Category Archives: The MboniShow- Marekani

Mahojiano: The Mboni show na Linda Bezuidenhout

Samahani wapendwa mimi bado sijaitizama, nitaangalia jioni ya leo na kutoa maoni yangu baadaye.

Update: Nimetizama mahijioni, nimecheka sana. Nice show! Sidhani kama kuna mtu atakuzuia kwenda Tanzania Linda! Mie naamini upo safe!

Tafadhali usipitwe na The MboniShow msimu mpya kila Ijumaa saa Moja!

“Thembonishow show msimu mpya unaanza na show za ughaibuni, show za nchini Marekani, Thembonishow ilipata mualiko maalum kutoka Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Dallas Texas nchini Marekani kwa ajili ya kufanya coverage ya shughuli iliyo andaliwa na jumuiya hyo iitwayo TANZANIA DAY. Kuna vitu vingi vilifanyika kwenye hiyo siku ya Tanzania Day, ilikuwa ni event ya siku tatu. Basi sisi Thembonishow tutawaletea matukio yote yaliyojiri siku hizo zote tatu na pia mtapata nafasi ya kuwasikia Watanzania waishio Marekani na shughuli zao kwa ujumla. Usikose kuangalia Show Ijumaa hii 2/6/2017 TBC1 kuanzia saa 1:00 Jioni.” ~~~~The MboniShow team

Alpha Igogo-blogger

Tafadhali, naomba usipitwe na msimu huu mpya wa The MboniShow kwani utakuwa umekosa kujifunza mengi mno kutoka kwa Watanzania waishio Marekani! Ni msimu wa wa kuvutia, unasisimua, na kufundisha mengi kuhusu maisha ya wana diaspora na watu wote ambao wanaoishi hapa haswa wale wenye asili ya Kitanzania! Yes! Nimeshajifunza kitu teyari; kuwa, ukichukua uraia wa nchi nyingine wewe sio tena MwanaDiaspora kwani Tanzania hairuhusu Dualcitizenship / raia pacha! Asante sana Ben kwa kutuelimisha………….Nitakuwa nawaletea Link ya hizo show hapa ili kwawale ambao hamko Tanzania muweze kutazama!