Category Archives: Rachel Bridal Shower

Bibi harusi mtarajiwa na wageni wake!

Mrembo wetu mgeni wetu wa heshima akiwa na muheshimiwa mpambe wake! Wamependezaje sasa, simple hakuna madoido mengi 😍😍 embracing their natural beauty πŸ‘Œβ€

 Mimi mwenyewe simmeniona aaa! Ningekosaje ukodak moment na bibi harusi, kuna mibaraka kupiga picha na bibi harusi ati 😍😍 Msije mkaanza kuwaganda maharusi kupiga picha lol! 

  Hii sherehe ilikuwa ya kipekee sana, simnaona watu wamefunga Khanga na wengine wamebeba, basi kila mtu alipewa zawadi ya khanga na mwiko wa kupikia all the way from Bongoland πŸ‘Œ wewe ulishawahi kwenda kwenye sherehe halafu ukapewa zawadi za huwakika kama hizi? Rachel siyo mtu wa spoti spoti ati 😍😍😍
 
     

Mtarajiwa wetu katika pozi!

 Jumapili ndio siku yake kuu, hivyo naomba nitumie siku hizi mbili kwa ajili yake 😍😍 Huyu ni dada yangu bwana na furaha sana kwa ajili yake. Yani nyie siku nikifunga harusi yani ni miezi mitatu picha zangu tuu 🀣🀣 mtakomaje sasa πŸ’ƒπŸ’ƒ
 Akikata keki iliyotenezwa kiumaridadi kabisa
Tulimpa zawadi chache lakini zauwakika! Ni zawadi ambazo atakuwa anatumia mara nyingi, ubora na viwango vilizingatiwa sana, siyo mambo ya buy one get one free hapana 🀣 chezea sisi πŸ™Œ

Mwenyezi Mungu amuweke salama Jumapili tushuhudie akiapa kiapo kitakatifu mbele zake Mungu nasi wengine tukiwa mashahidi wa hapa duniani! πŸ™πŸ½

Matukio katika picha: Rachel’s bridal shower

 Zifuatazo ni picha za sherehe ndogo ambayo bibi harusi mtarajiwa Rachel alifanyia na marafiki zake wa karibu pamoja na baadhi ya ndugu zake kama siju yao ya kufurahi pamoja kabla hajala kiapo kitakatifu ambacho siyo tu kitabadilisha cheong chake to Miss to Mrs bali hata majukumu yake pia yatabadilika. Lakini yote ni kwa utukufu wa Bwana.Β Shere hii ilifanyika nyumbani kwa rafiki yake Rachel aitwaye Mary (kulia), huko Manvel, Texas. Rachel na Mary wamekuwa marafiki kwa zaidi ya miaka 20, tangu wakiwa Secondary Jangwani, wakanda wote college, wakaishi wote Wichita, Kansas, Β na mpaka leo hii wako hapa wote katika state ya Texas.Β Β Hivyo kutokana na urafiki wao huo ambao umedumu zaidi ya miaka 20, nanupendo wao ukiwa imara kabisa bibi harusi ameona ni vyema akawa ndio msimamizi wake mkuu katika harusi yake (Maid of honor) Β Picha ni nzuri na nyingi sana, hivyo nawaleta bila kuwa kwenye mpangilio maalumu. BadoΒ       

Hapo πŸ‘† Rachel akitambulisha wageni na wenyeji wake. Bibi harusi aliona anajukumu la kutoa utamvulisho kwani watu wote waliofika hapo wamegusa maisha yake kwa njia moja ama nyingine.

mmmh! Mahanjumati! Wadada walipika  (nimesema walipika eeh 😍😍) vikapikika haswa watu tukala mpaka vikasaza! Hii ni sehemu ya kwanza picha zipo nyingi nitawaletea zingine baadaye 😍😍