Category Archives: Parenthood

Chuki, ubaguzi, na upendo mtoto ufundishwa na wazazi wake!

Chuki na ubaguzi mtoto ufunzwa na wazazi wake kama ilivyo upendo! Mtoto anazaliwa na kichwa che ubongo mtupu na safi! Sasa wazazi na walezi was hawa watoto ndio inategemea watajaza huo ubongo was huyo mtoto na vitu gani! ........Nisawa na elimu kuhusu Mungu, mtoto hawezi jua umuhimu was kuabudu na kumcha Mungu kama wazazi na walezi wake hawakumfundisha na kumuonyesha kwa vitendo kuwa kuna Mungu anaye stahili kuheshimiwa na kuabudiwa! Au utakuta Mzazi anamwambia mtoto wake hiyo nguo mbaya mpe fulani (ana taja jina la mtoto mwingine) hivyo mtoto anakua akijua kuwa kama kitu kibaya au kimezeeka ndio unagawa kwa wengine! Ambapo ni makosa makubwa sana! Mzazi mfunze mtoto wako kuoenda watu wote wa rangi zote bila kujali kipato chao cha kiuchumi!

Tamera amenifanya nijisikie kuolewa na mzungu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ I’m curious to see how my baby will look like πŸ™ˆπŸ™ˆ

Malia Obama ndani ya “hot topics”!

Ule usemi uliotumika sana na Β wahenga wetu kuwa “mtoto umleavyo ndivyo ukuavyo” unaweza usilete maana sana katika kulewa watoto wa karne hii ya 21! Hivi karibuni kama wiki na siku kadhaa zilizopita binti wa Mstahafu Rais Baraka Obama, ajulikanae kama Malia Obama alikutwa akibusiana na mwanaume ambaye aliaminika kuwa ni boyfriend wake katika viwanja vya chuo kikuu cha Harvard university na pia alionekana akivuta sigara. Tazama kwenye hii video kuanzia dakika ya 22.50 kama inavyoelezewa na gwiji wa “hot topics” Wendy Williams Β πŸ‘‡

Sipati picha Michelle Obama alikasirikaje, unaweza zimia bila “kizimio” 🀣🀣 Halafu sasa kutokana na sheria za huku Malia Obama anatambulika kama mtu mzima ambaye anaweza fanya maamuzi yake binafsi na wazazi wanatakiwa kuyaheshimu! Najua hata Africa ukishafika 18+ unatambulika wewe ni mtu mzima kwenye karatasi za serikali lakini kiuhalisia wazazi wetu wengi bado wanakuwa na mamlaka juu yetu na kutufanyia maamuzi mengi juu yetu. Ni mfumo wa tamaduni zetu ambao unafanya watu wengi kutokuwa na mawazo huru na kufanya maamuzi ambayo yanampendeza yeye na kwafaida yake kwanza. Funguo za furaha zetu zipo mikononi mwa watu kama wazazi, marafiki, na jamii na ndio maana wengi ni wanafiki na waongo kupita kiasi! Β Lakini vile vile lazima tukubaliane kuwa kila familia lazima iwe na identity yake! Kila mtu anazaliwa tofauti lakini kama familia lazima muwe na kitu kimoja ambacho watu watajua na kuwatambua nacho. Hivyo sishangai kwanini Michelle na Baraka wamekasirishwa na kitendo hicho. ……..Mungu atusaidie sisi ambao tunataka kuzaa na wale ambao wanalea katika karne hii ya 21 kwani changamoto ni nyingi mno!

The Teshas’!

What a beautiful picture! The Teshas’ katika ubora wao! Wamependeza sana! ❀ It! Β Quote for today:

“Not only the presence of love fed the life of a family but there’s more to it in reality…”~~~~ UnknownΒ 

