Category Archives: Leadership

Tanzania oyee! #Hapa Kazi tu! #ACACIA

Huu ushindi wa kishindo kikuu ni wakufurahiwa, kushangiliwa, na kujivunia kwa kila Mtanzania mzalendo mwenye mapenzi mema na nchi yetu! Tanzania oyee! Napia nampongeza sana baba yangu Dr Mgufuli kwa kusimamia kidete alichokiamini kuwa ni haki yetu sisi Watanzania japo  alipata kebehi nyingi lakini hakubadili msimamo wake! Thank you Dad ake, you made us so proud! 💪💪 ………..Umeandika history kubwa sana katika uongozi wako na uzalendo kwa taifa lako! Ubarikiwe sana……… 

#Mungu ibariki Tanzania #Mungu ibariki Africa

Siku ya mtoto wa kike duniani: “Thamani ya Binti Na Uongozi wa Maadili”

“Thamani ya Binti Na Uongozi wa Maadili”  “Mcis Kelvin kutoka skonga kushoto Katikati ni Dada Glory kutoka @mwanamke_na_uongozi Mwisho ni @temidayo_gm Photo credits. @timesfmtz”

Siku ya mtoto wa kike duniani: Jokate awa mgeni rasmi shule ya Turiani, Magomeni, Dar!

 

Jokate Mwegelo ndie aliye kuwa Mgeni Rasmi siku ya leo ambayo ni siku ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani yaliyofanyika katika shule ya sekondary ya Turiani Magomeni. Alipata nafasi ya kuongea na wanafunzi wa kidato cha kwanza na tatu yaliyo andaliwa na taasisi ya @mwanamke_na_uongozi Iliyokuwa na kauli mbiu Thamani Ya Binti Na Uongozi Wa Maadili! “Walikuja kunitembelea, nikawaalika chakula tukala wote then tukapozi kwa picha 😃” J. Mwegelo

Hongera sana Waziri Angellah Jasmine Kairuki!

Naomba nichukue nafasi hii kumpongeza Waziri mpya wa Madini, Mh Angellah Jasmine Kairuki! .......Kama kumbukumbu zangu zipo sawa basi naamini wewe ndio Waziri wa KWANZA MWANAMKE aliyewahi kushika wizara hiyo nyeti! Naamini utendaji wako unatija kwa taifa letu la Tanzania ndio maana Rais Dr. John Pombe Magufuli pamoja na washauri wake wakaona ni vyema ukabidhiwe hiyo wizara. ........Nakutakia utendaji na uongozi mwema ukizidi kuweka maslahi ya taifa letu mbele. Hongera sanaaaaaa! #Mungu Ibariki Tanzania #Mungu Ibariki Africa

“Nimeyachagua Mawe kuliko laana ya Mungu.”~~~` RC, Paul Makonda

“Mti wenye matunda ulichoka kupigwa mawe ukaamua kutokuzaa matunda lakini Yesu alipoukuta mti hauna matunda akaulaani. Nimeyachagua Mawe kuliko laana ya Mungu.”

Hayo 👆ni maneno yake Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kupitia page yake ya Instagram akiwa ameambatanisha na hiyo 👆 picha!………Swali la kujiuliza: Nikwanini wakazi walio wengi wa Da er salaam bado wanamkubali Paul Makonda? Je, ni mtendaji mwema?! Au anabahati ya kupendwa na watu?! You be the judge……!

