Category Archives: Tanzanian Houston Community -THC

President Lambert Tibaigana: Hatuta saidia mtu ambaye hasaidi wengine

Rais wa jumuiya ya Watanzania waishio katika jimbo la Houston, Texas Hon. Lambert Tibaigana akielezea kwa kina baadhi ya maazimio ambayo yalijadiliwa na kupitishwa na wana jumuiya hiyo na pia akigusia mambo machache ya msingi ambayo katiba ya jumuiya hiyo imezingatia.

Kama wewe ni Mtanzania unayeishi katika mji wa Houston na vitongoji vyake basi tunakuomba ujiunge na wanajumuiya wengine katika kuiendeleza jumuiya yetu. Tafadhali jiunge na jumuiya yetu, saidia viongozi wetu kwa kumtaharifu kila Mtanzania unaye mjua kuwa anaombwa ajiunge na jumuiya hii kwani inafaida sana kwa vizazi vyetu vilivyopo sasa na vijavyo! Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki THC.

Hongera viongozi wapya wa THC!

Wiki iliyopita Watanzania waishio katika jiji la Houston, Texas walichagua viongozi wapya wa jumuiya yao ambao wataanza kuongoza kuanzia mwezi wa kwanza mwakani kwa kipindi cha miaka miwili. Nikiwa kama mmoja wa Watanzania ambao tunaishi ndani ya jumuiya hii naomba niwape pongezi viongozi wote waliochaguliwa kutuongoza kwa kipindi kijacho. Japo sijakaa sana hapa Houston lakini naweza shuudia kuwa nimeona mambo mazuri toka kwa wanajumuiya ambayo naamini ni matunda ya uwongozi bora. Hivyo Kama ilivyo kwa wengine nami nategemea kuona mambo mazuri zaidi katika jumuiya yetu! Hongereni Sana! Vile vile pongezi kwa viongozi mliomaliza muda wenu kwa kutuongoza vyema.  Pichani katikati ndio Rais / Mwenyekiti mpya Mr Lambert Tibaigana. Kulia ni dada Anasa Kambi yeye ni Katibu wa jumuiya. Na Kushoto ni dada Aneti Asenga yeye ni Muweka Hazina........... Kwa  picha na maelezo zaidi bonyeza ?? THC