Category Archives: Leadership

Mama Salma Kikwete ndani timu ya netball!

Mama yetu kipenzi mama Salma Kikwete ndani ya kivazi mwanana kabisa teyari kwa kuingia uwanjani kucheza mashindano  ya netball za timu za Wabunge wa Africa Mashariki hapo juzi kati! Inapendeza sana, inavutia, na kutia moyo wanawake wengine na mabinti unapo ona powerful figure Kama mama yetu hapo akijishusha kwa unyenyekevu na kufurahia maisha na watu wengine! Safi sana na hongera nyingi mama yetu!………… Mwaka jana naye Dr. AshaRose Migiro alituonyesha ujuzi wake wakupiga dana dana  tazama ?? BigUpDrAshaRoseMigiro

Mhe. Anna Mghwira rasmi ndani ya Chama Cha Mapinduzi!

Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira mara baada ya kutangaza kuhamia Chama cha Mapinduzi CCM katika mkutano wa tisa wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.

Hatimaye yametimia! Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira ahamia rasmi CCM! Apokelewa kwa shamgwe na heshima zote mbele ya Mama wa Taifa mama Maria Nyerere!…….. Mimi siyo mwanachama wa chama chochote cha siasa lakini kama nikiambiwa nichague chama basi CCM kitakuwa chama changu siku zote! Yani ni kama leo hii mtu niambie nichague dini au dhehebu, jibu langu litakuwa mimi ni Mkristo wa dhehebu la Kisabato! Nitakuwa Msabato mpaka siku nakufa!  Hayo ni mawazo yangu na msimamo wangu kama yanakukwaza sorry but no sorry! …..Hivyo namtakia kheri Mhe. Anna Mghwira katika kutekeleza kazi ya ujenzi wa taifa kwa kupitia ilani ya CCM!

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira mara baada ya kuhamia rasmi katika Chama cha Mapinduzi CCM katika mkutano wa wa tisa wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.

***picha na caption zote kwa hisani ya IssaMichuziblog***

Kila kitu ni siasa!! Nani alituroga sisi?!

Mambo kama haya ndio yamenifanya nichukue siasa kwani ili uwe mwanasiasa lazima uwe muongo na upungukiwe na ubinadamu kidogo! Usichanganye, nimeongolea “siasa” sio “uongozi”! Kuna tofauti ya viongozi na wana siasa. Tatizo la Africa haswa Tanzania kuwa kiongozi unajikuta unalazimika kupitia siasa! Tuna baadhi ya viongozi wazuri sana ila wanashindwa kutekeleza majukumu yao kwani kila kitu kinahusishwa na siasa! Mbaya zaidi ni pale siasa inapo ingizwa kwenye mambo ambayo yanahatarisha uhai wa binadamu na watu wanaona ni sawa!! Katuroga nani sisi?! ……..Mimi nasema imefika wakati wa wanawake kuongoza ngazi zote hadi urais kwani hawa wanaume wana roho za paka!! Just unbelievable!!! “Nyufa kwenye hosteli za UDSM: Wahandisi na wataalamu wengine wa majengo wafanye ukaguzi na kuchukua hatua stahiki. Ni vyema hili jambo lisichukuliwe kisiasa. ”  Mhe ShyRose Bhanji

Alberto Msando: Ni suala la muda tu UKWELI utajulikana.

Repost from @albertomsando – @wemasepetu  

We spoke and I repeat “watakutukana, watajaribu kukudhalilisha, watatumia nguvu kubwa kuonyesha hufai, watakuombea mabaya, watatamani uanguke, watapenda uwe mnyonge. Ila UKWELI wanaujua”. Ni suala la muda tu UKWELI utajulikana. Muda ni kila kitu. Maamuzi haya ni sahihi. Na yeyote ambaye anakujali wewe kama rafiki ataelewa. Ni maisha yako. Ni kesho yako. Ni Tanzania yako. @wemasepetu #ForThoseWhoLoveToHate #HayaWataanzaUongoWao #MaamuziBinafsi #NaBado #Sindano #MaumivuYaKichwa #KuwaNgaziSasaBasi #TheDon @hpolepole #SheIsBack

 Haya hayo Ni maneno yake Mwanasheria kijana, msomi wa kuaminika na mataifa yote Mhe. Alberto Msando akimpa nguvu mrembo wetu Wema Sepetu ya kusimamia maamuzi mazito aliyo yafanya!

