Category Archives: Mahusiano

Mkuki kwa Nguruwe kwa binadamu mchungu……. !

Kuna watu wanajifanyaga kuwa wao wanajua jinsi ya kufanya maamuzi mazuri kuliko wenzao, wako wepesi sana kusema matatizo ya watu na kuhukumu wengine kwa maamuzi wanayo fanya! Sasa ikatokea maamuzi uliyofanya hayakuzaa matunda mazuri mbona utakoma! Lakini ikiwa yeye ndio  kafanya maamuzi ambayo siyo sahihi atatafuta kila njia ya   Ku justify hayo makosa na kutumia gharama zote kuficha makosa yao. Sasa huyu Tamar Braxton ni mmoja ya watu wenye tabia kama hizo. Yani huyu alikuwa mwepesi sana kusema dada zake kuwa wamechagua wanaume wasiofaa  na ndio maana ndoa zao zina matatizo. Msikilize hapa 👇

Kuna siku pia alimuita Ex husband wa dada yake kuwa ni "baby sitter" kwamba hana faida yoyote kwa dada yake wala watoto zaidi ya kuwa kama mfanyakazi wa kulea watoto. Dada yake alichukia sana na kuwambia kuwa Andre anaweza asiwe mume mzuri lakini ni baba mwema sana kwa watoto wao na hato weza kumvumilia kuona anamdhalilisha baba wa watoto wake. Tizama hao 👇

Sasa leo hii yamemkuta matatizo kwenye ndoa yake mpaka anadai talaka sasa amekuwa MBOGO! Hataki hata kuongea na familia yake kuwaelezea ukweli kuwa ndoa yake naye ilikuwa ni mbovu tu kama yao ila alikuwa anaficha. Yamemkuta yale yale aliyokuwa akiwaambia dada zake, kwa aibu anashindwa hata kuwaambia dada zake kuwa amekwenda mahakamani kudai talaka. Dada zake wamejua kuwa mdogo wao amekwenda mahakamani kudai talaka  baada ya kusoma  kwenye mitandao.  Halafu dada zake wanapotaka kumuuliza ili wajue ukweli anakuwa mkali kama pili pili!  Majibu ya shortcut huku akitumia Mic kama "defensive" mechanism! Embu mtazame hapo 👇

Unajua kama hayajakufika kama hujui ku sympathize na matatizo ya watu basi ni bora ujifunze kunyamaza kuliko kuhukumu wenzio unafanya wajione  like something is wrong with them! Wakati jambo kama hilo au tatizo lolote lile linapokukuta unakuwa mkali hutaki kuulizwa  wala husikii kitu!

Nasikia Tamar amekuwa very sensitive na ame withdrawal kutoka kwa familia yake. Yupo very protective kulinda image ya mume wake.

Masikini Vince anatia huruma! Anataka ku fight for his marriage. Nafikiri ni vile anajiona yeye ni yatima na amekuwa kwenye Braxton family karibia miaka 20 na zaidi. Kumbuka Vince alikuwa Manager wa Toni Braxton kwa takribani miaka 10. Mkataba wake wa umeneja ulisitishwa baada ya kuamua kumuoa  Tamar kwani Toni alisema hawezi kuchanganya undugu na kazi akimaanisha Vince amekuwa shemeji yake. Wakati huo huo kunatuhuma za domestic violence kati ya Vince na Tamar ambazo zimetolewa na mama yake Tamar. Kama asemacho mama mkwe wake  ni ukweli basi nitakuwa nimeshangaa sana!! Kupiga mwanamke?! No! big No!

Mmh! Wishing her the best, nimefurahi sasa atajifunza kutokana na makosa. Maybe she will learn to put her ego down because she learned her lesson in a very hard way!