“jukumu kubwa la nchi za Afrika ni kuhakikisha zinaweka mazingira wezeshi ya kuwaendeleza wanawake katika nyanja zote.”~~~~Mh. Samia Suluhu

Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema jukumu kubwa la nchi za Afrika ni kuhakikisha zinaweka mazingira wezeshi ya kuwaendeleza wanawake katika nyanja zote.  Samia ameyasema hayo leo kwenye Uzinduzi wa Jukwaa la Kuwawezesha na Kuwaendeleza Wanawake Afrika lililoandaliwa na Asasi ya Graca Machel na kufanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es salaam. Makamu wa Rais alisema pamoja na kuwepo kwa jitihada mbalimbali za kuwaendeleza wanawake bado mazingira hayampi nafasi mwanamke haswa yule anayeishi kijijini. Aidha, aliainisha baadhi ya changamoto hizo kuwa ni pamoja na sheria na sera zilizopo ambazo bado zinawanyima wanawake fursa ya kumiliki ardhi pamoja na haki ya kurithi hata kama haki hizo zipo kisheria. “Hii inatokana na utekelezaji mbaya wa sheria, unaosababishwa na uwepo wa mianya ya ubaguzi kwenye kwenye sheria hizo jambo ambalo linakinzana na mfumo rasmi wa kisheria zilizowekwa,” alisema Makamu wa Rais. Aidha alisema “Inasikitisha kuona kuwa ni zaidi ya miaka 20 baada ya Ulingo wa Beijing; kukamilika kwa utekelezaji wa Malengo ya Milenia; pamoja na kuanza kwa utekelezaji wa Malengo mapya ya Maendeleo Endelevu ambapo kuna lengo la pekee linalosimamia masuala ya usawa na kuwawezesha wanawake na watoto wa kike, bado kuna baadhi wanawake miongoni mwetu ambao wapo kwenye lindi la umasikini, wanafanya kazi kwenye mazingira magumu; kupata kipato tofauti na wanaume kwa kazi sawa; kutokuwa na sauti ya kufanya maamuzi kwenye maisha yao wala maamuzi ya kisiasa; kutokuwa na fursa ya kumiliki na haki ya kurithi ardhi, kukosa huduma za mikopo, afya na elimu; Ingawa wamezingirwa na fursa tofauti na mazingira wezeshi bado wanawake wengi wa Afrika hawachukuliwi kuwa sawa na wenzao wa kiume mbele ya sheria. Alimalizia kwa kusema kuwa muda umefika sasa kwa wanawake kuwa mfano, Kuungana na kuinuana ilikuweza kumkomboa mwanamke wa Kiafrika na kuhakikisha hamna anayebaki nyuma kwenye fursa za maendeleo. . . ( Picha na Ofisi ya #MakamuWaRais )

***Copy & Paste from CloudsTV  Instagram  page***

Bodi ya TANLAP yamuaga Dr Judith Odunga!

Bodi ya chama cha msaada wa kisheria- TANLAP (Tanzania Network Of Legal Aide Providers) siku ya leo masaa ya Afrika Mashariki walikutana na kufanya sherehe fupi ya kumuaga aliyekuwa Mwenyekiti wao Dr. Judith Odunga na kumkaribisha Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo Dr. Helen Bisimba. Sherehe hiyo ilifanyika katika hotel ya Millennium Seashells, Dar es salaam, Tanzania........Hongera sana my aunt and shosti wangu Dr Judith Odunga. Tunakutakia retirement njema. Natunaimani kuwa Dr. Helen Basimba atafanya kazi nzuri kwa manufaa ya taifa letu nasio maslahi benafsi!
Dr. Judith Odunga (In white & black outfit) and Dr. Helen Bisimba in aqua blue outfit
The outgoing TANLAP Board Chairperson Dr. Judith Odunga (sitting second left) with the new chairperson Dr. Helen Bisimba (first left) and Christina Kamili (ED) plus other Board Members and TANLAP staff at a farewell party held at the Millennium Seashells Hotel, DSM.  

