Category Archives: Spirituality

BAADA YA KUFA NINI KINAENDELEA? By Melania Shedrack

      *BAADA YA KUFA NINI
         KINAENDELEA?*VIFUATAVYO NI VITU VINAVYOTOKEA. I. *UKIFA HAUWEZI KUFAHAMU NENO LOLOTE* ....MHUBIRI 9:5-6,10 kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa. Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lo lote lililofanyika chini ya jua. Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe II. *MWANADAMU ANAPOKUFA HANA TOFAUTI NA MNYAMA* ....MHUBIRI 3:19-20 Kwa maana linalowatukia wanadamu linawatukia wanyama; jambo moja lawatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu; naam, wote wanayo pumzi moja; wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama; kwa maana yote ni ubatili.Wote huendea mahali pamoja; wote hutoka katika mavumbi; na hata mavumbini hurudi tena, ZABURI 49:12 Lakini mwanadamu hadumu katika heshima, Bali amefanana na wanyama wapoteao III. *UKIFA HAUWEZI KUJUA WATOTO WAKO WANAENDELEAJE* ..... AYUBU 14:21 Wanawe hufikilia heshima, wala yeye hajui; Kisha wao huaibishwa, lakini yeye hana habari zao IV. *UKIFA HAUWEZI TENA KUMSIFU MUNGU BALI UKIWA HAI* ........  ZABURI 146:2,4 Nitamsifu Bwana muda ninaoishi, Nitamwimbia Mungu wangu ningali ni hai. Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, Siku hiyo mawazo yake yapotea V. *WALIOKUFA WOTE BADO WAMELALA MAKABURINI WATAFUFULIWA YESU ANAPORUDI MARA YA PILI* ......  1 WATHESALONIKE 4:13-18 Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi, farijianeni kwa maneno hayo. Isaya 26:19 Wafu wako wataishi, maiti zangu zitafufuka; amkeni, kaimbeni, ninyi mnaokaa mavumbini, kwa maana umande wako ni kama umande wa mimea, nayo ardhi itawatoa waliokufa VI. *JE MUNGU ANAO UWEZO WA KUMRUDISHIA KILA KIUNGO AMBACHO MWANADAMU ANAKUWA NACHO WAKATI WA UHAI WAKE MF.NGOZI,NYAMA,,MIFU­­PA,,,!* .......  EZEKIELI 37:3-10 Akaniambia, Mwanadamu, je! Mifupa hii yaweza kuishi? Nami nikajibu, Ee Bwana MUNGU, wajua wewe. Akaniambia tena, Toa unabii juu ya mifupa hii, uiambie, Enyi mifupa mikavu, lisikieni neno la Bwana. Bwana MUNGU aiambia mifupa hii maneno haya; Tazama, nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi. Nami nitatia mishipa juu yenu, nami nitaleta nyama iwe juu yenu, na kuwafunika ngozi, na kutia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana. asi nikatoa unabii kama nilivyoamriwa; hata nilipokuwa nikitoa unabii, palikuwa na mshindo mkuu; na tazama, tetemeko la nchi, na ile mifupa ikasogeleana, mfupa kwa mfupa mwenziwe. Nikatazama, kumbe! Kulikuwa na mishipa juu yake, nyama ikatokea juu yake, ngozi ikaifunika juu yake; lakini haikuwamo pumzi ndani yake. Ndipo akaniambia, Tabiri, utabirie upepo, mwanadamu, ukauambie upepo, Bwana MUNGU asema hivi; Njoo, kutoka pande za pepo nne, Ee pumzi, ukawapuzie hawa waliouawa, wapate kuishi. Basi nikatabiri kama alivyoniamuru; pumzi ikawaingia, wakaishi, wakasimama kwa miguu yao, jeshi kubwa mno. VII. *HAIRUHUSIWI KUFANYA IBADA YA WAFU AU KUWAOMBEA ETI MUNGU AWABARIKI/AWASAMEHE* TORATI 18:9-11 Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, WALA MTU AWAOMBAYE WAFU VIII. *JE NI KWELI WAFU WAKIFA BAADAYE HUWATOKEA NDUGU ZAO?* ...... 2 WAKORINTHO 11:13-15 Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo. Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao. JIBU NI HAPANA -Wafu wanaowatokea watu na kuongea nao tena wanafanana kabisa na ndugu zao waliokufa hizo huwa ni roho za mashetani zinazojigeuza katika maumbile mbalimbali ya marehemu ili kuwadanganya watu kuwa hawafi huo ni udanganyifu mkubwa wa shetani *TAHADHARI:* Wafu hawaendi mbinguni wanapokufa bali huzikwa kaburini, pia hawawezi kusamehewa kama walikufa bila kuungama dhambi zao.

Kesha la asubuhi: Anakwenda Nyumba kwa Nyumba Pamoja na Watendakazi wa Injili

                  KESHA LA ASUBUHI

                            IJUMAA

                         18 MAY 2018

*Anakwenda Nyumba kwa Nyumba Pamoja na Watendakazi wa Injili* 📖 _Akawaita wale Thenashara, akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi. Akawatuma wautangaze ufalme wa Mungu, na kupoza wagonjwa. Akawaambia, Msichukue kitu kwa safari yenu, fimbo, wala mkoba, wala mkate, wala fedha, wala mmoja wenu asiwe na kanzu mbili. Na nyumba yo yote mtakayoingia kaeni humo, mpaka mtoke mjini. Luka 9:1-4._

✍🏽Bwana anawaita watu wake kuchukua njia mbalimbali za huduma za umisionari. Wale walioko katika njia kuu na walio katika sehemu zisizofahamika vizuri katika maisha wanapaswa kusikia ujumbe wa injili. Washiriki wa kanisa wanapaswa kufanya kazi ya uinjilisti katika kaya za majirani zao ambao bado hawajapata ushahidi mkamilifu wa ukweli ulio kwa ajili ya wakati huu.

✍🏽Hebu wale ambao wanachukua kazi hii wafanye maisha ya Kristo kuwa somo lao la kudumu. Hebu na kwa bidii sana, wawe wanatumia kila uwezo katika huduma ya Bwana. Matokeo yenye thamani sana yatafuatia juhudi za dhati zisizo na ubinafsi. Kutoka kwa Mwalimu mkuu watendakazi watapokea elimu ya juu kabisa kuliko zote. Lakini wale ambao hawagawi nuru hii waliyoipokea siku moja watatambua kuwa wamepata hasara ya kutisha.

✍🏽 Wengi wa watu wa Mungu inabidi watoke na machapisho kwenda katika sehemu ambazo ujumbe wa malaika wa tatu haujatangazwa. Kazi ya mwinjilisti wa vitabu ambaye moyo wake umejazwa na Roho Mtakatifu imejaa uwezekano wa ajabu wa mema. Uwasilishaji wa ukweli, katika upendo na usahili, kutoka nyumba moja hadi nyingine, unapatana na maelekezo aliyotoa Kristo kwa wanafunzi wake alipowatuma katika safari yao ya kwanza ya umisionari. Kwa nyimbo za sifa, maombi ya dhati, na uwasilishaji sahili wa ukweli katika familia moja, watu wengi watafikiwa.