Zamaradi Mketema: Mtazamo wangu- Part 1

Regrann from @zamaradimketema - PART 1

Wanawake kulegalega kwenye majukumu yao kunachangiwa sana na wanaume kuacha na kusahau WAJIBU wao ndani ya nyumba, lazima tuwe wakweli hivi vitu vinaenda pamoja

Kumekuwa na malalamiko mengi juu ya wanawake sikuhizi kuwa si watu wa kujali nyumba zao kama ilivyokuwa awali, na mzigo mkubwa wa lawama unatupiwa wanawake bila kuangalia kulia na kushoto kwenye MIANYA ya VYANZO vya namna hii

Katika majumba mengi sikuhizi ni ngumu kutofautisha nguvu ya mwanamke na mwanaume katika kile kinachowekwa mezani (kipato), zamani ilikuwa Baba ndio anaengaliwa kwa macho yote lakini sikuhizi wamama wamekuwa na mchango mkubwa sana kwenye familia nyingi, kitu ambacho ni kizuri na wote tunakubali, TUNACHOSAHAU kila Zuri linakuja na athari zake, tusifurahie tu mazuri halafu tukataka kufumbia macho NGUVU ZINAZOTUMIKA na JASHO LINALOTOKA katika kuleta mazuri hayo.

Hata vitabu vya MUNGU naamini vya pande zote vilizungumza juu ya MWANAMKE KUZAA KWA UCHUNGU na MWANAUME ATATAFUTA KWA JASHO. Lakini leo hii vitu ni tofauti, mwanamke haangaliwi kama mwanamke tena, na ndiomana hata waoaji wengi wa sikuhizi (sio wote) wanataka mwanamke atakaekuwa angalau na mchango kwenye familia, matokeo yake mwanamke anabeba misalaba yote na zaidi, atazaa kwa uchungu, atalea kwa mapenzi, na sio watoto tu hadi Baba, ataangalia na kulinda nyumba, na majukumu yote ya mwanamke yanayoonekana ni ya kwake, na pamoja na hayo yote BADO ATATAFUTA KWA JASHO, ambalo si jukumu lake, na kwa jinsi wanawake wa sikuhizi wanavyoweza kuchakarika hakuna ajabu ya kuona anachokileta nyumbani yeye ni kikubwa kuliko cha baba, kweli bila hata kufikiri mara mbili unaendelea kulaumu nwanamke wa namna hii kuwa labda hakai chini kumfulia mumewe n.k, hebu jiulize kuna MAJUKUMU MANGAPI yasiyo ya kwake anayojikuta ameyabeba!! 

Na huenda yalistahili kufanywa na mwanaume, Kazi yake sio kutafuta kwa jasho lakini anatafuta, na huenda bila yeye kuhangaika watoto hawatasoma inavyostahili, mbali na hiyo bado atahangaika kuhakikisha kila kitu kiko sawa nyumbani hata anapokuwa mbali, hali ya kuwa Baba ni Baba tu na jukumu lake moja tena mara nyingine HALIFANYI INAVYOTAKIWA, maana wanaume wengine utakuta aki

Zamaradi Mketema: Ni Makosa yetu wanawake

Miriam Kinunda author of  Taste Of Tanzania: Modern Recipe for the West https://www.instagram.com/miriamkinunda/

Regrann from @zamaradimketema -Kwenye comments nimegundua wanawake wanalalamika na mzigo wanaoubeba wao kwenye majukumu ya familia, ila MAKOSA mara nyingi yanaanzia kwetu, wanawake wengi WANAWALEMAZA sana wanaume wao wenyewe kwa kuhisi wanawasaidia, kwa bahati mbaya hii haina faida kubwa mbele ila hasara.

