Category Archives: politics

Rabierth Samrabs: Watanzania tuipende nchi yetu. Siasa si vita

Ukomavu wa Kisiasa Si Kuleta Maandamano na machafuko ya Kisiasa Katika Nchi. Nchi iliyokomaa Kisiasa huzingatia Amani na Usalama wa Raia wake. Watanzania Tuipende Nchi yetu. Siasa si vita. Siasa ni ukombozi wa Kifikra Kwa Lengo la Maendeleo ya Taifa.

Jokate Mwegelo: Muhimu kujipanga kutumia fursa hizi zinazotengenezwa na serikali zetu hizi

Jokate Mwegelo
Tarehe 14/01/2018. Rais Magufuli wa Tanzania alimkaribisha Rais @paulkagame wa Rwanda, Dar es Salaam- Tanzania katika ziara ya kikazi.  Katika ziara hii walirejea mazungumzo juu ya ujenzi wa reli kati ya Isaka na Kigali lakini pia reli hii itaenda mpaka Musongati- Burundi kupitia Keza. Reli iliyopo hivi sasa ni kati ya Isaka ambako kuna bandari kavu na Dar yenye urefu wa kilometa 970- reli ya kati. Na hii reli mpya kati ya Isaka na Kigali itakuwa ya urefu wa kilometa 494. Ujenzi huu utasaidia usafirishaji wa bidhaa na watu kwa urahisi na kupunguza gharama za usafirishaji lakini pia itasaidia kuboresha maendeleo ya kiuchumi. Nchi za Rwanda na Burundi na mpaka DRC ambazo ni “landlocked” watazidi kuona unafuu katika kutumia bandari yetu kutokana na usafiri kuwa wa kuaminika. Mradi huu unabeba pia dhima za EAC, CEPGL na COMESA zenye kuhamasisha “inter-state transportation structures”. Hizi ni hesabu nyepesi. Kwa miaka mingi maendeleo ya biashara ya bidhaa, huduma na usafirishaji wa mazao ya kilomo, madini mbalimbali n.k kati ya nchi za Afrika zimekuwa zikikabiliwa na changamoto ya gharama kubwa za uzalishaji ambapo pamoja na sababu nyingi zingine zimechangiwa sana na ukosefu wa usafirishaji wenye kueleweka. Ujenzi huu utasaidia kufungua maeneo haya na kugusa makundi mengi hasa vijana kiuchumi. Muhimu kujipanga kutumia fursa hizi zinazotengenezwa na serikali zetu hizi. Tufuate kule serikali inapowekeza na kuona jinsi gani tutaweza faidika. Pia tupende kujifunza juu ya mipango ya serikali na tuone tunanufaika vipi na tuhoji. Niwatakie siku njema. ❤️ 

Edward Julius: BABA WA FAMILIA NI LAZIMA ADUMISHE UHUSIANO MWEMA NA JIRANI ZAKE

Edward Julius

BABA WA FAMILIA NI LAZIMA ADUMISHE UHUSIANO MWEMA NA JIRANI ZAKE:

Kiongozi makini ni yule ambaye anatambua ya kuwa maendeleo ya kiuchumi ya nchi yake hayaji kwa nchi kujitenga na kujifanyia mambo yake peke yake, bali huletwa kwa juhudi za wananchi wake pamoja na kushirikiana vema na nchi majirani zake pamoja na jumuiya nzima ya kimataifa kwa mapana.  #VIVA_JPM

Mh.Edward Lowassa: Amenifanyia siku yangu kuwa njema sana. He has made my day

Siasa ni sera na itikadi siyo chuki wala uwadui! Wenyewe wenye lugha zao wanasema 'Politics is just a game'!  Na hapo ndio mimi nasema tusilazimishane kuupenda au kucheza mchezo huu!! Acha wale wanaopenda siasa wahubiri siasa, wale wanaopenda mambo ya kumtukuza Mungu wahubiri injili ya Mungu, wambea na wadaku wote washinde Facebook na Instagram kufuatilia maisha ya watu!! Kila mtu afanye kile kitu roho napenda!! Kwani siyo wote tunaoweza cheza mchezo huu wa siasa, wengine hatujui ku-control hisia zetu kuweka siasa kwenye maswala ya msingi!! Nasisitiza mimi sio mwanasiasa! Tusipangiane maisha!!

"He has made my day" hayo ni baadhi ya maneno ya Mh. Edward Lowassa baada ya kuonana na Rais Dr. John Pombe Magufuli siku ya jana. Naona wanachama wengi wa  Chadema wana lalamika kuwa wamesalitiwa??! Nikabaki kujiuliza, wamesalitiwa?? ?? na nani tena?! Kama ni usaliti basi ulifanyika 2015 pale kiongozi wenu alipo mchukua mtu ambaye hakuwa mwanachama wenu na kumpa nafasi ya kugombea urais bila hata aibu!! Ule ndio ulikuwa usaliti!!  Eti kwanini Mh. Lowassa hakushirikisha viongozi wa chama kabla ya kwenda kumuona Rais?!! ?? What a madness!! Are these people really know what they are saying! Hivi ukiwa mwanachama wa Chadema maisha yako yote ni mali ya chama??!! ?? ....Anyway Mh. Mbowe kawaelimisheni vizuri sana katika hili.  Msikilize hapo ?? Mh. Lowassa ni raia wa Tanzania kama walivyo raia wengine, kuonana na Rais ni haki yake kimsingi!! Haitaji kibali cha mtu yoyote yule kuendesha maisha yake nje ya chama.

