Category Archives: Lifestyle!

Wanaopenda kushangaa ndio wajanja!

Baadhi ya watu haswa sisi Watanzania huwa tunatabia yakutokupenda kuwa wadadisi wa jambo au mambo matokeo yake our ignorance is very High! 
Yani tupo radhi tuamini katika uongo au majungu / umbea kuliko kuchukua muda wako na kukisoma / chunguza kitu wewe mwenyewe ili uwe na huwakika wa kile unachokiongea. Utakuta mtu anahadithia kitu wewe utaamini ni kweli ameiona mwenyewe kwa macho yake au amesikia yeye mwenyewe kwa masikio yake kumbe naye kasimuliwa na rafiki yake ambaye nae huyo rafiki kasimuliwa na mtu mwingine 🙆‍♂️🙆‍♂️
Hiii no karai ya Chicago
Hii tabia kutopenda kuchukua muda wetu na kujifunza jambo fulani au kufatilia habari fulani bila ya wewe kuweka uongo wowote ndio imefanya Watanzania wengi wanapenda majungu sana, wanaamini ili uweze fanikiwa basi lazima umuharibie mwingine haswa kama yupo kwenye biashara au jambo ambalo na wewe unafanya! Inasikitisha sana kwani kwa hii tabia maendeleo ya taifa letu yatahitaji dictator!!  Juzi niliamua kwenda kuangalia hili 'karai' kubwa ambalo limeletwa hapa Houston, Texas kwenye chuo cha sanaa. Hili karai limetengenezwa Ulaya likaletwa hapa. Ni urembo wa aina unao vutia sana.  Katika mji wa Chicago nao wanao 'karai' kama hili limetengenezwa na mtu mmoja. Ila la Chikago limeinamishwa (kama inavyo onekana kwenye picha ya pili kutoka juu) hivyo watu wanaweza ingia katikati ya hili 'karai' nakupiga picha nzuri sana kama anavyoonekana mwanangu hapo pichani ☝ na pia tizama picha ya mama yangu na mdogo wangu hapo chini 👇
Hizo picha zilipigwa miaka 6 iliyopita kwenye hilo karai la Chicago. Kwa maoni yangu binafsi mimi napenda ya Chicago zaidi kwani imewekwa vizuri kwa watu kupiga picha na kitendo cha kulazwa chini imefanya hiyo sehemu iliyoingia ndani kuwa sehemu ya kivutionzaidi cha kupigia picha. Halafu maua na urembo ulioko pembezoni unahakisiwa na hiyo karai ambayo pia nikivutio.
Nilichotaka kuwaambia Watanzania wenzangu ni kuwa usiogope kushangaa! Hakuna njia nzuri ya kujifunza kitu kama kushangaa. Tena ukimpata mtu anayekupa maelezo basi wewe zidisha kushangaa ili akupe maelezo zaidi. Wanaopenda kushangaa ndio wajanja!

Zari don’t be fooled, stay awake!

Okay! I believe we all had a chance to listen to Diamonds ft Ravvyn new song #Iyena kwangu mimi naona wimbo upo kawaida japo video ni nzuri na nafikiri uwepo wa Zari mule umeongezea mvuto kwa kiasi kikubwa! Kama hujaona tazama 👇

Lakini sijali sana kuhu wimbo, ujumbe wangu ni kwa Zari kwani nineona mashabiki "maandazi" wanavyo ongea eti "warudiane" na Diamond 😳😳 I am like for real!! Who in a right mind will dare to say that?! Seriously people?  let us be real here for a second!! Hivi ni huyu huyu Diamond aliye m-cheat Zari na kuzaa nje baadaye akaomba msamaha Zari akamsamehe kwa moyo mkunjuvu na akasema "I made peace with his mistakes"!! Baada ya hapo nini kilitokea?!! Sindio akarudi kutoka South nakupokelewa na Wema Sepetu ukumbini na familia yake yote ikiwepo na Wema?! Na hapo ni baada ya mama Diamond kukaa South Africa kwa Zari zaidi ya mwezi pamoja na mumewe halafu kafika Bongo ndio huyo yupo busy na Wema? (With all due respect to Wema, mimi sinaga mambo ya timu bali nataka nifikishe ujumbe wangu vizuri ndio maana namtaja) Na bado picha na video akiwa na wanawake wengine zilirushwa kwenye mitandao na kila mtu anaona! Nyie watu acheni mzaha!! 
To you Zari, I'm not sure if you consider yourself "a celebrity" or a business lady who happened to be a "celebrity"! Celebrity is a culture, if you want to live a  celebrities culture then forget about your integrity, take Diamond back and prepare to lose respect from many people! What I am trying to say here you're way better off without Diamond! You stand as a very strong and powerful woman right now than those days you used to  zoom around  with Diamond everywhere like a homeless lady!!

You have added your value by showing people who you real are, how strong you can be, please don't trap kwa mama Diamond childish games! Adults, young girls and boys are looking up to you so do your children please don't let them down eti kisa nyimbo! Think about your daughter, you are laying a foundation of how boys and men should treat her be wise like snake! Build good foundation that every man will think twice before holding your daughter's hand! Teach young boys that women are not tools but rather are fellow human beings treat them with respect and dignity, not using them as "money making" machines!! Please, find a healthy  co-parenting way with Diamond and his family but don't take them back as family. That family is perfect but not for you, is perfect for those other women (if you know what I mean)! Achana nayo kabisa they don't deserve you even for a second. You were raised by a strong woman, whom she raised all those strong children alone why letting her down!! Usiseme eti watoto hata yatima pia ni watoto lakini wanakua!! That family isn't a healthy family to raise children with labda uwe unavuta bangi! Money is good but Not all money is great!! Choose your paycheck wisely! 