Tukirudi kwenye nature mwanamke ameumbwa kutunzwa hata vitabu vyote vya Dini vinasema hivyo, na ndiomana ikiwa tofauti madhara tunayaona, mwache mwanaume awe mwanaume hata kama umemzidi kipato, nature ya mwanaume ni KUTOA na kujihisi ANAMILIKI na ndio uanaume wake unapokuja, anapokutunza anafeel uanaume wake, hata uwezo wa kunguruma anaupata ndani, mpe hiyo nafasi usimnyime, hata kama wewe una mia yeye ana kumi hakikisha katika kumi yake lazima utaratibu wake wa kulisha nyumba ubaki palepale kwa kidogo chake hikohiko, we utatumia tu akili jinsi ya KUMSAIDIA ila usimlemaze akaona wewe ndio kilakitu na kumpa nafasi ya kutulia, hakikisha kila anapotoka anaacha kinachostahili hata kama ni mia tano, mfanye awe mume, maana athari za wewe kuibeba familia mara nyingine zinaenda pabaya zaidi hadi kuharibu mahusiano.

Na ndiomana kuna fikra isiyo rasmi kuwa wanaume wengi wanaoishi na wanawake wenye uwezo zaidi yao hutafuta nyumba ndogo pembeni za hali ya chini na kuzihudumia kwa hikohiko kidogo, lengo ni kutaka kuutoa uanaume wake, anataka mamlaka yake yaonekane, anataka akiongea asikilizwe, mpe nafasi hata kama una uwezo, hiyo ndiomaana ya kuwa KICHWA mfanye awe kichwa kwa vitendo, hata kwa umasikini wake onesha unamtegemea yeye na umtie moyo afanye kadiri ya uwezo wake, sio ndio unazo basi yeye anakuwa kama mtoto mdogo sasa ndani unamuacha moja kwa moja hapana, au unajifanya huhitaji kitu kwake unakosea. Ukitaka kujua hii ni nature hata kwa upande wa wanawake ndiomana hakuna feeling nzuri kama kupewa/kutunzwa na mwanaume wako hata kama una kilakitu, sababu nature iko hivyo!! Ndiomana si ajabu kukuta mwanamke tajiri lakini akamtamania mwenzie wa hali ya chini kwa kununuliwa mkufu tu, pamoja na kupata kilakitu kwa jasho lake bado kuna kitu kinamiss, kuona mtu anasimama kwake kama MLINZI na mtunzaji wa maisha yake, MUNGU ndio kaumba hivyo!! Ila siku hizi eti wanaume ndio wanalindwa. Ni Kosa!! Regrann from Zamaradi Mketema

Nguvu iliyowekwa ndani ya mwanamke inaweza kumpa furaha na amani kila mwanaume atakaye ijua nguvu hiyo!

IFIKE MAHALA WANAUME TUWAHESHIMU WANAWAKE KWA JINSIA YAO na sio kuwapa kipaumbele kwa haja zetu za ki mwili, Mwanamke hatajwi kama kiburudisho cha Mwanaume, Mwanamke anatajwa kuwa UBAVU WA MWANAUME... Mchukulie Mwanamke kuwa sehemu ya Maisha ya kila mwanaume aliye timilifu "RIJALI" na hapo ndipo heshima ya Mwanamke itapatikana ndani ya akili yako, Mwanaume kumchukulia Mwanamke kama chombo fulani ni kujilaani mwenyewe maana NGUVU ILIYOWEKWA NDANI YA MWANAMKE INAWEZA KUMPA FURAHA NA AMANI kila mwanaume atakaye ijua nguvu hiyo. Mwanamke anazo nafasi nyingi kwa Mumewe ikiwa atapewa heshima, kutomheshimu Mwanamke ni kujishusha ki akili maana Mwanzo wa Mwanamke ni DADA na baadaye anakuwa MAMA achilia mbali hayo Mwanamke ni PAMBO LA MOYO WA MUME! Kumuacha Mwanamke akihangaika na kuteseka na watoto "FAMILIA" ukaangukia kwenye uhuni usokuwa na maana ni kujiwekea laana na mahangaiko siku zote za maisha yako, Mwanamke anapokuwa ametelekezwa MAISHA YAKE YOTE HUISHI KWA MASONONEKO na mpweke, Hakuna mtihani mgumu kwa Mwanamke kama KUOLEWA NA MWANAUME ASOJUWA SABABU YA NDOA... Hakuna Mtoto hupatikana kwa bahati mbaya maana maandalio ya mtoto yanapatikana kwa muingiliano wa ki mwili baina ya Mwanaume na Mwanamke "TENDO LA NDOA" inapofika mahala wanaume wanashindwa kutambuwa majukumu yao ya ulezi kwa watoto wao ilihali wakati wa mahitaji ya ki mwili aliweza kupambana juu ya ushawishi ni DHAMBI! Nanyi wanawake muwage mnaangalia na wanaume mnaokutana nao, Saa zingine SURA HUONGEA na muda mwingi MTU MBAYA HUJIKITA KWENYE UONGO ili kuificha tabia yake halisi.