✍🏽 Mtendakazi mtakatifu atakuwapo kupeleka usadikisho kwa mioyo. “Mimi niko pamoja nanyi siku zote” (Mathayo 28:20) ndio ahadi. Kukiwapo uthibitisho wa uwapo wa kudumu wa Msaidizi wa jinsi hiyo, tunaweza kutenda kazi kwa imani na tumaini na ujasiri.

🙇🏽‍♂```Ukinaifu wa huduma yetu kwa Mungu unapaswa kuvunjwa. Kila mshiriki wa kanisa anapaswa kujiingiza katika huduma fulani maalum kwa ajili ya Bwana.

🙇🏽‍♂ Hebu wale ambao wamejiimarisha katika ukweli waende katika sehemu jirani, na kufanya mikutano. Hebu Neno la Mungu na lisomwe, na hebu mawazo yanayoelezwa yawe katika jinsi ambayo yataeleweka na wote bila shida. - Review and Herald, May 5, 1904```.

                   *MUNGU AKUBARIKI*

Nawatakieni Ramadhan njema!

Nawatakien Ramadhan njema kwa wasomaji wangu wote ambao ni waumini wa dini ya Kiislam. Tukumbukane kwenye dua zenu, na zaidi tuombee amani ndani ya miyoyo yetu na kwa taifa letu. Ramadan Mubarak!

Kesha la asubuhi: Ana shauku ya kuwasaidia walimu

           🌏 *KESHA LA ASUBUHI*🌏
                             Alhamisi
                          Mei 17, 2018

*ANA SHAUKU YA KUWASAIDIA WALIMU*
*_______________________________* 

📓 Fungu kiongozi
👇🏽
📖2 Wafalme 2:15.

_*"Na hao wana wa manabii, waliokuwako Yeriko wakimkabili, walipomwona, walisema, Roho ya Eliya inakaa juu ya Elisha. Wakaja kuonana naye, wakainama kifudifudi mbele yake".*_
📃➖➖➖📃📃➖➖➖📃

✅ Roho Mtakatifu alikuja katika shule ya manabii, akileta hata mawazo ya wanafunzi katika upatanifu na mapenzi ya Mungu. Kulikuwapo na muunganiko hai kati ya mbingu na shule hizi, na furaha na shukurani za mioyo yenye kupenda ilidhihirika katika nyimbo za sifa ambazo malaika walijiunga kuimba.

✅ Iwapo walimu wangelifungua mioyo yao kumpokea Roho huyu, wangelikuwa tayari kushirikiana naye katika kutenda kwa ajili ya wanafunzi wao; na pale anapopewa njia huru, atasababisha mabadiliko ya ajabu. Atafanya kazi katika kila moyo, akirekebisha ubinafsi, kuumba na kusafisha tabia, na kuleta hata mawazo kuwa mateka kwa Kristo. …

✅ Badala ya kunyamazishwa na kurudishwa nyuma, Roho Mtakatifu ingelifaa akaribishwe, na uwapo wake kuhimizwa. Wakati walimu wanapojitakasa wenyewe kupitia katika utii wa Neno, Roho Mtakatifu atawafanya kuona kidogo mambo ya mbinguni. Watakapomtafuta Mungu kwa unyenyekevu na bidii, maneno ambayo wameyazungumza kwa msisitizo thabiti yatachoma mioyoni mwao; ndipo ukweli hautafifia katika ndimi zao.

🔘 ```Uwakala wa Roho wa Mungu hauondoi kutoka kwetu umuhimu wa kutumia akili na vipawa vyetu, bali hutufundisha jinsi ya kutumia kila uwezo kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Akili za mwanadamu zikiwa chini ya uongozi maalum wa neema ya Mungu zinakuwa na uwezo wa kutumiwa kwa ajili ya kusudi lililo bora duniani. Kutokujua hakuongezi unyenyekevu au kumfanya mtu ye yote anayekiri kuwa mfuasi wa Kristo kuthamini zaidi mambo ya kiroho. Kweli za Neno takatifu zinaweza kufurahiwa vyema zaidi na Mkristo mwenye akili. Kristo anaweza kutukuzwa vyema zaidi na wale wanaomtumikia kwa akili. Kusudi kuu la elimu ni kutuwezesha kutumia uwezo ambao Mungu ametupatia kwa namna ile itakayowasilisha dini ya Biblia na kukuza utukufu wa Mungu.```
👆🏽 - North Pacific Union Gleaner, May 26, 1909.

*UWE NA TAFAKARI NJEMA MTOTO WA MUNGU*
_______________________________

Pastor Caleb Migombo: PUMZIKA KIDOGO / GET SOME REST

                   PUMZIKA KIDOGO

Kwanini Yesu, katikati ya siku yenye shughuli nyingi, aliwataka wanafunzi wake kuuacha umati wa watu na kwenda naye mahali pa faraga kupumzika? Alifahamu kuwa kadri walivyokuwa na kazi nyingi za kufanya ndiyo walivyohitaji kuweka muda wa kupumzika na kuwa pamoja na mwokozi wao. Kutofanya hivyo mwisho wake kungewaumizi wao wenyewe na wale wote waliokusudia kuwahudumia.

Sisi nasi leo, ni muhimu kuzingatia ukweli huu.

Mungu anajua shughuli zako na changamoto za Maisha yako ya kila siku – Iwe ni nyumbani, kazini, au Kanisani. Mungu anajua pia kuwa unahitaji hekima yake ili uweze kuwa na mtizamo sahihi wa kila shughuli na namna inavyopaswa kufanywa- na unahitaji pia nguvu kutoka kwake ili uweze kufanya kila jambo kwa usahihi. Kama hutapanga kuwa na muda wako wa kupumzika na kupata nguvu mpya (kimwili na kiroho)- upo uwezekano mbeleni wa wewe na wote uwapendao kuumia. Uchovu unaathiri kufikiri kwetu, namna tunavyowasiliana, na uwezo wetu wa kupenda wanaotunzunguka.

Yesu akawaambia, “Twendeni peke yetu mpaka mahali pa faragha mkapumzike kidogo.” Alisema hivyo kwa kuwa kulikuwa na watu wengi mno waliokuwa wanafika hapo na kuondoka hata Yesu na wanafunzi wake hawakuweza kupata nafasi ya kula chakula" Marko 6:31


                  GET SOME REST

Why, in the midst of such a busy day, did Jesus insist His disciples leave the crowds to rest and be alone with Him? He knew that the busier they were, the more they need to make time to rest and be alone with Him. If they didn’t, eventually they would hurt both themselves and those who they were seeking to help. The same is true for us

God knows the demands and responsibilities you face-at home, on the job, even in your church. But God also knows you need His wisdom to keep those things in perspective, and you need His strength to get them done rightly.