Wema Sepetu: Peace of mind is everything for me

“Siwezi Kuendelea kuishi kwenye Nyumba inayo nikosesha amani… Peace of mind is everything for me… Natangaza Rasmi kuondoka Chadema na Kurudi Nyumbani…. #ThereIsNoPlaceLikeHome… Feels good to be Back…

“Wow! Kwaniaba ya mdogo wangu kipenzi Magreth Otieno Olung’a Igogo ambaye ni mmoja wa mashabiki wakubwa wa Wema Sepetu na pia ni mwanachama muaminifu wa CCM naomba nichukue fursa hii kumkaribisha our Tanzania Sweetheart #nyumbani! CCM oyeeeeeee! Kidumu chama ???? O’Lord of Mercy!!…….Honestly, nampongeza sana Wema kwa maamuzi haya. Huwezi kuwa na amani kwenye chama ambacho Mwenyekiti wake amekutaka kimapenzi! Ndio maana hata amabavyo hujaenda kumuona uncle wako Mhe. Tundu Lissu mie sijashangaa kwani nilijua ni ngumu sana kwako kuonana na Freeman Mbowe uso kwa uso! Nafikiri it’s high time kwa wanawake kushika uongozi kwani hawa wanaume wanatuchanganyia habari tuu! Hongera sana Wema  ???  BTW, hivi mnajua jinsi gani mdogo wangu alikuwa anachukia niki mpost Zari humu zaidi ya Wema? Hahahaha! Haya Sasa nitakuwa na balance lol!

Jokate Mwegelo: Magufuli na kisa cha Mussa na Wana wa Israeli

Magufuli na kisa cha Mussa na Wana wa Israeli  

Jokate Mwegelo akiwa shule ya Msingi Mugabe

Musa alipitia vitu vingi ikiwemo kejeli, kujaribiwa na hatimae kufanikiwa kuwavusha Wana wa Israeli kuelekea nchi ya ahadi. Lakini kuna wakati wafuasi wake hao walipojaribiwa kidogo tu wakaanza kunung’unika na kumkebehi Musa kwamba ni kheri maisha waliyokuwa wanaishi Misri kwa Farao.

Rais John Pombe Magufuli ameianza safari yake nyingine baada ya Novemba 5 mwaka huu kufikisha miaka miwili madarakani. Napenda kuifananisha safari yake hiyo iliyosheheni mageuzi makubwa sawa na ile ya Wana wa Israeli walipokombolewa na Nabii Musa kutoka kwenye mikono ya utumwa chini ya Farao wa Misri. Uwajibikaji, Uzalendo, Utendaji

Kumekuwa na tatizo tatizo la watumishi wa Serikali kutokuheshimu misingi ya kazi zao katika utumishi wao wa umma, nidhamu ya kazi ilikuwa haipo. Ilifikia wakati watu walitunga safari za nje ilimradi tu wapate posho za kujiendeleza wao na familia zao.

Uzalendo wa nchi ukageuka kuwa uzalendo unaokimu mtu na familia yake na watu wake wa karibu. Fedha nyingi zikawa zinapotea angani na hata matunda ya safari tulikuwa hatuyaoni. Bado barabara na miundimbinu muhimu ilikuwa kasi yake ya kuimarishwa haikuwa nzuri sana.

Utendaji na ubunifu ulikuwa wa chini kwani hakukuwa na kitu kipya katika utendaji wa kazi kwa wengi zaidi ya kujitajirisha kupitia kodi za wananchi bila sababu zozote zile za msingi. Manung’uniko yalikuwa mengi juu ya rasilimali za taifa. Kulikuwa na makundi mengi yakizungumza kwa lawama namna rasilimali zilikuwa zinatumika vibaya. Makundi haya yakihusisha Wanasiasa, Wasomi na hata baadhi ya Wananchi wenye kufuatilia maslahi na rasilimali za taifa. Nchi yetu pendwa ya Tanzania ‘kuibiwa’ umekuwa ni mjadala wa muda mrefu bila utatuzi au hatua yoyote kuchukulliwa.

