Category Archives: Holidays greetings

Nawatakieni kheri katika kufunga mwaka na neema za mwaka mpya!

Wapendwa wasomaji wangu, ndugu jamaa, na marafiki, katika haya masaa machache yaliyobakia kumaliza mwaka huu wa 2017 napenda kuwatakia kheri katika kufunga mwaka na pia nawaombea neema na baraka zote za mwaka mpya ziwashukie na kukaa nanyi siku zote!   Blog hii nili register rasmi tarehe 15th Dec, 2015 hivyo mpaka sasa ninakuwa nimetimiza miaka miwili na wiki kama mbili hivi! Mwaka wa kwanza nilifanya vizuri sana tena sana! I was very proud of myself! Mwaka wa pili niliyumba kidogo kwasababu "vidudu mtu" wale mafundi wa majungu na fitina wakaingilia kati! Hivyo kimaendeleo ya blog sikufanya vizuri japo wasomaji wangu wameongezeka kwa zaidi ya 300%++ ukilinganisha na mwaka wa kwanza  Wanasemaga 'adui' ukimjua hakusumbui kichwa! Basi nami nashukuru kwa nafasi waliyonipa kwani nimewajua! Hawaniumizi kichwa, kwanza hata nguvu ya kusimama mbele yangu hawana! Wanajua sentence yangu moja inawatosha kuwapa "heart attack" ??  hawana uwezo wa kuniangusha mimi wamebakia kupiga majungu behind my back, and definitely that is where they belong "behind my back" I hope I "smell"  good enough to make them stay there forever ?? Siwapi nafasi tena! Yani huwezi amini wengine mpaka nacheka nao lakini akili kwa kichwa ati!!  2018 narudi kwenye mstari! Nawahaidi mambo mazuri kama yale ya mwaka wa kwanza! Tutajifunza na kucheka sana! Life is too short embu tujifurahie siye!.....Malengo yangu ni kwamba kila miaka 5 na make major move, lakini kama nitaweza kufanya hizo major move kabla ya miaka 5 nitashukuru sana! Just pray for me as I pray for you na sote tubarikiwe! Ukiona mapungufu yangu chukulia kama "fursa" kwako, kwani hata mimi niliona mapungufu ya wengine nikaona ni "fursa" yangu! Hivyo siku zote jifunze kutokana na makosa ya wengine siyo lazima yakukute wewe! Safari yangu ya kupunguza uzito! ?? Japo siwataharifu kila wiki kama nilivyo haidi lakini bado iko pale pale. Na ninepungua, sema lile tumbo la chini ndio bado?? Niliacha kuwapa progress kila wiki kwani ilikuwa inanikatisha tamaa kuona wiki nzima napungua 1Lb?? nikaona bora nifanye mazoezi na diet kimya kimya ikifika mwezi wa 5 mwakani nawapa report iliyo kamilika!   Nimepungua toka size 16 na 18 mpaka 12 na kuna nguo moja ndio 14, nafikiri inategemea na deaigner na material iliyotumika! Namshukuru Mungu kwa mambo mengi sana, na moja ya jambo ambalo ameweza kunibariki nalo mwaka huu ni kuonana na ndugu zangu. Miezi minne ya mwanzo mwaka huu nilikuwa Tanzania, nashukuru nimeweza kuonana na ndugu zangu wote! Mara nyingi nikiwa likizo kutoka na sababu za shule baadhi yao walikuwa nje ya Tanzania hivyo tulikuwa hatuwezi kukutana pamoja kwani ratiba zilikuwa tofauti sana. Mimi huwa siendi nyumbani mara kwa mara unless kuna kitu cha lazima ndio maana huwa nikienda nakaa miezi 3+! Mara nyingi kila baada ya miaka 2 ndio nakwenda. Kama kuna kitu nilifurahiya nilipo kuwa nyumbani ni kuwepo wakati wa birthday ya baba yangu! Miaka yote huwa na miss hii siku! Lakini safari hii Mungu alinibariki nilikuwa nyumbani na mimi ndio nilikuwa "master mind" behind hiyo surprise ?? Mimi hapa ndo huyo nimeshika camera ?? Kama kuna kitu namshukuru Mungu siku zote na nitamshukuru mpaka nakwenda kaburini ni zawadi ya hichi ? kiumbe! Sijui na wala sitaki kujua maisha yangu yangekuaje bila mwanangu! Mungu zidi kunilindia na kumbariki mtoto wangu! Jamani, nisiwachoshe na maneno mengi ?? Namshukuru Mungu kwa yote! Nawatakieni kheri ya kufunga mwaka na baraka na neema zote za mwaka mpya ziwashukie na kukaa nanyi! Happy New Year everybody! Love you all!

