Category Archives: Inspirational stories

Jacqueline Mengi: The day @drntuyabaliwe_foundation will be able to put up libraries in all regions and hopefully all districts of Tanzania will be the peak of my happiness

Regrann from @j_n_mengi - There’s so much joy in seeing a dream become a reality,and how that dream can change other peoples lives.I can’t even put in words how lucky and blessed I feel to be able to fulfill my dream of encouraging and enabling kids to develop the habit of reading. The day @drntuyabaliwe_foundation will be able to put up libraries in all regions and hopefully all districts of Tanzania will be the peak of my happiness. - #regrann 

KUWA NA SHUKRAN

KESHA LA ASUBUHI

IJUMAA

16/03/2018

*KUWA NA SHUKRANI*

📖 _Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu. 1 Wathesalonike 5:18._

✍🏽Kuna mashaka mengi sana yasiyo ya muhimu, wasiwasi mwingi kwenye akili za watu, juu ya mambo ambayo mtu hawezi kuyabadilisha. Bwana anatamani watoto wake wamtumainie Yeye kikamilifu. Bwana wetu ni Mungu mwenye haki na mwaminifu. Yapasa watoto wake watambue wema na haki yake katika mambo makubwa na madogo ya maisha.

✍🏽Wale wanaoendekeza roho ya wasiwasi na manung’uniko huwa wanakataa kutambua mkono wake unaoongoza. Wasiwasi usiohitajika ni jambo la kipumbavu; nalo hutuzuia tusisimame katika nafasi zetu halisi mbele za Mungu.

✍🏽Roho Mtakatifu anapotujia moyoni, hatutakuwa na hamu ya kulalamika na kunung’unika kwa sababu ya kutokuwa na kila kitu tunachokitaka; badala yake, tutampa Mungu shukrani inayotoka kwenye mioyo iliyojaa kwa sababu ya baraka tulizo nazo. Kati ya wafanyakazi wetu leo, lipo hitaji kubwa la kuwa na shukrani zaidi; na wasipofikia hatua ya kuwa na roho hii watakuwa hawajajiandaa kuwa na nafasi kwenye ufalme wa mbinguni.

✍🏽Kazi kubwa yapasa ifanyike kwa ajili ya kila mmoja wetu.
 Huwa tunaelewa kidogo sana kile Mungu anachokusudia kufanya kupitia kwetu. Inatupasa tujitahidi kutambua upana wa mipango yake na tufaidike kutokana na kila fundisho ambalo Yeye amekuwa akijaribu kutufundisha.

``` 🙇🏽‍♀Hali ya kudhamiria mabaya ipo kwa wingi mawazoni mwa mioyo na akili zetu tunapojitahidi kuenenda kwa namna yetu wenyewe kinyume na sheria ya wema. Hapa ndipo wengi wanaposhindwa. Huwa hatujengi welekeo wa wema; tunataka kila kitu kitujie kwa namna iliyo rahisi.```

```🙇🏽‍♀ Lakini swali lenye umuhimu mkubwa zaidi kwa kila mmoja wetu haipasi liwe juu ya namna tunavyotekeleza mipango yetu wenyewe dhidi ya mipango ya wengine, lakini namna tunavyoweza kupata uwezo wa kuishi kwa ajili ya Kristo kila siku. Kristo alikuja duniani na kutoa uhai wake ili tupate wokovu wa milele. Anataka amzingire kila mmoja wetu kwa angahewa la mbinguni, ili tuweze kuupatia ulimwengu mfano utakaoiheshimu dini ya Kristo. – Loma Linda Messages, uk. 602.```

Akin-Al: RULE YOUR LIFE OR BE RULED FOR LIFE!

Your feminist sister who says you don't need no man in your life already had 3 kids from her ex-relationships and your egocentric brother who says you don't need no woman in your life already had 5 kids from different women... Your fanatic friend who says social media are distractions to get to the kingdom of God has flat screen TVs and unlimited internet in his house. 