After all, you look more matured, focused, and well kept right now than ulipokuwa na Diamond. He stressed you out, took the strength out of you, misused your love, you didn't have peace at all.  Try to look at your old pictures you will agree with me!! They degraded you to accommodate and keep up with their uncivilized characters!! Trying to make money by destroying every woman that Diamond is involving with, I hope you are awake enough to smell the nasty coffee!!
Plus this babydaddy of yours care less about your life, he doesn't care if he would leave your children motherless perhaps even no parents at all that why he can't use any kind of protection-HIV is real woman! And what about Hippies, and Hepatitis C for God's sake!! Look how he was fooling around  with those ladies, let them recorded him with no fear or shame then shared them in social media?!! Guess what, that is the PROOF THAT HE DOESN'T LOVE YOU!! He is just using you! Selfish to the core!! If someone loves you will care about you, will always think about you before taking any action!! No one is perfect but some people are evil!! This is nothing but pure evil!!

You can do business with him but make sure every thing is clearly written and well documented. Make sure he is not a beneficiary of any of your money even if you happen to die today! Let ALL your children be the first beneficiaries, and your sisters legal guardian. You're better than this Zari don't let this family destroy the woman you are!! ..... In the end, it's your life we are just cheerleaders!!


“The Art Of Self -confidence”

Regrann from @lemutuz_superbrand - LIVE STRAIGHT TALK: The Art Of Self -confidence I mean huwa ninashindwa kuamini ninampigia simu Mbebezz anapokea Mwanaume na kujifanya kujitunisha please stop that guys unakuwa mjinga na utaishia kujiua cause Mwanaume unatafuta nini kwenye simu ya Mbebezz wala sio mke wako na hata kama angekuwa Mwanaume huingii kwenye simu ya Mbebezz cause utayakuta unayoyatafuta yaani Ugonjwa wa moyo ..kila binadam anahitaji nafasi au space to be themeselves sometimes na hakuna binadam anayeweza kumchunga mwingjne na mpaka kufanikiwa HAYUPO nina maana Mwanaume huwezi kumchunga Mbebezz ukafanikiwa utakwama tu kila binadam anahitaji uhuru wa kufanya mambo yake bila kuchungwa na kwenye mapenzi tunatakiwa kuongozwa na TRUST!
Now what is TRUST kwenye mapenzi wewe hakikisha you dont Cheat ukiweza hilo ujue na Mbebezz wako hata ku cheat ila kama wewe Mamen una Cheat ujue 100% Mbebezz wako naye ata Cheat tu yaani wewe ule wabebezz wa wenzako ila wako asiliwe wewe nani hapa.Duniani na nani kakudanganya kuwa inawezekana? ...guys kuna Sheria ya maisha sijaitunga mimi kua ukiona una cheat mke wako hakukamati ujue na yeye ana Cheat cause giza ni kwa giza na mwanga ni kwa mwanga babe yaani haiwezekani wewe U cheat mke wako asi cheat no way UNAJIDANGANYA TU hahahaha ...halafu guys acha utoto mpenzi wako akiamua kuku cheat haina maana hakupendi ila ni mapungufu tu ya kibinadam wote huwa tunapitiwa na jifunze kuwa kama mimi Sheria yangu ya maisha ni mpaka NIMKUTE MBEBEZZ WANGU RED HANDED ANA CHEAT ndio nitaamini ila siwezi kusikiliza maneno ya watu au majungu majungu au kwa vile nimeona sms ni Ujuha wa hali ya juu sana kukosa Kujiamini ...sawa mapenzi mapenzi lakini jifunze kwamba unampenda binadam mpungufu kwama wewe ulivyo so mpe nafasi usimbane mpaka anakosa pumzi U know ...kumpenda mpenzi wako sio kumfuatilia kwenye simu hapana mpe mapenzi ya kweli ataona huzuni na aibu kukuibia na ukiona mbebezz anaruka ruka ujue kuna kitu anakosa kwako muulize kwa upole atakuambia tu kuliko kujifanya mbabe na unajua kuchunga cause huwezi ...guys Mwanamke ni kama kisima cha maji huwezi kujua kuna mtu kachota ndoo moja mpaka umuone kama hukumuona hutajua so relax and chill like me! - @lemutuz_superbrand - #regrann

“I always knew I wanted the good life, like I wont even lie about it”

Regrann from @zarithebosslady - WCW inspirational moment: I always knew I wanted the good life, like I wont even lie about it but then again dont we all? Well, at 30 I was already employing 258 employees and that alone on its own made me grow up mentally. The responsibility that comes with managing companies in a foreign country where you are always targeted as a foreigner least i forget the tight competition especially if your on top of your game wasnt easy...... so whatever you do, do it with passion. Fall down 99 times, get up the 100th. One day, and I say it again one day, the universe will respond. #Persistence #Consistence (See my life at 30, huge office with a personal boardroom😁) me and Don started out in 2 offices, one PA, had just abit of ideas, got experts on board which we couldn't afford but they saw potential in us, did our logos which will forever remain a trademark and here is our recognized brand in the whole of SA www.brooklyncitycollege.co.za - #regrann Awiih! That's my gal! My true inspiration.  The real BossLady. Hakuiba kwa mume wa mtu akuuuu mtoto wa watu! Katafuta masiki mwenzake wakaanza kusaga visigido!! #I'mTheFoundationNotTheRoof ......I want good life too and hope to catch up with your achievement though I am in my 40s! Don't look down on me only God sits that high 😀 😍😍..... You go Zari! Keep winning! Keep shinning!