“….but attitude hata punda ako nayo” ~~~Akothee Akothee

haki I cant stand seing people asleep when am already awake by 6.00 am, I go round the house expecting to meet them awake about 8.00am, no way, only to find them fully covered in their warm blankets which they dont even know the prizes, then come to the kitchen and harrass the chef for breakfast at about 11.00 am, while the chef is already preparing for lunch, are this kind of people normal or am the abnormal one, or could I be jelouse that I cant sleep past 6.00 am & some could? am I the one who knows the value of time or am I working too hard and they be working smart under the blankets? call me acomplaining molecule, but this generation is lost period 😷😷 I like the way my kids look at me with bad eyes when I knock on their doors πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚, but attitude hata punda ako nayo , utaamka mama,
 Rule no. 
1 . No househelps should attend the girls rooms , nor their laundry 
2.  The cheff is for madboss so if you wake up late , prepare your own breakfast 
3. All the rooms in my house shoud ready by 10.00 am , so enda ulale kwa nyasi , ama uende kwako 
4. No one comes to the table for lunch with a night dress , please shower before we meet 
5. No tv during the day , no one is watching tv unless you are done with your work take it or leave it, you have freedom of migration. You cant migrate to anywhere, my girls follow suit, so any visitor should be at par with us πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Baba Oyoo & Baba Ojwang have no househelps, they do things by themselves yet they should be retiring, with full pockets, you that has no bank account, you are afraid of breaking your nails πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚, come slowly slaying queens, Oyoo and Ojwang knows that after food you take your plate back to the kitchen, so who are you?

Mother and daughter moment!

Beautiful Emelda Mwamanga na binti yake Gabby! So nice! Nivizuri kuwapenda watoto wetu zaidi wakiwa katika umri huu mdogo kwani inawajengea kuamini, kutambua thamani yao wakiwa wakubwa, Β na kuwa wajasiri! Mtoto yoyote yule anahitaji muongozo, na mipaka lakini pia anahitajika kuwa huru haswa kifikra! Hivyo nijukumu la mzazi kumjenga mtoto wazingira huru ya kujieleza na kutafakari ambayo yana boundaries at the same time!
Mtoto siyo mdoli jamani, mfunze mtoto maadili mema, na jinsi y kuweza kukabiliana na hali zote za maisha. Kwamfano hapo Gabby unaona amefundishwa kupika na kuchanganya vitu kwa kutumia blander hivyo hata akienda kwa watu ambao wanatumia "high tech" kitchen appliances hashangai sana. Napia anajua jinsi ya kutumia mikono yake kushika vitu! Nilishawahi kuona kwa macho yangu mtoto wa miaka nane (8yrs old) bado anatawazwa akimaliza kutumia choo πŸ™ˆπŸ™ˆ Yani anajisaidia haja kubwa halafu anita dada wa kazi au mama yake amsafishe! And the mother was very OK with it πŸ™ŠπŸ™Š Jamani!! Anyway, those are rich people problems, maskini kama sisi tutayawezea wapi? πŸ˜…πŸ˜…

 

Life has more to offer than just slaying ~~~~~ Akothee Akothee

Mwanamuziki toka Kenya Akothee Akothee, anasema hivi mjengee msingi mzuri wa maisha mtoto / watoto wako ili wawe na manufaa baadaye katika maisha yao! Maisha yanatoa maana nyingi zaidi ya kujipondoa tu! Mfundishe mwanao kupika, kufanya usafi, kuheshimu watu, jinsi ya kutumia na kutafuta pesa n.k Kuna wazazi wengine wamegeuza watoto kama toys! Yani ni kujiremba na fashion za nguo bila kujua watoto wanatakiwa kupewa muongozo wa maisha na maadili ya kuishi hapa duniani na kubwa zaidi kumjua, kumuheshimu, na kumtunikia Mwenyezi Mungu! ......... embu msome Build a foundation for your girlchild , so they become usefull in the near future , life has more to offer than just slaying , a woman has to know how to cook, we're learning how to cook ugali & chapati today , @ruebaby @ #teambigfive @fancy_makadia @veshashaillan we set 

Mother and son moment!

Wamependeza eeh! Glory na handsome boy wake! Nimependa sana nywele za Glory, zimempendeza mno! Nywele fupi zinawatu wake lazima kichwa kiwe kina "pembe" zilizo lingana Β lasivyo utachekesha wafiwa πŸ™ˆ .......Safi sana .....I ❀ it
Today's Quote : "Men are what their mothers made them."~~~~~~ Ralph Waldo Emerson
Eti jinsi mama umleavyo mtoto wako wa kiume ndivyo atakavyo kuwa atakapo kuwa baba / mume /mtu mzima! .......Kwa mfano, kama hauto mfundisha thamani ya mwanamke na jinsi ya kuwaheshimu wanawake basi hawezi elewa na akiwa mume / baba hatojua jinsi ya kuishi kwa kumuheshimu mumewe au watoto wake wakike kwani haukumfunza hivyo! Bible inasema mlee mtoto katika njia mpasayo naye hataiacha hata akiwa mzee! Anaweza akajikwaa na kutoka nje ya mafunzo au malezi uliompa lakini hato potea milele kwani lazima nafsi yake itamsuta kuwa haya niyatendayo siyo malezi niliyopewa na mama yangu. Hivyo atarudi katika njia sahii!...............Mbarikiwe sana wamama wote wenye mapenzi mema kwa watoto wenu.