Kuna wakati, nikiamini kwa nia njema na uchungu wa nchi yao na si siasa, baadhi ya wanasiasa walipaza sauti kusema kuwa ni aibu kubwa kwa nchi yetu kushindwa hata kumiliki ndege yetu. Walihoji: “Tutatangazaje utalii bila ya kuwa na ndege yetu?” Kwa ufupi kila kitu kilikuwa kikionekana kwenda sivyo. Na hapa sijagusia issue ya “mafisadi”

Kuingia kwa Magufuli madarakani miaka miwili iliyopita, ukiyatazama maisha yake, utakubaliana nami kuwa huyu ni kiongozi anayeishi na kujituma kwa ajili ya maslahi ya wananchi. Hii inanikumbusha nilipokuwa masomoni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam miaka kadhaa ya nyuma, niliwahi kumuona Rais wetu ambaye kipindi kile alikuwa ni Waziri akila sehemu mmoja wanafunzi katika kijiwe maarufu cha misosi kiitwacho “Harvard”.

Pale chakula ni cha bei ya chini kabisa, mlo kamili mzuri ulikuwa hauzidi elfu 1000. Ilikuwa ni sehemu ya sisi wanafunzi wa kawaida kula kwa sababu ya bajeti zetu ndogo. Kumuona yeye kama waziri pale kulipelekea mimi kuanza kuelewa Dkt. Magufuli ni mtu wa aina gani. Ni wazi kwamba ni mtu wa watu, hana makuu, hajikwezi na anapenda “ku-budget.”   Mageuzi na Mabadiliko

Sishangai miaka miwili tu ya uongozi wake akiwa ameacha tayari alama na mageuzi makubwa ya kukumbukwa. Kwa kifupi tu ametenda yafuatayo ya kukumbukwa:

· Kuwezesha elimu bure kuanzia shule ya Msingi hadi Sekondari;

· Kufufua shirika la ndege la ATCL kwa nunua ndege mpya sita;

· Kuongeza mapato ya ndani toka trilioni 9.9 kwa mwaka hadi trilioni 14 kwa mwaka;

· Kurejesha nidhamu na uwajibikaji kwa watumishi wa umma;

· Ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima, Uganda hadi Tanga, Tanzania

· Kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma;

· Kutimiza ahadi ya Serikali kuhamia Dodoma;

· Kukamilisha miradi mikubwa wa umeme wa Kinyerezi I-extension na Kinyerezi II;

· Kuanza ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge;

· Uzalendo kusimamia raasilimali za taifa yakiwemo madini;

· Kuanza ujenzi wa barabara za juu Tazara, Ubungo na daraja la wapiti kwa miguu Furahisha;

· Ujenzi wa madaraja ya kisasa mfano la daraja la Kilombero;

· Kusimamia uhakika wa madawati maabara na maktaba katika shule zote nchini;

· Ujenzi wa maduka ya kisasa ya dawa za ndani ya kila hospitali ya Serikali;

· Kupambana vikali dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya nchini;

· Kutoa bima za afya za matibabu ya bure kwa wazee

· Kuhakikisha wanafunzi wanaostahili kupata mikopo ya elimu ya juu wanapatiwa

· Kuhakikisha Tanzania inakuwa na viwanda vya kutosha nchini

· Kufuta kodi na urasimu kwenye kilimo na uwekezaji nchini

· Kuhakikisha serikali inasimamia uuzwaji wa mazao ya wakulima masokoni na kupata faida. Mfano wakulima walikuwa wakiuza korosho zao kwa tsh 800 kwa kilo mpaka tsh 4000 kwak kilo.

Nimesukumwa kuzungumzia na kuorodhesha mafanikio haya kwa ufupi ili tujue shabaha ya rais wetu. Rais wetu anataka kurudhisha heshima. Heshima hailetwi kwa blah blah, heshima huletwa kwa vitendo na kufanya vitu kwa njia ya kuwa “disruptive”-kutokufanya vitu kikawaida au kwa mazoea.  Msimamo mkali wa Rais

Rais Magufuli anataka kuona watu wakijituma na kuleta matokeo chanya. Hata ukiangalia safu zake za uongozi ni viongozi walioshiba kwenye nafasi zao. Na wanaonekana hawafai wanaondolewa. Ila bado kuna makundi ya watu kwenye jamii wanaona anachofanya ni kazi bure na kufikia hatua ya kuaminisha umma kuwa Serikali hii ya Awamu ya Tano imefanya hali imekuwa ngumu na eti haina malengo na kuwa imepoteza dira.

