Category Archives: General

Baada ya Rais kujithibitisha kwamba hali haikuwa imetendeka, ni nini kinafuata…..!

@Regranned from @mutwiba – Wakati Rais akifanya maamuzi ya kuwaachia familia ya Nguza Viking, anafungua mjadala mpya na muhimu wa kisheria na haki Tanzania

Binafsi ningependa kujua ni kipi ambacho Mahakama ZOTE zilijithibitisha “beyond shadow of a doubt” kwamba familia hii ilitenda makosa yaliyosababisha kuhukumiwa kifungo na kunyimwa dhamana na hata msamaha walioomba, na umekuwaje sasa imejulikana kwamba hayakutendeka?Swali la ziada (ambalo siamini kama kuna atakayeuliza waziwazi ๐Ÿคฆ๐Ÿฟโ€โ™‚) ni kwamba……
Baada ya Rais kujithibitisha kwamba hali haikuwa imetendeka, ni nini kinafuata kwa waliohusika ama mfumo mzima kuhakikisha kwamba hawatokei kina Babu Seya wengine? – #regrann

#FBF #2010BongoStarSearch

Since its Friday, let us flash-back some memories ๐Ÿ˜ย  Hapa ilikuwa Bongo Star Search ya 2010 behind the scene. Huyo binti ni mwanangu akiwa na Diamond Plutnumz, TMK-Wanaume, na Marlow. Yuko wapi Marlow siku hizi?! ย Anyway natumaini baadhi ya hizi picha ย zitakupa faraja na natumaini wewe uliyekata tamaa.! ย Muwe na weekend njema. Mbarikiwe wote

Lelya Bezuidenhout: baba yangu ni Magambo Makongoro Nyerere

Haya msikilize kwa makini muimbaji chipukizi anayekwenda kwa jina la Princess Lelya! Ni interview nzuri mtoto kaongea kwa confidence nzuri sana. Nakutakia mafanikio mema Lelya Bezuidenhout ๐Ÿ™

Mwanasheria Alberto Msando arejea CCM kwa unyenyekevu!

Yule Mwanasheria wa kujitegemea, msomi wa kuaminiwa na mataifa yote, ย Alberto Msando arejea CCM kwa unyenyekevu mkuu! Akiri kuwa alipotea njia, alikuwa kipofu na sasa anaona kwani hataki kuongozwa na chama ambacho kina Mwenyekiti mmoja kwa zaidi ya miaka 10! Kwani huo pia ni udikteta ๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆย ย ……Alberto anakuwa mwanasheria wa pili (Lau Masha alirudi wiki iliyopita) ambao walikuwa upinzani na sasa wameamua kurudi kundini! ……As I always say, ” I’m not a politician” hence, my comment is respectfully reserved! Just wishing him the best of all!

Stay strong Lulu!

Mungu utengeneza njia pale panapo onekana kukosa njia!……..Pole sana Lulu, shika imani kwani Mungu ni mweza wa yote! Hata hili litapita. ๐Ÿ™