#Elista_kasema_ila_sio_sheria 😉

***Imenukuluwa kutoka Elista Realif For Heart*** 

Joyce Kiria: Haya MACHOZI yangu namlilia Mungu wangu aliye juu, yeye ndo ataamua

@Regranned from @joycekiriasuperwoman - Changamoto kubwa 2018 #Kipigo
Sikutegemea kama ipo siku kwa mkono wako ungeunyanya KUNIPIGA @kilewo2020mwanga 😭😭😭😭 * Ukasahau kabisa! Ukasahau yooooote.. nimeharibu career yangu kupigania ndoto yako kwa kugawa watu wangu kwenye biashara zangu, nimepoteza ndugu jamaa na marafiki, umeniachia nimebeba mzigo wa familia kwa muda wote... Malipo yako ni KUNIPIGA/ KUNIDHALILISHA/ KUNITOA MACHOZI😭😭😭
Umenipiga kwa sababu Mimi Ni MNYONGE siyo! SINA NGUVU, kwa sababu ni MWANAMKE Sina nguvu za kupigana na MWANAUME ... Umeniumiza mwili wangu unauma kila mahali umefiria damu na kichwa ukanigongesha kwenye gari, ili iweje? Nia yako ilikuwa ninini? kuniua??? Mungu amenipigania.

 Haya MACHOZI yangu namlilia Mungu wangu aliye juu, yeye ndo ataamua...😭😭😭😭😭😭 Kama NI Mimi niliandamana na watoto, nikakufanyia kampeni na deni kubwa nikaingia mpaka nikafungiwa Kipindi hewami, ninakutunza wewe na Watoto wako kwa miaka yote, MUNGU YUPO.... LEO UMENIPIGA @kilewo2020mwanga ??? Sawa watakusifia hao wanaokusifu ujinga, wanaokuambiaga Mimi sikuheshimu, badala wakwambie ufanye kazi utunze familia, Leo watakuona wewe ni MWANAUME kwa KUNIPIGA... - #regrann

Zamaradi Mketema: Kumbuka details ndio zinazotengeneza PACKAGE, na package ya ukweli unayoifahamu ni wewe

@Regranned from @zamaradimketema – Ukiona MAAMUZI yako yanaangalia sana watu ujue una hatihati ya kuharibu maisha yako, kuna watu wanategemea sana ushauri na APPROVAL za ndugu, jamaa wa karibu na marafiki katika kila kitu bila kuchuja mengine aone ni ya kwake na yanamuhusu yeye tu, tusichofahamu linapokuja swala la hisia na mahusiano hakuna ubaya wa kusikiliza lakini fata kulingana na moyo wako, wengi wanaokushauri watakushauri kulingana na interest zao juu ya huyo mtu au vile wanavyomuona nje, lakini kumbuka wewe ndio unaishi nae na ndio mwenye moyo. Na zaidi kuna vingi unavyovijua ambavyo wao hata wawe karibu kiasi gani hawatakaa wavione, na hata kama mnahadithiana mara nyingi mnaongelea matukio na sio DETAILS, na kumbuka details ndio zinazotengeneza PACKAGE, na package ya ukweli unayoifahamu ni wewe, ila kwa kutaka kuridhisha watu unaweza jikuta unaacha kufanya maamuzi sahihi kwakuwa fulani kakwambia sio sawa tena kwa kuangalia tu kile ULICHOMUAMINISHA NACHO ama kumwambia, mwisho wa siku athari za UKWELI unabaki nazo wewe. Kumbuka tu Washauri ni wengi kwenye maisha lakini hawana msaada wowote na wewe pale linapokukuta, watu wapo kila siku lakini hupaswi kuwazingatia kiasi mpaka ukasahau lenye umuhimu na wewe kwa kuwapendezesha wao, wao wanafanya ya kwao bila kujali utawahukumu vipi na ya kwako yatakapoharibika utakaekaa ndani kulia ni wewe peke yako, na zaidi hawatakuwepo muda wote kwa ajili yako. – #regrann