Hakuna ukombozi uliofanyika bila kutoa jasho, kutokwa damu na kutumia mbinu za kujifunga mikanda. Mheshimiwa Rais anafanya hilo, ni lazima kujitoa mhanga kwa kipindi hiki kwa ajili ya mafanikio ya muda mrefu. Nilifikiria viongozi wetu hasa wa upinzani wangefurahia mabadiliko haya kwa maana ndio kitu hasa walichokuwa wakikitamani na wakishiriki kikamilifu katika kutoa mawazo yenye kujenga ila hali imekuwa ni tofauti.

Hapa ndio maana nimekikumba kisa cha safari ya Mussa-maana nalifananisha hili na kadhia ya wale Wana wa Israeli kufikia hatua mpaka kumkufuru Mwenyezi Mungu na wakaona kuwa ni kheri wangebaki kule Misri. Kama kumbukumbu ya kuku, nao walisahau walipotoka.  Ushauri

Natambua ni vigumu kumuaminisha kila mtu ukweli kama tayari anaamini uongo, kama ilivyo vigumu kumuaminisha uongo yule ambaye anaamini ukweli. Ila kama vijana na taifa lililo la vijana, imefika wakati wa kila mmoja kusimamia kila anachokiamini, LAKINI asiamini kile alichoaminishwa. Vijana tuache siasa za kupikwa na kuungaunga, tusimame katika ukweli na mambo yale ambayo yana maslahi kwa taifa letu na si maslahi binafsi. Tujiulize: Inakuwa vipi, wanasiasa na wanaharakati wale wale ambao walikuwa wanapigania vitu flani vifanyiwe kazi, sasa vinafanyiwa ndiyo wa kwanza kununa na kufanya ‘confusion’ mbele ya Jamii?

Ndani ya chama cha Mapinduzi tunaamini Umoja ni Ushindi. Huu ni wakati wa kuungana na Mheshimiwa Rais katika ukombozi wa Watanzania, lazima tuelewe shabaha ya Rais wetu kuwa ana nia njema na maendeleo ya nchi yetu.

Hii safari sio rahisi, hakuna aliyemkamilifu ila wote tunaitumainia Tanzania yenye neema. Vijana tuache kupokea mapokeo ya wanasiasa wasio na nia njema na nchi yetu, tufanye kazi kwa kushirikiana katika kuiletea nchi hii neema. Hapa Kazi Tu! Jokate Mwegelo,

Kaimu Katibu Idara Ya Uhamasishaji,

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) makao makuu.

**Chanzo cha habari hii ?  JamiiForum**

Waziri Kairuki afanya mazungumzo na Balozi wa Kuwait nchini leo hii!

Waziri wa Madini Mhe Angellah Kairuki siku ya leo masaa ya Africa Mashariki amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Kuwait nchini. …..kwa picha na maelezo zaidi bonyeza ??  IssaMichuziblog

David Kafulila avua magwanda ya Chadema!

Mwanasiasa David Kafulila avua magwanda ya Chadema! Je, anahamia CCM au anakuja na chama chake? Hilo kwa Sasa hatujui lakini najua tutajua hivi karibuni!  Naona “Mgufulicillin” is working really well ??. Wishing you all the best!

Robert Mugabe ameng’oka!

Ni nderemo zimerindima ndani ya nchi ya Zimbabwe!! Ameng’oka!! Robert Mugabe is no longer in power!…….Mimi siyo mwanasiasa hivyo sijui kama hii italeta amani na maendeleo zaidi au La! Lakini naweza sema ni mmoja ya watu ambao nilikuwa sipendezwi na kuwa na Rais  mmoja kwa miaka yote hiyo! Kunatofauti kubwa sana kati ya chama kimoja kuwa madaraka na Rais mmoja kuwa madarakani!! Hivyo kwahili naungana na Wazimbabwe wote kusherekea ushindi huu!…..Mungu ibariki Africa!