The journey to motherhood: Congratulations Nambua Cassandra!

Alpha Igogo -bloggerWapendwa wasomaji wangu, naomba niwaletee tukio zuri sana la safari ya kuzaliwa mtoto Prince. Ni tukio ambalo limekuwa recorded na shemu ya hiyo video imeonyeshwa na mama mzazi kwa kupitia account yake ya Instagram! ……….. Kwanza nianze kwa kusema hongera sana kwa Nambua kwa kujaliwa mtoto wa kiume! Mungu amlinde akuwe katika kimo na hekima. Akampendeze Mungu kwanza na kisha wanadamu! Karibu katika chama cha wakinamama/ wazazi! Safari hii ni ndefu, yenye changamoto nyingi lakini ni tamu mno! Nasema nitamu mno kwani kama kuna kitu nime furahia kwa 100% Β na bado naendelea kufurahia with all the pride is being a mother! Lakini kila siku namrudishia sifa na utukufu kwakwe Mungu maana bila yeye hakuna litakalo wezekana! ……..kwakweli nimependa sana hii familia ya Mr and Mrs Mlaki! Nimependa sana their spirit, wako so open and together, inapendeza sana mfano mzuri sana wa kuigwa katika jamii! Hii dunia imeshabadilika (21st century) kuna mambo mengi ya karne 19 inabidi kuyaacha maana siyo tu jamii haiipi nafasi bali pia hata technology haivitaki! Kwa mfano katika karne hii 21 n* kitu cha kawaida kabisa katika jamii zilizo ona mbele mama na kijana wake kuwa ndani ya chumba cha upasuaji wakimuangalia binti/ dada akileta kiumbe kingine duniani! Wakati jambo kama hilo bado linaweza likawa tatizo katika sehemu nyingi za Africa! ……….. Maelezo yote ambayo yameambatana na picha yameandikwa na Nambua ambaye ni mama mzazi wa Prince! Β #NaniKamaMama.Β Yesterday 4th June, 2017 was one of my big day osn earth. Nimepata experience ya ajabu sana katika maisha yangu. Mwenyenzi Mungu Muumba Mbingu na Nchi amenijalia kujifungua mtoto wa kiume 9.25am South African time. HIYO NI FIRST FOTO ALIPOTOKA TUMBONI KWANGU, ALIPOTOLEWA KAANZA KULIA. Ilikuwa sala yangu kujifungua mtoto wa kwanza DUME. I’M OFFICIALLY A MOTHER. Jana usiku sijalala kabisa nimekaa natoa macho, namshangaa huyu mtoto. Bado siamini kama ni mtoto wangu, namuona stranger, mgeni flani hivi. Na sikujua watoto wanatoka mbali hivi. Heshima kwa wamama wote waliozaa.Β πŸ˜˜πŸ˜™. Napenda kuwashukuru wote waliokuwa na mimi katika hii safari yangu. Nikisema nitaje majina mengi sitamaliza. Surely it was a long trip. My brother @laumlaki huyu ni commando aliingia theatre aka record tukio zima la Cesarean operation na mama yangu @lwisemanka amempokea mjukuu wake. Lord Jesus I give you glory. In Christ I have made it to God be the Glory. Yeremia 29:11 HAKIKA MAWAZO YA BWANA NI MEMA JUU YANGU, Yeremia 33:3…… BWANA AMENIONYESHA MAMBO MAKUBWA MAGUMU NISIOYAJUA.