Then, because so many people were coming and going that they did not even have a chance to eat, he said to them, “Come with me by yourselves to a quiet place and get some rest.” Mark 6:31

Kesha la asubuhi: Anaongoza Utakaso wa Familia

                   *KESHA LA ASUBUHI*

                 _ALHAMISI MEI 10, 2018_

           *Anaongoza Utakaso wa Familia* _Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee. Mithali 22:6._

📝 Ninawasihi wazazi kujiweka tayari wao wenyewe na watoto wao kujiunga na familia ya juu. Kaa tayari, kwa ajili ya Kristo, kaa tayari kukutana na Bwana wako kwa amani. Anza kufanya kazi katika familia yako kwa namna itakayoleta matokeo mema. Anza katika mzizi wa jambo lenyewe. Leteni ukweli katika nyumba zenu, ili kuwafanya kuwa watakatifu na kuwatakasa. Usiuache katika ua wa nje. Ni vipofu kiasi gani wale wanaodai kuwa Wakristo kuhusu maslahi yao wenyewe! Ni kiasi gani wanashindwa kabisa kuona kile ambacho Kristo angeliwatendea iwapo angeliruhusiwa kuingia katika nyumba zao.

📝 Hebu Wakristo na watende kwa bidii ili kupata taji ya uzima kama vile walimwengu wanavyotenda ili kupata manufaa ya kidunia, na kanisa la Mungu kwa hakika litasonga mbele likiwa na nguvu. Roho Mtakatifu hutoa matendo ambayo yanapatana na sheria ya Mungu. Kazi ya kuhuisha ya Roho itaonekana katika familia zenye kujitahidi ili kuonesha wema, uvumilivu, na upendo. Uwezo wenye nguvu zote uko kazini, ukiandaa akili na mioyo ipate kujisalimisha kwa uwezo unaoumba wa Roho Mtakatifu, ukiwaongoza wazazi kujitakasa wao wenyewe, ili watoto wao pia wapate kutakaswa.

📝 Nyumba ambayo washiriki wake ni Wakristo wapole, waungwana huweka mvuto wenye ushawishi mwingi kwa ajili ya wema. Familia zingine watazingatia matokeo yaliyopatikana na nyumba kama hizo, na watafuata mfano uliowekwa, kwa upande wao wakilinda kaya zao dhidi ya mivuto ya kishetani.

📝 Malaika wa Mungu mara nyingi watatembelea makazi ambayo ndani yake mapenzi ya Mungu yanatawala. Chini ya nguvu ya neema ya Mungu kaya kama hiyo inakuwa ni mahali pa kuburudisha kwa wasafiri dhaifu na wachovu. Kwa kulinda kwa uangalifu, nafsi inazuiwa kujionesha kuwa na haki. Mazoea sahihi yanatengenezwa. Kuna utambuzi makini kuhusu haki za watu wengine. Imani itendayo kazi kwa upendo na kuitakasa roho inashikilia usukani, na kuitawala kaya yote. Chini ya mvuto mtakatifu wa kaya kama hiyo, kanuni za udugu zilizowekwa katika Neno la Mungu zinatambuliwa kwa upana zaidi na kutiiwa. - Southern Watchman, Jan. 19, 1904.

   *MUNGU AKUBARIKI   UNAPOTAFAKARI*

Kesha la asubuhi: Anajibu maombi ya kutaka msaada wa Mungu

         *KESHA LA ASUBUHI*
                 JUMATANO
                    09/05/2018
*_ANAJIBU MAOMBI YA KUTAKA MSAADA WA MUNGU _* 📖 _Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo. Kumbukumbu 6:6, 7_.

✍🏽Akina baba na akina mama, nitawezaje kupata maneno ya kuelezea jukumu lenu kubwa! Kwa tabia mnayoidhihirisha mbele ya watoto mnawafundisha kumtumikia Mungu au kuitumikia nafsi. Basi toa maombi yako ya dhati kwa mbingu kwa ajili ya msaada wa Roho Mtakatifu, ili mioyo yenu ipate kutakaswa, na kwamba njia mnayoifuata iweze kumheshimu Mungu na kuwavuta watoto wenu kwa Kristo.

✍🏽 Inapasa kuwapa wazazi hisia ya umakini na utakatifu wa kazi yao, pale wanapotambua kuwa kwa mazungumzo au matendo ya kizembe wanaweza kuwapoteza watoto wao.

✍🏽Wazazi wanahitaji uongozi wa Mungu na Neno lake. Wasipoyasikiliza mashauri ya Neno la Mungu, wasipofanya Biblia kuwa mshauri wao, kanuni ya maisha, watoto wao watakua wakiwa wazembe na watatembea katika njia za kutokutii na kutokuamini.

✍🏽 Kristo aliishi maisha ya kazi na kujikana nafsi, na alikufa kifo cha aibu, ili apate kutoa mfano wa roho ambayo itawachochea na kuwatawala wafuasi wake. Kadiri ambavyo wenzi wa maisha wanajitahidi nyumbani kwao kufanana na Kristo, mvuto wa mbinguni utaenezwa katika maisha ya familia yao.

🙇🏽‍♂```Katika kila nyumba ya Kikristo Mungu anapaswa kuheshimiwa kwa dhabihu za asubuhi na jioni za sifa na maombi. Kila asubuhi na jioni maombi ya dhati inabidi yapande kwa Mungu kwa ajili ya baraka na uongozi wake. 
Je Bwana wa mbingu atapita katika nyumba kama hizo na asiache baraka hata moja pale? Hapana, kwa kweli.

🙇🏽‍♂ Malaika wanasikia utoaji wa sifa na maombi ya imani, na wanabeba maombi kwenda kwake yeye anayehudumu katika patakatifu kwa ajili ya watu wake, na kukiri ustahili wake kwa niaba yao. Maombi ya kweli hushikilia nguvu za Mungu na kuwapa watu ushindi. Juu ya magoti yake Mkristo anapata nguvu ya kupinga jaribu. - Review and Herald, Feb. 1, 1912.```

*MUNGU TUWEZESHE KUTAMBUA KIMBILIO LETU NI WEWE TU*

Kesha la asubuhi: Kando ya akina mama akiwaongoza watoto wao

        *KESHA LA ASUBUHI*

        _JUMANNE MEI 08, 2018_

_Kando ya Akina Mama Akiwaongoza Watoto Wao_  _Naliomba nipewe mtoto huyu; Bwana akanipa dua yangu niliyomwomba; kwa sababu hiyo mimi nami nimempa Bwana mtoto huyu; wakati wote atakaokuwa hai amepewa Bwana. Naye akamwabudu Bwana huko. 1 Sam 1:27, 28._

🔶 Akina mama Wakristo wanapaswa kutambua kuwa wao ni watendakazi pamoja na Mungu wakati wanapowafundisha na kuwaadabisha watoto wao katika namna ambayo itawawezesha kuakisi tabia ya Kristo. Katika kazi hii watakuwa na ushirikiano wa malaika wa mbinguni; lakini ni kazi ambayo kwa masikitiko imepuuzwa, na kwa sababu hii Kristo ananyang’anywa urithi wake-washiriki walio wadogo wa familia yake. Lakini kupitia kwa ukaaji ndani wa Roho Mtakatifu, ubinadamu unaweza kutenda kazi pamoja na uungu.

🔷 Somo la Kristo wakati wa kuwapokea watoto, linapaswa kuacha alama yenye kina juu ya mioyo na akili zetu. Maneno ya Kristo yanawahimiza wazazi kuwaleta watoto wao kwa Yesu. Wanaweza kuwa wakaidi, na kuwa na hisia kali kama zile za kibinadamu, lakini hii haipasi kutukatisha tamaa ya kuwaleta kwa Kristo. Aliwabariki watoto waliopagawa na hisia kali kama yake mwenyewe.