Kuna maisha nje ya siasa na hayo ni maisha yako wewe mwenyewe  hayamilikiwi na mtu yoyote! Una uhuru wa kujumuika, kufanya biashara, kula, kuoa, kusali na mtu mwingine yoyote yule ambaye siyo adui (mf. Mtu ambaye gaidi) wa inchi yako! Siyo ndugu zako wote ni wanasiasa au wafuasi wa chama chako sasa utavunja undugu kwasababu ya Siasa?!! Kuna watu naona wanaingiza siasa mpaka kwenye maswala ya ndoa? Jamani hivi hii ni Siasa au ushetani!! Ndoa ni agano takatifu, leo hii mnataka watu waliokula kiapo mbele za Mungu waachane kwasababu ya Siasa?!! Huyu shetani anaye waingia Watanzania niwakukemewa kwa nguvu zote!! Embu turudi nyuma kidogo, sinimekwambia kuwa wenyewe wanasemaga Siasa ni mchezo tu! Sasa hapo mastering wa hii game kwa upande wa Chadema ni Mh. Edward Lowassa na Mh. Freeman Mbowe! Kumbuka Mh. Lowassa alijiunga na Chadema kwa mkataba wa kupewa nafasi ya kugombea urais na hiyo ndio imekuwa nia na lengo lake mpaka wiki kama tatu zilizopita, msikilize ?? akiwa bado anaomba Mungu amsaidie kushinda Urais 2020

Umemsikia eeh! Wakati huo huo Mh. Mbowe ameshaona kuwa Mh. Lowassa is not a great candidate kwa 2020 hivyo target yake ni Mh. Tundu  Lissu.  Lakini kwakuwa bado anamuhitaji Mh. Lowassa kwaajili ya nguvu ya umma na kifedha inabidi aendelee kumlaghai akae ndani ya chama mpaka 2020 halafu wamfanyie ule mchezo aliomfanyia Dr. Slaa  ?? but Mh. Lowassa is too smart for that ndio maana anaanza kuwafanyia maigizo kwani ameshaona dalili za yeye kufanyiwa mchezo aliomfanyia Dr Slaa! ??? Hivi huwa wanasema eti "Karma is a........" and what goes around always huwa linarudi kinyume nyume eeh ?? I love it when politicians played themselves! Mh. Edward Lowassa amekwishaona hana tena maslahi yakudumu na Chadema sasa sibora arekebishe huku kwingine before it's too late! Nammemsikia akisema anaona miaka mingine 5-10 ya uongozi bora wa Dr Magufuli ??? should I say CCM oyee ee on behalf of CCM members or will I be morally wrong since I am a blogger I should stay neutral and keep my mouth shut ?? #IHatePolitics #HeHasMadeMyDay  Btw, swala la Mh. Lowassa kuwa ni mtu muungwana na mstarabu hata mimi niliwahi sema huko nyuma, soma ?? Mr&MrsMkapaGoldenAnniversary
NilisemagaHukoNyuma

2020, je! Oprah Winfrey atajitosa kugombea urais wa Marekani?!

Hatuba fupi aliyoitoa Oprah Winfrey wakati akipokea tuzo za Cecil B. de Mille Awards kwenye Golden Globes hapo juzi kati imefanya watu wengi wajiulize kama mwanadada huyo ambaye ni billionaire mwenye mvuto mkubwa wa kushawishi watu atakuja kugombea kiti cha urais ifikapo 2020! Oprah Winfrey aliongea kwa hisia kali kuelezea jinsi wanawake wanavyokuwa wakinyanyasika, kudhalilishwa katika nyanja zote za maisha, malalamiko yao yamekuwa yakipuuzwa siku zote nasasa wakati wa hawa wanaume wanyanyasaji  umefika mwisho, "their time is up" Oprah alisema kwa ushujaa huku watu wakimshangilia. Embu msikilize kwanza ?

Kwakweli mimi nilikuaga siyo mapenzi au shabiki sana wa kuona Rais mwanamke, lakini jinsi nilivyokaa nikachukua muda wangu kuwatizama hawa wanasiasa wa kiume, honestly I now strongly supporting for a Female President! Their time is up for real! Labda tukiwa na viongozi wakuu wakike wengi kwenye dunia hii hali itabadilika kidogo, we may make this world a better place to live again! Hawa wanaume hakuna wanafanya zaidi ya ku-feed their stupid ego and using women as tools!!
Oprah Winfrey na mpenzi wake Stedman Graham
Kama Oprah aliweza kumfanikisha Rais Baraka Obama kuwa Rais wa kwanza mwenye ngozi nyeusi hapa Marekani, trust me with what is going on right now in America? Oprah Winfrey will definitely be the First Female President in America and she is BLACK!! .......Katika tuzo hiyo Oprah Winfrey ndio mwanamke wa kwanza muafrica aliyewahi pata tuzo hiyo. Sydney Portie're ndio alikuwa muafrica wa kwanza kupata, hivyo mpaka sasa ni hao wawili tu kwa upande wa watu weusi ambao wamefanikiwa kupata tuzo hiyo!