“We need to be able to tell our own story…….we need to rebrand Africa”~~~~Akon

 

Jamani msinicheke, yani mie my brain ipo very “selective” inapokuja kwenye vitu vya kusikiliza, kutazama, au kukaa…….. Ubongo wangu ukigoma kuwa that’s not for you, basi inatuma msg kwa  hisia / feelings zangu nazo zinagoma kabisaaaa! Ndio maana nasema msinicheke nikiwaambia kuwa leo hii ndio kwa mara ya kwanza namsikia huyu mwanamuziki maharufu aitwaye Akon  kwasababu ni nadra sana utanikuta nikisiliza  hiyo aina ya music anayo imba! Hivi unajua sijui hata wimbo mmoja wa Kanye West 🙈🙈 at least Jaz najua ule wa “All I need in this life of sin its me and my girlfriend” 😅😅 Sasa kama na wewe ni kama mimi ngoja nikwambie kwa kifupi tu kuwa Akon ni mwanamuziki Mmarekani ambaye asili yake anatoka Senegal. Alizaliwa Marekani, wakarudi Senegal na wazazi wake mpaka alipofika umri wa miaka 7 akaridu U.S.A tena. Lakini pamoja na kuwa maisha yake yamekuwa hapa U.S.A roho yake bado ipo Africa na anataka tuitengeneze Africa yetu iwe kama mataifa hayo makubwa kwani inawezekana. Na jambo kuu la kwanza ni kuanza ku “rebrand” Africa kwa kutumia Waafrica, kulingana na maadili yetu, matamanio yetu, na mtazamo wetu! ………..tafadhali msikilize vizuri kwenye hii video 👇 kama lugha ni changamoto basi tafuta mtu akusaidie kukueleza…………. kusoma zaidi juu yake na malengo yake nenda 👉👉 (Akon_Africa)

Mama Salma Kikwete umekosea sana! Hiyo inaitwa institutionalized discrimination!

Mama yangu, ninacho jaribu kukwambia ni kwamba fungua macho yako utazame hii hoja yenu kwa macho mapana utaona jinsi gani imejaa ubaguzi na unyanyapaaji wa hali ya juu kwa mabinti wanao pata mimba wakiwa shuleni! Kama mmeamua kufukuza shule wanafunzi basi mfukuze wote wanaofanya ngono wakike na wakiume kwa ujumla wao na siyo kubagua wanaopata mimba tu! Hivi mama Salma, kweli unataka kusimama hapa na kuiambia dunia, mbele za Mungu kuwa huyu binti yako mwenye gauni jeusi bado ni bikira?! Au kwasababu hajapata mimba kwahiyo unamuona mtakatifu?!! Kumbuka kabla ya kutunyooshea kidole sisi hakikisha kucha zako ni safi! Maana lazima tutazikagua!! Hizi sheria mnazoziweka bila kutafakari madhara yake katika jamii ipo siku damu zenu zitazilipa tu! Yawezekana leo hii haitamkuta binti yako lakini huenda kesho yakamkuta mjukuu wako! Oh! Nimekumbuka nyie ni “high profile” people, you do “high profile crimes” bila sisi walalahoi kujua, mama kumbuka Mungu anawaona!!

Kumnyima mtoto yoyote haki ya ku-access education ni kinyume na haki za binadamu. Kwani kupata elimu ni haki ya msingi ya binadamu wote! Wanafunzi wanaopata mimba wanatakiwa waachwe waendelee na masomo yao kama kawaida bila kubaguliwa na mtu yoyote yule. Kama hiyo ni ngumu basi wapewe “sick leave” wakisha jifungua waendelee na masomo yao.  Au kama hizo mimba zinawakera sana basi wafungulieni Abortion clinics ili wawe wanakwenda kuzi-abort huko, labda roho zenu zitafurahia!!

Kumbuka kuwa unapomnyima mama moja  haki ya kuelimika inamaana unatengeneza jamii / community ya watu wasio na muelekeo wa maisha na kuendeleza mila ambazo hazina tija kwa taifa! Mama ndio nguzo za familia nyingi haswa Africa. Hakuna njia mbadala katika hili swala zaidi ya kuwaacha waendelee na masomo yao bila ubaguzi wowote ule kwa faida zao binafsi, vizazi vyao, na taifa kwa ujumla!