🔴 Mara nyingi tunakosea kuwafundisha watoto. Mara nyingi wazazi wanawaendekeza watoto katika kile kilicho cha kibinafsi na chenye kuharibu maadili, na, badala ya kuwa na uchungu wa roho kwa ajili ya wokovu wao, wanawaacha kuzurura bila malengo wala mwelekeo, na kukua wakiwa na tabia potovu na mienendo isiyopendeza. Hawakubali wajibu wao waliopewa na Mungu kuwaelimisha na kuwafundisha watoto wao kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Hawaridhishwi na tabia za watoto wao, na kuvunjwa moyo wanapotambua kuwa makosa yao ni matokeo ya uzembe wao wenyewe, na kisha wanakatishwa tamaa.

🔵 Lakini ikiwa wazazi wangelihisi kwamba kamwe hawawekwi huru kutokana na mzigo wao wa kuwaelimisha na kuwafundisha watoto wao kwa ajili ya Mungu, iwapo wangelifanya kazi yao kwa imani, wakishirikiana na Mungu kwa maombi na kazi ya dhati wangelifanikiwa katika kuwaleta watoto wao kwa Mwokozi. Hebu akina baba na akina mama wajitoe wao wenyewe, roho, mwili, na nafsi kwa Mungu kabla ya kuzaliwa kwa watoto wao. - Signs of the Times, Apr. 9, 

*TAFAKARI NJEMA NA MUNGU AKUBARIKI*

Kesha la asubuhi: Mwenye Wazazi Wanaojali

      *KESHA LA ASUBUHI*

     _JUMATATU MEI 07, 2018_

    *Mwenye Wazazi Wanaojali*  _Usinitenge na uso wako, Wala roho yako mtakatifu usini-ondolee. Unirudishie furaha ya wokovu wako; Unitegemeze kwa roho ya wepesi. Nitawafundisha wakosaji njia zako, Na wenye dhambi watarejea kwako. Zaburi 51:11-13._

📚Ni ombi la namna gani hili! Ni dhahiri kiasi gani kuwa wenye dhambi walioko nyumbani hawapaswi kutendewa kwa kutokujali, bali kwamba Bwana anawaangalia kama walionunuliwa kwa damu yake. Katika kila kaya ambamo ndani yake wamo ambao hawajaongoka, inapaswa kuwa kazi ya wale ambao wanamjua Bwana kutenda kwa hekima kwa ajili ya wongofu wao. Bwana kwa hakika atabariki juhudi za wazazi, wakati ambapo kwa kicho na upendo watajitahidi kuokoa roho za walio katika kaya zao. Bwana Yesu anasubiri kuonesha neema.

📚 Kwamba kazi ingelianza moyoni! “Maana hupendezwi na dhabihu, au ningeitoa, Wewe huridhii sadaka ya kuteketezwa. Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; Moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau.” (Zaburi 51:16, 17). Basi hebu na ifahamike na wanakaya wote kwamba kazi hii lazima ianze moyoni. Moyo lazima utiishwe na kufanywa kuwa na toba kupitia katika uwezo wa Roho Mtakatifu unaoumba, na kufufua. Kwa kutambua msaada wa wakala huyu mwenye nguvu, je wazazi hawawezi kufanya kazi kwa ari na upendo zaidi kwa ajili ya wongofu wa watoto wao kuliko walivyowahi kufanya hapo nyuma?

📚Ahadi ya Bwana ni kwamba “Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.” (Ezekieli 36:25-27).

📚 Roho wa Bwana anapofanya kazi katika mioyo ya wazazi, maombi na machozi yao yatakuja mbele za Mungu, watasihi kwa bidii, na watapokea neema na hekima kutoka mbinguni, na watakuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa ajili ya watoto wao ambao hawajaongoka. Kadiri Roho huyu anapodhihirishwa nyumbani, ataletwa kanisani, na wale ambao ni wamisionari wa nyumbani nao pia watakuwa mawakala wa Mungu kanisani na katika dunia. Taasisi ambazo Mungu amezipandikiza zitabeba tabia tofauti kabisa. - Review and Herald, March 14, 1893.

*TAFAKARI NJEMA NA MUNGU AKUBARIKI MTOTO WA MFALME*

Kesha la asubuhi: Bado tunapendwa ijapokuwa tunakosea

      *KESHA LA ASUBUHI*

     _JUMAMOSI MAY 5, 2018_

   *Bado Tunapendwa Ijapokuwa Tunakosea* _Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki. 1 Yoh. 2:1._

✍🏿 Wale ambao wako katika muunganiko na Mungu ni mifereji kwa ajili ya nguvu ya Roho Mtakatifu. Iwapo mtu ambaye kila siku anawasiliana na Mungu atakosea njiani, iwapo atageuka hata kidogo na kuacha kumtazama Yesu kwa uaminifu, hiyo si kwa sababu anatenda dhambi kwa makusudi; kwa kuwa anapoona kosa lake, anarejea tena, na kukaza macho yake kwa Yesu, na ukweli kwamba amekosea haumfanyi kuwa na thamani pungufu moyoni mwa Mungu. 

✍🏿 Anafahamu kuwa ana mawasiliano na Mwokozi; na anapokemewa kwa ajili ya kosa lake katika jambo fulani la hukumu, hatembei kwa kinyongo, na kumlalamikia Mungu, bali huligeuza kosa lile kuwa ushindi. Anajifunza somo kutoka katika maneno ya Bwana, na kuchukua tahadhari asije akadanganyika tena.

✍🏿 Wale ambao wanampenda Mungu kwa kweli wanao ushahidi wa ndani kuwa wao ni wapendwa wa Mungu, kwamba wana mawasiliano na Kristo, kwamba mioyo yao inachochewa kwa upendo motomoto kwake. Ukweli kwa ajili ya wakati huu unaaminiwa kwa imani hai. Wanaweza kusema kwa uhakika wote, “Maana hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu, tulipowajulisha ninyi nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na kuja kwake; bali tulikuwa tumeuona wenyewe ukuu wake. … 

✍🏿 Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing’aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.” (2 Petro 1:16-19). Maisha ya ndani ya roho yatajidhihirisha yenyewe katika mwenendo wa nje. Hebu acha Neno la Mungu libebe ushuhuda wake badala ya mjumbe ambaye kupitia kwake Mungu ametuma ujumbe katika siku hizi za mwisho ili kuwaandaa watu waweze kusimama katika siku ya Bwana. 

✍🏿 “Jinsi ilivyo mizuri juu ya milima Miguu yake aletaye habari njema, Yeye aitangazaye amani, Aletaye habari njema ya mambo mema, Yeye autangazaye wokovu, Auambiaye Sayuni, Mungu wako anamiliki!” (Isaya 52:7). Hekima ya wale wanaoitwa wasomi haiwezi kutegemewa, isipokuwa wamejifunza na kila siku wanajifunza masomo kutoka katika shule ya Kristo. Wanadamu, katika hekima yao ya kudhaniwa, wanaweza kupanga na kubuni nadharia na mifumo ya falsafa, lakini Bwana anawaita bure na wapumbavu. Bwana anasema, “Upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu.”(1 Wakorintho 1:25). - Review and Herald, May 12, 1896.