Joyce Kiria: Maisha ya Ndoa bana yana mambo jamaniii mwee……!

Joyce Kiria

Maisha ya Ndoa bana yana mambo jamaniii mwee, unaanza vizuuri kabisa kuwa “Mke” mtamuuuuu, kisha Polepole unakuwa “mama Fulani” Mke wa mtu, kisha taratiiibu unakuwa “Mlinzi” baadae “mlezi” kuna “mtunza nyumba” kuna “Mpishi” kuna “mfuaji” kuna “furniture” uuuuuuwwwwiiii nkinkiiii ruwa mangiiii ?? (Usiombe Mume awe chini ya Miaka 45😢) utashaaaaaaaaaa…. — Jipe tuu Furaha mwenzangu, tuishi kama single flani amazing, akiwepo sawa akisepa sawa, tusingoje Furaha Toka kwa Mwanaume.. Tutaiskia kwenye filamu! Akili za usiku #NaesabuBati 😢😢 #NikoDirishani ##AnatokeaWapiNifungueMlango

ASANTE SANA @didavitengewear kwa mwonekano wa kitenge… @rosebrazilian kwa Nywele… Twende SAWA… Kama una neno lolote weka hapa

 

“Ukiniuliza Mimi nitakuambia huyo asiyekua lolote wala chochote Leo ndio mzuri….”~~~Rose Shaboka

Nguo unayoinunua dukani ikiwa READY MADE wakati mwingine sio rahisi kuirekebisha iwe exactly unavyotaka. Lakini nguo unayoenda kushona kwa Fundi kuanzia mwanzo ni rahisi sana kuitengeneza ikawa exactly kile unachotaka. Msichana unayetaka na kuomba mwanaume ambaye tayari ana kila kitu (ready made) hujui unachokiomba. Sio vibaya ukipata mtu ambaye ana kila kitu tayari lakini nakuambia usimkatae wala kumdharau huyo ambaye hana kitu Leo. Ukiniuliza Mimi nitakuambia huyo asiyekua lolote wala chochote Leo ndio mzuri na ukishirikiana na Mungu vizuri unaweza kumtengeneza akawa unavyotaka na anachotakiwa kuwa kirahisi sana kuliko yule ambaye ameshatengenezwa usivyotaka. Mimi kama Fundi ukiniletea hicho kitambaa ambacho hakijashonwa ni rahisi kutengeneza unachotaka kuliko ukiniletea nguo ambayo ilishashonwa kitu kingine niitengeneze iwe kitu kingine. Huyo mwanaume asiye na chochote Leo ni kitambaa kipeleke kwa Fundi anaitwa Yesu akutolee style moja matata itakayokutosha katika hali zote ambayo macho hayajawahi kuona, masikio hayajawahi kusikia wala akili za mwanadamu hazijawahi kufikiria Yale mambo Bwana amewaandalia wampendao.

#mchungaji anapokua Fundi cherehani hata kwenye vitambaa vya kushona anapata mafunuo#
#kila jambo lina majira, hata kukosa kuna mwisho hatakua maskini milele, usimdharau#
#pastors new day church, power house#
#victoria petrol station#