Ngoja nimalizie kwa kusema kuwa, tatizo wazazi wengi wa Africa wanataka waonekane kuwa wao ni malaika hawajawahi fanya mistakes yoyote ile maishani mwao! Ndio maana wako guilty na busy kuwahukumu watoto kwa kuwapa adhabu za ajabu ajabu badala ya kuwaelekeza juu ya maisha. Unajua yale mambo ya kila mzazi anajifanya alipata ‘A’ darasani, alikuwa wakwanza siku zote, na kila mwanamke aliolewa akiwa bikira! Just a bunch of nonsense (Excuse my language)!. Uongo mwingi kwa watoto zenu bila sababu yoyote ya msingi!  Btw, hii ni karne ya 21, mama yangu where have you been?! Unaona statistics za dunia zinavyo kwambia yani karne hii wazazi nmnatakiwa kuongea na watoto / wajukuu zenu juu ya sex / elimu ya kujamiiana kabla ya miaka 10! Kwani watoto wa miaka 10 siku hizi wako sexually active na wengine wanabeba mimba! How? I don’t know usiniulize mimi lakini hiyo ndio hali halisi ya sasa, just get with the program mama!!

CHADEMA HAINA HATI MILIKI YA KUWA UPINZANI PEKEE NCHINI. -Peter Sarungi

 Nilipokuwa natafakari maamuzi ya kwenda kugombea Spika wa bunge niligundua kuwa kama wewe ni mchezaji mzuri wa mpira wa miguu na unajiamini basi si lazima usajiliwe na timu kubwa kama Simba, Yanga ana Azam ili ucheze ligi kuu, kumbe unaweza kucheza ligi kuu hata kupitia Mbao Fc, Ndanda Fc, majimaji au hata Costal Union. Kinachotakiwa ni siku timu yako ikikutana na Simba ama Yanga hakikisha unafunga walau goli moja tu hata kama wao wataifunga timu yako kwa magoli 10. Hilo goli lako wataondoka nalo likiwa na jina lako. Hii ni bora zaidi kuliko kusajiliwa Simba ama Yanga halafu ukakaa benchi kwa sababu wachezaji ni wengi. Nchi yetu ni nchi ya demokrasia na nchi yenye kufunya siasa ya vyama vingi. Kuwepo kwa wingi wa vyama vya siasa ni moja ya tendo la demokrasia tunayo ikubali kila siku. Tanzania kuna vyama vya siasa zaidi ya 25 vyenye usajili wa kudumu vinavyo ruhusiwa kushiriki katika siasa zote za nchi. Ni kwa bahati mbaya Chama tawala hakijawahi kupoteza kushika dola huku vyama vya upinzani viki badilika badilika katika kuwa na wafuasi na nguvu za kisiasa hadi kupewa kijiti cha kuitwa chama kikuu cha upinzani. TLP, NCCR Mageuzi na CUF zimewahi kuwa na nguvu katika chaguzi zilizopita na kuwa chama kikuu cha upinzani wakati huo vyama kama Chadema Tanzania vilikuwa vipo chini sana na vilikuwa havijulikani kwa Watanzania walio wengi. 

Leo Bunge la Tanzania lina vyama 5 vyenye uwakilishi Bungeni huku CHADEMA kupitia muunganiko wa UKAWA wakiwa ni chama kikuu cha upinzani. Ukawa inabebwa na wabunge kutoka CUF, CDM na NCCR huku ACT ikiwa iko peke yake lakini katima kapu la upinzani ikiwa na haki zote kikatiba na hata kwa sheria za uchaguzi na za bunge.

Kumetokea taharuki kidogo juu ya nafasi za wabunge wa Afrika Mashariki hasa kwa upande wa vyama vya upinzani. Mnyukano ulikuwa ni kati ya UKAWA na ACT wazalendo juu ya nafasi 3 za upinzani. Mnyukano huo umeendelea hadi yalipo patikana maamuzi kutoka kwa Speaker juu ya mgawanyo.