*MUNGU AKUBARIKI MTOTO WA MFALME*

Kesha la asubuhi: Kuzungukwa na ngao ya Mungu

*KESHA LA ASUBUHI*

*Alhamisi 03/05/2018*

*Kuzungukwa na Ngao ya Mungu*

Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa, na wewe utanitukuza. Zaburi 50:15.

📖Majaribio yanapoinuka ambayo yanaoelekea kutoku-elezeka, hatupaswi kuruhusu amani yetu kuharibiwa. Hata tutendewe isivyo haki kiasi gani, hebu hasira kali isiinuke. Kwa kuendekeza roho ya kulipiza kisasi tunajidhuru sisi wenyewe. Tunaharibu imani yetu wenyewe kwa Mungu, na kumhuzunisha Roho Mtakatifu. Kando yetu yuko Shahidi, Mjumbe wa mbinguni, ambaye atainua kwa ajili yetu bendera dhidi ya adui. Atatufungia ndani kwa miale angavu ya Jua la Haki. Shetani hawezi kupenya ndani ya miale hii. Hawezi kuipita ngao hii ya nuru takatifu.

📖Wakati dunia ikisonga mbele katika uovu, asiwepo hata mmoja kati yetu atakayejidanganya kwamba hatutakuwa na magumu. Bali ni magumu haya haya ndiyo yanayotufikisha katika chumba cha uwapo wa Mungu. Tunaweza kutafuta ushauri wa Yeye asiye na kikomo katika hekima.

📖Bwana anasema, “Ukaniite siku ya mateso” (Zaburi 50:15). Anatualika kumpelekea matatizo yetu pamoja na mahitaji ya lazima, pamoja na hitaji letu la msaada wa Mungu. Anatuambia omba haraka. Mara tu tatizo linapoinuka, tunapaswa kumtolea maombi yetu ya uaminifu na ya dhati. Kwa kuombaomba sana kwetu tunatoa ushahidi wa imani yetu kubwa kwa Mungu. Hisi ya uhitaji wetu hutuongoza kuomba kwa bidii, na Baba yetu wa Mbinguni anaguswa na kusihi kwetu. Mara nyingi wale wanaoshutumiwa au kuteswa kwa ajili ya imani yao wanajaribiwa kufikiri kwamba wameachwa na Mungu. Katika macho ya wanadamu wako upande wa wachache. Katika mwonekano wote adui zao wanaonekana kushinda juu yao. Lakini hebu na wasikiuke dhamiri yao. Yeye aliyeteseka kwa niaba yao, na kubeba huzuni na mateso yao, hajawaacha.

📖Watoto wa Mungu hawajaachwa peke yao na kuwa bila ulinzi. Maombi hugusa mkono wa Mwenyezi. Maombi “hushinda milki za wafalme, kufunga vinywa vya simba, kuzima nguvu ya moto” – Tutaelewa kinachomaanishwa pale tutakaposikia taarifa za wafia dini ambao walikufa kwa ajili ya imani yao- “walikimbiza majeshi ya wageni” (Waebrania 11:33, 34). – Christ’s Object Lessons, uk. 171, 172.

*MUNGU AKUBARIKI UNAPOTAFAKARI*

Kesha la asubuhi: Kuweka msingi thabiti

*KESHA LA ASUBUHI*

_JUMAPILI APRILI 29, 2018_

*Kuweka Msingi Thabiti*

🗓 Sauti ya Mungu inanena nasi kupitia katika Neno lake na zipo sauti nyingi tutakazozisikia; lakini Kristo amesema tuwe macho dhidi ya wale watakaosema, Kristo yupo hapa au Kristo yuko kule. Sasa, tutajuaje kwamba hawana ukweli, kama tusipoleta kila kitu kwenye Maandiko? Kristo ametuonya kuwa macho na manabii wa uongo ambao watatujia katika jina lake, wakisema kwamba wao ni Kristo.

🗓 Sasa, ikiwa utakuwa katika mtazamo kwamba sio muhimu kwenu kuelewa Maandiko ninyi wenyewe, mtakuwa hatarini kupotezwa na mafundisho haya. Kristo amesema kwamba kutakuwa na kundi ambalo siku ile ya malipo hukumuni litasema, “Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Lakini Kristo atasema, “Ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu” (Mathayo 7:22, 23)…

🗓 Muda unakuja ambapo Shetani atafanya miujiza mbele za macho yenu, akidai kwamba ndiye Kristo; na kama miguu yako siyo imara kwenye ukweli wa Mungu, utapelekwa mbali kutoka kwenye msingi wako. Usalama wako pekee ni kuchunguza ukweli ili kupata hazina zilizofichwa. Chimbua ukweli kama mtu achimbaye hazina ardhini nawe wasilisha Neno la Mungu, Biblia, mbele za Baba wa mbinguni, na kusema, Niangazie; nifundishe kile kilicho kweli.

🗓 Roho wake Mtakatifu atakapowajia mioyoni mwenu, ili kuweka mguso wa ukweli nafsini mwenu, haitakuwa rahisi kwenu kuuachia. Mmepata uzoefu huo katika kuyachunguza Maandiko, kiasi kwamba kila sehemu imethibitishwa. Na ni muhimu kwamba mdumu kuchunguza Maandiko. Inakupasa uhifadhi Neno la Mungu moyoni; kwani mnaweza kutenganishwa na kuwekwa mahali ambapo hutakuwa na fursa nzuri ya kukutana na watoto wa Mungu. Hapo ndipo mtakapohitaji hazina za Neno la Mungu mioyoni mwenu na wakati upinzani utakapowajia ukiwazingira, mtahitaji kuleta kila kitu kwenye Maandiko. Review and Herald, Aprili 3, 1888.

 

*TAFAKARI NJEMA NA MUNGU AKUBARIKI*

Kesha la asubuhi: Kuweza Kubainisha Ukweli Kutoka Katika Uongo

                *Kesha la Asubuhi*

        *Ijumaa : Tarehe 27/4/2018*

*Kuweza Kubainisha Ukweli Kutoka Katika Uongo* 🙏Maana watu kama hao ni mitume wawawe uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza mfano wa mitume wa Kristo. Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. 2 Wakorintho 11:13, 14.*

🙏Ukweli ni madhubuti na kupitia katika utii uwezo wake huwa unaubadili moyo uwe na sura ya Yesu. Ni ukweli kama ulivyo katika Yesu ambao unahuisha dhamiri na kubadilisha moyo; kwani moyoni huwa unaambatana na Roho Mtakatifu. Wapo wengi ambao, huku wakipungukiwa utambuzi wa kiroho, huchukua tu herufi za Neno, na kukuta kwamba haliambatani na Roho wa Mungu, kwamba halihuishi nafsi, halitakasi moyo. Mtu anaweza kunukuu kutoka Agano la Kale na Jipya, anaweza kujua amri na ahadi za Neno la Mungu; lakini Roho Mtakatifu asipouweka ukweli moyoni, akiangazia akili kwa nuru ya kimbingu, hakuna nafsi itakayouangukia Mwamba na kuvunjika; kwani ni wakala huyu wa kimbingu anayeunganisha nafsi na Mungu.