Ivana Trump: I am First Lady Trump

#Feud in the WhiteHouse........Mambo hayo! Who does he belong to and whos is the "first"?!ย  Mipasho ndani ya WhiteHouse! Kweli wanawake wote ni sawa hata uwe nani! Wakati mwingine anasema sasa nini mimi ndio mke wake wa kwanza! Mwingine anasema haijalishi kwani mimi ndio First Lady ๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€ shughuli imewapata washughulikaji ๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆ yale yale ya Kanye West na Ray J ๐Ÿ™Œ ......Kama huelewi hiyo lugha ni hivi aliyekuwa mke wa kwanza (wamesha achana) wa Donald Trump amabye pia ndio mama wa watoto wakubwa watatu wa Mr Trump ambaye anajulikana kama Ivana Trump (hakubadilisha jina baada ya divorce) anasema yeye ni first lady wa Mr Trump kwani ndiye mke wake wakwanza na ndio mama wa hao watoto wenye maadili mazuri! Sasa mke wa Mr Trump wa sasa (mke wa tatu) ambaye ni First Lady Melanie Trump anasema so what!?! kwani yeye ndio First Lady wa Marekani! Mambo ya "title deed"ย  hayo ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ msifikiri ni kwa Zari na Hamissa tu hapana! Mpaka kwenye WhiteHouse ya Marekani ๐Ÿ™†๐Ÿ™† Bora hata hawa wanarushiana vijembe kwa millionaire sasa wengine mtukanane kwa mwanaume wa $50 anaye ishi kwa pesa ya paycheck to paycheck kama akina Alpha hapa inahusu ๐Ÿ˜Ž๐Ÿ˜Ž mwanaume anaye abudu LIKES kwenye Facebook na followers kwa Instagram ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ pole zenu! Mie nipe kwanza ATM card yako ndio nitafanya huo ujinga. mkono mtupu haulambwi jama ๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆย  ......Nafikiri wakati Melanie Trump anarusha mipasho kwa kutumia wimbo wa "The boy is mine" naye Ivana Trump akatumia wimbo wa "he wasn't a man enough for me" kama ifuatavyo -:

Mr Trump and First Lady
You need to give it up.ย Had about enoughย It's not hard to seeย The boy is mineย I'm sorry that youย Seem to be confusedย He belongs to meย The boy is mine


Mr Trump and First wife
Who do you think I am?ย Don't you know that he was my man?ย But I chose to let him goย So why do you act like I still care about him?ย Looking at me like I'm hurtย When I'm the one who said I didn't want it to workย Don't you forget I had him first?ย What you thinkin'?ย Stop blamin' meย He wasn't man enough for meย If you don't know, now here's the chanceย I've already had your manย Do you wonder just where he's been, yeah?ย Not be worried about himย Now it's time you know the truthย I think he's just the man for you

Haya mchukuwe notes za jinsi ya kulea watoto haswa nyie wenye pesa zenu!

Mungu awe nawe Lulu a.k.a Elizabeth! Pole sana mama Kanumba!

Nimenyama na hili swala la Lulu siyo kwamba simpendi au namtakia mabaya, hapana! Hili ni swala sensitive sanaaaaaaa! Pia kwenye familia yetu right this very moment tunapitia kitu ambacho karibia kinafanana na hili swala la Lulu japo mdogo wangu haikuwa swala la mapenzi na bado hajafariki!!ย  Yupo kwenye koma wiki ya tatu sasa anapumulia mashine!! Hivyo, nimejaribu kuvaa viatu vya Lulu kwakweli vimenibada mno! Napia nilipojaribu kuvaa viatu vya mama Kanumba kwakweli vimekuwa ni vikubwa sana havinienei! Kwa maneno hayo, nimeamua kunyamaza na kuomba Mungu kuwa hekima itumike zaidi! Mungu ampe huyo Judge hekima na kuzingatia mambo yote kwani hata Lulu naye ni victim. Bila kusahau kuwa Lulu alisha kaa ndani / jela karibia miaka miwii, kama ataweza ampe hata kifungo cha nje! ………..Mungu awe nanyi nyote poleni sana.

Tamar Braxton amekwenda mahakamani kuomba talaka!

Nashindwa kuelewa ni kitu gani huwa kinatokea, ndani ya miezi michache watu wanakataa kabisa kuwa ndoa yao ipo sawa na hizo rumors ni maneno tu yamtaani!! Wanathubutu hata kumtaja Mungu!! Halafu hamjakaa sawa mnasikia wame file for divorce kuwa wameshindwana! Sasa najiuliza why lying!?! Kama ndoa inamatatizo si unasema tu, kuwa ndoa yetu haipo sawa lakini we are working on it, just pray for us!! Kuliko kudanganya!! Kama hapo ๐Ÿ‘‡kwenye video Tamar na mumewe walivyo jieleza kwenye Wendy Williams show mwezi wa tatu mwaka huu embu wasikilize

Kana kwamba hiyo haitoshi hata mwezi uliopita alipo ulizwa akasema yupo teyari kufanya chochote kile kulinda ndoa yake. Na hivyo kitu chakwanza ambacho anafanya ili kuokoa ndoa yake ni kuachana na "showbiz business" ataacha kutengeneza album za nyimbo mpya! Sasa within 30 days inakuwaje mtu huyo huyo ndio anakuwa wakwanza kudai talaka ๐Ÿ™‰๐Ÿ™‰ย  I don't get it!.......