Kama hujawahi kwenda mtoni kuteka maji huwezi jua thamani ya tone la maji!

Watanzania wengi siku hizi wamekuwa na tabia ya kutaka kulazimisha kila mtu mwenye uwezo au mfanyabiashara mkubwa awe "mwanasiasa" au "mwana harakati wa siasa" kitu ambacho siyo sahii hata kidogo! Siyo kila raia wa Tanzania anatakiwa kujihusisha na siasa! Hapana! Kuwa kwenye siasa au ku support chama fulani hayo ni maamuzi binafsi, na biashara ni mtu binafsi! Mmiliki wa biashara ana hiyari ya kujihusisha moja kwa moja na siasa au akakataa, na lazima kila mtu haeshimu maamuzi yake! Unapoanzisha biashara unless ni biashara ya "siasa" then utalega kupata wanasiasa otherwise unafungua biashara kwaajili ya kuhudumia watu wote bila kujali itikadi zao!  Kama hujawahi kwenda mtoni kuteka maji huwezi jua thamani ya tone la maji! Nasema hivi kwasababu watu wengi ambao mnalaumu baadhi ya wafanyabiashara ukiwachunguza utagundua kuwa hawajahi kujaribu kutengeneza kitu chochote au kuangaika from the scratch mpaka kitu kikatembea na watu wakaona ndio maana hamuwezi jua thamani ya kupoteza kitu chako ulicho kiangaikia wewe mwenyewe toka chini! Hamuwezi jua mtu alijinyima kiasi gani ili apate kitu chake mwenyewe! Hamjui mtu huyo alifunga na kuomba Dua kwa muda gani ili Mungu ambariki na biashara yake! Hamjui ni mara ngapi amelia akiona ndoto yake haifanikiwi! Halafu leo hii akubali tu kirahisi rahisi kuharibu mali zake kwasababu ya siasa?! Kuna njia nyingi za kushiriki kuleta amani na maendeleo katika nchi yako bila kujiingiza kwenye siasa!

Siyo kila mtu anajali nani yupo madarakani, wengine wanachotaka ni amani kwani wanajua gharama ya kukosa amani! Msilazimishe kila mtu awe mwanasiasa au mshiriki wa chama fulani kwani kila mtu ana uhuru wa kufanya maamuzi yake na jinsi ya kuendesha maisha yake! Sasa leo mkilazimisha kila mtu awe mwanasiasa then what next? Mtakuja kulazimisha kila mtu awe Muislamu au Mkristo? Nahata katika ukristo bado kuna madhehebu, sasa itakuwaje? Mtakuja kulazimisha wakristo wote wasali Roman? Unafikiri mimi ambaye ni Msabato nitakubali?! Wakati najua thamani na raha ya kuwa Msabato!! ........ Embu acheni ujuaji usiyo na kichwa wala miguu! Mpaka siku ile utajifunza jinsi ya kubeba maji yako mwenyewe kutoka mtoni hauto kaa ujua gharama ya kumwagika kwa tone la maji!

Mhe. Anna Mghwira rasmi ndani ya Chama Cha Mapinduzi!

Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira mara baada ya kutangaza kuhamia Chama cha Mapinduzi CCM katika mkutano wa tisa wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.

Hatimaye yametimia! Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira ahamia rasmi CCM! Apokelewa kwa shamgwe na heshima zote mbele ya Mama wa Taifa mama Maria Nyerere!…….. Mimi siyo mwanachama wa chama chochote cha siasa lakini kama nikiambiwa nichague chama basi CCM kitakuwa chama changu siku zote! Yani ni kama leo hii mtu niambie nichague dini au dhehebu, jibu langu litakuwa mimi ni Mkristo wa dhehebu la Kisabato! Nitakuwa Msabato mpaka siku nakufa!  Hayo ni mawazo yangu na msimamo wangu kama yanakukwaza sorry but no sorry! …..Hivyo namtakia kheri Mhe. Anna Mghwira katika kutekeleza kazi ya ujenzi wa taifa kwa kupitia ilani ya CCM!

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira mara baada ya kuhamia rasmi katika Chama cha Mapinduzi CCM katika mkutano wa wa tisa wa UWT uliofanyika mjini Dodoma.

***picha na caption zote kwa hisani ya IssaMichuziblog***

Kila kitu ni siasa!! Nani alituroga sisi?!

Mambo kama haya ndio yamenifanya nichukue siasa kwani ili uwe mwanasiasa lazima uwe muongo na upungukiwe na ubinadamu kidogo! Usichanganye, nimeongolea “siasa” sio “uongozi”! Kuna tofauti ya viongozi na wana siasa. Tatizo la Africa haswa Tanzania kuwa kiongozi unajikuta unalazimika kupitia siasa! Tuna baadhi ya viongozi wazuri sana ila wanashindwa kutekeleza majukumu yao kwani kila kitu kinahusishwa na siasa! Mbaya zaidi ni pale siasa inapo ingizwa kwenye mambo ambayo yanahatarisha uhai wa binadamu na watu wanaona ni sawa!! Katuroga nani sisi?! ……..Mimi nasema imefika wakati wa wanawake kuongoza ngazi zote hadi urais kwani hawa wanaume wana roho za paka!! Just unbelievable!!! “Nyufa kwenye hosteli za UDSM: Wahandisi na wataalamu wengine wa majengo wafanye ukaguzi na kuchukua hatua stahiki. Ni vyema hili jambo lisichukuliwe kisiasa. ”  Mhe ShyRose Bhanji

Alberto Msando: Ni suala la muda tu UKWELI utajulikana.

