Category Archives: Womanhood

Womanhood!

Much respect to all hustling hard to improve their reality while most are escaping theirs…… www.brooklyncitycollege.co.za find us….📚👩‍🎓👨‍🎓
Giiiirrlllll listen, there is no elevator to success. You have to take the stairs. @luluzhair

Jojo! Katika ubora wake!

Need I say more! My girl Jojo looking A-maz-ing as always! Unajua siku zote hakikisha you look intelligent than “sexy” utaheshimika sana! Looking sexy is okay but its just not right!   My Jojo looks beautiful, elegant, and intelligent 💗 it!

Mama Igogo katika ubora wake!

Mama Igogo akifanya yake katika ubora wake, na Tshirt yake ya “I ❤ Halotel”!  This lady can’t sit down 😅😅 Yani ukimuona mama yangu amekaa chini yani kule ku-relax nyumbani absolutely doing nothing but enjoying yourself; basi jua ni mgonjwa siku hiyo 🙉 Kupika aliacha long time ago, rarely utamkuta akipika ila mambo yake ni kama haya analima bustani zake za mboga, viazi vitamu, mahindi, n.k….. Kama hayupo kwenye bustani ya vyakula basi kwenye banda lake wa kuku wa kienyeji, ni shidaaaa! Btw, hapo ni nje tu ya nyumba yake hivyo haitaji dereva kumpeleka shamba 🙈🙈 Mama yangu was raised with two great human being I have never met before! Babu yangu na bibi yangu mzaa mama walikuwa watu wakarimu mno! Wenye upendo wa hali ya juu, waungwa sana, na wanyenyekevu kupita kipimo! Hivyo simshangai sana mama yangu kuwa hivi alivyo! Namuombea maisha marefu yenye afya njema sana na amani tele ndani ya moyo wake! Huyu ni my niece Sarah! Ni mtoto wa dada yangu Grace-AnyangoNyoyoo, lakini analelewa na bibi yake (my parents). Naona yupo likizo sasa anadeka na kwa bibi na babu 😍 Missing you mwanangu mie, love you always! Janeth, katoka kwake Mbezi kuja kuchuma mboga kwa mama,  kaiba na ujuzi akaenda kulima kwake 😍……… siye wengine kulima hatukusaidii lakini kwenye kuvuna tutavuna na kuvifaidi wote 😅😅 …….. I ❤ my family!

My favorite people in one picture!

My new found mama. She’s such a poser🙌🏽😍, so ICONIC. Africa’s Princess @yvonne_chakachaka 💖#howmanytimesdoyougettopowderalegend #imeeeeean #rightbeforeshehitsthestage ☺️

Wow! There are some of my very few favorite people, all in one picture!!! I’m smiling like #Zezeta………. Yani utafikiri mie ndio Jojo katika picha, Jojo please kiss her some more just for me 😂😂 ……. Powerful women in Africa right there representing two different generations! Look at that natural beauty #BlackDon’tCrack   🙌🙌🙏❤❤

“Tusiwe wepesi wa kupungukiwa na imani, tena tusichoke njiani.”~~~~ Faraja Nyalandu

Neema ya Mungu haina kipimo tena hutenda kwa wakati wake. Hakuna lililo gumu mbele za Mungu. Hakuna ajuaye kesho ila Yeye mwenye mamlaka yote. Kila aliloahidi anaenda kulifanya. Asante dada @ladivamillen, ushuhuda wako ukaseme na kila aliyekata tamaa. Tusiwe wepesi wa kupungukiwa na imani, tena tusichoke njiani. God reigns! #TearsOfJoy #BabyKairo

**ngoja nikusindikizie huu ujumbe wako na huu wimbo**
 

The shade of Blue by Wema Sepetu!

What a beauty! Wema mdogo wangu wewe ni mrembo mno! Mungu took some extra time just for you! Naamini mama Sepetu kila mara akuonapo  machoni pake lazima atakuwa anasema " Alhamdulillah" na tabasamu laini moyoni 😍😍 You are so beautiful my dear and Yes! BLUE is your color! Inakupendeza sana na kukupa nuru nzuri mno! I just love it on you! "Rolls-Royce or Bentley don't have to run commercials because they know the values of their product &  that value brings customers to them. When you know your value you don't have to beg for anybody to spend time with you or even love you.  Everybody can't AFFORD or even HANDLE  luxury.......or  your trials ..........The diamond cannot be polished without friction, nor the man perfected without trials" >>>>>>>>>> Bishop Larry Boyd Stay strong our sweetheart. God will surely grant you all the good things that your heart desires! 🙏  💖

Womanhood!