My MCM is Edger Gasper, from Bongoland
Never allow the music in other peoples lives determine the dancing steps in your own life...RULE YOUR LIFE OR BE RULED FOR LIFE!..... Akin Al Ameen®™2017

***Edger picture has nothing to do with the story***

Uzalendo huanzia nyumbani kwako!

"Picha hii ilipigwa siku ambayo nilitangaza kuwa sitagombea tena Ubunge, baada ya kuwatumikia kwa miaka 10. Sita sahau hisia zetu siku hiyo, jinsi mioyo yetu ilivyo vunjika kwa kujua kuwa mazoea yetu yatabadilika. Nina uhakika upendo wetu umebaki daima. Ndugu zangu Singida mjini ninawakumbuka sana! ❤ MO" // This picture was taken the day I announced to my constituents that I won’t be running for parliament, after serving them for 10 years. I won’t forget our emotions that day, a deep sense of heartbreak knowing that our interactions will change but the love will forever remain. My fellow Singida Urban brothers and sister, I miss you dearly! ❤️ MO"

Biblia inasema kuwa mtu asiyependa wakwao ni mbaya kuliko mtu asiye amini! Yani ni bora  mpagani anaonekana mtakatifu mbele za Mungu kuliko yule anaye sema anamuamini Mungu wakati anachukia na kutojali wakwao! Kuna watu wengi sana tena wengine wapo mbele ya macho yetu kila siku baadhi yetu wanawachukulia kama "role model" wao bila kutafakari kwa kina kuhusu hao "role model" zao! Je,  umewahi kuwachunguza kama kweli wanapenda wakwao? Au ni watu wa 'mikakati' yani they have an hidden agenda ya kutaka kupata pesa kutoka kwa wazungu na sponsors wa mambo yao! Kama ni kusaidia je  umeshaona wakisaidia wakao? Au ndio wale watu ambao ndugu zao wote ni wa "mujini wenye pesa" ukiishi uswahili kwetu kule Keko wewe siyo ndugu yao hawakujui!! Uzalendo unaanzia nyumbani kwako kwani hata hao ndugu zako ni Watanzania hivyo ukiwasaidia unasaidia taifa la Tanzania. .............Binafsi naheshimu nakupanda  watu wenye tabia ya kutoa jasho lao na kusaidia watu bila kuomba au kubugudhi wengine. Mfano ni Mh. MO Dewji, ShyRose Bhanji, Dr. Ntuyabaliwe  Foundation, Rita Paulsen, Flaviana Matata Foundation, Kidoti na wengine. Sipendi mtu anayetaka kusaidia wengine kwa kulazimisha wengine wamchangie kwani kusaidia mtu ni ibada, hivyo ni siri ya mtu na Mungu wake. Usinielewe vibaya kuna kuchangia kwingine naunga mkono kabisa kama mambo ya cancer, shule, n.k (for special cause). Ninacho ongelea hapa ni kusaidia watu binafsi......... Anyway, napenda vile Mh. MO anavyo wajali watu wa kwao huko Singida mjini. Mfano mzuri wa kuwa uzalendo, unaanzia ndani ya nyumba yako!

Akin Akman inspirational: They call it pride, I call it class. Lions don’t mingle with cats.

They call it pride, I call it class. Lions don’t mingle with cats. No matter the economy of the jungle, lions will never eat grass. Respect everyone but never ever forget that you’re equally important. Be friendly to everyone but never try to be everybody’s friend. Be open but selective. If you flock with penguins, you will never fly like eagles. If you’re NOT being treated with love & respect, check your “price tag”. Perhaps you have marked yourself down. If you present yourself funny, people will treat you like a joke. No one can sit on your back if you’re standing on your feet. Sometimes where you stand determines how people values you in life, and the price you put on yourself determines your worth. Get off the “clearance rack” and get behind the GLASS where they keep all the “valuables and NEW ARRIVALS. Once you know your worth, how people values you becomes irrelevant. Akin Al-Ameen®™2017 . 