🙏Bila kuangaziwa na Roho wa Mungu, hatutaweza kuutambua ukweli toka katika uongo nasi tutaanguka chini ya majaribu stadi na udanganyifu ambao Shetani atauleta duniani. Tumekaribia kufungwa kwa pambano kati ya Mfalme wa nuru na mfalme wa giza na muda sio mrefu udanganyifu wa adui utazijaribu imani zetu, zionekane ni za namna gani. Shetani atafanya miujiza machoni pa mnyama na kudanganya “wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama” (Ufunuo 13:14).

🙏Lakini japo mfalme wa giza atafanya kazi kuifunika dunia kwa giza, na kwa giza nene kabila za watu, Bwana atadhihirisha uwezo wake wa kuongoa. Sharti kazi ikamilishwe duniani inayofanana na ile iliyofanyika wakati wa kumwagwa kwa Roho Mtakatifu katika siku zile za wanafunzi wa awali, walipomhubiri Yesu, Yeye aliyesulubiwa. 

Wengi wataongolewa kwa siku; kwani ujumbe utaenda kwa nguvu. Ndipo itakaposemwa: “Injili yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu” (1 Wathesalonike 1:5). Ni Roho Mtakatifu anayewavuta watu kwa Kristo; kwani huwa anachukua mambo ya Mungu na kumwonesha mwenye dhambi. Yesu alisema: “Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari” (Yohana 16:14). – Review and Herald, Nov. 29, 1892.

Kesha la asubuhi: Kuweza kutambua nadharia za uongo

                    KESHA LA ASUBUHI 

                             ALHAMISI

                             26/04/2018

*_KUWEZA KUTAMBUA NADHARIA ZA UONGO_* 

📖 *Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu. Yuda 3.*

✍🏽Yuda analeta ujumbe huu ili kulinda waumini dhidi ya mivuto inayodanganya ya walimu wa uongo, watu wenye mfano wa utauwa lakini wasio viongozi salama.

 Katika siku hizi za mwisho, walimu wa uongo watainuka na kuwa watendaji wenye ari. 

✍🏽Nadharia za naomba zote zitawasilishwa ili kupotosha akili za wanaume na wanawake kutoka kwenye ukweli unaoonesha kile tunachoweza kukisimamia bila wasiwasi wakati huu, huku Shetani akifanyia kazi kwa nguvu washika dini, akiwaongoza kuwa na mfano wa kuwa wenye haki, lakini wakishindwa kujiweka chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu.

✍🏽Mafundisho ya uongo yatachanganywa na kila hatua ya uzoefu na kutetewa na bidii ya kishetani ili kushikilia akili ya kila mtu ambaye hana mzizi na msimamo katika ujuzi kamili wa kanuni takatifu za Neno. 

✍🏽Katikati yetu kabisa watainuka walimu wa uongo, watakaosikiliza roho zinazodanganya ambazo chanzo cha mafundisho yake ni Shetani. Walimu hawa watavuta wanafunzi wawafuate. Wakijipenyeza bila kuonekana, watatumia maneno ya kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa na kufanya mawasilisho yasiyo sahihi kwa ustadi huku wakitumia mbinu za udanganyifu.

✍🏽Tumaini la pekee la makanisa yetu ni kudumu kuwa macho. Wale wenye msimamo mzuri kwenye ukweli wa Neno, wale wanaojaribu kila kitu kwa “BWANA asema hivi” wako salama. 

Roho Mtakatifu atawaongoza wale wanaothamini hekima ya Mungu kuliko mafumbo yanayodanganya ya mawakala wa kishetani. 

✍🏽Hebu na pawepo kuomba kwingi, sio katika mtazamo wa kibinadamu bali chini ya uvuvio wa upendo wa ile kweli kama ilivyo katika Kristo Yesu. Familia zinazoamini ukweli yapasa zinene maneno ya hekima na akili – maneno yatakayowajia kama matokeo ya kuyachunguza Maandiko.

🙇🏽‍♂ ```Huu ndio muda wetu wa kutahiniwa na kujaribiwa. Sasa ndio wakati ambapo washiriki wa kila familia inayoamini ni lazima wafunge midomo dhidi ya kunena maneno ya kushtaki ndugu zao. Hebu na wanene maneno yanayoleta ujasiri na kuimarisha imani itendayo kazi kwa upendo na kusafisha mioyo. – Kress Collection, uk. 5.```

*MUNGU AWE NANYI MNAPOTAFAKARI NENO LAKE.*

Kesha la asubuhi: Kutotumainia Maono Yetu

*KESHA LA ASUBUHI*
_JUMATATU APRILI 23, 2018_
 *Kutotumainia Maono Yetu* _Nitayatafakari mausia yako, Nami nitaziangalia njia zako. Nitajifurahisha sana kwa amri zako, Sitalisahau neno lako. Zaburi 119:15, 16._

✍🏿 Mungu amewapa watu ujuzi ulio muhimu kwa ajili ya wokovu kwenye Neno lake. Maandiko Matakatifu yapasa yakubaliwe kama udhihirisho wa mapenzi yake wenye mamlaka, usiokosea. Maandiko Matakatifu ni kiwango cha kupimia tabia, mdhihirishaji wa mafundisho, na kipimo cha uzoefu. “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema” (2 Timotheo 3:16, 17).

✍🏿 Hata hivyo, ukweli kwamba Mungu amedhihirisha mapenzi yake kwa watu kupitia kwa Neno lake hakujaondoa umuhimu wa kuwepo kwa Roho Mtakatifu na uongozi wake. Kinyume chake, ahadi ya Roho ilitolewa na Mwokozi wetu, ili afungue Neno kwa watumishi wake, aangaze na kuweka mafundisho yake katika matumizi. Na kwa sababu ni Roho wa Mungu aliyevuvia Biblia, haiwezekani kwamba mafundisho ya Roho wakati wowote yawe kinyume na yale ya Neno.

✍🏿 Roho hakuletwa – wala kamwe hawezi kutolewa – ili kuizidi Biblia; kwani Maandiko yanasema wazi kabisa kwamba Neno la Mungu ni kipimo ambacho kwa hicho mafundisho yote na uzoefu ni lazima yajaribiwe. Mtume Yohana anasema, “Msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani” (1 Yohana 4:1). Naye Isaya anatamka, “Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi” (Isaya 8:20).

✍🏿 Kazi ya Roho Mtakatifu imetupiwa lawama kubwa kutokana na maovu ya kundi la watu ambao, huku wakidai kuwa na ujuzi juu yake, wanadai kutokuwa na hitaji zaidi la uongozi kutoka kwenye Neno la Mungu. Hawa wanaongozwa na fikra ambazo wanadai kuwa ni sauti ya Mungu moyoni. Lakini roho anayewatawala siyo Roho wa Mungu. Hali hii ya kufuatilia fikra hizi, huku Maandiko yakipuuziwa, inaweza tu kufikisha katika machafuko, udanganyifu na uharibifu. Hii inaendeleza tu mipango ya yule mwovu.

✍🏿 Kwa sababu huduma ya Roho Mtakatifu ina umuhimu mkubwa kwa kanisa la Kristo, ni mbinu ya Shetani, kupitia kwa makosa ya wenye itikadi kali na misimamo mikali, kutweza kazi ya Roho na kusababisha watu wa Mungu kupuuzia chanzo hiki cha uwezo ambacho Bwana wetu mwenyewe ametupatia. – The Great Controversy, uk. vii, viii.