Zari Hassan: I am The FOUNDATION Not The Roof

  Regrann from @zarithebosslady - Pale unaposkia pesa za urithi... apo vipi. Success isnt sexually transmitted my dear. Endeleeni kudanga thinking some rich guy will knock you off your feet and success will happen over night. Even if he did you will be like part of the furniture he has a right to take out old ones and bring in new ones, as for me its not easy to get rid of me. IAM THE FOUNDATION not the roof...haha.  Anyway we are commemorating Ivans one year since his passing and i thought I'd motivate someone out there with these old images.
Dont downlook broke guys, God is for all, tables turn! Poor thing worked day and night to get me this car at 22 because he saw the woman in me. And yes, it didnt work out no matter how much i tried, Started from the bottom, right! Rest his soul in peace! - #regrann  

Ni maneno mazito sana kaandika Zari katika kukumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kifo  cha Ivan Ssemwanga ambaye alikuwa mume wake na walijaliwa kupata watoto watatu. Ujumbe huu mzuri sana kwa wale wanaofikiria na kutwa kumsakama Zari kuwa anafuataga pesa kwa wanaume aliokua nao. Haya ushahidi huo mmeuona sasa muache kumsakama mtoto wa watu na mumpe heshima yake anayostahili!!  Jibu safi sana kawapa  "I am the FOUNDATION not the Roof"😍😍 Ten 🙌 across the board!! Ngoja leo niseme; katika wanawake wote ninaowapenda kwenye Social media kwakweli I have to sincerely admit Zari is number one!! Nikiangalia alipotoka na mambo aliyopitia, na jinsi anavyo yakabili kwakweli she is MORE than 'Woman and half'!!  Hivi utawezaje kuvunja Msingi!! Kama ni nyumba inamaana lazima greda lipite nyumba yote idondoke ndio ufutilie mbali Msingi! Only fools do that!!!
Kama mnakumbuka huko nyuma niliwahi kuandika kuwa kuna wanawake wengine huwezi kupata "mbadala wake"  you can not  replace her no matter what (soma 👉 In loving memory of Ivan Ssemwanga: "I think I was prepared for death") na Zari ni one of those very few women! Yani kama vile Oprah, hakutakaa kutokee Oprah mwingine duniani! Wengine watajaribu kuwa kama yeye lakini they will never be her! Sio kwasababu ni wazuri wasura na maumbile, hapana! Is the Brain, the courage, behind that beauty is a whole game changer ma'am!! Unfortunately I have to say this, with all due respect to Ivan Ssemwanga, but he was part of Zari's journey and not the destiny!! The best of Zari is yet to come!! So do Diamond, yale yalikuwa ni mapito tuu lakini safari ya Zari inaendele na ni nzuri zaidi kuliko alivyokuwa na Diamond!! Just keep watching her. Yani naamini hata Diamond huko aliko anajuta sana kimoyo moyo kwani anajua kuwa hata hafanyeje haitokaa apate mwanamke kama Zari. Atapata hao wauza sura wakupenda drama na ujinga wa social media but not another Zari! He was just soooooo lucky to have Zari on his hands! Na bahati haiji mara mbili! Kwanza Zari sasa hivi ndio mambo  🔥🔥🔥 Keep on shining Zari!  😘 ❤ #IamTheFoundationNotTheRoof

Madam Rita Paulsen: I can proudly say I know how she feels

Regrann from @mspaulsen - The smiles when a you are a single mother and get to wittness your daughter,s wedding...... I can proudly say I know how she feels. It's the best achievement and a blessing . The feeling is unexplainable. I wish this to all single mothers out there we rock 💪💪💪thanks God and our daughters for making us proud - #regrann Maneno ya kugusa moyo haya kutoka kwa Madam Rita Paulsen. Je, wewe umeahawahi kukutwa na hali kama iliyomkuta Madam Rita? Yani ukaona mtu anapitia jambo au anakutwa na kitu fulani (jema au baya) halafu zile hisia zake ukahisi ni wewe kwasababu huwenda nawe unapitia kitu hichohicho au ulishawahi kupitia huko nyuma? Kwanini nime share nanyi hii " status" ya Madam Rita, nikuwa maisha ni fumbo, ukimwona kichaa yupo uchi usimcheke kwani hujui yakesho! Watu pekee ambao wanaweza kuelewa kwanini yule kichaa yupo uchi na nijinsi gani anajisikia niwale ambao walishawahi kuweuka! Nawale  ambao wanajua thamani ya kuwa na akili timamu niwale wale uliowahi kuwa vichaa. Ndivyo ilivyo hapa, only those who are or have been single mothers before ndio wanaoelewa ujumbe wa Madam Rita na furaha ya mama Princess Megan.  ***Siku zote dharau maiti siyo binadamu mwenye pumzi ya uhai***

‘Life is just a moment’

“A man died…

When he realized it, he saw God coming closer with a suitcase in his hand.

Dialog between God and Dead Man: 

God: *Alright son, it’s time to go*

Man: So soon? I had a lot of plans…

God: *I am sorry but, it’s time to go*

Man: What do you have in that suitcase?

God: *Your belongings*

Man: My belongings? You mean my things… Clothes… money…

God; *Those things were never yours, they belong to the Earth*

Man: Is it my memories?

God: *No. They belong to Time*

Man: Is it my talent?

God: *No. They belong to Circumstance*

Man: Is it my friends and family?

God: *No son. They belong to the Path you travelled*

Man: Is it my wife and children?

God: *No. they belong to your Heart*

Man: Then it must be my body

God: *No No… It belongs to Dust*

Man: Then surely it must be my Soul!