Augustine Mkude: Kile kipindi kigumu Cha maisha kilinijenga nifanye kazi zaidi na zaidi ili nisirudi nyuma


Sikiliza historia ya maisha ya mtanzania Augustine  Mkude ambaye anaishi hapa Marekani katika jiji la Houston, Texas Kama anavyojielezea kupitia show ya The Untold inayo ongozwa na mtangazaji mkongwe wa kimataifa Sunday Shomari!

Familia nyingi za kiafrika hulazimisha mambo yawe jinsi familia inataka bila kujua kila mtu Mungu amemuandikia safari yake kwa njia yake ya kipekee! Kitendo cha familia ya Augustine kukataa kumsaidia eti kwasababu amekataa kuwa Padri niseme kuwa ni hali halisi ya familia nyingi sana, nakwakweli si kizuri hata kidogo. Nafikiri Kuna haja ya kuelimisha jamii kuwa siyo kila mtu lazima aende Morogoro kwa kina Mkude kwa kupanda basi la Abood! Nasio wote watakao kwenda Morogoro kutoka Dar bila kushuka njiani au kupumzika. Just because my enroute is different from yours it doesn’t mean am in a wrong path!

I’m very impressed na huyu Augustine Mkunde. Anaoneka ni mtu mkarimu na mkweli. Wana Houston haya let support Mkunde, Safi sana! …….Hilo swala la kuulizwa “Do you speak English” hata mimi ilinikuta kwenye nursing home moja huko Michigan, sema mimi mgonjwa alisema  “Alpha can you speak English? this is America!” 😂😂😂😂 jamani niliishiwa nguvu nikabaki kucheka tu!…….Anywa, nimependa sana hii show. But mbona sehemu ya nne na ya tano hazipatikani kwa YouTube? Mara yakwanza nipo angalia like a week ago kulikuapo zote sasa leo nimetafuta wee wapi naona mwisho sehemu ya tatu! Vipi? Nataka ile sehemu ya Kilimanjaro connection bwana  😀😀 that was naked truth 🙈🙈

You see this lady!?! Don’t give up!

Zarinah Hassan: We have been created so different, the type of humans who can multi task

“There is so much in a woman that most people don’t know. We have been created so different, the type of humans who can multi task. A man can watch a game and not hear what one said while a woman can watch a movie and still hear, still know the stove is on, and so on (the list is endless). So here is to all the multi tasking women juggling through life as mothers, wives, momprenuers aka business women, caregivers and many more. You are appreciated! It’s all about knowing what comes 1st #prioritize. Salute🍾 help me tag one woman who inspires you. @lukambaofficial 📸” ——-Zarinah Hassan

RARE Magazine yatumia page mbili kuandika ‘Bio’ ya LB!

Kwakutumia social media accounts zake Linda Bezuidenhout alielezea furaha yake na kumshukuru Mungu kwa mibaraka hiyo kama unavyosomekahapa chini 👇 “Wow! Please zoom to read my bio and all the achievements Thanks to God Alhamdulilah 🙏🏾. My bio keeps growing we now need 2 pages to complete all the awards and achievements WOW! The RARE Magazine based in NY used 2 pages just for my bio and other pages for my designs….. please if you haven’t seen the cover of the magazine with an LB dress go to @linda_bezuidenhout_couture …soon we will add the resent events on our website which are among the major events we participated (LB COUTURE ) My Accolade Media Award and to showcase for 50 Shades Of Pink.
One more Amazing event to come for this year InshaAllah 🙏🏾 God Willing. Listen 👂 everybody Listen!! THANKS FOR YOUR LOVE AND SUPPORT. MashaAllah Bio yangu na matukio makubwa niliofanya ni mengi mpaka ina chukua kurasa mbili kwenye gazeti. Hilo kwenye gazeti kubwa sana la NY. Tukuio na tunzo niliopata za juzi juzi hatujaweka bado kwenye website … InshaAllah kuna tukio lingine kubwa moja kwa mwaka huu limebaki 🙏🏾. NAWASHUKURU KWA MAPENZI YENU NA SUPPORT YENU 🙏🏾” LB  Nami napenda kumpongeza sana Linda kwa mafanikio haya. Kweli Mungu si Athumani, nani alijua kuwa “Fundi cherehani” anaweza kutumia page mbili kuandikiwa Bio! Very inspiring! Ubarikiwe sanaaaaaa! 💪💪