*MUNGU AWABARIKI MNAPOTAFAKARI NENO*

ULAFI NA KUTOKUWA NA KIASI

ULAFI NA KUTOKUWA NA KIASI: Ulafi na kutokuwa na kiasi ndiyo msingi wa anguko kuu la upotovu wa maadili katika ulimwengu wetu. Shetani analifahamu hili na daima huwajaribu wanaume na wanawake waendeleze ladha ya kionjo kwa gharama ya afya nahai wenyewe. Kula, kunywa na kuvaa yamefanywa kuwa lengo la maisha kwa ulimwengu. Hali ya mambo imekuwa sawa naile iliyokuwa kabla ya gharika, na hali hii ya ubadhirifu ni moja ya ushahidi bayana Wa ukaribu Wa kufungwa kwa historian ya Dunia hii.

Tunajua kwamba Bwana anakuja mapema sana. Ulimwengu unaharakisha kuwa kama ulivyokuwa katika siku za Nuhu. Umejikita kwenye kuendekeza ubinafsi. Kula na kunywa hufanywa kupita kiasi. Watu wanakunywa Vileo vyenye sumu ambayo huwafanya kuwa wehu. Kitabu cha matukio ya siku za mwisho, UK, 21.

**Nimeitowa kwa rafiki yangu Facebook**

Kesha la asubuhi: Kutokuongozwa kwa hisia

                KESHA LA ASUBUHI 

                        JUMAPILI

                        22/04/2018

*_KUTOKUONGOZWA KWA HISIA_*
📖 *Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu. Zaburi 119:105.*

✍🏽Utakaso sio hali ya hisia ya furaha inayotawala kwa muda mfupi, sio kazi ya mara moja, bali kazi ya maisha yote.

Yeyote akidai kwamba Bwana amemtakasa na kumfanya kuwa mtakatifu, uthibitisho wa dai lake la kuwa na hiyo baraka utaonekana kwenye matunda ya upole, subira, uvumilivu, ukweli na upendo.

✍🏽 Ikiwa baraka ambayo wale wanaodai kuwa wametakaswa inawaongoza kutegemea namna fulani ya mhemko, nao wanasema kwamba hakuna hitaji la kuchunguza Maandiko ili wapate kujua mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa, basi, hiyo baraka inayotajwa ni ya bandia, kwani inawaongoza wale walio nayo kuthamini mihemko na matamanio yasiyo takaswa na kufunga masikio yao dhidi ya sauti ya Mungu katika Neno lake.

✍🏽Kwa nini wale wanaodai kuwa wamekuwa na udhihirisho wa pekee wa Roho, na ushuhuda kwamba dhambi zao zimesamehewa zote, wahitimishe kwamba wanaweza kuiweka Biblia pembeni na kuanzia hapo watembee peke yao? Tunapowauliza wale wanaodai kupata utakaso wa ghafla, ikiwa wanayachunguza Maandiko kama Yesu alivyowaambia wafanye, 

✍🏽kuona kama hakuna ukweli wa ziada kwa ajili yao kuukubali, huwa wanajibu, “Mungu huwa anatufahamisha mapenzi yake moja kwa moja katika ishara maalum na mafunuo nasi tunaweza kuiweka Biblia pembeni.”

✍🏽Wapo maelfu wanaodanganywa kwa kutumainia mihemko fulani maalum na kutupilia mbali Neno la Mungu. Hawa hawajengi kwenye msingi ambao ndio pekee ulio salama na wa hakika – Neno la Mungu. Dini inayoelekezwa kwa viumbe wenye akili itaonesha vithibitisho vya kimantiki vinavyoonesha uhalisia wake, kwani kutakuwa na matokeo dhahiri moyoni na kwenye tabia. Neema ya Kristo itadhihirishwa kwenye mwenendo wao wa kila siku. 

✍🏽Bila wasiwasi tunaweza kuwahoji wale wanaodai kutakaswa, “Matunda ya Roho yanaonekana maishani mwako? Je, unadhihirisha upole na unyenyekevu wa Kristo na kufunua ukweli kwamba unajifunza kila siku kwenye shule ya Kristo, ukijenga maisha yako kulingana na mfano wa maisha yake yasiyo na ubinafsi?

🙇🏽‍♂```Ushuhuda bora zaidi ambao yeyote kati yetu anaweza kuwa nao juu ya uhusiano wetu na Mungu wa mbinguni ni kwamba tunazishika amri zake.

🙇🏽‍♂ Uthibitisho bora zaidi wa imani katika Kristo ni hali ya kutojitumainia nafsi na kumtegemea Mungu. Uthibitisho pekee wa kuaminika wa sisi kuwa katika Kristo ni kuiakisi sura yake. Kadiri tunavyofanya hivi, tunathibitisha kwamba tunatakaswa kwa njia ya ukweli, kwani ukweli unaoneshwa katika maisha yetu ya kila siku. – Signs of the Times, Feb. 28, 1895.```

*MUNGU AWE NANYI MNAPOTAFAKARI*

Kesha la asubuhi: Kuongozwa kwa Njia ya Ushuhuda Ulioandikwa

*Kesha la Asubuhi*

*Alhamisi, Tarehe 19/4/2018*

*Kuongozwa kwa Njia ya Ushuhuda Ulioandikwa*

▶Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi. Isaya 8:20.

▶Daima Roho Mtakatifu anaongoza kwenye Neno lililoandikwa na huwa anavuta usikivu katika suala la kiwango kikuu cha maadili cha uadilifu. Kuheshimiwa na Mungu kwa namna hiyo kwa kupata fursa hii ya pekee kushuhudia ukweli ni jambo la ajabu. Kristo aliwaambia wanafunzi wake mara kabla ya kupaa juu na wingu la malaika kumpokea na kumwondoa machoni pao, “Mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi” (Matendo 1:8). Walifanywa wafae kumshuhudia Kristo kutokana na karama ya kimbingu ya Roho Mtakatifu.

▶Natamani kuwasisitizia ukweli kwamba wale ambao Yesu anakaa mioyoni mwao kwa imani kwa kweli wamempokea Roho Mtakatifu. Kila mtu anayempokea Yesu kama Mwokozi wake binafsi kwa uhakika pia anampokea Roho Mtakatifu kuwa Mshauri, Mtakasaji, Kiongozi na Shahidi wake. Kadiri muumini anavyotembea kwa karibu na Mungu, ndivyo ushuhuda wake unavyozidi kuwa wazi na kama matokeo yaliyo ya hakika, ndivyo mvuto wa ushuhuda wake utakavyokuwa wenye nguvu zaidi kwa wengine kuhusu upendo wa Mwokozi; ndivyo atakavyozidi kuonesha uthibitisho kwamba anathamini Neno la Mungu. Hiki ndicho chakula chake, ndicho kinywaji chake, kwa ajili ya kuridhisha nafsi iliyo na kiu. Anathamini fursa hii ya pekee ya kujifunza mapenzi ya Mungu kutoka katika Neno lake.