God: *You are sadly mistaken son. Your Soul belongs to me.*

Man with tears in his eyes and full of fear took the suitcase from God’s hand and opened it…

Empty… With heartbroken and tears down his cheek he asks God…

Man: I never owned anything?

God: *That’s Right. You never owned anything*.

Man: Then? What was mine?

God: your *MOMENTS*.  Every moment you lived was *yours*.

Do Good in every moment

Think Good in every moment

Thank God for every moment

Life is just a Moment.

Live it…

Love it…

Enjoy it…… ”

#Mama

#AboutSabbathDay

#GodIsGood

ULAFI NA KUTOKUWA NA KIASI

ULAFI NA KUTOKUWA NA KIASI: Ulafi na kutokuwa na kiasi ndiyo msingi wa anguko kuu la upotovu wa maadili katika ulimwengu wetu. Shetani analifahamu hili na daima huwajaribu wanaume na wanawake waendeleze ladha ya kionjo kwa gharama ya afya nahai wenyewe. Kula, kunywa na kuvaa yamefanywa kuwa lengo la maisha kwa ulimwengu. Hali ya mambo imekuwa sawa naile iliyokuwa kabla ya gharika, na hali hii ya ubadhirifu ni moja ya ushahidi bayana Wa ukaribu Wa kufungwa kwa historian ya Dunia hii.

Tunajua kwamba Bwana anakuja mapema sana. Ulimwengu unaharakisha kuwa kama ulivyokuwa katika siku za Nuhu. Umejikita kwenye kuendekeza ubinafsi. Kula na kunywa hufanywa kupita kiasi. Watu wanakunywa Vileo vyenye sumu ambayo huwafanya kuwa wehu. Kitabu cha matukio ya siku za mwisho, UK, 21.

**Nimeitowa kwa rafiki yangu Facebook**

Yes! Zari goes to church!

Regrann from @zarithebosslady – All my days are for God, but Sunday I go all out…. #Church – #regrann

Hayo ni maneno yake Zari Hassan the Bosslady kupitia Instagram page yake. I am happy for you Zari keep that spirit God is everything! I hope one day you will warship on Sabbath with me here in Houston or you want me to come to South Africa? I can 😍🙈…. Bwt, you look Amazing! 👌 Be blessed mama Tee 😘❤

Toni Braxton akubali pete ya Mr Birdman

Je, wewe unampenda mtu kwa muonekano wake, taiba, familia aliyotoka, akili zake, sura, pesa, jinsi anavyokuonyesha heshima n.k?  Mwanamuziki Brian a.k.a The Birdman  anasema "so what? What that gotta do with love?"  Hayo yalikuwa ni maneno yake baada ya Talk show host Wendy Williams kusema kuwa yeye alikuwa mtu wa kwanza kusema "hapana" aliposikia Toni Braxton ana mdeti The Birdman! Wendy amemueleza Mr Birdman kuwa muonekano wake na Toni ni tofauti sana hapo ndipo Mr "The Birdman" akasema vinahusiana nini na kupenda?! Yeye ni 'certified gangsta' 😀🙈 aliye kuzwa na street kwasababu mama yake alikufa akiwa na miaka miwili (2), baba naye japo hakuwa sana kwenye maisha yake naye alikufa, kaka, dada, bibi, babu wote wamekufa hivyo vitu hivyo vinemfanya asijue nini maana na thamani ya upendo lakini siyo kwamba hajui kupenda!  "I’m just a gangster, that don’t mean nothing. Certified too. What that gotta do with love?" Wendy alishikwa na kigugumizi baada ya jibu hilo! 

Hilo nalo ni somo kwa wengi wetu tunaopenda kusema "kampendea nini?" Wewe ukiona watu wanapendana kama huna jema lakusema nyamaza lakini ukitaka kujua kampendea nini utaumbuka kwani hayo ni ya Ngoswe muachie Ngoswe mwenye! Kila mtu ana kitu chake ambacho anatafuta katika kumpenda mtu sasa mambo ya kujifanya mimi sijui "Engineer" ooh mimi "mfanya biashara" sijui msomi gosh!! What that gotta do with love?!! Kwani siku ukiwa huwezi kunyanyuka kitandani hizo degree zako zitakunyanyua kitandani? 👀😏 Watu wanaangali potential ulizo nano! Unaweza ukawa mzuri na elimu nzuri lakini akili ya maisha hauna azidi ya kutaka kuwa "trophy wife" au "Mario" ulishwe na kuvishwa na mwanamke halafu bado utake uitwe mume 🤔 anyway, Birdman amemvisha Toni pete yenye thamani ya $5,000,000

The Birdman siyo mwanaume pekee ambaye anatarajia kufunga ndoa na mtu ambaye watu wengi walidhani haiwezekani. Prince Harry naye mwaka jana mwishoni alimvisha pete ya uchumba muigizaji wa kimarekani ajulikanaye kama Megan Markle. Kwa hapa Megan ni mkubwa kwa Prince Harry kwa miaka mitatu (3yrs) na pia huko nyuma alishawahi kuolewa na kuachika. Ndoa yake ya kwanza ilidumu kwa miaka miwili (2 yrs) baada ya kudate kwa kwa muda wa miaka 6 👀🙈 Hivi ndivyo vitu ambavyo sivielewi watu wadate kwa miaka sita halafu ndoa idumu kwa miaka 2 tu!! Tena hapo mpaka divorce imetoka ina maana atakuwa walitengana at least miezi 6 kabla 🙆‍♂️🙆‍♂️ Haya huyu Prince Harry ame mvika pete baada ya kumdate kwa muda wa miezi 15 (sawa na mwaka mmoja na miezi 3). Je, nitakuwa sahihi kusema ngoja tuone hii itadumu kwa muda gani au tuwatakie kheri tu 🙈

Btw, hata Toni Braxton hii itakuwa ndoa yake ya pili! Ndoa yake ya kwanza ilikuwa na mwanaume mwenye asili ya ngozi "nyeupe" ilidumu kwa muda wa zaidi ya miaka kumi na mbili (12  yrs) na alizaa watoto 2, Toni ana miaka 50 sasa.....Haya wale tunao pendeza hii show ya Braxton Family Values ndio tutakao faidi uhondo wote 😍 Siamini siku hizi nimemuambukiza mama yangu kupenda hizi show 😂😂 anajua mpaka ratiba zake 🙈🙈

Timu vibonge amkeni twende!