A day in the life: Siku ya maisha yangu na Emelda Mwamanga

Emelda Mwamanga (Kushoto) pamoja na Dorothy Kipeja ambaye ndiye mmiliki wa show hii ya A day in the life

Wow! I’m super happy Bang Magazine is coming back!!! My wishes came true! Ni miezi michache iliyopita nilikuwa nauliza kuhusu Bang Magazine kama itarudi sokono (SomaHapa), na katika video hii fupi inayo onyesha maisha ya Mama / Mke / C.E.O / Entrepreneur lady / Motivational speaker and now what an Author?!  (ma’am this lady can do it all huh!! I only have this blog and can’t even keep up with it 😂😂🙈🙈)  Emelda Mwamanga ambaye ndiye mmiliki wa Bang Magazine ametamka kuwa Bang Magazine inarudi sokoni muda si mrefu! ………So happy for you Emelda! Nice show, good job! Love it!!

Jacqueline Mengi: Love is an act of endless forgiveness!

Nimeenda kuchungulia kwa Mrs Mengi nikakutana na picha nzuri sana zakwake na maneno Fulani amazing hivi, "love is an act of endless forgiveness"! Haya ni maneno rasmi aliyo yatamka Beyonce baada ya kumsamehe Jay Z kwenye ile "cheating scandle" nakusema kuwa amejifunza upendo ni tendo la kusamehe bila ukomo / kukoma! Dah! Haya maswala ya mapenzi namwachia Jacqueline na Dr Mengi wake maana site wengine tulishaga achana nayo  😂😂🙈🙈. 
Kuna mtu aliandika article akisema Beyonce amemsaidia sana kwa maneno yake hayo ............."The best part of the show is when Beyoncé gives us the quote about forgiveness.

Love is an act of endless forgiveness. Forgiveness is me giving up my right to hurt you for hurting me. Forgiveness is the final act of love” 

All this while getting shot in a wedding dress. Yes, shit gets THAT real.
We’ve all been there for before where we wanted to hurt the one we love because they hurt us. Why? Because no one can hurt you more than the ones you care for. They know you best and you feel so vulnerable to them.

It is a valuable lesson to be learned here. In order to sustain love, you have continuously BE love. You have to be willing to love through thick AND thin. It’s easy to stop loving once you’ve been hurt but as the late Maya Angelou once said, “Have enough courage to trust love one more time, and always one more time.”

If two people can put aside their ego and realize that mistakes will be made; and know that nothing worth having will come without HARD work to keep it, you can really have that ever lasting love you seek." ............unaweza soma article you kwa kubonyeza 👉👉 (LoveIsAnActOfEndlessForgiveness).  

“If you are happy with yourself it’s very easy for others to make you happy”JNM……….Umependeza sana! Super clean and beautiful!

Zamaradi Mketema: Usiangalie mawe kama SILAHA ukayakimbia ila badala yake yafanye ZANA katika kusimamisha himaya yako. MAWE yanasaidia KUJENGA!!