Repost from @albertomsando – @wemasepetu  

We spoke and I repeat “watakutukana, watajaribu kukudhalilisha, watatumia nguvu kubwa kuonyesha hufai, watakuombea mabaya, watatamani uanguke, watapenda uwe mnyonge. Ila UKWELI wanaujua”. Ni suala la muda tu UKWELI utajulikana. Muda ni kila kitu. Maamuzi haya ni sahihi. Na yeyote ambaye anakujali wewe kama rafiki ataelewa. Ni maisha yako. Ni kesho yako. Ni Tanzania yako. @wemasepetu #ForThoseWhoLoveToHate #HayaWataanzaUongoWao #MaamuziBinafsi #NaBado #Sindano #MaumivuYaKichwa #KuwaNgaziSasaBasi #TheDon @hpolepole #SheIsBack

 Haya hayo Ni maneno yake Mwanasheria kijana, msomi wa kuaminika na mataifa yote Mhe. Alberto Msando akimpa nguvu mrembo wetu Wema Sepetu ya kusimamia maamuzi mazito aliyo yafanya!

Wema Sepetu: Peace of mind is everything for me

“Siwezi Kuendelea kuishi kwenye Nyumba inayo nikosesha amani… Peace of mind is everything for me… Natangaza Rasmi kuondoka Chadema na Kurudi Nyumbani…. #ThereIsNoPlaceLikeHome… Feels good to be Back…

“Wow! Kwaniaba ya mdogo wangu kipenzi Magreth Otieno Olung’a Igogo ambaye ni mmoja wa mashabiki wakubwa wa Wema Sepetu na pia ni mwanachama muaminifu wa CCM naomba nichukue fursa hii kumkaribisha our Tanzania Sweetheart #nyumbani! CCM oyeeeeeee! Kidumu chama ???? O’Lord of Mercy!!…….Honestly, nampongeza sana Wema kwa maamuzi haya. Huwezi kuwa na amani kwenye chama ambacho Mwenyekiti wake amekutaka kimapenzi! Ndio maana hata amabavyo hujaenda kumuona uncle wako Mhe. Tundu Lissu mie sijashangaa kwani nilijua ni ngumu sana kwako kuonana na Freeman Mbowe uso kwa uso! Nafikiri it’s high time kwa wanawake kushika uongozi kwani hawa wanaume wanatuchanganyia habari tuu! Hongera sana Wema  ???  BTW, hivi mnajua jinsi gani mdogo wangu alikuwa anachukia niki mpost Zari humu zaidi ya Wema? Hahahaha! Haya Sasa nitakuwa na balance lol!

Jokate Mwegelo: Magufuli na kisa cha Mussa na Wana wa Israeli

Magufuli na kisa cha Mussa na Wana wa Israeli  

Jokate Mwegelo akiwa shule ya Msingi Mugabe

Musa alipitia vitu vingi ikiwemo kejeli, kujaribiwa na hatimae kufanikiwa kuwavusha Wana wa Israeli kuelekea nchi ya ahadi. Lakini kuna wakati wafuasi wake hao walipojaribiwa kidogo tu wakaanza kunung’unika na kumkebehi Musa kwamba ni kheri maisha waliyokuwa wanaishi Misri kwa Farao.

Rais John Pombe Magufuli ameianza safari yake nyingine baada ya Novemba 5 mwaka huu kufikisha miaka miwili madarakani. Napenda kuifananisha safari yake hiyo iliyosheheni mageuzi makubwa sawa na ile ya Wana wa Israeli walipokombolewa na Nabii Musa kutoka kwenye mikono ya utumwa chini ya Farao wa Misri. Uwajibikaji, Uzalendo, Utendaji

Kumekuwa na tatizo tatizo la watumishi wa Serikali kutokuheshimu misingi ya kazi zao katika utumishi wao wa umma, nidhamu ya kazi ilikuwa haipo. Ilifikia wakati watu walitunga safari za nje ilimradi tu wapate posho za kujiendeleza wao na familia zao.

Uzalendo wa nchi ukageuka kuwa uzalendo unaokimu mtu na familia yake na watu wake wa karibu. Fedha nyingi zikawa zinapotea angani na hata matunda ya safari tulikuwa hatuyaoni. Bado barabara na miundimbinu muhimu ilikuwa kasi yake ya kuimarishwa haikuwa nzuri sana.

Utendaji na ubunifu ulikuwa wa chini kwani hakukuwa na kitu kipya katika utendaji wa kazi kwa wengi zaidi ya kujitajirisha kupitia kodi za wananchi bila sababu zozote zile za msingi. Manung’uniko yalikuwa mengi juu ya rasilimali za taifa. Kulikuwa na makundi mengi yakizungumza kwa lawama namna rasilimali zilikuwa zinatumika vibaya. Makundi haya yakihusisha Wanasiasa, Wasomi na hata baadhi ya Wananchi wenye kufuatilia maslahi na rasilimali za taifa. Nchi yetu pendwa ya Tanzania ‘kuibiwa’ umekuwa ni mjadala wa muda mrefu bila utatuzi au hatua yoyote kuchukulliwa.