Regrann from @open_kitchen2014 - If you dont know my journey its better to be quiet from size 22/24 to size 14/16 53kgs nimezitoa all kwa juhudi zangu nikiwa nimezungukwa na chakula kitamu na vitu vitamu lakini nimejenga discipline ya ajabu .

.kila kitu kinawezekana Amka twende - #regrann

Jamani timu "vibonge" amkeni twende sambamba na mama wa Mahanjumati, Open_kitchen kakata manyama uzembe hiyo ni picha ya zamani ukitaka kuona picha zake zasasa hivi na jinsi anavyofanya mazoezi tembelea Instagram page yake. Hongera sana mpendwa ...... Jamani mimi tumbo limegoma ,😭😭😭 napambana nalo najua one day litatoka tu! Amkeni jamani vibonge wenzangu tupambane na hali zetu 😂😂😂😂💃🕺

Be the person you want to attract!

 Regrann from @cheyennebbostock – Be the person you want to attract. If you want a rich man, start by being a rich woman. 👌🏾 Despise the free lunch! Quality men of substance are attracted to independence and self-sufficiency. Get there! 👌🏾 – #regrann  

Stop allowing people to take up space in your life that they haven’t earned and don’t deserve!

Regrann from @cheyennebbostock – Stop allowing people to take up space in your life that they haven’t earned and don’t deserve. You are worth more! #CheyenneBostock – #regrann  

Zamaradi Mketema: Ni Makosa yetu wanawake

Miriam Kinunda author of  Taste Of Tanzania: Modern Recipe for the West https://www.instagram.com/miriamkinunda/

Regrann from @zamaradimketema -Kwenye comments nimegundua wanawake wanalalamika na mzigo wanaoubeba wao kwenye majukumu ya familia, ila MAKOSA mara nyingi yanaanzia kwetu, wanawake wengi WANAWALEMAZA sana wanaume wao wenyewe kwa kuhisi wanawasaidia, kwa bahati mbaya hii haina faida kubwa mbele ila hasara.

Tukirudi kwenye nature mwanamke ameumbwa kutunzwa hata vitabu vyote vya Dini vinasema hivyo, na ndiomana ikiwa tofauti madhara tunayaona, mwache mwanaume awe mwanaume hata kama umemzidi kipato, nature ya mwanaume ni KUTOA na kujihisi ANAMILIKI na ndio uanaume wake unapokuja, anapokutunza anafeel uanaume wake, hata uwezo wa kunguruma anaupata ndani, mpe hiyo nafasi usimnyime, hata kama wewe una mia yeye ana kumi hakikisha katika kumi yake lazima utaratibu wake wa kulisha nyumba ubaki palepale kwa kidogo chake hikohiko, we utatumia tu akili jinsi ya KUMSAIDIA ila usimlemaze akaona wewe ndio kilakitu na kumpa nafasi ya kutulia, hakikisha kila anapotoka anaacha kinachostahili hata kama ni mia tano, mfanye awe mume, maana athari za wewe kuibeba familia mara nyingine zinaenda pabaya zaidi hadi kuharibu mahusiano.

Na ndiomana kuna fikra isiyo rasmi kuwa wanaume wengi wanaoishi na wanawake wenye uwezo zaidi yao hutafuta nyumba ndogo pembeni za hali ya chini na kuzihudumia kwa hikohiko kidogo, lengo ni kutaka kuutoa uanaume wake, anataka mamlaka yake yaonekane, anataka akiongea asikilizwe, mpe nafasi hata kama una uwezo, hiyo ndiomaana ya kuwa KICHWA mfanye awe kichwa kwa vitendo, hata kwa umasikini wake onesha unamtegemea yeye na umtie moyo afanye kadiri ya uwezo wake, sio ndio unazo basi yeye anakuwa kama mtoto mdogo sasa ndani unamuacha moja kwa moja hapana, au unajifanya huhitaji kitu kwake unakosea. Ukitaka kujua hii ni nature hata kwa upande wa wanawake ndiomana hakuna feeling nzuri kama kupewa/kutunzwa na mwanaume wako hata kama una kilakitu, sababu nature iko hivyo!! Ndiomana si ajabu kukuta mwanamke tajiri lakini akamtamania mwenzie wa hali ya chini kwa kununuliwa mkufu tu, pamoja na kupata kilakitu kwa jasho lake bado kuna kitu kinamiss, kuona mtu anasimama kwake kama MLINZI na mtunzaji wa maisha yake, MUNGU ndio kaumba hivyo!! Ila siku hizi eti wanaume ndio wanalindwa. Ni Kosa!! Regrann from Zamaradi Mketema

Watoto wanahitaji malezi ya mzazi! Mali na pesa siyo malezi!