Sisi Binaadamu wengi ni watu tunaohofia MAWE, tunaishi katika hali ya kutafuta njia za kila aina za kukwepa kabisa kurushiwa na kuziba mianya yote itayoweza kutoa chakusema kwa adui zako kitu kinachopelekea kujikuta unaishi hadi maisha FAKE kwa kuhofia tu binaadamu, bila kufahamu mara nyingine ni vizuri kuyaacha yaje ili kujua yanatokea upande gani, yana sababu gani, yatakusaidia vipi na yatabadilisha nini pia kwenye maisha yako. Kwa upande wangu NIMECHAGUA kuyaokota na kujengea NYUMBA yangu, kila jiwe litakalorushwa kwangu nahakikisha siachi lipotee, nitaliokota na kuliongezea tu kwenye ujenzi wa nyumba yangu, hata kama lengo la mawe ni kuniumiza, nitahakikisha yananisaidia pia. Mawe ni BARAKA, mawe ni ongezo, na ni mafundisho pia. Tunajifunza mengi kupitia mawe yanayorushwa kwetu, tunakua zaidi, tunaimarika na kujijenga, tunafahamu nguvu tulizonazo na zaidi tunajifunza hata KUJIHADHARI Kupitia unavyonifikiria na kuyawaza juu yangu unafanya nijue nini natakiwa kufanya, unanifundisha wapi sitakiwi kuwepo nakadhalika, kiufupi UNANIAMSHA, na hata ule udhaifu unaohisi unaniumiza nao usichofahamu unanifundisha jinsi ya kuishi nao na zaidi kuufanyia kazi na kuufuta kabisa kama upo. Unaposema na kunisimanga juu ya jambo ni kunizindua juu ya jambo hilohilo hivyo kama lengo ni kukomoa unajikuta unafeli maana athari njema ulizoziacha utakuja kugundua ni nyingi kuliko zile mbaya ulizodhamiria.

Angalia kila jambo katika hali chanya na utaona faida yake, Usiangalie mawe kama SILAHA ukayakimbia ila badala yake yafanye ZANA katika kusimamisha himaya yako. MAWE yanasaidia KUJENGA!!

Better late than never!……Hongera sana Diamond!

 Japo karibia wiki inafika tangu ushindi huu upatikane -AFRIMMA 2017 Best Male East Africa hakuna ubaya kwa mimi kutoa pongezi kwa kuchelewa kwani wenzetu wanasema “better late than never”!……..Hongera sana Diamond hakika umeitangaza🇹🇿 Tanzania katika nafasi ya kipekee sana. Ubarikiwe zaidi ya hapa! We are all proud of you the former ” Tandale” boy!  #Viva Diamond #Viva Wasafi 🙌🙏

Flaviana Matata: The truth is that we can only unleash the power of young girls through access to quality and safe education.

“Today is #InternationalDayOfTheGirl and the focus is on the power of adolescent girl. The truth is that we can only unleash the power of young girls through access to quality and safe education. I am here with one of our scholars Nyamizi who is in her last year of high school. Young girls like Nyamizi have the potential to be scientists, teachers, farmers, artists, mothers, but that is only possible if they are provided with a conducive environment to thrive. @flavianamatatafoundation strongly believes that an educated girl will be a better mother that will nurture and raise her children to be better citizens. Educating a girl is a smart investment because it’s an investment into the prosperity of communities and nations. #FlavianaMatata”

Ridhiwani Kikwete: #sikuyamtotowakike; Huyu ni Binti yangu. Furaha yangu Ukamilika ninapomuona amefurahi

“#sikuyamtotowakike Huyu ni Binti yangu. Furaha yangu Ukamilika ninapomuona amefurahi. Namuona Mama,Namuona Mlezi, Najiona Mimi , Ninaiona Tanzania. Nakupenda sana Mwanangu.”~~~~~~ Mbunge. Ridhiwani Kikwete

Idriss Sultan: Unaweza ukawa loyal lakini usiwe blind!

Hii interview naona ilinipita ndio nimeiona leo!