With my girls…@irenekiwia and @mama_alaska
Wahenga walisema kuwa kaa karibu na waridi unukie! Jamani hii ni kweli kabisa! Watu ambao unakaa nao muda mwingi wanachangia sana kukujenga katika fikra na tabia zako! Inawezekana wakakujenga kwa ubora wa utu na maadili au wakakujenga katika udhaifu wa kupungukiwa na utu na maadili! Surround yourself with greatness! Ukizungukwa na watu ambao wanafurahia kuona wengine wakitahabika na kusononeka basi nawe utajikuta unakuwa na roho hiyo hiyo! Surround yourself with those on the same Mission as you! .........Mmependeza sana wadada!

#WanawakeNaMaendeleo

#WanawakeTunaweza

#UkomboziWaMwanamkeUtaletwaNaMwanamkeMwenyewe

Mama Salma Kikwete akabidhi kijiti!…….Mama Samia Suluhu awa mlezi mpya wa Girl Guides Association!

 Kilikuwa kipindi kizuri na chenye mafanikio kwa wasichana na wanawake kwa muda wote tuliokuwa pamoja na mama yetu Mhe Mama Salma Kikwete kama mlezi wa chama chetu cha Tanzania Girl Guides Association na hatimae leo hii kukabidhi kijiti kwa Makamu Wa Rais Mama Samia Suluhu kama mlezi mpya wa chama. Tunategemea mengi mazuri kutoka kwa Mama Samia hasa katika malezi ya mtoto wa kike #TanzaniaGirlGuidesAssociation #Wagggs #FriendsOfGirlGuidesTanzania ❤️ My Jojo you too cute like Cookie Iyobo, are guys related or because I love y'all ndio mkaamua ku-look alike 🙈🙈 pendeza sana! Yes! Ukisikia mwingine jua katoka China au Thailand. 😂😂    #FakeZoneCountries 
Hongera sana mama yetu kipenzi Mh. Samia Suluhu kwa majukumu mapya ya ulezi wa watoto wakike! Najua na ninaamini wadogo zetu na mabinti zetu wakike watakuwa salama chini ya uwangalizi wako! Asante sana mama Salma Kikwete kwa kuifanya kazi hiyo vyema. 🙏  Mbarikiwe mama zetu 😘

#WanawakeTunaweza 
#UkomboziWaMwanamkeUtaletwaNaMwanamkeMwenyewe

Womanhood!

I said last week, she's not a Diva! Soma 👉👉  NaweweNikamaMimi 
 anaweza kwenda popote pale na akaishi bila tatizo! Yani ni mtu anayependa vitu vizuri na maisha mazuri lakini hajui kuringa! Divas wanamaringo, nyodo, na dharau za kufa mtu! Yani vitu fulani hivi ambavyo vipo so annoying in a normal life!.........But Zari, you know how I love you! You are like my best friend that  I have not met yet 🙈🙈 So, honestly, watsup with your man? Is he  just a "social jack" or something is going on that we need to know? .......This evening through his Snapchat he was dancing like nothing but a total jack at his mom's birthday party! I don't have Snapchat but my daughter does. She was shocked, decided to share with me! Like really! Is that type of a "father figure" you want for your boys? Watsup my dear! Think deep and do some before it's too late! ......❤❤

Wema Sepetu katika ubora wake!

Wema Sepetu katika ubora wake! Vazi limemkaa haswa aaa! Kapendeza sana! My dear Wema naomba leo nikushauri, unajuwa wewe ni our Sweetheart! Tunakupenda sana na kukutakia mema! Naomba usichukie kuhusu ushauri wangu kwani unatoka from a good place of my heart, na pia sio lazima uhufuate unaweza ukasoma na ukauwacha kama ulivyo! Na ninakuhakikishia bado nitakupenda bila kinyongo! …… Wema sikiliza: 《1》Hii karne ya 21 kuzaliwa mzuri tu haitoshi! Wewe ni mzuri sanaaaaaa! Lakini unamengi ya ku-prove ili umpate yule mume / partner unaye stahili kuwa naye KAMA KWELI HILO NI HITAJI LA MOYO WAKO!