Lakini ukiangalia kwaundani utagundua huyu Tamar kuacha kuimba siyo kwasababu alikuwa anataka kuokoa ndoa yake bali ni njia ya kumuondoa mumewe kuwa Manager na producer wake. Kama mnakumbuka how Lady JayDee alivyo mfanyia Captain Garnder Habash ๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆ smart lady huh! .......Jamani let your husband be your husband! Mambo ya mumeo kuwa Manager wako kwakweli naona ndoa nyingi zinavunjika ni wachache mno wamefanikiwa. Labda kama huyo mumeo hachukui pesa yoyote kwenye hiyo production yako. Your husband / wife is your business partner and advicer but not someone to manage you everyday, no no! You can only meet at the board meetings or kwenye weekly business meeting. Lakini kila mtu awe na ofisi yake na wafanyakazi wake nafikiri kwa njia hii itapunguza tension fulani zisizo na ulazima!

Halafu pia kitu ambacho nimeona wanandoa wengi ambao wako kwenye the same industry ndoa zao hazidumu au zinakuwa na matatizo sana. Kwamfano, hapa Tamar ni muimbaji na reality TV star wakati mume wake ni producer mkubwa kwenye music na TV show hivyo wote wapo kwenye spotlight na mzunguko wa watu hao hao kila wakati! Lazima wanandoa wawe makini sana mnapokuwa kwenye maswala ya business ili ndoa yenu iwe na amani.  Sasa Tamar na Vince walipo owana hawakupeana "prenuptial agreements" kwani walikubaliana kuwa divorce is NOT an option! Sasa pale divorce inapokuwa ni the only option sijui itakuwaje kwani Tamar anataka full custody ya mtoto wao na pia anasema Vince asipewe spouse support. Kumbuka wakati Tamar anaolewa na Vince, Vince ndio alikuwa anatengeneza pesa nyingi lakini baadaye Tamar akawa super star na kutengeneza pesa nyingi zaidi ya Vince hivyo sasa itabidi Tamar amlipe Vince pesa za kujikimu baada ya divorce..... Vince ni yatima na kwao alizaliwa mwenyewe hivyo hana ndugu wa tumbo moja wala wazazi! So sad!

Couple nyingine ambayo imeshangaza watu ni ya huyu mwanadada wa The Real talk show ๐Ÿ‘†๐Ÿ‘† Jeanie Mai na mumewe Fredy! Hapa mwanamke ndiye aliyesema kuwa yeye hataki kuwa na watoto kwani haoni kama atakuwa mama mzuri kwani kulea kiumbe kingine na kumfanya awe ni kiumbe bora is a tough job ambayo yeye hawezi. Pia kwasasa yupo busy na "carrier" yake wakati mumewe anataka wazae watoto kitu ambacho hawezi fanya. Kutokana na history yake ya kutoka kwenye familia duni wazazi wake waliangaika sana wakaja Marekani kutafuta maisha bora haswa kwa watoto wao. Hivyo kuwa na watoto kuta slow down dream zake ambazo yeye na wazazi wake wameteseka sana kuzipata. Nabado kuna watu masikini kwenye familia yake ambao anaona kuwa anawajibu wa kuwasaidia hivyo kuleta watoto duniani itakuwa ni mzigo mwingine wa watu wanao mtegemea! Hayo ni maisha ya Marekani kule kwetu Africa masikini ndio wanazaa zaidi ya matajiri wanajua mjomba/ baba mdogo au shangazi atawalea tu bila shida ๐Ÿ™†๐Ÿ™†

Hivi, mimi nashindwa kuelewa hivi dunia hii kunawatu wanaowana bila kujadili kama wanataka watoto au hapana!! Hivi si vitu vinajadiliwa kabla hata ya kuchumbiana au mie ndio sijui ๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆ nielewesheni ๐Ÿ˜†๐Ÿ˜† mie I would love to know what am I signing up for, sorry naogopa sana kujifunga kitanzi mwenyewe! Naogopa surprises .........Kumbuka Tamar Braxton alikuwa kwenye show hii kabla ya ufukuzwa mwaka jana!