Hapo niko theatre (operation room) najindaa nimlete mwanangu duniani. Nacheka cheka tu naona wanachelewa……πŸ˜€. Niko na mama na mdogo wangu @laumlaki paparazzi. Hili tukio kwangu ni very historical considering mahala nilipotoka. Nilisema Im going to record kila kitu wakati najifungua niweke ktk dvd. Namshangaa Bwana Yesu na matendo yake makuu juu yangu. Nawashukuru sana MEDICLINIC, SANDTON. Doctors & Nurses are very friendly na makini ktk kazi. Biblia inasema katika torati: Mateso ya mwenye haki ni mengi, lakini BWANA humponya nayo yote.πŸ€”πŸ€”πŸ˜πŸ˜πŸ˜ƒ Amen.Β 

My mother @lwisemanka, my mdogo @laumlaki and my photographer ms melody, hawa nilikuwa nao theatre. Walitaka waone ceserean section inavyokuwa, yani kila kitu na wawe wa kwanza to see my baby. Nimewaita mashilawadu wangu.πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€…….. love you all. Kweli watoto wanatoka mbali sana. Halafu hili zoezi nimelipenda sana la kuingia theatre na familya yako au photographer wako.

Hapo nimetoka kutoa mtoto tumboni naumwa sana, nimezinduka. Koo limekauka kwani niliwekewa oxygen. Yani kuitwa mama aisee ni kazi! Nafundishwa kunyonyesha naona ni adhabu halafu siamini kama nitaitwa mama. Shikamoo mwanamke. Naomba wanaume wawaheshimu wale wanawake waliozaa wakawafanya wakaitwa wababa. Hii experience ni ya ajabu. Wamama shikamooni. Kuanzia leo simgombezi tena mama yangu……. Biblia inasema ZABURI 34:19-21 MATESO YA MWENYE HAKI NI MENGI LAKINI BWANA HUPONYA NAYO YOTE.HUIHIFADHI MIFUPA YAKEΒ MY FIRST BORN,UZAO WANGU WA KWANZA…… BWANA MUNGU AKASEMA HAKIKA NITAKUBARIKI NAE AKANIBARIKI NA HUYU KIUMBE KATIKA JINA LA YESU …………… PRINCE THAT HIS NAME.NI PRINCE MTOTO WA MFALME WA WAFALME, JEHOVAH RAPHA. TODAY HE IS ONLY 15DAYS OLD NA AMEANZA TO POZI TAJIRI MTOTO. I LOVE YOU MY SON. I LOVE YOU. HUYU KIUMBE NIMEMJUA SIKU 15 ZILIZOPITA ILA NAMPENDA KULIKO VIUMBE VYOTE DUNIANI…….😘😘😘😘 MY LIFE HAS CHANGED 100%. #nambuacassandra @baby.mix.baby.Β 

Me and My baby PRINCE that his name (tajiri mtoto)…… hapo yuko 12days oldπŸ˜€πŸ˜πŸ˜‡πŸ˜˜. Na nilipokuwa natafakariπŸ€”πŸ€” siku zangu duniani, Nae Mungu akasema na mimi akaninong’oneza MWANANGU NEEMA YANGU YATOSHA JUU YAKO. MGHH SIKUAMINI……. ILA LEO NIMEIONA NEEMA YAKE KWA KUNIZAWADIA MTOTO WA KIUME SAWASAWA NA HAJA YA MOYO WANGU. (Heart desires) πŸ˜‡πŸ˜‡πŸ˜‡ Neno la Mungu linasema (Torati) Zaburi 37:4-6 Nawe utajifurahisha kwa BWANA. Naye atakupa haja za moyo wako. Umkabidhi BWANA njia yako, Pia umtumaini, naye atafanya. Ataitokeza haki yako kama nuru. Na hukumu yako kama adhuhuri……. #nambuacassandra #huumchezohauhitajihasira