Wahenga walisema kulea mimba si kazi kazi kulea mwana! Ukiwa mjamzito kike kiumbe ulichobeba hata kama hutaki kikuwe kitakuwa tu! Sasa ni hiyari yako kula vizuri na kujijali ili uzae kiumbe chenye afya bora na salama. Mama uliyebeba hicho kiumbe ni jukumu lako kutafakari matendo na tabia zako wakati wa ujauzito huo kwani huyo mtoto anauwezekano mkubwa sana wa kuhakisi tabia zako akiwa tumboni mwako!  Huo ni mtihani wa kwanza katika malezi ya mtoto!  Jana nilisoma post ya Jackie ikanikumbusha mtihani wa pili katika malezi ya mtoto ambapo wazazi wengi huwa wanafeli! Pia ikanikumbusha kuhusu wazazi fulani ambao wapo kwenye  reality show fulani inaitwa “Married to Medicine” wote ni madaktari na mama anaumizwa na kitendo cha wao kuwa busy na kazi kiasi kwamba wanakuwa hawana nafasi ya kukaa na watoto zao! Napia ikanikumbusha interview ya Naomi Campbell aliyofanyaga na Oprah Winfrey mwaka 2010 ambapo Naomi alisema kuwa siku zote amejisikia mpweke toka akiwa mdogo kwani wazazi wake wahakuwa nae karibu. Mama yake Naomi yeye aliamini kuwa anafanya kitu kizuri kufanya kazi sana ili kuweza kumpatia mtoto wake vitu vizuri, kusoma shule za private n.k ………. Soma na tazama video hapo chini 👇@Regranned from @j_n_mengi – Dear parents, I know you’re busy working hard to feed and raise your kids but please remember that your physical presence is very important to your child. You need to invest more than money to your child, they need to talk to you, they need your hugs and reassurance and most importantly they need you to teach them to be good human beings.”

Pesa na mali ni vizuri kama ukiwawekea watoto wakawa navyo kwani hilo ni jukumu lako kama mzazi! Kumbuka “Pesa na mali ni urithi mtu apataye kutoka kwa babaye” hayo ni maandiko ya Biblia siyo mimi! Lakini kabla ya kuwapa hizo pesa na mali ni vyema ukawafundisha jinsi ya kupata hizo pesa na mali ili nao waweze fundisha watoto zao! Hata hivyo, kabla ya kuwafundisha jinsi ya kutafuta pesa na mali watoto wanatakiwa kufundiswa maadili!

Watoto wanatakiwa kuonyeshwa upendo iliwajifunze kwa matendo, watoto wanatakiwa kufundishwa elimu ya Mbingu kabla hujampa elimu ya duniani! Kwamfano, kabla ya kumfundisha mtoto wako kuhesabu embu hakikisha anajua kusali au kusema sala ya Bwana kwanza! Mfano mwingine, kabla hujamfundisha mtoto wako kusema “naomba” mfundishe kushukuru kwa kila kitu anachopewa, hakikisha anajua kusema “asante” kwanza kabla ya kusema “naomba”!

Kumvalisha mtoto wako nguo za designer maharufu siyo malezi! Surely, itamfanya aonekane vizuri lakini haita msaidia kuwa kiumbe bora! Kumlaza mtoto wako kwenye nyumba ya mamilioni ni vizuri lakini haita mpa confidence au kuacha kuwa muongo na mwizi! Watoto wanahitaji malezi ya wazazi! Pesa na mali siyo malezi!!

My son enjoying his New Year breakfast!

Yaas! That is my son! Enjoying his New Year breakfast in Nairobi. At age 2 1/2 he got all his table manners in place 👌👌 way to go son! Wasichana itabidi wajipange sana tu! Kama hawakufunzwa ustarabu na mama zao wakwende huko hatuwataki sisi 🤣🤣 We are raising a gentleman right here I hope someone is raising a Queen for him 😍😍  maana Mimi mama mkwe nitamkagua kabla hajaingia ndani ya nyumba ya mwanangu 🤣🤣🤣 chezea mama mkwe wa dotcom! Kama tunataka tuondoe unyanjasaji na ukiritimba kwa wanawake inabidi wakina mama muwe teyari kulea vijana wenu katika maadili, na mambo yanayofaa! Na mambo hayo huanzia katika umri huu! Usisubiri akifika sijui miaka 6 that is way too late! Pia watoto wakike muwafunze tabia njema, kujithamini, good touch and bad touch mara tu wanapojua kuongea na kutembea! Usingoje mtoto sijui aote maziwa ndio unaanza "kubwabwaja"!! Kama tunataka ukombozi wa mtoto wa kike na mabadiliko ya tabia za wanaume wa Kiafrika basi wakina mama lazima mkubali kubadilisha tabia ya malezi yale ya kizamani kuwa mtoto wa kiume ni "King" na mtoto wa kike ni "servant"!! Kuwa mtoto wakiume haitaji kupewa malezi yenye maadili ya jinsi ya kuwa kaka, baba, mume, na raia mwema isipokuwa toto wa kike tu! Yeye ndiyo anatakiwe afunzwe kuwa dada mwema, mama mzuri, mke bora, na raia mwema,  swali linakuja awe mwema kwa nani?!! Mwaume mbakaji? Au mwanaume katili? Au a cold-hearted killer? Au mwanaume mnyanyasaji asiye hata na chembe chembe ya hofu ya Mungu?!! Mothers I'm raising my gentleman because I don't want him to be part of that ugly statistic!!What about you!! .........Happy New Year everybody!

Mlee mtoto katika njia impasayo!