Kilicho nisikitisha katika mnyukano huo wa hoja ni baadhi ya makada wa CDM kwa makusudi ama kwa kutojua kuhamisha mjadala wa kibunge na kuuweka kwa wananchi huku wakitoa lawama, matusi, kejeli na hata dharau kwa hoja iliyo tolewa na ACT kupitia mwakilishi wake Mh. Zitto Zuber Kabwe iliyotaka ACT wapate nafasi ya kugombea ubunge wa Afrika Mashariki. 

ZZK ametukanwa sana na baadhi ya makada wa mtandaoni wa CDM huku wakiamini wao ndio wapinzani pekee walio teuliwa na Mungu kuja kuwasemea watanzania. Mimi niwakumbushe tu makada wa CDM kwamba hata wao walikuwa kama mchicha kipindi CUF wakiwa Upinzani imara, Pia wakumbuke hata wao hawana HATI MILIKI ya kuwa UPINZANI pekee nchini. Wasikasirike, kubeza na kupinga wanapoona mbegu zingine za upinzani zinapo chepua kwa kasi, ipo siku mtahitaji ushirika wao ili kufikia malengo yenu.

By the way, inasemekana hata mgogoro wa CUF unawafurahisha sana CDM kuliko CCM, Maana wapo tayari na wamefungua milango kwaajili ya kuwasajili akina Seifu, Mtatiro na wengine pindi chama hicho kikifutwa kama alivyo sema Lissu kwenye mahojiano ya Azam… Daah kufa kufaana.

Msijisahau mkalewa kwa sifa na ubinafsi, ni kweli umoja ni nguvu lakini ni umoja wenye maslahi sawiha ulio Imara na wenye Nguvu.

Wasalam.

SIASA ZENYE MLENGO WA UCHUMI. -Peter Sarungi

SIASA ZENYE MLENGO WA UCHUMI.

Peter Sarungi (The next time)

Kuna Siasa za kuegemea uchumi (Political Economy), Siasa za kisayansi (Political Science) na Siasa za Kisanii (Political Art).

Hizi aina zote zina faida na hasara zake na kila moja ina nafasi yake katika kustawisha jamii.

Nimegundua kuwa serikali ya JPM inafanya siasa zenye kuegemea uchumi. Nasema hayo kutokana na budget ya sasa inayoonesha vipaumbele vya utawala huu ni vile vinavyo chochea uchumi ikiwa ni sector ya usafirishaji na miundo mbinu. Tunaona budget ikitupilia mbali miradi mipya ya afya, elimu, michezo, kilimo, viwanda, maji, umeme, utalii, uvuvi, ajira na kukuza sector binafsi. Budget imeweka mkazo kwenye Ujenzi, Ujenzi,Ujenzi pamoja na ununuzi wa ndege.

Kwa budget hii, fedha nyingi bado zitakwenda kwa wageni ambao watahusika na ukandarasi wa ujenzi wa Reli inayokusudiwa, ujenzi wa fly overs zinazokusudiwa na kampuni ya kutengeneza ndege. Kwa maana hiyo bado pesa haitakuwepo kwenye mzunguko wa ndani wa fedha, matokeo yake ni UKATA, UKATA. 

Aina hii ya siasa ina faida ya kukuza uchumi wa nchi na serikali yake baada ya mda wa miaka 3 na kuendelea. Serikali inakuwa na uchumi mzuri kuliko sector binafsi, Serikali inakuwa imejiingiza katika kushikilia vyanzo vya kuendesha uchumi. Ubaya wa aina hii ya siasa ni wananchi kudhoofika kiuchumi kiasi kwamba wanakuwa tegemezi kwa kila kitu kwa serikali yao. Tatizo lingine ni kwa serikali kuwa na tabia ya  kujiondoa katika kusimamia na kuendeleza miradi yenye kutoa huduma za jamii kwa wananchi wake, hili ni Tatizo kubwa sana mbeleni.