Nyalandu ang’atuka! Abwaga manyanga ya CCM!

Hayawi hayawi sasa yamekuwa! Mwanzoni ilikuwa ni hisia, baadaye dalili zikaonyesha, na sasa yametimia! Mh. Nyalandu Mbunge wa Singida Kaskazini katangaza rasmi kung’atuka nyadhifa zote ndani ya CCM na kubwaga manyanga ya chama hicho pamoja na ubunge wao! Ameyasema hayo kwa kupita Instagram page yake kama inavyosomeka hapo chini ?? …….Mmh! Mimi siyo mwanasiasa hivyo I will respectfully reserve my comment! Just wishing him the best! “NIMEAMUA kujiuzulu NAFASI yangu ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama kuanzia leo, Oktoba 30, 2017. HALIKADHALIKA, asubuhi ya leo nimemwandikia Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai, Mb., barua ya kujiuzulu nafasi yangu ya UBUNGE wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia tiketi ya CCM, nafasi ambayo nimeitumikia kwa vipindi vinne mfululizo tangu nilipochaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2000 hadi Sasa.

AIDHA, Nimechukua UAMZI huo kutokana na kutorishwa kwangu na mwenendo wa hali ya Kisiasa nchini, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa HAKI za Kibinadamu, ongezeko la vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa baadhi ya watanzania wenzetu, na kutokuwepo kwa mipaka ya wazi kati ya MIHIMILI ya dola (Serikali, Bunge, na Mahakama) kunakofanya utendaji kazi wa Kibunge wa Kutunga Sheria na wa Kuisimamia Serikali kutokuwa na uhuru uliainishwa na kuwekwa bayana KIKATIBA.

VILEVILE, Naamini kwamba bila Tanzania kupata Katiba Mpya Sasa, hakuna namna yeyote ya kuifanya mihimili ya dola isiingiliane na kuwepo kwa ukomo wa wazi na kujitegemea kwa dhahiri kwa mihimili ya Serikali, Bunge na mahakama ambayo ndio chimbuko la Uongozi Bora wa nchi, na kuonesha kwa uwazi kuwa madaraka yote yatokana na wananchi wenyewe, na kwamba Serikali ni ya Watu kwajili ya Watu.

MIMI Naondoka na kukiacha Chama Cha Mapinduzi CCM, nikiwa nimekitumikia kuanzia ngazi ya Uenyekiti wa UVCCM Mkoa, Ujumbe wa Kamati za Siasa Wilaya na Mkoa, Ujumbe wa Kamati ya Wabunge Wote wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM TAIFA, kwani nimejiridhisha kuwa kwa mwenendo wa hali ya kisiasa, kiuongozi na kiuchumi uliyopo Tanzania Sasa, CCM imepoteza mwelekeo wake wa kuisimamia Serikali kama ilivyokuwa hapo awali. AIDHA, Naamini kuwa, kama ilivyotokea kwa mihimili ya Bunge na Mahakama kutokuwa na uhuru kamili, bila kuingiliwa kiutendaji kwa namna Moja au nyigine, CCM nayo imekuwa Chini ya miguu ya dola badala ya chama kushika hatamu na kuikosoa Serikali inapobidi kama yalivyokuwa maono ya Baba wa TAIFA MWALIMU Julius Kambarage Nyerere.

HIVYOBASI, kwa dhamira yangu, na kwa uamuzi wangu mwenyewe, nikiwa na haki ya KIKATIBA, natangaza KUKIHAMA Chama Cha Mapinduzi CCM l” Mh. Nyalandu

Hongera sana Mh. Nicholaus B.William!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza Mhe Nicholaus B. William aliyemuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017. Kulia ni mke wa Mhe. William Bi. Foster Mbuna.
Napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza sana Mh. Nicholaus B. William kwa kuteuliwa kwake kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, na Michezo. Sijawahi kukutana nawe lakini sifa zako nyingi nilizipata kutoka kwa mdogo wangu Advocate Janeth O.O Igogo jinsi ulivyo mnyenyekevu, usiye jikwenza, mchapa kazi, na muungwana. Tabia yako ya kujiona wewe ni sawa na wengine inawavutia na kuwaacha wengi kujiuliza jinsi mlivyo lelewa. Kweli kuwa mtoto wa Rais hakubadili tabia ya mtu kwani tabia ya mtu ni mtu mwenyewe! Mimi naamini hayo yote ni matunda ya kuwa na walezi wazuri na mke mwema! Hivyo nategemea hakuna kitu kubadilika zaidi ya uongozi bora toka kwao! Hongera sana. #VijanaTunaweza

Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Africa

**Picha na caption kwa hisani ya Issa Michuzi blog. Kwa maelezo na picha zaidi bonyeza ?? (MichuziBlog-Matukio)**

Ziara ya Balozi Wilson Masilingi jijini Houston,Texas

Wiki iliyopita tarehe 21 na 22 mwezi huu wa kumi, Balozi wa Tanzania nchini Marekani, na Mexico alitembelea jimbo la Houston, katika state ya Texas ili kuwafariji Watanzania waliopatwa na maafa ya mafuriko ya Hurricane Harvey mwishoni mwa mwezi wa nane!

Mh. Balozi Masilingi

Balozi pia alikutana na viongozi wa jumuiya na kukutana na wanajumuiya wote nakubadilisha mawazo, kutoa muongozo katika maswala yanayohusu Diaspora. Kwa maelezo na picha zaidi bonyeza ?? (TanzanianHoustonCommunity-THC)

 

Hongera Mh. Janeth Masaburi

Well! Kama nilivyo wahi sema huko nyuma kuwa kuna ndugu zagu ambao ni wanasiasa, hivyo inapofikia kwenye kutoa pongezi basi sina budi! Kwa maneno hayo, napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza my aunt Mrs Janeth Masaburi kwa kuteuliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. ......Hongera sana, natumaini kuona sheria nzuri za kulinda na kutetea watoto na wanawake haswa katika kutimiza malengo ya dunia ya uchumi wa viwanda kwa wanawake!

Tanzania oyee! #Hapa Kazi tu! #ACACIA

Huu ushindi wa kishindo kikuu ni wakufurahiwa, kushangiliwa, na kujivunia kwa kila Mtanzania mzalendo mwenye mapenzi mema na nchi yetu! Tanzania oyee! Napia nampongeza sana baba yangu Dr Mgufuli kwa kusimamia kidete alichokiamini kuwa ni haki yetu sisi Watanzania japo  alipata kebehi nyingi lakini hakubadili msimamo wake! Thank you Dad ake, you made us so proud! ?? ………..Umeandika history kubwa sana katika uongozi wako na uzalendo kwa taifa lako! Ubarikiwe sana……… 

#Mungu ibariki Tanzania #Mungu ibariki Africa

Siku ya mtoto wa kike duniani: “Thamani ya Binti Na Uongozi wa Maadili”

“Thamani ya Binti Na Uongozi wa Maadili”  “Mcis Kelvin kutoka skonga kushoto Katikati ni Dada Glory kutoka @mwanamke_na_uongozi Mwisho ni @temidayo_gm Photo credits. @timesfmtz”

Siku ya mtoto wa kike duniani: Jokate awa mgeni rasmi shule ya Turiani, Magomeni, Dar!

 

Jokate Mwegelo ndie aliye kuwa Mgeni Rasmi siku ya leo ambayo ni siku ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani yaliyofanyika katika shule ya sekondary ya Turiani Magomeni. Alipata nafasi ya kuongea na wanafunzi wa kidato cha kwanza na tatu yaliyo andaliwa na taasisi ya @mwanamke_na_uongozi Iliyokuwa na kauli mbiu Thamani Ya Binti Na Uongozi Wa Maadili! “Walikuja kunitembelea, nikawaalika chakula tukala wote then tukapozi kwa picha ?” J. Mwegelo

Hongera sana Waziri Angellah Jasmine Kairuki!