《2》 Achana kabisa na watu /fans wako ambao saa zote wanakueweka katika muonekano wa “mashindano” na mtu fulani haswa Zari, wakati Zari got no time for nobody yani yupo busy na maisha yake! Wewe ishi maisha yako bila kupigizana kelele na mtu! Au kuweka mazingira fulani yanayo onyesha some sort of competition! Kumbuka mtu yeyote yule ambaye anataka kushindana na mtu jua huyo mtu teyari umesha mzidi ndio maana anataka aku-drug down to  his /her level! Always choose “highway” na sio mashindano! 《3》Ngoja nikwambie ukweli, wewe na Zari wote ni wazuri sana tena to be fair labda niseme wewe umependelewa zaidi na figure kuliko Zari! Hata hivyo any man ambaye ni potential au well successful will absolutely pick Zari over you! Unajua kwa nini? Zari has proven herself kuwa (a) she knows what she wants in her life! And happiness is her number one priority! Na ndio maana aliamua kuachana na marehemu Ivan Ssemwanga na kuwa na Diamond! She prefers happyness over money (b) Zari has proven kuwa she can make her man to be the best of all! She did that twice! Kwa marehemu Ivan Ssemwanga na sasa kwa Diamond! Ndio, unaweza sema ulimpenda Diamond akiwa bado “Nasib Abdul” but mdogo wangu, wenyewe wanasema hivi “a man with dreams need a woman with vision”! Na hapo ndipo Zari alipokupiga bao! You knew Nasib’s dreams but you didn’t have VISION to take Diamond where he needs to be! Plus badala ya kuwa team player ukawa kama una compete na Diamond; kumbuka zile kauli kuwa “anatembelea nyota yako” toka kwa mashabiki wako na watu wako wakaribu! Zari aliacha yote kumjenga Diamond at least for the first two yrs ya relationship yao. Building Diamond ikamsaidia kujiendeleza na yeye pia kwa ku-expand her empire in Tanzania. Wakati alionekana kama amepoteza Dira ya maisha  kwenye macho ya watu wenye mtazamo finyu lakini kwetu sisi wengine tulijua Zari is going to surprise them big time and she surely did! Kumbuka nimekwambia kuwa Zari nia yake ni kuwa na mwanaume ambaye will make her happy, and that is what exactly Diamond is doing! Spoiling her right before your eyes! Pia angalia Ivan Ssemwanga, pamoja na yote bado Zari alikuwa ndio Kimbilio na tegemeo lake! Kitu ambacho wewe mpaka dakika hii pamoja na kuteka people’s heart but none of them can trust you with their “treasure” or legacy! (c) Zari has proven kuwa she is not only a great partner but  she can hold down a family as well! She’s strong, has good family values enough to make her own family kitu ambacho wanaume wengi waliofanikiwa wanapenda kuwa nacho! Na hapa siongelei kuwa na watoto kwani watoto ni mipango ya Mungu! Ninacho kisema hapa nikuwa “grounded” enough to make someone’s house a family friendly place ambapo mtu kama Dr. Mengi atakuwa excited, and proud enough kusema I’m going home na once in a while kuwaita some of his friends for dinner! Mpaka sasa kwa hili mdogo wangu Wema, umefeli kabisa! Siku zote waliokuzunguka mmh! only God knows who they are! Embu jifunze kitu kutoka kwa aunt Ezekiel! 《4》 My dear Wema, achana na kutafuta attention zisizo na kichwa wala miguu! Don’t let them losers and fools use you my dear! Kama kweli you want to have that potential man holding your hand then you need to prove kuwa you are a woman of character! Make your man feel secured kuwa hayupo kwenye “competition” with another man! Yani kuwa akija mwenye hela zaidi yake he’s out of the league! Hii inaweza ikawa ngumu kunielewa lakini mpaka utakapo elewa hichi ninacho kwambia basi tegemea kutumika na wanasiasa pamoja na wenye pesa za “mission-town” ambao wanatafuta kuandikwa kwenye magazeti ya udaku!

《5》 Kama nilivyo sema kuwa you’ve  a lot tu-prove na kitu kingine ni kuonyesha kuwa you can stand strong alone na kua-achieve something for your own good! Kwamfano mimi sio such a “career woman” but I managed to get my college education. Nasio hivyo tu, nimelea mwanangu ambaye niko so proud of her! Plus, naishi mwenyewe hapa Marekani bila msaada wa mwanaume hivyo mwanaume yoyote yule atajua kuwa kama tumependana ni kwasababu zingine na mapenzi ya kweli nasio ugumu wa maisha wa hapa Marekani! Angalia, mfano wa karibu ni Jokate, she’s a great example kama utataka kujifunza kutoka kwake! You have to show some potentials!