PIGO KWA JAMII YA WALEMAVU! R.I.P Mh. Dr Macha

Jamii ya watu wenye ulemavu imesikitika sana kupokea taarifa za msiba wa mama yetu na mtetezi wetu aliyekuwa anatuwakilisha bungeni kama mbunge viti maalum wanawake kwa upande wa walemavu Mh. Dr. Elly Macha kupitia Chadema Tanzania. Dr. Macha amefariki dunia akiwa nchini Uingereza kwenye Matibabu.

Binafsi mara ya mwisho kuonana na huyu mtetezi ni mwaka 2015 nilipokuwa naomba fursa ya kuwa spika, maneno yake yalinipa nguvu na sababu za kuendelea kutetea jamii ya walemavu katika nchi na hata kimataifa. Aliamini mabadiliko ya kuikomboa jamii ya walemavu yatapatikana kupitia walemavu wenyewe na ikiwa watashiriki katika vyombo vya maamuzi kama bunge, mahakama na hata ndani ya serikali. Bado naamini katika maneno yake na yataendelea kuishi na ipo siku yatatimizwa na walemavu wenyewe. 

Peter Sarungi (The next time)

Natoa pole kwa familia yake,jamii ya watu wenye ulemavu, ndugu, jamaa, marafiki, viongozi na wapenzi wote wa CHADEMA kwa kumpoteza mama yetu tuliye mpenda lakini Mungu amempenda zaidi yetu. Tuwe wavumilivu na wenye matumaini katika kipindi hiki kigumu huku tukiamini ipo siku tuta onana naye.

Amen  Nami naomba nitoe salamu zangu za pole nyingi sana kwa wana familia, ndugu, jamaa, marafiki, pamoja na jukwaa zima la walemavu Tanzania na duniani kote! Taifa limepoteza msomi mmoja ambaye pengo lake halito zibika!

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake libarikiwe!……. R.I.P Mh. Dr. Macha

KATAZO LA KUSAFIRISHA MCHANGA WA DHAHABU-2 -Peter Sarungi

KATAZO LA KUSAFIRISHA MCHANGA WA DHAHABU 2

Peter Sarungi (The next time)

Sehemu ya II – Ijue Sector ya Madini Tz

Sector ya madili ilianza kutambulika rasmi wakati wa utawala wa awamu ya tatu chini ya Raisi mstaafu Mh. Ben Mkapa kupitia sera ya uwekezaji. Mh. Mkapa aliamini maendeleo ya nchi yatasaidiwa ikiwa tuta ruhusu uwekezaji mbalimbali ikiwemo sector ya madili. Aliamini nchi itafaidika kwa kupata teknolojia mpya, mitaji mikubwa, elimu mpya katika sector hiyo pamoja na kuongeza ajira kwa wananchi na mapato ya serikali. Wawekezaji wakubwa walianza kujitokeza mwaka 2001 Geita na Kahama. Madini yanayopatikana nchi ni mengi kwa aina tofauti kama vile dhahabu, almasi, ruby, Tanzanite, Copper, Silver na mengine mengi ingawa zaidi ya 80% ya machimbo nchini yanajihusisha na uchimbaji wa madini ya Dhahabu. 

UZALISHAJI WA DHAHABU

Mpaka sasa tuna machimbo makubwa ya dhahabu yapatayo sita ambayo ni Bulyanhulu(BGM), Geita(GGM), Buzwagi(BZGM), Biharamulo, North Mara na New Luika. Kwa mwaka migodi hii huzalisha 1.37Million troy ounce ambayo ni zaidi ya kilogram 50,600 ya dhahabu safi kwa mwaka huku GGM ikiongoza kwa uzalishaji wa 38.6% na ya mwisho ikizalisha 1.5%. Kwa viwango hivi, Dhahabu inachangia zaidi ya 90% ya uzalishaji wa madini yote inchini kwa mwaka.