Naomba nichukue nafasi hii kumpongeza Waziri mpya wa Madini, Mh Angellah Jasmine Kairuki! .......Kama kumbukumbu zangu zipo sawa basi naamini wewe ndio Waziri wa KWANZA MWANAMKE aliyewahi kushika wizara hiyo nyeti! Naamini utendaji wako unatija kwa taifa letu la Tanzania ndio maana Rais Dr. John Pombe Magufuli pamoja na washauri wake wakaona ni vyema ukabidhiwe hiyo wizara. ........Nakutakia utendaji na uongozi mwema ukizidi kuweka maslahi ya taifa letu mbele. Hongera sanaaaaaa! #Mungu Ibariki Tanzania #Mungu Ibariki Africa

“Nimeyachagua Mawe kuliko laana ya Mungu.”~~~` RC, Paul Makonda

“Mti wenye matunda ulichoka kupigwa mawe ukaamua kutokuzaa matunda lakini Yesu alipoukuta mti hauna matunda akaulaani. Nimeyachagua Mawe kuliko laana ya Mungu.”

Hayo ?ni maneno yake Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kupitia page yake ya Instagram akiwa ameambatanisha na hiyo ? picha!………Swali la kujiuliza: Nikwanini wakazi walio wengi wa Da er salaam bado wanamkubali Paul Makonda? Je, ni mtendaji mwema?! Au anabahati ya kupendwa na watu?! You be the judge……!

“jukumu kubwa la nchi za Afrika ni kuhakikisha zinaweka mazingira wezeshi ya kuwaendeleza wanawake katika nyanja zote.”~~~~Mh. Samia Suluhu

Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema jukumu kubwa la nchi za Afrika ni kuhakikisha zinaweka mazingira wezeshi ya kuwaendeleza wanawake katika nyanja zote.  Samia ameyasema hayo leo kwenye Uzinduzi wa Jukwaa la Kuwawezesha na Kuwaendeleza Wanawake Afrika lililoandaliwa na Asasi ya Graca Machel na kufanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es salaam. Makamu wa Rais alisema pamoja na kuwepo kwa jitihada mbalimbali za kuwaendeleza wanawake bado mazingira hayampi nafasi mwanamke haswa yule anayeishi kijijini. Aidha, aliainisha baadhi ya changamoto hizo kuwa ni pamoja na sheria na sera zilizopo ambazo bado zinawanyima wanawake fursa ya kumiliki ardhi pamoja na haki ya kurithi hata kama haki hizo zipo kisheria. “Hii inatokana na utekelezaji mbaya wa sheria, unaosababishwa na uwepo wa mianya ya ubaguzi kwenye kwenye sheria hizo jambo ambalo linakinzana na mfumo rasmi wa kisheria zilizowekwa,” alisema Makamu wa Rais. Aidha alisema “Inasikitisha kuona kuwa ni zaidi ya miaka 20 baada ya Ulingo wa Beijing; kukamilika kwa utekelezaji wa Malengo ya Milenia; pamoja na kuanza kwa utekelezaji wa Malengo mapya ya Maendeleo Endelevu ambapo kuna lengo la pekee linalosimamia masuala ya usawa na kuwawezesha wanawake na watoto wa kike, bado kuna baadhi wanawake miongoni mwetu ambao wapo kwenye lindi la umasikini, wanafanya kazi kwenye mazingira magumu; kupata kipato tofauti na wanaume kwa kazi sawa; kutokuwa na sauti ya kufanya maamuzi kwenye maisha yao wala maamuzi ya kisiasa; kutokuwa na fursa ya kumiliki na haki ya kurithi ardhi, kukosa huduma za mikopo, afya na elimu; Ingawa wamezingirwa na fursa tofauti na mazingira wezeshi bado wanawake wengi wa Afrika hawachukuliwi kuwa sawa na wenzao wa kiume mbele ya sheria. Alimalizia kwa kusema kuwa muda umefika sasa kwa wanawake kuwa mfano, Kuungana na kuinuana ilikuweza kumkomboa mwanamke wa Kiafrika na kuhakikisha hamna anayebaki nyuma kwenye fursa za maendeleo. . . ( Picha na Ofisi ya #MakamuWaRais )

***Copy & Paste from CloudsTV  Instagram  page***

Womanhood!

Hatuna budi kuwashukuru, kuwatambua na kuwaenzi dada, mama na bibi zetu waliotutengenezea njia kwa mengi tunayofurahia kama wanawake leo hii. Na hasa kujitambua na kutambua uwezo tulio nao. Asante mama Gertrude Mongella! #WAAFORUM2017 ~~~~ Faraja Nyalandu