《6》Lamwisho, achana na mashoga a.k.a “wadada wa mujini”! You have your sisters make them marafiki zako wa karibu. Unaweza ukawa na baadhi ya marafiki wazuri kwa kula “bata” but don’t let them be your close friends! Kwasababu naona wengi wao sio wazuri na mkikorofishana siri zako  zote wanakutolea nje wakati wewe sioni kama unatabia ya kutoa siri za watu! Hivyo achana nao kabisa! Otherwise, mie nakupenda sana na nakutakia mafanikio mema. Najua bado unanafasi ya kufanya matengenezo! Kama nimekosea naomba unisamehe sana. ❤

The journey to motherhood: Congratulations Nambua Cassandra!

Alpha Igogo -bloggerWapendwa wasomaji wangu, naomba niwaletee tukio zuri sana la safari ya kuzaliwa mtoto Prince. Ni tukio ambalo limekuwa recorded na shemu ya hiyo video imeonyeshwa na mama mzazi kwa kupitia account yake ya Instagram! ……….. Kwanza nianze kwa kusema hongera sana kwa Nambua kwa kujaliwa mtoto wa kiume! Mungu amlinde akuwe katika kimo na hekima. Akampendeze Mungu kwanza na kisha wanadamu! Karibu katika chama cha wakinamama/ wazazi! Safari hii ni ndefu, yenye changamoto nyingi lakini ni tamu mno! Nasema nitamu mno kwani kama kuna kitu nime furahia kwa 100%  na bado naendelea kufurahia with all the pride is being a mother! Lakini kila siku namrudishia sifa na utukufu kwakwe Mungu maana bila yeye hakuna litakalo wezekana! ……..kwakweli nimependa sana hii familia ya Mr and Mrs Mlaki! Nimependa sana their spirit, wako so open and together, inapendeza sana mfano mzuri sana wa kuigwa katika jamii! Hii dunia imeshabadilika (21st century) kuna mambo mengi ya karne 19 inabidi kuyaacha maana siyo tu jamii haiipi nafasi bali pia hata technology haivitaki! Kwa mfano katika karne hii 21 n* kitu cha kawaida kabisa katika jamii zilizo ona mbele mama na kijana wake kuwa ndani ya chumba cha upasuaji wakimuangalia binti/ dada akileta kiumbe kingine duniani! Wakati jambo kama hilo bado linaweza likawa tatizo katika sehemu nyingi za Africa! ……….. Maelezo yote ambayo yameambatana na picha yameandikwa na Nambua ambaye ni mama mzazi wa Prince!  #NaniKamaMama. Yesterday 4th June, 2017 was one of my big day osn earth. Nimepata experience ya ajabu sana katika maisha yangu. Mwenyenzi Mungu Muumba Mbingu na Nchi amenijalia kujifungua mtoto wa kiume 9.25am South African time. HIYO NI FIRST FOTO ALIPOTOKA TUMBONI KWANGU, ALIPOTOLEWA KAANZA KULIA. Ilikuwa sala yangu kujifungua mtoto wa kwanza DUME. I’M OFFICIALLY A MOTHER. Jana usiku sijalala kabisa nimekaa natoa macho, namshangaa huyu mtoto. Bado siamini kama ni mtoto wangu, namuona stranger, mgeni flani hivi. Na sikujua watoto wanatoka mbali hivi. Heshima kwa wamama wote waliozaa. 😘😙. Napenda kuwashukuru wote waliokuwa na mimi katika hii safari yangu. Nikisema nitaje majina mengi sitamaliza. Surely it was a long trip. My brother @laumlaki huyu ni commando aliingia theatre aka record tukio zima la Cesarean operation na mama yangu @lwisemanka amempokea mjukuu wake. Lord Jesus I give you glory. In Christ I have made it to God be the Glory. Yeremia 29:11 HAKIKA MAWAZO YA BWANA NI MEMA JUU YANGU, Yeremia 33:3…… BWANA AMENIONYESHA MAMBO MAKUBWA MAGUMU NISIOYAJUA.