               NJIA ZA UZALISHAJI

Uzalishaji wa dhahabu upo wa aina mbili maarufu ingawa kuna nyingine ya tatu, aina hizi zinatokana na utofauti wa miamba ambayo dhahabu hupatikana. Kuna miamba ambayo ina oxide na zingine zina sulphide.

Dhahabu inayopatikana katika Miamba yenye oxide ina zalishwa kupitia njia za gravity na Cabon process (cabon in loucher CIL na cabon in pulmp CIP). Njia hizi ni common na zipo nyingi katika migodi yetu hadi kwa wachimbaji wa kati. Migodi yenye miamba ya oxide inayotumia njia hii ni nne kati ya zile sita yaani GGM, North Mara, Biharamulo na New Luika. Hivyo uzalishaji katika migodi hii hufanyika na kumalizika ndani ya nchi. Migodi hii haisafirishi mchanga kwenda nje.

Dhahabu inayopatikana katika miamba yenye sulphide ina zalishwa kupitia njia ya gravity, caborn process na kuhitimishwa na smelter. Njia za gravity na Carbon process huzaliza 40% pekee huku smelter ikizalisha 60% ya dhahabu. Dhahabu inayopatikana katika miamba yenye sulphide ina ugumu wa kunyonywa kupitia njia zilizopo nchini kutokana na dhahabu hiyo kuungana na madini mengine ya copper na silver, hivyo ili kuitoa dhahabu hiyo ni lazima uwe na tanuru kubwa (smelter) lenye uwezo wa kuyetenganisha madini hayo kutokana na utofauti wa melting point za madini hayo. Hivyo ni lazima mchanga unaozalishwa baada ya mchujo kwa njia za kwanza usafirishwe kwenda nje kwaajili ya kuzalisha 60% iliyobaki. Migodi yenye miamba yenye sulphide inayotumia njia hizi zipo 2 kati ya sita nazo ni BGM na BZGM. Migodi hii ndioyo husafirisha mchanga kwenda china na japan 🇯🇵 kwaajili ya uchenjuaji.

Mpaka hapo kama kuna swali unaweza kuuliza kabla sijakwenda mbele zaidi. Uliza ndani ya maelezo hayo, usitoke nje maana bado kuna makala nyingi zinakuja

Asanteni.

KATAZO LA KUSAFIRISHA MCHANGA WA DHAHABU -Peter Sarungi

KATAZO LA KUSAFIRISHA MCHANGA WA DHAHABU

Peter Sarungi (The next time)

Sehemu ya I – Utangulizi

Mkuu wa Kaya ali ahidi kusimamia sector ya madini kwa umakini ili sector hiyo iweze kuleta tija na faida kwa Taifa. Hivyo serikali ya Mkuu wa kaya imezuia usafirijashi wa mchanga wa dhahabu kwa makampuni ya uchimbaji yaliyopo nchini kwa muda usio julikana.

Lengo la zuio hilo lililotokana na kauli za mkuu wa kaya ni kuhakikisha serikali ina ondoa mianya ya kuibiwa madini hayo ambayo yana chujwa nje ya nchi huku sisi tukipewa mrejesho ambao kwa hisia za mkuu wa kaya anao mrejesho bado una ukakasi. Lakini pia mkuu wa kaya alitamani kabla ya kuwa Mkuu na anaendelea kutamani kujengwa kwa hilo Tanuru kubwa la kuchuja dhahabu, shaba na copper hapa Tanzania ili kufikia ndoto za kuwa na Tanzania ya Viwanda.

Pamoja na dhamira njema ya mkuu wa kaya, ni vizuri na sisi watanzania tukajua kinachoendelea katika sector hii ili tupate kujua faida na hasara za zuio hili ikiwa ni pamoja na changamoto za kufikia shauku la mkuu wa kaya la kuwa na Tanuru hilo lijulikanalo kama Copper Concetrate Smelter  Hivyo nita toa makala ya kueleza hali halisi za sector hii ikiwa ni sehemu ya kwanza na makala nyingine ya kueleza faida, hasara na changamoto ya kufikia ndoto ya mkuu wa kaya ya kuwa na Tanuru la kuchuja madini hayo Tanzania.