Kwanza nianze kwa kusema hongera sana Idriss Sultan kwa kupata mkataba mzuri wa kuigiza nchini Marekani. Nakutakia mafanikio mema najua utatutoa kimaso maso!.......Unajua mimi nilionaga zile picha za jeshini nikajua kuwa ni mambo yako ya comedy! Kumbe ulienda JKT 🙈🙈

TRUST: Interview yako nimeipenda sana. Hasa somo la kuwa "Loyal but not blind"!! Nafikiri wengi inatuchukua muda kuelewa hilo mpaka yatakapo kutokea zaidi ya mara moja ndio somo linaanza kuingia. Mimi nasema ukiona rafiki yako hapendi maendeleo ya wengine kaa naye mbali! Ukiona rafiki yako haguswi na upotevu au huaribifu wa mali zako au pesa zako hata kama ni Shilingi moja  achana naye kabisa! Ukiona rafiki ambaye siku zote anataka utumie njia ambayo itakughalimu zaidi achana naye! Ukiona rafiki yako ni rafiki wa karibu sana na watu wanaopinga maendeleo yako (mwenye tabia ya kuuma na kupuliza) muogope huyo rafiki! Ukiona rafiki ambaye pesa ni muhimu kwake kuliko UTU mkimbie haraka sana! Watu wanamna hiyo siku zote siyo waungwana, na wala hawana utu! BE LOYAL BUT NOT BLIND!! Somo zuri sana! BETRAYAL: Asikudanye mtu, betrayal hurts! Inauma sana kwani betrayal involves emotions which are your feelings! Hisia zako ndizo zinakufanya wewe jinsi ulivyo, hivyo mtu anapo kugeuka kwa kusudi la kukuangamiza au kusudi lolote haina tofauti na mtu anayekuchoma kisu bila ganzi! Ndio maana wenzetu wanasema "you stab me in my back"........ Naona wewe upo kama mimi ni ngumu sana kwangu kuwa na rafiki ambaye ameni betray! Don't get me wrong, nitakusamehe, tutasalimiana tukionana, hata kucheka naweza cheka nawe lakini urafiki na wewe ni MWIKO!  "When people show you who they are believe them" ~~~ Maya Angelou

KUTHUBUTU: Pole sana kwa changamoto ulizo pitia, na pia hongera sana kwa kuto kukata tamaa. Naamini wengi tutajifunza kutoka kwako japo wengine tu wakubwa zako. Maisha ni somo endelefu ambalo unaweza lipata toka kwa mtu yoyote bila kujali umri! You have inspired me!

WEMA: Masikini, ninesikitika sana kumbe Wema alikuwa mjamzito? Tena twins!! Dah! Pole yake sana. Mungu atampa wengine muda ukifika. Nimependa the way you talk about her you didn't trash her at all! 

LIFESTYLE: Jamani wanawake 30÷÷ eeh! Hivi huu UKIMWI unachagua ama?! Gosh!! What about magonjwa yazinaa yasiotibika hamyaogopi?! I hope you will well behave huko Hollywood maana huko ndiko kuna jehanam ya magonjwa ya zinaa!! ...........Otherwise, Congratulations! 

 

Hongera sana Zamaradi Mketema!

 Alhamdulillah! Alhamdulillah! Alhamdulillah! Ndoa yenu idumu milele zote! Furaha amani na baraka zote za Mwenyezi Mungu zifuatane nanyi! Ubarikiwe uzao wenu vizazi na vizazi! Alhamdulillah! Though bado nashangaa what happened from 👉👉 “Umeniweza, Nimekuweza, Tumewezana” to the New “Sheriff” in town? What a difference 4 months can make!!Mkague mpenzi, kwa raha zako bibi! Hujaiba ni wako, privately owned by You! I mean you only siyo kama yule “shirika la UMMA”  Ugawaji, linagawa chakula kila mtaa 😀😀😀…………… Hongera sana!

“good things come to those who hustle” ~~~~~ Major General

 “Last thursday of the month, not sure what motivation is needed but I know i gotta put the past behind me and focus on the future…. good things come to those who hustle #WorkMode”~~~~Zari. a.k.a  Major General

Embu leo tumsikilize Yvonne Chaka Chaka!

Kumbe jina lake halisi ni Yvonne Machaka! Hilo Yvonne Chaka Chaka ni jina la kiusanii tu (stage name)!……. Embu msikilize anavyoelezea alipotokea kimuziki,  walivyo baguliwa kwasababu ni weusi, na jinsi baba yake alivyokuwa baba mwema anayejali familia yake!……super nice! Halafu nimekwenda kwa Instagram page yake nikakuta masaa 11 yaliyopita aliweka picha hii ambayo ni layout yakwakwe na Jokate na hayo maneno alioandika just melted my heart! What a super humble lady!