***HONGERA SANA NAMBUA CASSANDRA***

Step-Dads, Boyfriends and Other REAL Dads Take One For the Team

Bado tupo kwenye moment au mwezi wa kusherekea na kuwaenzi baba zetu! Baba si yule aliye kuzaa na kukubwaga bila kujua nini kinaendelea kwenye maisha yako au hata kama yupo hachukulii swala la malezi yako kama jambo muhimu katika majukumu yake! Ili uwe baba kamili lazima ushiriki katika malezi ya mtoto kwani hayo ndiyo yatakayo mfanya awe kiumbe kilicho kamilika hapa duniani. Mtoto si kumpa pesa tu! Mtoto anatakiwa kufunzwa manners na life values ili aweze kuishi vyema hapa duniani!…….Sasa kuna wanaume wengi ambao wanalea watoto wa wanaume wengine kwa viwango ambavyo huwenda hata baba zao halisi wasingeweza kufanya hivyo lakini inatokea watoto au jamii haitambui mchango wao kitu ambacho kinasikitisha sana! Β Hii article imeandikwa na blogger mmoja aishie Marekani (Sarah Maizes) ambaye ni a single mama na watoto wake kwa 100% wamelela na mwanaume mwingine ambaye si baba yao mzazi. Lakini pamoja na mambo yote anayowafanya bado watoto wake hawaoni umuhimu wake na kumpa heshima yake kama baba!My boyfriend and I have been together for almost 8 years and he has helped me raise all three of my kids. My oldest is 15 and my twins are 12 and he taught each of them how to ride their bikes, how to rollerblade, and assisted each of them in building kick-ass volcanos for Science Lab. He listens to all of their problems, goes to all of their games, and buys them frozen yogurt with extra toppings when they lose. He even talked my son through his first little broken heart. He enforces chores, doles out consequences, and is all-too-often the target of the tweenage, hormone-fueled frustrations that rage under our roof. We’re a team. But, nobody thinks of him as “dad.”Β When my kids’ friends come over to our house they ask, “Is that your dad?” and my kids say “No. That’s just Scott.” Invariably, the friend shrugs and gives a confused wave before moving on down the hall towards the XBox. And you know what? I feel a little bad for him every time they do. Not because they should call him Dad – we both agree they shouldn’t. They already have a dad they see on Sundays and for dinner once a week. But after giving up eight years of his own life to be whined at, puked on and giving up his only chance to have his own kids to raise mine (and somebody else’s) with me, he deserves to be recognized as something more than “just Scott.”

This post comes from the TODAY Parenting Team community, where all members are welcome to post and discuss parenting solutions. Learn more and join us! Because we’re all in this together.

Quote for today!

Nimependa hii picha ya Kiki na baba yake. Naamini sio mimi tu naweza sema kwa mara ya kwanza kumuona baba yake mzazi Kiki. Mara nyingi nimekuwa namuona na mama yake pamoja na ndugu zake wengine. Wanafanana haswa pua. …….Wamependeza sana 😍 

QUOTE FOR TODAY!….
β€œA man’s worth is measured by how he parents his children. What he gives them, what he keeps away from them, the lessons he teaches and the lessons he allows them to learn on their own. Thankfully, there is no measurement great enough to measure the worth of my father.”― Lisa Rogers

“MTOTO ANAFUNDISHWA NYUMBANI.”~~~~~`Zamaradi Mketema

TV host Zamaradi Mketema

Kwangu mtoto kufanya hivi sio fahari ni Aibu, Hawa ndio aina ya watoto anakuwa anawaza kitu kimoja tu kichwani mwake, Kumridhisha mwanaume, juhudi zake atazielekeza kwenye kutafuta style mpya, bila kusahau vitu mbalimbali vya kupagawisha wanaume. Na wengi wa aina hii bahati mbaya waliowazunguka wanaendelea kuwatengenezea mazingira ya namna hii, wanakuwa wakiamini MAISHA NI MWANAUME TU, na ili uishi nae nguvu yako uilekeze kwenye KITANDA TU. Asilimia kubwa ya maongezi yao yamejaa hayo akiamini ndio UBORA, wanasahaulishwa kabisa kuwa kuna zaidi ya hayo kwenye maisha, wanabaki na mawazo mgando na kubaki kwenye dunia yao ya peke yao, ndio wale utasikia wanamtukana mwanamke mwenzao eti HUJAFUNDWA WEWE!!

Hapondiohuwainachekeshasababukwabahatimbayaufundajimwingiunaangaliasehemumoja tu and am sorry to say wengi WALIOUABUDU wanakuwa na mawazomgando mno yanayopeleke akuachwa na Dunia nyingine. Wadogozangu kitanda ni muhimu lakini haijawahi kuwasehemu KUU pekee ya UKAMILIFU wa mwanamke ama kumshika mwanaume, na kwa ulimwengu wa sasa kama unachojua ni kitanda tu.kunaathari nyingi utakazo kumbananazo hata katika hiyo ndoa unayoiabudu, na hakuna faida yoyote utakayo ipata, maishani zaidi ya kitanda. Mapenzi ni zaidi ya style mpya! Wamama tunaokuja tujitahidi kutotengeneza kizazi cha aina hii, tunaumiza watoto wetu, wanaishia kuwa malosers, washamba, akili ndogo, na hakuna cha maana kwenye maisha yao. Ninachoamini mtoto hafundwi siku moja, wiki moja, wala mwezi mmoja. Mtoto anaanza kufundwa tangu anazaliwa na katika ukuaji wake, MTOTO ANAFUNDISHWA NYUMBANI, Na ndio mafunzo mazuri au mabaya yanapotokea kulingana na imani unayomlisha, mazingira unayomkuza nayo na hata picha unayoionesha.