Nitatumia vikao mbalimbali nilivyoweza kuudhuria vya wataalum wa madini, ripoti mbalimbali kutoka TMAA na machapisho mbalimbali ya kimataifa kama vyanzo vya habari katika kusapoti andiko langu.

Asanteni

“Republicans and their “pipe dream” of appealing and replacing Obamacare.” – Chege Kilahala

Republicans and their “pipe dream” of appealing and replacing Obamacare…….

If you can’t marshal enough votes in a house (the congress) where you have a comfortable majority. Then your chance of passing it the senate where you have a very thin majority is non-existent…..

Now, we can toast and celebrate that, Obamacare is the law of the land….and it will carry on being so…….I look forward to seeing a universal healthcare system in the USA; one day soon. Just like whats found in Canada and Scandinavian countries….

UKIMWINDA SANA MJUSI ANAGEUKA NYOKA. -Peter Sarungi

UKIMWINDA SANA MJUSI ANAGEUKA NYOKA. 

Peter Sarungi (The next time)

Huu ni msemo wa wahenga ambao uhalisia wake unaonekana mara chache porini lakini hutokea sana kwa maisha ya binadamu. Naamini kuna watu walisha wahi kumwinda mjusi kipindi walipokuwa watoto na katika kumwinda mjusi gafla walipo toa jiwe wakakutana na nyoka, inapofika hapo lazima hali ya hatari itatokea.

Naiona nchi yangu kwa mbali inakaribisha hali ya hatari. Mkuu wa kaya alianza kuongoza nchi yake kwa misingi ya sheria huku akijitambulisha kuwa yeyeni mkali kwa maneno na matendo yake. Baada ya kuwa mkali sana watoto wakaanza kulalamika huku wakionesha kuto ridhika na maamuzi ya baba. Watoto wakaanza kumwinda baba kwa vifungu vya sheria huku wakimtangaza baba kuwa ni dikteta. Na kwa jinsi baba alivyo na msimamo, hakuwahi kurekebisha makosa yake hasa yale yaliyovunja sheria na hata kuonesha upendeleo wa wazi wazi huku akiwagawa watoto wake kwa kauli na matendo.

Kwa sasa hali imekuwa mbaya maana watoto wameanza kumkana baba yao kwa kutumia mama yao Katiba. Wana mshawishi mama yao (Katiba) awaoneshe baba mwingine kwa kutamka kuwa huyu sio baba mzazi na wamtafute baba mwingine.

Kwa hatua ya mawindo yalipo fikia,  nawaona watoto wanahisi wanaye  mwinda ana fanana na Mjusi hivyo wanaongeza jitiada za makusudi wakiamini nguvu za mjisi zipo mkiani na wala sio nguvu za kuogopesha kiasi cha kutaka kumtoa kwenye pango lake.

Lakini nahofia sana hasira za baba, baba akikasirika na kuamua kutumia nguvu zake basi anaweza akawalazimisha watoto kuendelea kuitwa baba kwa kumtishia mama na hata kuwa adhibu vikali watoto wanao kwenda naye kinyume, na akiona bado anapingwa basi anaweza kumbadili mama mwingine na kufunga ndoa ya kudumu. Kwa hatua hii, baba hatakuwa tena mjusi bali atakuwa ni nyoka.

Kwa sasa watoto wajiandae kukutana na nyoka katika mawindo yao, wasidhani wataendelea kukutana na mjusi walie mzoea kumwinda. Wajiandae na plan B,C na hata C ya kukutana na Nyoka.

By the way baba amesha geuza kichwa bado mkia wa nyoka tu aanze mashambulizi kwa watoto wanao winda. 

“Be careful and watch it” Mkuu wa kaya 24/3/2017