Happy birthday mama Salome!

Nyumba aliyokuwa anaishi mama Salome na watoto wake
"Maisha ya kila mwanadamu yana historia yake. Ndugu zangu ebu niwape history fupi wapi nimetoka 👀. Hapo ndipo alipokua anaishi Mama yetu. This is our House👌Jamani msinichukulie poa, sijakulia chips kuku mimi wala sausage 😀😀. Vitu hivi nimekuja kuvijulia ukubwani; so when I say let me enjoy my life, let me enjoy bwana kwasababu I really deserve it. Niko proud na tulipotoka 💪 na tulipo sasa, mimi ni mtoto wa kwanza katika family ya watoto wanne and my Mom ni Nurse. Sasa why huyu Mama ananitoa machozi?? niko proud nae sana tena sana. Huyu Mama ni mwanamke muhimu sana katika maisha siachi kusema Mungu mpe maisha marefu Mama yangu maana pamoja na hali yake hii amehakikisha wote sisi tumeenda shule💪alipambana na kila kitu ili sisi tukue.😭😭 Dah! nashindwa hata kuandika 😭....... Sasa basi Leo ni Birthday ya Mama yangu. Katika maisha yangu ya kawaida hii hali ya maisha yetu ilinisukuma sanaa tena sanaa mimi kufanya kazi kwa bidii maana nilijua mimi Ndio mkubwa nina wadogo zangu nyuma, kila siku nikawa napiga goti na kumwambia Mungu nisaidie nisikate tamaa katika biashara zangu. Nilitembeza nguo barabarani nilipita kila kona bila kuona aibu wala kujali nani ananicheka kumbe najua nini nafanya na nini nataka! Kuna vitu vingi nilitamani na nilikua na-dream navyo lakini kikubwa nilitamani na kumuomba Mungu amuweke mama yangu mpaka siku moja aje afurahi na kucheka katika maisha yake yote yaliyobaki mpaka anaingia kaburini 🎁 Imagine mama Nurse wa kawaida sana akiwa na watoto wanne lakini alitulea, kama single mama katika kila namna tusikose maihitaji ya muhimu.......... maisha yetu yamenisukuma sana kufanya kazi kwa bidii 💪 Mama, Mama, u deserve something 🙌....Can't wait 👀" ~~~~~~ Salome akielezea hisia zake

"Once again Happy Birthday mama yangu😍 as your first daughter sijui ni kitu gani cha kukupa ili uwe na furaha katika maisha yako yote na ukasahau machungu yote uliyopitia. Niliwaza sana nikupe nini mama yangu ?? Nikawa sipati jibu je nikupe Range Rover 😀😀😀 nikagundua Hapana! Nikawaza je nikununulie V8?? Nikasema No Kwani ni Sh ngapi hiyo???😀😀🏃🏻‍♀️🏃🏻‍♀️ basi nikasema ebu nikupe heshima unayodeserve katika maisha yako yote. Today I decide to give you the Gift of the New House.🎁🏠 Pumzika hapa Mama yangu enjoy maisha kipenzi chetu. Once Again Happy Birthday Mama Salome" ~~~~hayo ni maneno yake Salome

Mama yake Salome akimshukuru Mungu kwa mibaraka yake
Salome akilia kwa furaha huku mama yake mzazi (kushoto) pamoja na mama yake mkubwa (kulia) wakiwa sambamba naye
Mama Salome akiwa na watoto wake

Siwajui hawanijui lakini nimevutiwa na kuguswana story yao nikaona ni vyema ku share nanyi. ……….Happy birthday mama Salome. Nakutakia furaha zaidi, amani tele, na afya njema. Mzidi barikiwa. …….Hongera sana Salome!