Hajawahi tabia mbaya alioishi nayo mtoto ndani ya miaka 13 au 14 ikabadilika ndani ya wiki moja za kumuweka ndani, hakuna!! Atawasikiliza tu lakini kama ana asili ya uchoyo ataendelea kuwa mchoyo, kama ana kaumalaya katakua, n.k Tuangalie RIGHT TIME ya kuwafunza hata hayo tulioamua kuwafunza kama ndio kudumisha mila na tamaduni, hakuna ubaya wa kumfunda mtu anaeingia kwenye ndoa lakini hakuna utamu wowote wa kumfunda mtoto wa miaka 12, 13, 14 au 15 ambae hana pa kuyapeleka hayo mafunzo, na hata hao wanaoingia kwenye ndoa kuna haja ya kuwapa LIFE SKILLS na sio kuwashibisha kimoja tu kisichokuwa na faida ya moja kwa moja katika ndoa yake!! Maisha yana changamoto nyingi sana, tusiwatengenezee utumwa wa akili na kuwafunga humo, kwanza angalia hata watoto ama wasichana wengi waliokulia kwenye imani ya kufundwa na kufundana katika hali ya kuabudu walivyo ama wanavyoishi kwenye jamii zao ama ndoa, kama hajaachika basi ana ndoa ya pili au ya tatu, wengi WANASHINDWA KULINDA NDOA ZAO na mpaka sasa nimefeli kujua kwanini!!

Walichokishiba wao ni kimoja tu. Hakuna bingwa wa malezi lakini mengine tunayatengeneza wenyewe, maana hapo utakuta mama yuko pembeni anashangilia na kupiga makofi huku akiona fahari mwanae anavyoyakata, jamani hata ukate mauno mpaka juu ya dari kama kuna vitu huna na hujielewi na kujitambua HAUTATHAMINIKA hata siku moja kwenye ndoa yako, na hao unaowaita wasiofundwa wataishia kukupiga bao tu kwenye maisha. TUAMKE.

Mother and son moment: DONT STOP BECAUSE YOU ARE TIRED, STOP WHEN YOU HAVE ACHIEVED

Awii! Aren’t they cute! The legendary Bosslady Zari Hassan na soldier wake katika ubora wao! Ee Mungu wabariki na uzidi kuwalinda πŸ™πŸ˜πŸ˜……………Embu soma haya maneno matamu ya kutia moyo kwa wakina mama toka kwa mwanamuziki mashuhuli kutoka nchini Kenya ajulikanaye kama Akothee Akothee:

As a mother you have no time to sit & wait , you have no time to compare your present & past , all you have is to sort out the situation at hand , it doesnt matter who is watching just do your thing , dont think of what people think about you , because most of the time people think about their own problems , so why even care about them . Do some justice to yourself , live your life, for the rest are making noise, try drop your children at your friends house for a week & lets see if the next time you call to drop the kids they will answer your call , lets see if you wont be the topic of the group charts on how irrespossible you are , bottom line is , any woman who has had a child has a wondering heart , your heart never settles not unless you have all your children under one roof , I dont know your method of hustling as long as it can pay your bills hold on to it , be proud of what you do , be happy that the children are healthy & that you have something to do ,when you feel tired of your current job , remember how they used to laugh at you when you dint have a job, remember how hard you prayed to God to give you any job , remember how you used to ask for used weaves & borrow people clothes for occasions , be patient , be kind , be gratefull , your day is coming . DONT STOP BECAUSE YOU ARE TIRED , STOP WHEN YOU HAVE ACHIEVED #TEAMPOSITIVITY.