My 2017 Hottest and Best Couple wakiwa na mziwanda wao!

Simnawakumbuka eeh! Hii ndio ilikuwa my 2017 Hottest And Best Couple Of The Year! Mr and Mrs Joseph Musira kutoka Kamunyonge, Musoma, Mara!…. kama ulipitwa soma ?? (2017HottestAndBestCouple) Hapo kwenye picha  wapo na mziwanda wao baada ya kutoka kwenye ibada ya kufunga na kufungua mwaka! Nawatakia mwaka mpya mwema, upendo na neema za Mungu zikaambatane nao katika mwaka mpya! Nawapenda sana. Kama wewe ni mgeni wa hii blog hii blog basi naomba ujue kuwa kila mwaka siku ya Valentine huwa nachagua wapendanao wawili kuwa the best couple of the year. Hivyo ukitaka kujua nani atashika taji mwakani wewe endelea kutembelea hii blog bila kuchoka nani 2018 itapendeza zaidi ?? Mtu na daddy ake, deka mdogo wangu ??

“Hatuna formula sometimes hata hatuelewi what we are doing…ila tunachojua tunapendana”

My bestie and I #FBF

My bestie and I somewhere in Masaki, Dar es salaam earlier this year!……..Sidhani kama nilishawahi kuwaeleza kuwa huyu rafiki yangu kipenzi ni shemeji yake na Freeman Mbowe kabisaaaa! Napia ni daughter inlaw wa Dr. Reginald Mengi ?? anyway that is not the point nawala havihusiani na urafiki wetu! Sisi tulisoma wote college pale CBE, Dar napia tulikuwa room mates! Namtakia kheri ya kufunga mwaka 2017 na baraka zote za kuanza mwaka 2018! Love her dearly! #FBF #2017

Merry Christmas from Lyimo and Adhero families!

Family over everything! Familia ya Lyimo kutoka  Ohio state (upande wa kulia) wakiwa ndani ya Kansas State ambapo wamekwenda kufurahi pamoja na ndugu zao wakati huu wa Christmas! Kushoto ni familia ya John Adhero na wanawe. Mke wa John ni dada mdogo (tumbo moja) wa Jackson Lyimo. Hivyo hapo ni ugeni mzito haswa kwani shemeji mkubwa na mkewe wako ndani ya mji wa Adhero ?? ........Btw, John Adhero is my cousin ??  mtaalamu wa kujipendekeza simnanijua? Sasa nisipo jipendekeza kwa ndugu zangu nitajipendekeza kwa nani tena?!! ?? honestly, he's my cousin, baba yake ni kaka wa ukoo na mama yangu mzazi ??  So beautiful! Merry Christmas to you the Adheros and Lyimos family!

Merry Christmas from my cousin Gloria and her family!

Wamenoga eeh! So beautiful, they look so much blessed ?? Merry Christmas from Gloria and her family Ndugu zangu wazurijee sasa ?? Asante Mungu wazuri wasura mpaka roho ?❤

Happy Holidays from Mwajuma and her family!

Awwih! Mahaba haya si muchezo ati ? Mwajuma na mapigo ya moyo wake ? bwana mie jina la shemeji silijui ? Ila Mwajuma ni dada yangu, tumekuwa wote mtaa mmoja, nyumba zetu zinapakana ukuta hadi leo hii ninapo ongea. Yani nivile tu tumekuwa na maisha yakatupeleka sehemu tofauti. Yeye anaishi UK na familia yake nami niko U.S.A. Tumeishi sisi kama ndugu na majirani zetu hadi raha. Watoto wa KekoJuu siye wazazi wetu walikuwa waungwana sanaaa! Ndio maana mpaka leo sisi tunapendana.....Happy holidays Mwajuma and your family ?❤  

Merry Christmas from the Nyalandu!