Kuna wakati, nikiamini kwa nia njema na uchungu wa nchi yao na si siasa, baadhi ya wanasiasa walipaza sauti kusema kuwa ni aibu kubwa kwa nchi yetu kushindwa hata kumiliki ndege yetu. Walihoji: “Tutatangazaje utalii bila ya kuwa na ndege yetu?” Kwa ufupi kila kitu kilikuwa kikionekana kwenda sivyo. Na hapa sijagusia issue ya “mafisadi”

Kuingia kwa Magufuli madarakani miaka miwili iliyopita, ukiyatazama maisha yake, utakubaliana nami kuwa huyu ni kiongozi anayeishi na kujituma kwa ajili ya maslahi ya wananchi. Hii inanikumbusha nilipokuwa masomoni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam miaka kadhaa ya nyuma, niliwahi kumuona Rais wetu ambaye kipindi kile alikuwa ni Waziri akila sehemu mmoja wanafunzi katika kijiwe maarufu cha misosi kiitwacho “Harvard”.

Pale chakula ni cha bei ya chini kabisa, mlo kamili mzuri ulikuwa hauzidi elfu 1000. Ilikuwa ni sehemu ya sisi wanafunzi wa kawaida kula kwa sababu ya bajeti zetu ndogo. Kumuona yeye kama waziri pale kulipelekea mimi kuanza kuelewa Dkt. Magufuli ni mtu wa aina gani. Ni wazi kwamba ni mtu wa watu, hana makuu, hajikwezi na anapenda “ku-budget.”   Mageuzi na Mabadiliko

Sishangai miaka miwili tu ya uongozi wake akiwa ameacha tayari alama na mageuzi makubwa ya kukumbukwa. Kwa kifupi tu ametenda yafuatayo ya kukumbukwa:

· Kuwezesha elimu bure kuanzia shule ya Msingi hadi Sekondari;

· Kufufua shirika la ndege la ATCL kwa nunua ndege mpya sita;

· Kuongeza mapato ya ndani toka trilioni 9.9 kwa mwaka hadi trilioni 14 kwa mwaka;

· Kurejesha nidhamu na uwajibikaji kwa watumishi wa umma;

· Ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima, Uganda hadi Tanga, Tanzania

· Kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma;

· Kutimiza ahadi ya Serikali kuhamia Dodoma;

· Kukamilisha miradi mikubwa wa umeme wa Kinyerezi I-extension na Kinyerezi II;

· Kuanza ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge;

· Uzalendo kusimamia raasilimali za taifa yakiwemo madini;

· Kuanza ujenzi wa barabara za juu Tazara, Ubungo na daraja la wapiti kwa miguu Furahisha;

· Ujenzi wa madaraja ya kisasa mfano la daraja la Kilombero;

· Kusimamia uhakika wa madawati maabara na maktaba katika shule zote nchini;

· Ujenzi wa maduka ya kisasa ya dawa za ndani ya kila hospitali ya Serikali;

· Kupambana vikali dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya nchini;

· Kutoa bima za afya za matibabu ya bure kwa wazee

· Kuhakikisha wanafunzi wanaostahili kupata mikopo ya elimu ya juu wanapatiwa

· Kuhakikisha Tanzania inakuwa na viwanda vya kutosha nchini

· Kufuta kodi na urasimu kwenye kilimo na uwekezaji nchini

· Kuhakikisha serikali inasimamia uuzwaji wa mazao ya wakulima masokoni na kupata faida. Mfano wakulima walikuwa wakiuza korosho zao kwa tsh 800 kwa kilo mpaka tsh 4000 kwak kilo.

Nimesukumwa kuzungumzia na kuorodhesha mafanikio haya kwa ufupi ili tujue shabaha ya rais wetu. Rais wetu anataka kurudhisha heshima. Heshima hailetwi kwa blah blah, heshima huletwa kwa vitendo na kufanya vitu kwa njia ya kuwa “disruptive”-kutokufanya vitu kikawaida au kwa mazoea.  Msimamo mkali wa Rais

Rais Magufuli anataka kuona watu wakijituma na kuleta matokeo chanya. Hata ukiangalia safu zake za uongozi ni viongozi walioshiba kwenye nafasi zao. Na wanaonekana hawafai wanaondolewa. Ila bado kuna makundi ya watu kwenye jamii wanaona anachofanya ni kazi bure na kufikia hatua ya kuaminisha umma kuwa Serikali hii ya Awamu ya Tano imefanya hali imekuwa ngumu na eti haina malengo na kuwa imepoteza dira.

Hakuna ukombozi uliofanyika bila kutoa jasho, kutokwa damu na kutumia mbinu za kujifunga mikanda. Mheshimiwa Rais anafanya hilo, ni lazima kujitoa mhanga kwa kipindi hiki kwa ajili ya mafanikio ya muda mrefu. Nilifikiria viongozi wetu hasa wa upinzani wangefurahia mabadiliko haya kwa maana ndio kitu hasa walichokuwa wakikitamani na wakishiriki kikamilifu katika kutoa mawazo yenye kujenga ila hali imekuwa ni tofauti.