Mother and daughter moment: Mama Essy na Essy

Ain’t they cute! Lawyer Janeth Igogo and her beautiful daughter Essy looking beautiful in a custom made African print dress! Wamependeza sana 😍😍

Mother and son moment: Mama Zion na King Zion

Ni picha ya muda kidogo lakini nimependa! Dina Marios na mtoto wake #King Zion handsome boy wa nguvu!…….Nimependa sana muonekano wao na maneno ya kwenye Tshirt! Wamependeza sana!……..Kuna video fulani inaonyesha Dina akimfundisha Zion kukaanga Kuku, nimependa sana! Dunia ya sasa maswala ya kupika siyo kazi ya Mwanamke peke yake! Hapana! Hata wanaume nao wanahitajika kujua kupika ili waweze saidiana na mke ndani ya nyumba πŸ™‚ Dunia imebadilika! …..Mbarikiwe sana mama Zion na King Zion!

Father and son moment: The Teshas’

Manhood! What an amazing picture of JT and his son! Just lovely!……mbarikiwe sana!

Don’t miss, the Mother and Child Gala April 22, 2017!

o.k.

Mother and daughter moment

Katika wazazi ambao nawahurumia pia na mu-admire sana ni mama yake Wema Sepetu! Ni mmoja wa wazazi ambao wanapitia changamoto nyingi sana katika maisha ya kila siku kutokana na maisha ambayo binti yake ameamua kuishi; hivyo kahilo namuhurumia sana! Lakini kama nilivyowai kusema huko nyuma (somahapa) kuwa ni mama ambaye ananifurahisha sana na jinsi anavyo simama bega kwa bega na binti yake, katika mabaya na mazuri! Kwa wazazi wa Kiafrika ni ngumu sana! Wachache mno wanaweza fanya afanyavyo mama Sepetu! Na kwasababu hiyo anakua mfano mzuri sana wa kuigwa! Mtoto wako ni mzigo wako mpaka kifo. Huwezi mkana au mkataa mtoto wako eti kwasababu tu haendani na maisha utakayo! Big up mama Wema!

 

Mother and son moment

Penny na kijana wake wakifurahia weekend. Wamependeza sana!Β Mwaju na first born wake. Wamependeza sana! The smile tells it all!

TAIFA LA JANA, LEO NA KESHO…. na Peter Sarungi

Imeandikwa….

1. Baba bora ni yule anayelinda na kutetea familia yake, anaye tengeneza urithi mzuri kwa watoto, wajukuu hadi vitukuu na anaye hashimu familia yake.

2. Mke mwema ni yule anaye jenga familia yake bila kuharibu kwa mikono yake, anaye lea watoto katika maadili mema na anaye simama imara na mumewe katika hali ya hatari, dhiki, shida, raha, hofu, furaha, matatizo kama ya siasa, umasikini, chuki, wakati wa ujana na uzee, wakati wa afya na magonjwa.

3. Mtoto bora ni yule anaye heshimu wazazi wake na kujifunza maadili na maarifa kutoka kwa walio mtangulia. Ambaye anapenda kuwa kichwa na si mkia.Β 

Na Peter Sarungi (Next Speaker)

#MyTake.

Vijana ambao wamefika umri wa kujenga familia wachukue hatua kufanya hivyo, wasisubiri harusi na madoido ya kifahari maana kuna maisha ya ndoa baada ya kupata sifa za harusi.

πŸ‘‡πŸ‘‡Fidel Pilato alikuwa akiangalia post zangu Β za nyuma huku akijaribu kuuliza maswali katika lugha nisiyo tambua.πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€…Hao ndio watu wazima wadogo, Taifa la kesho.Β NIWATAKIE MWANZO MZURI WA WIKI………MUNGU BARIKI KAZI YA MIKONO/AKILI ZENU.

Mother and daughter moment!

Mimi hapa na mommy anguΒ πŸ™‚Β hapa ni siku ya Juma Mosi iliyopita tukiwa nyumbani Keko Juu teyari kwa mtoko wa harusi ya mtoto wa jirani yetu and a good friend to mama…….Jamani sasa hivi tunaishi mbali hivyo tukitaka kwenda kwenye sherehe za maeneo ya Tabata, Mbezi n.k inatubidi tulale kwenye mji wetu wa zamani (Keko Juu) kwani wakati wakurudi kuna kuwa mbali na kabla ya kufika home kuna pori fulani hivi huwa hatupendi kupita usiku sana….Sasa hivi nafikiri itabidi kuangalia sana sherehe za kwenda kwani usalama wetu ni muhimu sana japo so far hatujawahi sikia kitu chochote kile ambacho ni cha kutishia amani au usalama wa eneo hilo!