@Regranned from @farajanyalandu – Merry Christmas to you and yours! #LetLoveLead

Merry Christmas from Open_Kitchen2014 and family!

Merry Christmas from Open_Kitchen2014 and her family!

Merry Christmas from Mashimis’ family!

Season to reconnect, recharge, and celebrate with family and friends! Here is the Mashimis’ family from Atlanta, Georgia. Merry Christmas to you!

It’s all about family moments: merry Christmas from Mbwanas’ family

  @Regranned from @meckmbwana - Wishing you Merry Christmas from our home to yours. May you be blessed with love, joy and peace. ??

Its all about family moments: Merry Christmas from Mndalilas’ family!

Stephen Mndalila and his beloved wife and son all the way from Indiana. ……Merry Christmas to you! 

 

Merry Christmas from mama Mbuna and family!

"Merry Christmas from Mama EvalyneMbuna's home to yours. For the first time Christmas without Sam Mbuna , Eriq Mbuna and 9th Christmas without Dad! No matter what we still give Glory, Honour, Praise and Thanks to God Almighty for taking us thus far! We are more than conquerors through Christ who Strengthens us. Once again Merry Christmas"   

Merry Christmas my dearest!

Nawatakieni kheri na baraka zote za Christmas wapendwa wangu! Mzipokee na mfurahiye neema na baraka za Mungu Baba kwa kipindi hichi tunapo furaha kuzaliwa kwa Mkombizi wetu. Ni mimi Blogger wenu kipenzi Alpha Igogo ?? Nawapenda sana! Wishing you a very Merry Christmas my dearest friends, family, and my loyal readers! May you receive and enjoy all the blessings that come with this joyful season! I love you!

 

Wema Sepetu: You have so many different images our Lord, but we all define you as our Savior! Happy birthday Jesus Christ

@Regranned from @wemasepetu:- Always stay Positive, it will help you through a lot......Keep a smile on your face at all times... Although kunawakatiinakuwangumu but Force it out........ And let it stay there... As a human being it can get pretty crazy controlling them feelings(Trust me, Experience has been my Teacher through it all??) But one thing I've learnt, Its all Me.........  My Life, My Decisions, My Choices, My Everything... And at the same time, its all You... Your Life, Your decisions, your choices, your everything... So mine doesn’t have to matter to you, & yours doesn’t have to matter to me....... Try that formula and live a Happy life........I'm doing it now & best believe I am a Happy soul... I do wat matters to Me, Myself & I... My mama didn't give birth to me so that I can come to this world to please people......??? Positivity all the way.... To a Positive 2018 Ladies & Gents...... Nawapenda..... #AlhamdulillahYanguYananiendea?????? - #regrann 

Happy 4th of July Americans!

Happy Independence Day Americans! May you celebrate with joy and harmony the day that gave its citizens  the freedom of thought, actions, faith, speech, and many other aspects of life! The country of immigrants we celebrate your birth day! Happy 4th of July!

Eid Mubarak wapendwa!

Sheikh Juhju katka ubora wake!

Eid Mubarak to all my Muslim family members, friends, my loyal readers, and. everyone else! Mungu awabariki sana muwe na sherehe njema! Nawapa mkono wa Eid wapendwa!

Ramadan njema kwa Waislamu wote duniani!

Nawatakieni Ramadan njema waumini wa dini ya Kiislamu wote katika hii dunia! Muwe na mwenzi uliotukuka sana mtukumbuke na sisi katika dua zenu! Happy holy month to you!

 

Happy New Year my beloved!

Happy New Year to my good readers! Binafsi namshukuru sana Mungu kwa kuweza kunipa nafasi nyingine yakufanya matengenezo katika maisha yangu kimwili na kiroho, kijamii na kiuchumi! Jina lake litukuzwe siku zote!