 

Ziara ya Balozi Wilson Masilingi jijini Houston,Texas

Wiki iliyopita tarehe 21 na 22 mwezi huu wa kumi, Balozi wa Tanzania nchini Marekani, na Mexico alitembelea jimbo la Houston, katika state ya Texas ili kuwafariji Watanzania waliopatwa na maafa ya mafuriko ya Hurricane Harvey mwishoni mwa mwezi wa nane!

Mh. Balozi Masilingi

Balozi pia alikutana na viongozi wa jumuiya na kukutana na wanajumuiya wote nakubadilisha mawazo, kutoa muongozo katika maswala yanayohusu Diaspora. Kwa maelezo na picha zaidi bonyeza ๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰ (TanzanianHoustonCommunity-THC)

 

Get well soon!

Kama binadamu na Mtanzania naomba nichukue nafasi hii kumtakia Mh. Tundu Lissu matibabu mema na uponyaji wa haraka! Mkono wa Mungu wa uponyaji ukawe nawe siku zote! Get well soon ๐Ÿ™๐Ÿ™

Siku ya maisha yangu: Ndani ya maisha ya designer Kiki Zimba

ย “Siku ya Maisha Yangu na @kikizimba @kikisfashion Siku Ya Maisha Yangu Ni show inayo onyesha maisha ya kila siku ya watu mbali mbali wanao toka kwenye mazingira tofauti. Tuna angalia wafanya biashara, wajasiriamali, wana siasa, watu mbali mbali Walio fanikiwa kwenye kazi zao mbali mbali, wakurugenzi, washawishaji, watu wanao julikana kwenye jamii, Na watu ambao wanafanya vitu vikubwa kwenye jamii hata Kama hawa julikani. Je kwenye Siku Yao huwa wana fanya nini tangia Asubuhi mpaka wana maliza siku? Je nini kiini cha mafanikio Yao Na vitu gani vina wasukuma kufanya mambo mengi makubwa wanayo yafanya. Lengo la kipindi cha Siku ya Maisha Yangu Ni kujifunza, kuhamasisha, kuwezesha, kushawishi kupitia watu mbali mbali. Nenda kwenye Bio Na fungua link kuangalia kipindi. #sikuyamaishayangu #kikizimba #kikisfashion” Dorothy Kipeja

Mr and Mrs Kimesera katika ubora wao!

Awiiiihh! Wamenoga eeh!! Wow! Super cute, couple yangu ya ukweli hii! Yani wanavutia na kuwapa moyo wengine kuwa True Love still exists ๐Ÿ˜๐Ÿ˜ Kama wewe ni mgeni basi naomba ujua kuwa hi couple ndio ilikwa my 2016 Hottest And Best Couple Of The Year (SomaHapa). Nawapenda sana ๐Ÿ˜˜๐Ÿ˜˜………Baadaye kuna post inakuja ya kuipongeza LB kwa award waliyo pata. Sasa hivi nipo busy kidogo hivyo naishia hapa!

Jacqueline Mengi: Love is an act of endless forgiveness!

Nimeenda kuchungulia kwa Mrs Mengi nikakutana na picha nzuri sana zakwake na maneno Fulani amazing hivi, "love is an act of endless forgiveness"! Haya ni maneno rasmi aliyo yatamka Beyonce baada ya kumsamehe Jay Z kwenye ile "cheating scandle" nakusema kuwa amejifunza upendo ni tendo la kusamehe bila ukomo / kukoma! Dah! Haya maswala ya mapenzi namwachia Jacqueline na Dr Mengi wake maana site wengine tulishaga achana nayoย  ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆ. 
Kuna mtu aliandika article akisema Beyonce amemsaidia sana kwa maneno yake hayo ............."The best part of the show is when Beyoncรฉย gives us the quote about forgiveness.

