kiofisi mbali na watu kumfata, kwa watakaopenda kuwasiliana nae namba zake ni 0654 197952, swipe kuona picha zaidi ama mfollow ili kuangalia anachokifanya.  Hongera sana na MUNGU abariki juhudi zako mama - #regrann

Kama hujawahi kwenda mtoni kuteka maji huwezi jua thamani ya tone la maji!

Watanzania wengi siku hizi wamekuwa na tabia ya kutaka kulazimisha kila mtu mwenye uwezo au mfanyabiashara mkubwa awe "mwanasiasa" au "mwana harakati wa siasa" kitu ambacho siyo sahii hata kidogo! Siyo kila raia wa Tanzania anatakiwa kujihusisha na siasa! Hapana! Kuwa kwenye siasa au ku support chama fulani hayo ni maamuzi binafsi, na biashara ni mtu binafsi! Mmiliki wa biashara ana hiyari ya kujihusisha moja kwa moja na siasa au akakataa, na lazima kila mtu haeshimu maamuzi yake! Unapoanzisha biashara unless ni biashara ya "siasa" then utalega kupata wanasiasa otherwise unafungua biashara kwaajili ya kuhudumia watu wote bila kujali itikadi zao!  Kama hujawahi kwenda mtoni kuteka maji huwezi jua thamani ya tone la maji! Nasema hivi kwasababu watu wengi ambao mnalaumu baadhi ya wafanyabiashara ukiwachunguza utagundua kuwa hawajahi kujaribu kutengeneza kitu chochote au kuangaika from the scratch mpaka kitu kikatembea na watu wakaona ndio maana hamuwezi jua thamani ya kupoteza kitu chako ulicho kiangaikia wewe mwenyewe toka chini! Hamuwezi jua mtu alijinyima kiasi gani ili apate kitu chake mwenyewe! Hamjui mtu huyo alifunga na kuomba Dua kwa muda gani ili Mungu ambariki na biashara yake! Hamjui ni mara ngapi amelia akiona ndoto yake haifanikiwi! Halafu leo hii akubali tu kirahisi rahisi kuharibu mali zake kwasababu ya siasa?! Kuna njia nyingi za kushiriki kuleta amani na maendeleo katika nchi yako bila kujiingiza kwenye siasa!

Siyo kila mtu anajali nani yupo madarakani, wengine wanachotaka ni amani kwani wanajua gharama ya kukosa amani! Msilazimishe kila mtu awe mwanasiasa au mshiriki wa chama fulani kwani kila mtu ana uhuru wa kufanya maamuzi yake na jinsi ya kuendesha maisha yake! Sasa leo mkilazimisha kila mtu awe mwanasiasa then what next? Mtakuja kulazimisha kila mtu awe Muislamu au Mkristo? Nahata katika ukristo bado kuna madhehebu, sasa itakuwaje? Mtakuja kulazimisha wakristo wote wasali Roman? Unafikiri mimi ambaye ni Msabato nitakubali?! Wakati najua thamani na raha ya kuwa Msabato!! ........ Embu acheni ujuaji usiyo na kichwa wala miguu! Mpaka siku ile utajifunza jinsi ya kubeba maji yako mwenyewe kutoka mtoni hauto kaa ujua gharama ya kumwagika kwa tone la maji!

Mc.Pilipili: HUU NI UKICHAA WA MAPENZI

Regranned from @mcpilipili - HUU NI UKICHAA WA MAPENZI. 🔵Kushika mimba ukadhani ni mtego ili uolewe.
🔵 Kutafuta mkamilifu wakati tabia zako tunakuvumilia tu.
🔵 Kutafuta msichana mrembo wakati huna pesa.
🔵 Kutafuta mke mwema kanisani wakati we unaenda kanisani wakati wa maombi ya Christmas tu.
🔵 Kusema wanawake wote sawa.
🔵 Kuendelea kuchagua wanaume wakati unajua waoaji siku hizi wachache.
🔵 Kuishi na mpenzi wako kabla ya ndoa, unamfulia, unampikia na unampa penzi wakati unajua hujulikani kwao, ukiachwa unatafuta ushauri mitandaoni.
🔵Kusema umeokoka lakini unazini na mchumba kama kawaida kwa kisingizio kwamba soon mtakuwa mke na mume!
🔵Kuogopa kuongozana na msichana au mvulana eti mtaingia majaribuni, unajua kutamani tu ni uzinzi?
🔵 Kufikiri kwamba utampata mtu mwenye sifa mia nane unazozitaka labda umuumbe mwenyewe!
🔵Kujifanya unapendwa wakati moyoni unajua wazi mtu kakuchoka, na amekwambia kabisa anatafuta mtu mwingine!
🔵 Kumhonga mwanaume ili akuoe!
🔵 Kudhani kwamba kutoolewa ni laana, hii ni bangi mbaya!
🔵 Kumtongoza mchumba au mke wa rafiki yako!
🔵 Kuoa wakati huna kazi /chanzo cha kipato!
🔵 Kufikiri eti wanaume wa kiafrika wanaweza kufanya mambo ya kwenye tamthiliya za kifilipino.
🔵 Kumsomesha mtu ili uje umuoe!
🔵 Kumng'ang'ania mtu asiyekupenda, utazimia ukialikwa harusini!
🔵Kuwaeleza mashosti zako 'utam' anaokupa mtu wako!
🔵 Kumwambia bebi wako anunue gari wakati amepanga chumba kimoja……..