Mwaka niliufunga kwa kuanzia kanisani kuabudu siku ya Sabato kisha tukaenda na mdogo wangu kula mihogo Coco beach! Baada ya hapo mida ya jioni nilikwenda msalimia baba yangu mkubwa Charles O. Igogo na familia yake wao wanaishi hapo OysterBay. Tulikaa hapo mpaka majira ya saa nne usiku kisha tukarejea nyumbani. Tukapiga story na kufurahi pamoja!…… Siku ya tarehe moja 2017 ndio tulihama rasmi ambapo palikuwa makazi yetu ya kudumu kwa muda wa zaidi ya miaka 30! Hivyo sasa naweza sema rasmi kuwa tumehama Keko Juu na sasa tunaishi Kibada, Kigamboni!

Sarah (left) na Magreth

Basi siku ikaisha kwa kwenda kwenye mgahawa mmoja hapo Kibada ujulikanao kama Silver Shark tukiwa mimi, baba yetu, mdogo wangu Magreth, na my niece Sarah. Tulikula Mbuzi, kuku, na chips za kumwaga! Sorry picha zote zilipigwa na simu ya baba amesafiri kabla sijazitoa ?? Tunamshukuru Mungu kwa yote!…….Too bad sitaweka ahadi yoyote ile kwa blog kwani I’m a woman and certainly I’m allowed to change my mind  🙂 🙂 🙂 Happy New Year Everybody!Be blessed! ? ??

NIWATAKIE HERI YA MWAKA MPYA 2017 WENYE BARAKA NA MAFANIKIO TELE- Peter Sarungi

Peter Sarungi a.k.a The Next Speaker-Baba Pilato!

Kwanza: kabisa, tumshukuru Mungu kwayote yaliyojiri mwaka 2016 yawe mabaya ama mazuri bado tuna wajibu wa kushukuru maana fikra na malengo yetu sio ya Muumba

Pili: Tumshukuru Muumba kwa kuendelea kutupa Uhai usiokuwa na upungufu hata kama upo kitandani ukiwa hoi kwa magonjwa na maumivu makali ama upo bar unakunywa pombe na kufanya starehe mbalimbali, wote yatupasa kumshukuru Muumba kwa huruma yake na upendeleo.

Tatu: Tupeane pole kwa wote tuliopatwa na kuguswa na misiba mbalimbali katika kipindi cha mwaka 2016, tuwaombe wapendwa wetu kwa mungu awarehemu na kuwahifadhi mahala pema mbinguni. Safari ni yetu sote, wao wametangulia tu.

Nne: Tusikate tamaa kwa matarajio tuliyoshindwa kufikia na wala tusibweteke kwa majarajio tuliyafikia katika kipindi cha mwaka 2016 maana Maisha ni mchakato. Ni harakati za kukusanya mambo manne (4) kwa pamoja ili kupata furaha (happy), mambo hayo ni pesa, heshima, afya na mapenzi. Hivyo jua kama wewe una afya njema jua kina mwenzako yuko maututi, kama wewe unapendwa kwa dhati jua kuna mwingine ana danganywa, kama wewe una pesa ya kukidhi mahitaji yako jua kuna mwingi ni fukara asiye na matumaini na kama wewe una heshimika basi jui kuna mwenzako amekuwa teja anayekosolewa mitandaoni. 

Tano na Mwisho, Niwatakie Mwanzo na mwendelezo mwema wa mwaka 2017 ukiwa na baraka, amani, furaha na mafanikio tele katika mipango yako ya mwaka mpya. Mungu akupe nguvu na ujasiri wa kutambua uwezo na karama yako ili uweze kufanya mambo makubwa na uyapendayo katika mwaka 2017. Mwaka 2017 uwe ni mwaka wa kujivunia tofauti na mwaka 2016 ingawa ni mwaka usio gawanyika kwa 2 kama tulivyo aminshwa na wakubwa zetu hapo zamani.

Mungu awa bariki sana na asanteni kwa kuwa mmoja kati ya marafiki wengi, ndugu wengi na jamaa wengi tulio shirikiana kipindi cha mwaka 2016.