Hapa ndio maana nimekikumba kisa cha safari ya Mussa-maana nalifananisha hili na kadhia ya wale Wana wa Israeli kufikia hatua mpaka kumkufuru Mwenyezi Mungu na wakaona kuwa ni kheri wangebaki kule Misri. Kama kumbukumbu ya kuku, nao walisahau walipotoka.  Ushauri

Natambua ni vigumu kumuaminisha kila mtu ukweli kama tayari anaamini uongo, kama ilivyo vigumu kumuaminisha uongo yule ambaye anaamini ukweli. Ila kama vijana na taifa lililo la vijana, imefika wakati wa kila mmoja kusimamia kila anachokiamini, LAKINI asiamini kile alichoaminishwa. Vijana tuache siasa za kupikwa na kuungaunga, tusimame katika ukweli na mambo yale ambayo yana maslahi kwa taifa letu na si maslahi binafsi. Tujiulize: Inakuwa vipi, wanasiasa na wanaharakati wale wale ambao walikuwa wanapigania vitu flani vifanyiwe kazi, sasa vinafanyiwa ndiyo wa kwanza kununa na kufanya ‘confusion’ mbele ya Jamii?

Ndani ya chama cha Mapinduzi tunaamini Umoja ni Ushindi. Huu ni wakati wa kuungana na Mheshimiwa Rais katika ukombozi wa Watanzania, lazima tuelewe shabaha ya Rais wetu kuwa ana nia njema na maendeleo ya nchi yetu.

Hii safari sio rahisi, hakuna aliyemkamilifu ila wote tunaitumainia Tanzania yenye neema. Vijana tuache kupokea mapokeo ya wanasiasa wasio na nia njema na nchi yetu, tufanye kazi kwa kushirikiana katika kuiletea nchi hii neema. Hapa Kazi Tu! Jokate Mwegelo,

Kaimu Katibu Idara Ya Uhamasishaji,

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) makao makuu.

**Chanzo cha habari hii ?  JamiiForum**

Waziri Kairuki afanya mazungumzo na Balozi wa Kuwait nchini leo hii!

Waziri wa Madini Mhe Angellah Kairuki siku ya leo masaa ya Africa Mashariki amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Kuwait nchini. …..kwa picha na maelezo zaidi bonyeza ??  IssaMichuziblog

David Kafulila avua magwanda ya Chadema!

Mwanasiasa David Kafulila avua magwanda ya Chadema! Je, anahamia CCM au anakuja na chama chake? Hilo kwa Sasa hatujui lakini najua tutajua hivi karibuni!  Naona “Mgufulicillin” is working really well ??. Wishing you all the best!

Robert Mugabe ameng’oka!

Ni nderemo zimerindima ndani ya nchi ya Zimbabwe!! Ameng’oka!! Robert Mugabe is no longer in power!…….Mimi siyo mwanasiasa hivyo sijui kama hii italeta amani na maendeleo zaidi au La! Lakini naweza sema ni mmoja ya watu ambao nilikuwa sipendezwi na kuwa na Rais  mmoja kwa miaka yote hiyo! Kunatofauti kubwa sana kati ya chama kimoja kuwa madaraka na Rais mmoja kuwa madarakani!! Hivyo kwahili naungana na Wazimbabwe wote kusherekea ushindi huu!…..Mungu ibariki Africa!

Mwanasheria Alberto Msando arejea CCM kwa unyenyekevu!

Yule Mwanasheria wa kujitegemea, msomi wa kuaminiwa na mataifa yote,  Alberto Msando arejea CCM kwa unyenyekevu mkuu! Akiri kuwa alipotea njia, alikuwa kipofu na sasa anaona kwani hataki kuongozwa na chama ambacho kina Mwenyekiti mmoja kwa zaidi ya miaka 10! Kwani huo pia ni udikteta ??  ……Alberto anakuwa mwanasheria wa pili (Lau Masha alirudi wiki iliyopita) ambao walikuwa upinzani na sasa wameamua kurudi kundini! ……As I always say, ” I’m not a politician” hence, my comment is respectfully reserved! Just wishing him the best of all!

Mwanasheria mahiri Lau Masha “atua mtungi” wa Chadema!

Imenibidi niblog wapendwa maana siyo kwa ‘breaking news’ hizi ???…… Yule Mwanasheria mahiri msomi wa kimataifa Mh. Lawrence Masha ambaye alikuwa mwanachama wa CCM na kushika nyadhifa mbali mbali ndani ya chama hicho na serikali zake baadaye akahamia Chadema. Sasa si aliubeba mtungi wa Chadema kwa ngata nene na ndefu ili uonekane hata kwa nchi za mbali?! Sasa basi leo hii ameamua kuutua “mtungi” wa Chadema kwenye kichwa chake yeye mwenyewe kwa hiyari yake!! Kwani ni mzito wakati hauna sababu yoyote ya msingi ya kuufanya uwe mzito kiasi hicho ?? Nafikiri Mh Masha hakujua kuwa debe tupu haliachi kupiga kilele ?? just kidding, wanachadema msinimeze.  Anyway mie siyo mwanasiasa hivyo sina cha kumshauri zaidi ya kumtakia kila la kheri katika kila kitu!