Diamond: Ili ufanikiwe ni lazma Udharirike kwanza

@Regranned from @diamondplatnumz - lli ufanikiwe ni lazma Udharirike kwanza...  Yaani lazima uwaonyeshe watu kuwa kitu fulani mie nakiweza........na katika kuwaonyesha huko kunawengine watakudharau, watakubeza, na kukucheka.........ila kuna wengine watakipenda, watathamini, kukikubali na kukupanafasi........ Maisha ndio yako hivyo........ Kadri unavyozidi kuogopa na kuona "watanichukuliaje" ndio unazidi kuchelewa kufikia ndoto zako...........Amka sasa Ukawaonyeshe! - #regrann

Mc PiliPili: ISHUSHE hiyo mizigo kama kweli inahitaji kusonga mbele

@Regranned from @mcpilipili – *JE UNAJUA KWA NINI HUFANIKIWI?* Una mizigo mingi isiyo ya lazima wala faida ambayo umeibeba:- 

1. Umejipa jukumu la kuwa “mpelelezi” wa maisha ya wengine na umesahau maisha yako.

2. Umebeba vinyongo na visasi moyoni vinavyokufanya uwafikirie waliokuumiza zaidi kuliko kufikiria furaha na maendeleo yako.

3. Una marafiki wengi ambao ni kama kupe, wapo kukutumia tu na hawachangii lolote katika maendeleo zaidi ya kujifanya ndio watu wako karibu lakini kumbe wapo kwa maslahi yao!

4. Umeweka mbele zaidi “watu watanichukuliaje” kuliko kuangalia maisha yako.Watu ndio wanakuchagulia aina ya maisha unayoishi na unajilazimisha kuishi kama wao hata kama huna uwezo huo.

5. Unaongea zaidi ya kasuku lakini vitendo hakuna.Unatamani mafanikio tu moyoni lakini huna mipango ya kuyafikia.

6. Maisha yako yote umeyaweka kwenye mitandao ya kijamii.Huna siri hata moja!Hivyo unalazimika kuishi aina ya maisha ambayo yataendelea kufanana na yale uliyoyaweka kwenye mitandao ya jamii kwa sababu ukibadilika tu watasema “umefulia”

7. Kila aliefanikiwa ni rafiki yako au utasema ni mtu wako wa karibu na unaishia kuwasifia tu na kupiga nao picha lakini hujifunzi kutokana na mafanikio yao na wala hutumii fursa hiyo ya kujuana nao.

8. Upo sahihi kila siku(you are always right). Huambiliki, hushauriki na kila wazo atakalotoa mwenzako basi si zuri ila la kwako ndio sahihi na utataka litekelezwe hilo hilo. Mwisho wa siku kila mtu anakukimbia hakuna wa kukuambia “hapa umekosea” kwa sababu ya ujuaji wako.

9. Hujifunzi maarifa mapya.Mara ya mwisho kusoma kitabu ilikuwa ni “Ngoswe, penzi kitovu cha uzembe” Tena ni kwa sababu ilikuwa ni kwa ajili ya kujibia mtihani. Hujifunzi “life skills” wala ujuzi mwingine.

10. Unazurura mno mitandaoni bila faida. Kwako wewe intaneti ni kwa ajili ya kuchati tu na kufuatilia habari za mjini ambazo tangu umeanza kuzifuatilia hujawahi kuingiza hata shilingi moja, zaidi unateketeza tu hela yako ya vocha.

ISHUSHE hiyo mizigo kama kweli inahitaji kusonga mbele

Chuki, ubaguzi, na upendo mtoto ufundishwa na wazazi wake!

Chuki na ubaguzi mtoto ufunzwa na wazazi wake kama ilivyo upendo! Mtoto anazaliwa na kichwa che ubongo mtupu na safi! Sasa wazazi na walezi wa hawa watoto ndio inategemea watajaza huo ubongo wa huyo mtoto na vitu gani! ........Nisawa na elimu kuhusu Mungu, mtoto hawezi jua umuhimu wa kuabudu na kumcha Mungu kama wazazi na walezi wake hawakumfundisha na kumuonyesha kwa vitendo kuwa kuna Mungu anaye stahili kuheshimiwa na kuabudiwa! Au utakuta Mzazi anamwambia mtoto wake hiyo nguo mbaya mpe fulani (ana taja jina la mtoto mwingine) hivyo mtoto anakua akijua kuwa kama kitu kibaya au kimezeeka ndio unagawa kwa wengine! Ambapo ni makosa makubwa sana! Mzazi mfunze mtoto wako kupenda watu wote wa rangi zote bila kujali kipato chao cha kiuchumi!

Tamera amenifanya nijisikie kuolewa na mzungu 😂😂😂 I’m curious to see how my baby will look like 🙈🙈