โ€œLove is an act ofย endlessย forgiveness. Forgiveness is me giving upย myย right to hurt youย for hurting me.ย Forgivenessย is the final act of love”ย 

All this while getting shot in a wedding dress. Yes, shit gets THAT real.
Weโ€™ve all been there for before where we wanted to hurt the one we love because they hurt us. Why? Because no one can hurt you more than the ones you care for. They know you best and you feel so vulnerable to them.

It is a valuable lesson to be learned here. In order to sustain love, you have continuouslyย BEย love. You have to be willing to love through thick AND thin. Itโ€™s easy to stop loving once youโ€™ve been hurt but as the late Maya Angelou once said, โ€œHave enough courage to trust love one more time, and always one more time.โ€

If two people can put aside their ego and realize that mistakes will be made; and know that nothing worth having will come without HARD work to keep it, you can really have that ever lasting love you seek." ............unaweza soma article you kwa kubonyeza ๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰ (LoveIsAnActOfEndlessForgiveness).ย ย 

“If you are happy with yourself it’s very easy for others to make you happy”JNM……….Umependeza sana! Super clean and beautiful!

Imbumba Yamadoda: What I am doing for myself I am actually doing it for you! And what you are doing for yourself you also doing for me!

A must watch to all African men!! Hii video niliiona almost two months ago, but nikawa nasubiria a “proper” day kuiweka. Sasa kwakuwa bado tupo kwenye furaha ya maadhimisho ya mtoto wa kike duniani basi nimeona ni vyema kuiweka! Kwakweli huu ni ukweli kabisa! Watoto wa Africa haswa wakike wamewekwa kwenye “pressure” of how to become a good citizens, great mothers, wives, sisters, and aunties bila kujua kuwa it always takes two to tangle!! Unakuta mtoto wa kike very well organized mentally, spiritually,ย  physically, na hata financially lakini anaangukia kwenye mikono ya mwanume asiye jielewa kabisa!! Mnyanyasaji na mambo mengi ambayo yanafanya maisha yao kutokuwa na furaha! A totally unprepared man for familyhood!! Na ukijaribu kuuliza hawa wadada utasikia ma’am! “All men are the same”!! Hivyo hakuwa na chaguo zaidi ya ku settle down for less!! ………Wazazi, waleeni vijana wenu ukijua kuwa kesho atakuwa mume wa mtu, mmoja ya wana jumuiya hivyo lazima awe teyari kuwa good citizen! Kuwa na hela doesn’t make someone a good citizen or good husband tabia yake na malezi ndio vitaeleza huyo kijana wako ni mtu wa namna gani! Nimeona vijana wenye pesa na ni wanyanyasaji wa wanawake mpaka inaogopesha! Wengine ni rapists and molesters! Tuwalee watoto katika njia ipasayo ili wasiwe mzigo kwa wengine na taifa analo ishi ni jukumu lako wewe kama mzazi!

 

Siku ya walimu duniani: Leo ni siku ya walimu duniani. Je nimwalimu yupi unamkumbuka?!

Leo ilikuwa siku ya walimu duniani. Jokate akauliza je, ni Mwalimu yupi unamkumbuka?………….. Binafsi nawakumbuka walimu wangu wote kuanzia vidudu mpaka secondary lakini hawa walimu wangu wa vyuoni nawakumbu baadhi tu kwasababu ni wengi na wanakufundisha kwa semester! …….Kwa elimu yangu ya vidudu / cheke chea na grade one to two namkumbuka Mwalimu Jenifer ambaye alinifundisha vidudu pale Mgulani chini! Grade one and two namkumbuka sana Mama Mwalimu Massamu. Japo walimu wote ni muhimu sana katika kila level ya elimu lakini hawa walimu wangu wa elimu ya awali nawashukuru sana tena mno! Wanasema kuwa Mwalimu ni wito lakini kufundisha elimu ya awali ni zaidi ya wito! Mungu awabariki walimu wote duniani ambao wanafundisha kulingana na maadili ya uwalimu!