Hapo niko theatre (operation room) najindaa nimlete mwanangu duniani. Nacheka cheka tu naona wanachelewa……😀. Niko na mama na mdogo wangu @laumlaki paparazzi. Hili tukio kwangu ni very historical considering mahala nilipotoka. Nilisema Im going to record kila kitu wakati najifungua niweke ktk dvd. Namshangaa Bwana Yesu na matendo yake makuu juu yangu. Nawashukuru sana MEDICLINIC, SANDTON. Doctors & Nurses are very friendly na makini ktk kazi. Biblia inasema katika torati: Mateso ya mwenye haki ni mengi, lakini BWANA humponya nayo yote.🤔🤔😍😍😃 Amen. 

My mother @lwisemanka, my mdogo @laumlaki and my photographer ms melody, hawa nilikuwa nao theatre. Walitaka waone ceserean section inavyokuwa, yani kila kitu na wawe wa kwanza to see my baby. Nimewaita mashilawadu wangu.😀😀😀😀…….. love you all. Kweli watoto wanatoka mbali sana. Halafu hili zoezi nimelipenda sana la kuingia theatre na familya yako au photographer wako.

Hapo nimetoka kutoa mtoto tumboni naumwa sana, nimezinduka. Koo limekauka kwani niliwekewa oxygen. Yani kuitwa mama aisee ni kazi! Nafundishwa kunyonyesha naona ni adhabu halafu siamini kama nitaitwa mama. Shikamoo mwanamke. Naomba wanaume wawaheshimu wale wanawake waliozaa wakawafanya wakaitwa wababa. Hii experience ni ya ajabu. Wamama shikamooni. Kuanzia leo simgombezi tena mama yangu……. Biblia inasema ZABURI 34:19-21 MATESO YA MWENYE HAKI NI MENGI LAKINI BWANA HUPONYA NAYO YOTE.HUIHIFADHI MIFUPA YAKE MY FIRST BORN,UZAO WANGU WA KWANZA…… BWANA MUNGU AKASEMA HAKIKA NITAKUBARIKI NAE AKANIBARIKI NA HUYU KIUMBE KATIKA JINA LA YESU …………… PRINCE THAT HIS NAME.NI PRINCE MTOTO WA MFALME WA WAFALME, JEHOVAH RAPHA. TODAY HE IS ONLY 15DAYS OLD NA AMEANZA TO POZI TAJIRI MTOTO. I LOVE YOU MY SON. I LOVE YOU. HUYU KIUMBE NIMEMJUA SIKU 15 ZILIZOPITA ILA NAMPENDA KULIKO VIUMBE VYOTE DUNIANI…….😘😘😘😘 MY LIFE HAS CHANGED 100%. #nambuacassandra @baby.mix.baby. 

Me and My baby PRINCE that his name (tajiri mtoto)…… hapo yuko 12days old😀😍😇😘. Na nilipokuwa natafakari🤔🤔 siku zangu duniani, Nae Mungu akasema na mimi akaninong’oneza MWANANGU NEEMA YANGU YATOSHA JUU YAKO. MGHH SIKUAMINI……. ILA LEO NIMEIONA NEEMA YAKE KWA KUNIZAWADIA MTOTO WA KIUME SAWASAWA NA HAJA YA MOYO WANGU. (Heart desires) 😇😇😇 Neno la Mungu linasema (Torati) Zaburi 37:4-6 Nawe utajifurahisha kwa BWANA. Naye atakupa haja za moyo wako. Umkabidhi BWANA njia yako, Pia umtumaini, naye atafanya. Ataitokeza haki yako kama nuru. Na hukumu yako kama adhuhuri……. #nambuacassandra #huumchezohauhitajihasira

***HONGERA SANA NAMBUA CASSANDRA***

“Asante mume wangu kwa kunipenda na kunijali….!” Mrs. Maria Makonda

Wiki iliyopita niliwaelezea sakata la mke wa  TV icon and comedian Mrs Bill Cosby a.k.a Camille Cosby jinsi alivyojitokeza saa za mwisho bega kwa bega na mumewe huku aki-smile kwa raha zake! Kama ulipitwa basi soma 👉👉 MrsBillCosby