“Tusimame pamoja kama Watanzania kupambana na uovu kwenye jamii” -ShyRose Bhanji

CHADEMA HAINA HATI MILIKI YA KUWA UPINZANI PEKEE NCHINI. -Peter Sarungi

 Nilipokuwa natafakari maamuzi ya kwenda kugombea Spika wa bunge niligundua kuwa kama wewe ni mchezaji mzuri wa mpira wa miguu na unajiamini basi si lazima usajiliwe na timu kubwa kama Simba, Yanga ana Azam ili ucheze ligi kuu, kumbe unaweza kucheza ligi kuu hata kupitia Mbao Fc, Ndanda Fc, majimaji au hata Costal Union. Kinachotakiwa ni siku timu yako ikikutana na Simba ama Yanga hakikisha unafunga walau goli moja tu hata kama wao wataifunga timu yako kwa magoli 10. Hilo goli lako wataondoka nalo likiwa na jina lako. Hii ni bora zaidi kuliko kusajiliwa Simba ama Yanga halafu ukakaa benchi kwa sababu wachezaji ni wengi. Nchi yetu ni nchi ya demokrasia na nchi yenye kufunya siasa ya vyama vingi. Kuwepo kwa wingi wa vyama vya siasa ni moja ya tendo la demokrasia tunayo ikubali kila siku. Tanzania kuna vyama vya siasa zaidi ya 25 vyenye usajili wa kudumu vinavyo ruhusiwa kushiriki katika siasa zote za nchi. Ni kwa bahati mbaya Chama tawala hakijawahi kupoteza kushika dola huku vyama vya upinzani viki badilika badilika katika kuwa na wafuasi na nguvu za kisiasa hadi kupewa kijiti cha kuitwa chama kikuu cha upinzani. TLP, NCCR Mageuzi na CUF zimewahi kuwa na nguvu katika chaguzi zilizopita na kuwa chama kikuu cha upinzani wakati huo vyama kama Chadema Tanzania vilikuwa vipo chini sana na vilikuwa havijulikani kwa Watanzania walio wengi. 

Leo Bunge la Tanzania lina vyama 5 vyenye uwakilishi Bungeni huku CHADEMA kupitia muunganiko wa UKAWA wakiwa ni chama kikuu cha upinzani. Ukawa inabebwa na wabunge kutoka CUF, CDM na NCCR huku ACT ikiwa iko peke yake lakini katima kapu la upinzani ikiwa na haki zote kikatiba na hata kwa sheria za uchaguzi na za bunge.

Kumetokea taharuki kidogo juu ya nafasi za wabunge wa Afrika Mashariki hasa kwa upande wa vyama vya upinzani. Mnyukano ulikuwa ni kati ya UKAWA na ACT wazalendo juu ya nafasi 3 za upinzani. Mnyukano huo umeendelea hadi yalipo patikana maamuzi kutoka kwa Speaker juu ya mgawanyo.

Kilicho nisikitisha katika mnyukano huo wa hoja ni baadhi ya makada wa CDM kwa makusudi ama kwa kutojua kuhamisha mjadala wa kibunge na kuuweka kwa wananchi huku wakitoa lawama, matusi, kejeli na hata dharau kwa hoja iliyo tolewa na ACT kupitia mwakilishi wake Mh. Zitto Zuber Kabwe iliyotaka ACT wapate nafasi ya kugombea ubunge wa Afrika Mashariki. 

ZZK ametukanwa sana na baadhi ya makada wa mtandaoni wa CDM huku wakiamini wao ndio wapinzani pekee walio teuliwa na Mungu kuja kuwasemea watanzania. Mimi niwakumbushe tu makada wa CDM kwamba hata wao walikuwa kama mchicha kipindi CUF wakiwa Upinzani imara, Pia wakumbuke hata wao hawana HATI MILIKI ya kuwa UPINZANI pekee nchini. Wasikasirike, kubeza na kupinga wanapoona mbegu zingine za upinzani zinapo chepua kwa kasi, ipo siku mtahitaji ushirika wao ili kufikia malengo yenu.

By the way, inasemekana hata mgogoro wa CUF unawafurahisha sana CDM kuliko CCM, Maana wapo tayari na wamefungua milango kwaajili ya kuwasajili akina Seifu, Mtatiro na wengine pindi chama hicho kikifutwa kama alivyo sema Lissu kwenye mahojiano ya Azam… Daah kufa kufaana.

Msijisahau mkalewa kwa sifa na ubinafsi, ni kweli umoja ni nguvu lakini ni umoja wenye maslahi sawiha ulio Imara na wenye Nguvu.

Wasalam.

SIASA ZENYE MLENGO WA UCHUMI. -Peter Sarungi

SIASA ZENYE MLENGO WA UCHUMI.

Peter Sarungi (The next time)

Kuna Siasa za kuegemea uchumi (Political Economy), Siasa za kisayansi (Political Science) na Siasa za Kisanii (Political Art).

Hizi aina zote zina faida na hasara zake na kila moja ina nafasi yake katika kustawisha jamii.

Nimegundua kuwa serikali ya JPM inafanya siasa zenye kuegemea uchumi. Nasema hayo kutokana na budget ya sasa inayoonesha vipaumbele vya utawala huu ni vile vinavyo chochea uchumi ikiwa ni sector ya usafirishaji na miundo mbinu. Tunaona budget ikitupilia mbali miradi mipya ya afya, elimu, michezo, kilimo, viwanda, maji, umeme, utalii, uvuvi, ajira na kukuza sector binafsi. Budget imeweka mkazo kwenye Ujenzi, Ujenzi,Ujenzi pamoja na ununuzi wa ndege.