New song: I miss you by Lady Jaydee

Japo hakuna ninaye m-miss, am happy with my life now as I just”dodged” the bullet ๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆย  …….. Wimbo mzuri sana, ni tofauti na tulivyo mzoea Lady Jaydee na nyimbo zake za nyingine. Huu ameuwimba kiupole zaidi (slow motion). Video ni nzuri sana. Kiukweli huwa napenda uvaaji wa Lady Jaydee kwenye video zake. Siyo mtu wa kujiacha uchi! Video zake mnaweza angalia watu wa rika zote na mkawa comfortable! ……kazi nzuri sana!

Its always business on this side! #UtelGlobal Call Center

Our new call center is almost ready ๐Ÿ’ช๐Ÿ’ชand it looks Spectacular ๐Ÿ‘Œ๐Ÿ‘Œ We glorify the Almighty God for all the blessings ๐Ÿ™๐Ÿ™ #UtelGlobal #Viettel-Tanzania #Halotel #PPFTower

Janeth Igogo a.k.a Mrs Nyagilo

“Call Center Set-up Final touches… Supporting Family business #Wives’ work behind the scenes.”~~~~ Mrs Nyagiloย  The Lawyer herself! Katika ubora wake ๐Ÿ˜๐Ÿ˜ My babysister is cuter and smarter than yours ๐Ÿ˜—๐Ÿ˜—

Shilawadu! Shilawadu! Naomba mumuache Zamaradi alone!

Nimeingia Instagram hasubuhi hii nikaona Zamaradi akiwalalamikia “Shilawadu” ikabidi niingie nisome maana nilikuwa sijui hiyo account yao!………Eti wanamuita mume wa Zamaradi “Mission town”?! Hivi kuna mission town kuliko Wahaya?! Hata hapa Marekani wapo mnataka tuwataje ๐Ÿ™†๐Ÿ™†? Halafu kwani yeye ndio wakwanza kuwa mission town mbona hata huyo Ruge alikuaga mission town before ๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰ “Ruge & Kusaga” sasa chaajabu ni nini? Watu wote huwa wanaanza huko hivyo yeye siyo wakwanza na wala hatakuwa wamwisho!! Na Mungu anajua kuwa Zamaradi anaweza akamtoa kwenye mission town na kuwa Boss mkubwa tu hapo Bongo! Hivyo hayo ya mission town muachieni mwenyewe Zamaradi nyie fanyeni yenu!………. Kwanza bora mission town anaye jiheshimu kuliko mwenye pesa ambaye ni “mali ya Umma” kila mwanamke wa mujini ana share zake hapo! Sasa si bora huyo Ruge atembee bila nguo watu wajue kachanganyikwa? Kha!!…….. Halafu mnamuita mission town wakati huyo teyari niย  “step dad” wa watoto wa Ruge? Yani hapo bado hamjamkuta kwenye pozi la picha na Juhjuh na Shubi ndio mmepagawa hivyo? Hivi siku Ruge akisikia Juhjuh na Shubi wanamuita huyo mission town “Baba” si atazimia kabisa?? ………. Haya acha mission town akulele mama watoto wako na wanao, mpaka siku akili zirudi wenzako watakuwa wana wajukuu ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ Huu ubuyu mtamu zaidi yaule wa Diamond na Zari ๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆย  ……….Hawa Wahaya wanajifanya wataalamu wa kuonyesha watu jinsi ya kukamata fursa wakati wao fursa zinakuja na kukaa kwenye malango yao lakini wanashindwa kuzikamata ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ Hivi mnajua sasa hivi Wahaya wangekuwa wameandika history ya kuwa na mke muendesha ndege?!! Do you guys remember Captain Hilda Ringo Vs Mujuni Makubo?! (Wahenga wa ma blog mtatujua. tu ๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆ)ย Eti wakamzingua Captain Hilda kwakuwa hajui kupika?! Like WHAT???!! Mtu anaendesha ndege bado wanataka awe mtaalamu wa kupika?!! ๐Ÿ™‰๐Ÿ™‰ Hivi unajua ali sacrificed vingapi kujifunza kuendesha ndege?! Mimi mwenyewe naogesha wazee na bado chapati zimenishinda kupika sasa itakuwa Captain wa ndege? ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ you must be kidding me?!๐Ÿ™ˆ๐Ÿ‘Ž Halafu kama walikuwa wanataka mtoto wao aowe mwanamke anaye jua mapishi si wangemwambia akatafute mama ntilie aowe? ๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆ………..Haya Zamaradi huyo naye kawatoa nishai sasa mmebaki kusema “mission town”! Semeni tena habari ya mission town niwaonyeshe mission town wa Kihaya hapa Marekani ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ Vita ya Shilawadu na Mission Town haijawai kumuacha mtu salama๐Ÿ™†๐Ÿ™†……….Finally, leave my brother Paul Makonda out of your mess! Kuoa mshindwe nyie halafu hasira mzimalizie kwa kaka yangu?! Shame on you!