🔽Baadhi ya watu wanaodai kuwa waumini wameweka pembeni, wamegeukia mbali na Neno la Mungu. Wameipuuzia Biblia, Mwongozo ulio wa ajabu, kipimo cha kweli cha mawazo yote na wanadai kwamba wanaye Roho anayewafundisha, kwamba hili linafanya suala la kuchunguza Maandiko lisiwe la muhimu. Wote wa namna hii wanasikiliza hila za Shetani, kwani Roho na Neno wanakubaliana. Maandiko yanasema, “Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi.” Yeye ambaye ukweli unamweka huru ndiye mtu ambaye yuko huru kweli. – Manuscript Releases, vol. 14, uk. 70, 71.

Kesha la asubuhi: KUTAKASWA KWA NJIA YA NENO

                  KESHA LA ASUBUHI

                          JUMATANO

                         18 Apr 2018

*_KUTAKASWA kWA NJIA YA NENO_*
📖 *Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli. Yohana 17:17.*

✍🏽Mzigo wa ombi la Yesu ulikuwa kwamba wale waliomwamini Yeye waweze kulindwa dhidi ya uovu wa dunia na kutakaswa kwa njia ya ile kweli. Yeye huwa hatuachi katika hali ya kubuni kusiko na uhakika kama ukweli ni nini, bali huongezea, “Neno lako ndiyo kweli.”

✍🏽 Neno la Mungu ni njia ambayo kwayo utakaso wetu ni lazima ukamilishwe. Kwa hiyo, ni jambo la muhimu sana, kwamba tujifahamishe maelekezo matakatifu ya Biblia. Ni jambo la muhimu kwetu kuelewa maneno ya uzima kama ilivyokuwa kwa wanafunzi wa awali kufahamishwa kuhusu mpango wa wokovu.

✍🏽Hatutakuwa na udhuru ikiwa, kutokana na uzembe wetu wenyewe, hatutajua madai ya Neno la Mungu. Mungu ametupatia Neno lake, udhihirisho wa mapenzi yake naye amewaahidi Roho Mtakatifu wale wanaomwomba, ili awaongoze kwenye kweli yote; na kila nafsi ambayo kwa uaminifu inatamani kufanya mapenzi ya Mungu itayajua mafundisho.

✍🏽Dunia imejazwa na mafundisho ya uongo; na tusipochunguza Maandiko kwa ajili yetu wenyewe kwa makusudi, tutakubali makosa yake kana kwamba ndio ukweli, tutakubali mila zake na kudanganya mioyo yetu wenyewe.

✍🏽 Mafundisho na desturi za dunia vinatofautiana na ukweli wa Mungu. Wale wanaokusudia kugeuka kutoka katika kuitumikia dunia ili wamtumikie Mungu watahitaji msaada wa kimbingu. Itawapasa kukaza nyuso zao kama chuma kuelekea Sayuni. Watahisi upinzani wa dunia, mwili na mwovu, nao itawapasa waende kinyume cha roho na mivuto ya dunia.

✍🏽Tangu nyakati Mwana wa Mungu alipokabiliana na chuki zisizo na sababu na majivuno na hali ya kutokuamini ya watu, hakujawa na badiliko katika mtazamo wa dunia kwa dini ya Yesu. Watumishi wa Kristo ni lazima wakutane na roho ile ile ya upinzani na shutuma na ni lazima kwenda “nje ya kambi, tukichukua shutumu lake” (Waebrania 13:13).

🙇🏽‍♂```Utume wa Yesu ulidhihirishwa kwa miujiza ambayo haikuwa na mashaka. Mafundisho yake yaliwashangaza watu. Mafundisho yake hayakuwa lugha za kitaalamu zilizokinzana za waandishi, zilizokuwa zimejawa na imani za mafumbo, ambazo zilikuwa na mizigo ya mifumo ya kipuuzi na ulazimishaji usio na maana;

🙇🏽‍♂ lakini ni mfumo wa ile kweli ambao ndio uliokutana na mahitaji ya moyo. Mafundisho yake yalikuwa wazi, bayana na yenye upana. Ukweli halisi aliousema ulikuwa na uwezo wa kusadikisha, nao ulivutia usikivu wa watu. – Review and Herald, Feb. 7, 1888.```

*MUNGU AWABARIKI NYOTE MNAPOTAFAKARI NENO LAKE.*

Kesha la asubuhi: Kufurahi katika neno

*Kesha la asubuhi*

_Jumanne Aprili 17, 2018_

*_Kufurahi Katika neno_* _Maneno yako yalionekana, nami nikayala; na maneno yako yalikuwa ni furaha kwangu, na shangwe ya moyo wangu; maana nimeitwa kwa jina lako, Ee Bwana, Mungu wa majeshi. Yeremia 15:16._

📝 Katika kutekeleza dini ya Biblia, kuna hitaji la subira, uungwana, kujikana nafsi na kujinyima. Lakini, kama Neno la Mungu litafanywa kuwa kanuni inayodumu maishani mwetu, kila linachotwambia inatupasa kufanya, kila neno, kila tendo lililo dogo, litadhihirisha kuwa sisi ni raia wa Yesu Kristo, kwamba hata mawazo yetu yamewekwa kwenye kifungo chake. Neno la Mungu likipokelewa moyoni, litaondoa nafsini hali ya kujitosheleza nafsi na kuitegemea nafsi.

📝 Maisha yetu yatakuwa nguvu kwa ajili ya kutenda mema, kwa sababu Roho Mtakatifu atajaza mioyo yetu kwa mambo ya Mungu. Dini ya Kristo itatekelezwa nasi; kwani nia zetu zipo katika upatanifu kamili na mapenzi ya Mungu. Baadhi ya wale wanaodai kuwa na dini ya kweli inasikitisha kwamba huwa wanapuuzia Kitabu kilicho Mwongozo utokao kwa Mungu ili kuelekeza kwenye njia ya mbinguni. Wanaweza kusoma Biblia, lakini kusoma tu Neno la Mungu, kama mtu asomaye maneno yaliyoandikwa kwa kalamu ya mwanadamu, kutampa mtu ujuzi wa juu juu tu.

📝 Kuuzungumza ukweli hakutatakasa wapokeaji. Wanaweza kudai kufanya kazi ya Mungu, wakati ambapo, kama Kristo angekuwa kati yao, sauti yake ingesikika, akisema, “Mwapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu” (Mathayo 22:29). Watu wa namna hiyo hawataweza kujua kile dini ya kweli inachokimaanisha.

📝 Kristo alisema, “Maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima” (Yohana 6:63). Yeremia anashuhudia juu ya Neno la Mungu akisema, “Maneno yako yalionekana, nami nikayala; na maneno yako yalikuwa ni furaha kwangu, na shangwe ya moyo wangu.” Kuna uponyaji wa kimbingu katika Neno la Mungu, ambao wale waitwao wenye hekima na busara hawawezi kuupata, lakini ambao unadhihirishwa kwa watoto.

📝 “Kufafanusha maneno yako kwatia nuru, Na kumfahamisha mjinga” (Zaburi 119:130). Kama Neno hili litahifadhiwa moyoni, litakuwa ni hazina ya moyo, ambako vitatoka ndani yake vitu vipya na vya kale. Hatutaendelea kufurahia kufikiria mambo duni ya dunia, bali tutasema, “Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu” (aya ya 105). – Review and Herald, Mei 4, Mei 4, 1897.

_TAFAKARI NJEMA MWANA WA MUNGU_