 Kwanza naomba mniwie radhi wapendwa wangu ambao ni Waislam. Mimi ni Mkristo hiyo mambo mengi nikiongea nita refer to the Holy Bible kwani hicho ndicho kitabu nakijua na pia sipo hapa kwaajili ya dini hivyo sitokaa ni compare Quran na Bible! Sasa Biblia katika kitabu kile cha Mithali 22:6 inasema mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atakapokuwa  mzee! Hizi picha za birthday ya Nillan ambazo zinaonyesha wako mezani wakila chakula na kunywa zimenifanya nikumbuke hilo fungu la Mithali 22:6!  Hivi wazazi wangapi mnawalea watoto wenu kwa kuwafundisha kuwa chakula ni kitu cha kuheshimiwa hivyo ukila lazima uwe na nidhamu?! Kuwa hupaswi kutembea huku unakula kama mkimbizi au mtu aliye vitani!! Unamfunza mtoto kuwa ni lazima ukae chini / mezani wakati wa kula napia ni marufuku kuongea nachakula mdomoni!!  Kama wewe ni mzazi unaye ishi katika mazingira mazuri na ungependa mtoto wako aende mbali zaidi ya hapo ulipo wewe, je umemwandaa mtoto wako kukabiliana na mazingira hayo?! Kwamfano, ungependa mtoto wako awe na uwezo wa kwenda naye kwenye 5* hotel nakula chakula mbele za watu nilazima umfunze mwanao kukaa mezani wakati wakula na atulie mpaka atakapo maliza chakula. Nilazima umfunze mtoto kutumia visu, uma, na kijiko tena umfunze mara kwa mara ili azoee kuvitumia kama Zari alivyofanya kwa watoto wake. Hao watoto kukaa mezani kwa utulivu hivyo nakula kwa ustarabu si kitu ambacho wamefanya mara moja, hapana! Hao watakuwa wamefunzwa na wamezoea! Ni malezi mazuri sana haswa kwa karne hii ya 21 ambapo dunia imekuwa kama kijiji  huwezi jua ni wapi na nani mwanao atakutana naye hivyo lazima kujua jinsi ya kumudu mazingira!  Nilipokua nyumbani Tanzania mwanzoni mwa mwaka huu, watoto wake mdogo wangu walikuja kunitembelea. Sasa wakati wakula mie nikamwambia dada wa kazi kuwa haina haja ya kuweka chakula mezani aweke mkeka tukae chini tule! Tuliokulia kwenye mikeka utatujua tu 😂😂😂  mwe! Kwani hao watoto waliweza kula?! Mara namuona yule mdogo anaangaika kuvuta kiti karibu na mkeka  na mkubwa  wa kike kalalia tumbo huku akijaribu kula 🙊🙊 Nikawa nashanga, ndio mama yao akasema unajua wanangu hawajui kula huku wakiwa wamekaa kwenye mkeka!! Akasema "Wakenya hao wanajua kula ni mezani tu" 😀😀 mbona yalinishuka ikabidi tuhamishie chakula mezani, basi wakawa na amani wakala kwa furaha!  Mdogo wangu alipoona hizi picha za Tiffah akanitumia na kusema kama mtoto wake angepiga picha hiyo ambayo ameshikilia glass ya juice baada ya picha za birthday ya Nillan kutoka basi baadhi ya watu angefikiri kuwa ameiga kumbe hivyo ndivyo alivyo walea watoto wake!...... Wazazi embu achaneni na kuwapa watoto glass za plastic kwanza zinaleta Cancer 😂😂  honestly, bora umpe mtoto kikombe cha bati kuliko plastic! Nunua zile glass ngumu mfundishe mtoto kushika na kutumia bila kuvunja ili siku ukiwanae 5* hotel upati shida kwani kazoea! #Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee!!

""* Picha zote za Tiffah nimezitoa kwa Instagram page ya princess_Tiffah***

My 2017 best Tweet: “You are the air that I breathe”Kuna comment nyingi kwenye hii tweet ambazo zinachekesha sana sema nimechagua hizo tu!    

Ngoja niwaambie, kwakweli hakuna kitu kizuri kama kumuona mtu kama Dr Mengi anajishusha na kumuheshimu. kumpenda  mwanamke namna hii! Yani inavutia sana kuona mtu mwenye elimu yake nzuri sana, anapesa zake, na all the power kwenye public and yet he can humble himself like that! "You are the air that I breathe"! Hivi niwanaume wangapi wa Kitanzania ambao wamesoma labda wana Masters tu wanaweza kusema maneno Kama haya kwa mkewe ambaye elimu yake ni sawa na "sifuri" kwake?!! Enyi vijana wa Kitanzania jaribuni kuiga wazee kama akina Dr Mengi mtabarikiwa zaidi! ........And Nope! Wakubwa hawafaidi!! Muheshimu na umpende mkeo kwa dhati in private and in public nawe uone kama hauta faidi!! Muache ukatili!!!...........Kwa maana hiyo hii imekuwa my best tweet for 2017! Kama mjuavyo hii blog upendo ndio dini yetu, basi tumefurahi sana na hii tweet!

Baba_Dangote: when I say I love you true means it agah!…..The only thing I have in my life is you!

Love in the air! Hivi mnakumbuka wakati nilimtakia mama Diamond kheri ya kutimiza  miaka 50 nikauliza where is "step dad" kwasababu miaka khamsini bado kijana kabisa! Embu soma hapa (kheriyamiaka50MamaDiamond) Eeh, unajua haikukaa sana tukaanza kusikia fununu kuwa mama yake Diamond kaolewa!