Kwa budget hii, fedha nyingi bado zitakwenda kwa wageni ambao watahusika na ukandarasi wa ujenzi wa Reli inayokusudiwa, ujenzi wa fly overs zinazokusudiwa na kampuni ya kutengeneza ndege. Kwa maana hiyo bado pesa haitakuwepo kwenye mzunguko wa ndani wa fedha, matokeo yake ni UKATA, UKATA. 

Aina hii ya siasa ina faida ya kukuza uchumi wa nchi na serikali yake baada ya mda wa miaka 3 na kuendelea. Serikali inakuwa na uchumi mzuri kuliko sector binafsi, Serikali inakuwa imejiingiza katika kushikilia vyanzo vya kuendesha uchumi. Ubaya wa aina hii ya siasa ni wananchi kudhoofika kiuchumi kiasi kwamba wanakuwa tegemezi kwa kila kitu kwa serikali yao. Tatizo lingine ni kwa serikali kuwa na tabia ya  kujiondoa katika kusimamia na kuendeleza miradi yenye kutoa huduma za jamii kwa wananchi wake, hili ni Tatizo kubwa sana mbeleni.

KATAZO LA KUSAFIRISHA MCHANGA WA DHAHABU-2 -Peter Sarungi

KATAZO LA KUSAFIRISHA MCHANGA WA DHAHABU 2

Peter Sarungi (The next time)

Sehemu ya II – Ijue Sector ya Madini Tz

Sector ya madili ilianza kutambulika rasmi wakati wa utawala wa awamu ya tatu chini ya Raisi mstaafu Mh. Ben Mkapa kupitia sera ya uwekezaji. Mh. Mkapa aliamini maendeleo ya nchi yatasaidiwa ikiwa tuta ruhusu uwekezaji mbalimbali ikiwemo sector ya madili. Aliamini nchi itafaidika kwa kupata teknolojia mpya, mitaji mikubwa, elimu mpya katika sector hiyo pamoja na kuongeza ajira kwa wananchi na mapato ya serikali. Wawekezaji wakubwa walianza kujitokeza mwaka 2001 Geita na Kahama. Madini yanayopatikana nchi ni mengi kwa aina tofauti kama vile dhahabu, almasi, ruby, Tanzanite, Copper, Silver na mengine mengi ingawa zaidi ya 80% ya machimbo nchini yanajihusisha na uchimbaji wa madini ya Dhahabu. 

UZALISHAJI WA DHAHABU

Mpaka sasa tuna machimbo makubwa ya dhahabu yapatayo sita ambayo ni Bulyanhulu(BGM), Geita(GGM), Buzwagi(BZGM), Biharamulo, North Mara na New Luika. Kwa mwaka migodi hii huzalisha 1.37Million troy ounce ambayo ni zaidi ya kilogram 50,600 ya dhahabu safi kwa mwaka huku GGM ikiongoza kwa uzalishaji wa 38.6% na ya mwisho ikizalisha 1.5%. Kwa viwango hivi, Dhahabu inachangia zaidi ya 90% ya uzalishaji wa madini yote inchini kwa mwaka.

               NJIA ZA UZALISHAJI

Uzalishaji wa dhahabu upo wa aina mbili maarufu ingawa kuna nyingine ya tatu, aina hizi zinatokana na utofauti wa miamba ambayo dhahabu hupatikana. Kuna miamba ambayo ina oxide na zingine zina sulphide.

Dhahabu inayopatikana katika Miamba yenye oxide ina zalishwa kupitia njia za gravity na Cabon process (cabon in loucher CIL na cabon in pulmp CIP). Njia hizi ni common na zipo nyingi katika migodi yetu hadi kwa wachimbaji wa kati. Migodi yenye miamba ya oxide inayotumia njia hii ni nne kati ya zile sita yaani GGM, North Mara, Biharamulo na New Luika. Hivyo uzalishaji katika migodi hii hufanyika na kumalizika ndani ya nchi. Migodi hii haisafirishi mchanga kwenda nje.

Dhahabu inayopatikana katika miamba yenye sulphide ina zalishwa kupitia njia ya gravity, caborn process na kuhitimishwa na smelter. Njia za gravity na Carbon process huzaliza 40% pekee huku smelter ikizalisha 60% ya dhahabu. Dhahabu inayopatikana katika miamba yenye sulphide ina ugumu wa kunyonywa kupitia njia zilizopo nchini kutokana na dhahabu hiyo kuungana na madini mengine ya copper na silver, hivyo ili kuitoa dhahabu hiyo ni lazima uwe na tanuru kubwa (smelter) lenye uwezo wa kuyetenganisha madini hayo kutokana na utofauti wa melting point za madini hayo. Hivyo ni lazima mchanga unaozalishwa baada ya mchujo kwa njia za kwanza usafirishwe kwenda nje kwaajili ya kuzalisha 60% iliyobaki. Migodi yenye miamba yenye sulphide inayotumia njia hizi zipo 2 kati ya sita nazo ni BGM na BZGM. Migodi hii ndioyo husafirisha mchanga kwenda china na japan ?? kwaajili ya uchenjuaji.

Mpaka hapo kama kuna swali unaweza kuuliza kabla sijakwenda mbele zaidi. Uliza ndani ya maelezo hayo, usitoke nje maana bado kuna makala nyingi zinakuja

Asanteni.