Haya wale wadada wa “fursa” kamateni fursa hiyo …..!

Pale mzee wa kuonyesha fursa anapogeuka kuwa fursa ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ Haya wadada wa mujini waini fursa hiyo msitoane roho tu, he is officially Back in the Market and Ready to Mingle ๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆ…………. Ruge! Ruge! Ruge! What are we gonna do with you? Hivi unajua mwanamke alipewa uwezo na Mungu ambao anaweza akamfanya mwanaume aonekane kuwa shujaa (hero) katika macho ya jamii au akamshusha na kuonekana the biggest loser!?! Sasa wewe juzi tulikuona shujaa lakini sasa? Dah!!ย  Tatizo lenu nyie Wahaya mmezowea kuweka wanawake zenu “vimada” hivyo mnafikiri kila mwanamke ni Muhaya! Hamjui kutofautisha wanawake wa kuwachezea na ambao wanafaa kuoa! Sasa Zamaradi kakutia adabu!………Wewe watoto wawili umetoa “advance” kwao halafu kuoa uowi? Shame on you! Nasikia wewe ni kama shirika la UMMA, yani nikufananishe na DAWASCO unasambaza maji kila kona ya jiji la Dar ๐Ÿ˜ท๐Ÿ˜ท Yani wewe huko kwenye Media umeenda kwenye wrong field kwakweli ๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€ ………Haki kabisa nilikuwa nimepani nikuchambe sana (hata Muhaya mwenzako nilimwambia kuwa nitakuchamba sana…….nayeye zamu yake inakuja)ย  sema huruma ikaniingia then I started to look at it in a different angle! Inaelekea watu wengi ambao wako very talented like you huwa hawa settle down, yani family life kwao ni tatizo kubwa! Mfano, Simon Cowell, Ryan Seacrest, late Michael Jackson n.k

Eti! Hawezi taja idadi ya watoto wake ni swala personal!?! Sasa mbona amemtaja Juhjuh na Shubi? ๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆ…….R.I.P Mr Hugh Hefner your legacy will forever live hasa kwa Wahaya ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆ………..But sincerely, from the bottom of my heart I feel bad for you! Pole sana mtani wangu!

Embu tucheke kidogo na Fred Omondi

Don’t play with Otienos’ย  siyo watu wa spoti spoti eeh ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ unajua baba yangu his first name ni Otieno, the dreams he described utafikiri anamuongelea yeye ๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆ na huyo mwanamke mwenye dream yakuwa “OW” A.K.A “Otieno’s wife” ni shida! But kuna wanawake wa hivyo ambao wanakwenda shule nia yao kulewa na madokta, professos, au wafanya biashara wakubwa!……… So funny!