Mama Diamond siku ya harusi yake
Najuzi kati kwenye harusi ya Romy Jones akatokea naye pia  mama Diamond alisema rasmi kuwa kaolewa na tusubirie mziwanda anakuja 😂😂 uzee mwisho 'kanda ya Ziwa' huku Pwani wote baby 😂👯🙌

Sasa naona kila mtu ameshakubaliana na hiyo hali na baba wa kambo naye kawa huru hata kumposti mkewe na familia yake kwenye social media! Baba kafa kazimia kwa mama, mpaka kaamua kujiita "baba Dangote" kwenye account zake za Instagram ili kuendana na jinsi mama yake Diamond anavyo jiita kwenye social media. Binafsi, I don't see a big deal at all!! After all ni mumewe halali siyo boyfriend so what the fuzzy is all about! Ingekuwa just a "strange man" sawa lakini huyu kaka kafuata mila na sheria zote za dini ya Kiislamu kuoa hivyo sasa kunatatizo gani mtu kumposti mkewe wapekee hakuna maswala ya ukewenza kusema anampendelea?!! Jamani life is too short let others be!

Baba na binti yake
Maisha ya wanawake wengi wa Kiafrika ni ya shida, many don't get the privilege to enjoy their youth! Yani kuna maisha yaliyopangiliwa na familia pamoja na jamii mtu binafsi hupati nafasi ya Ku experience life and choose what is best for you! Nakama bado haitoshi, wengi wanafiikiria ndoa zitawapa furaha matokea yake emotional abandonment is all they experiencing!!.......... Kama kwa wenzetu Waislam wanaruhusiwa kuachana kiurahisi hivyo wanawake wengi wanaishia kuteseka kulea watoto wenyewe bila msaada wa baba zao! Hivyo, pale mwanamke anapopata mtu wa kumfanya ajisikie 16 again why not?!! Let her enjoy the youth life that was once snatched away from her!! Mimi hizi double standard za Wabongo hata sizielewi!! Wanaume wanaoa wasichana ambao wamepishana hata zaidi ya miaka 30 na watu mnaona sawa tu! Lakini mama wa watu wamepishana miaka kumi tu inakuwa shida?! Ni wivu ama?? Tatizo Nyota aa  😂😂😂  Haya, wenzenu wako honeymoon South Africa wakati nyie mnaojiona wasichana wabichi mnaambulia kupelekwa  Ramada Inn Bagamoyo, kwani mmekuwa waganga wa kienyeji  😂😂  🎵🎵🎤 napenzi kama bia nileweshe ee chupa kilo mia nibebeshe ee 🎶🎶  Halafu Baba Dangote handsome boy kweli kweli, he truly needed a "Nanny" to babysit him 🙈🙈 BTW, hivi huyu stepdad hana watoto eeh? Mbona anasema "the only thing I have in my life is you"?! Kama hana basi hapo bi Sandra ata enjoy sana maana hakuna mambo ya ada za shule sijui uniform za watoto, Mara oh, watoto wanaumwa makamasi 😂😂 inahusu?!💃🏼💃🏼  #RULE YOUR LIFE

Crush diets vs Healthy eating

@Regranned from @open_kitchen2014 – Naomba leo kutoa ka elimu kidogo hizo picha mbili zote ni za mwaka huu hiyo ya kushoto ilikuwa mwezi wa nne na hiyo ya kulia ni december ila utaona kuwa kuna tofauti kubwa sasa hapo ndio uelewe tofauti ya bad crush diets na healthy eating with lots of muscle buiding kipindi cha mwezi wa tatu mpaka wa nne nilijaribu kila mbinu ili nipungue kilo 10 za mwisho zilikuwa zinanitesa sana sasa nikaanza crush diets na mazoezi yaani kwanza nilipozitoa zile kilo 10 ndani ya mwezi mmoja mwezi unao fuata zilirudi zote na zaidi nikawa very upset ndio nikaanza kusoma na kujifunza kuhusu crush diets vs healthy eating na pia nikaamua kuaza weight lifting vs cardio maana with cardio nilikuwa nanyooka tu sitengenezi shape at all nilikuwa kama mti wa fenesi 😂😂😂😂😂😂 lakini sasa hivi kidogo Alhamdulillah hata kijingu cha kukorogea uji kinaonekana japo sio cha kusimamisha chupa ila maji yanatuama kidogo 😂😂😂😂😂😂😂 .
So naomba ujue kuwa crush diets are not healthy kabisa kwasababu kwanza sukari yangu ilikuwa inashuka sana because nilikuwa nakula kidogo nafanya mazoezi zaidi and that was very dangerous nakumbuka kuna siku nimetoka kukimbia 10k nikahisi kuzimia nakuja kupima sukari ipo 3 yaani i was so scared so ni muhimu kuelewa madhara ya crush diets na pia ngozi yangu ilikuwa mbaya sana yaani nilikuwa najitahidi sana ku moisturise lakini bado ilikuwa haina mvuto mda mwingi ilikuwa inabebwa na make up 😂😂😂😂 na pia nilikuwa so weak mda mwingi nina fatigue sana so i stopped huo ujinga kabis a .
..
Sasa hivi navaaa size 14/16 mwili wangu upo shaped vizuri na ninaendelea kila siku kuutengeneza sitaki kupungua zaidi ya hapo nimeridhika kabisa mimi sina skinny body frame so mwili wangu hauwezi kuwa kama beyonce never ever 😂😂😂😂 lazima uwe na target inayoendana na body frame usije ukawa kama a walking zombie maana kila nguo ukivaaa unaoneka kama imetundikwa , uso mpaka unakosa nuru mtu akikuangalia sura inakuwa kama inamzomea 😂😂😂😂mambo gani sasa hayo ..
. . So sasa hivi yes mwili wangu unaoneka thicker na abit more masculine and i love it AMKA TWENDE HATA WEWE UNAWEZA –