Basi leo tena na waletea maneno aliyo andika Mke wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mrs Maria Makonda au kwa jina maharufu ni “Mrs Daudi Bashite” 😀😀 hizi social media ni shidaaa! Btw, kabla sijaendelea naomba ieleweke kuwa sina chuki na Makonda wala familia yake japo simuungi mkono kwa mambo aliyo yafanya kama kiongozi! Hata hivyo mimi sio mwana siasa wala sio mwanaharakati wa siasa hivyo hayo ninawaachia wataalamu wa mambo hayo ku-deal nayo! Hii blog is all about love, spirituality, family, friendship, relationships, sisterhood, brotherhood, parenthood, empowerment, na mambo mengine kama hayo ambayo yana inspire jamii! Kama kuna mtu anataka siasa tafadhali usisite kwenda  kwa Mange Kimambi, Peter Sarungi,  na Lemutuz! Haya back to our topic! ……….. Juzi kati kwa kupitia account yake ya Instagram Mrs Makonda aliandika maneno haya “Asante sana mume wangu kwa kunipenda na kunijali. Mungu akutunze”! 👇👇 Haya maneno anayaandika baada ya scandals zote ambazo zimemuandama mumewe kuanzia sakata la vyeti feki, vita feki ya madawa ya kulevya, na mengine mengi bila kusahau kuhusishwa na scandal za kuwa na mahusiano ya kimapenzi na muigizaji Kajala Masanja pamoja na Agnes Masogange! …….. Mimi nasema waacheni watu na ndoa zao kwani hakuna mtu anaejua sababu haswa zinazowafanya wanawake wengi wasimame na waume zao hata pale ambapo watu wengi wanaona ni wakati wa kumuacha “high and dry”! Sijui ni kwasababu ya kiapo #Kitakatifu. au mapenzi au ni huruma tu ambayo mwanamke ameumbwa nayo! Simnaona hata mimi hapa bado nimesimama kidedea na my Muhaya yani hapa ni Kigoma mwisho wa reli  😀😀😀  kama nawaona wapika majungu sura zao zinavyo pooza 😷😷 Haachwi mtu hapa poleni sana mtahachika nyie na ndoa zenu fake za Facebook 🙆🙆 #StandByYourMan #GodHelpUs

Camille Cosby hatimaye bega kwa bega na mumewe!

Mimi naamini kuzaliwa “mwanamke” ni mtihani tosha, lakini kuwa mke unayebeba jukumu lako la kuwa mke kikamilifu ni mtihani mgumu na mzito zaidi! Ukiwa umekula kiapo kile “KITAKATIFU” kuwa KATIKA TABU NA RAHA yani utakuwa unajifikiria mara mbili mbili na kujikuta unasimama hata pale usipo taka! Haya ndio yalio mkuta Mrs Bill Cosby a.k.a Camille Cosby! Baada ya ukimya na kujificha kwa takribani miaka 3, finally amejitokeza saa za mwisho bega kwa bega na mumewe ambaye anashitakiwa kwa makosa ya ku-drug wanawake na kufanya nao mapenzi bila hidhini yao ( sex assault).  As I said before being a woman is not a joke but I can only imagine how hard it is to be a fully committed wife!!

Sidhani kama Camille Cosby angekuwa na uwezo wa kujificha forever asinge fanya hivyo kwani aibu na fedhea ambayo mumewe amempa ni kubwa mnooooo! Angesema akaye pembeni society bado ingemuhukumu kwa kutokuwa “woman enough” kusimama na mumewe!! Shame! As Bill Cosby’s lawyer said in the court room kuwa the real victim here is a long  suffering Camille Cosby! Which in somehow nakubaliana naye kwani huyu ni mke walio owana kwa miaka 53, amemjua mume wake kama; mume muaminifu, baba na mwanaume ambaye siku zote analinda na kuheshimu wanawake. Akajenga “image” hiyo katika dunia kuwa yeye ni “Family man” na mkewe na watoto wake wakawa very proud of him! Sasa leo hii mbele ya uso wa dunia anatakiwa afute hiyo “image” aliyo wajengea na kuwaaminisha watu kuwa Nope! That ain’t him! Ni ngumu kueleweka na fedheha kubwa sana kwa mkewe na watoto wake wakike! Naamini sababu kuu ya Mrs Cosby kukwepa kuwepo mahakamani wakati victim wakitoa ushahidi ni kwasababu hakutaka kuweka mambo yatakayo semwa mahakamani kwenye akili yake ambayo yangemfanya aanze kutafakari na kumuangalia mumewe katika sura mpya! I believe she wants to continue to remember her husband the way she knows / knew him and not otherwise! Maana zile testimony ukizisikiliza unaweza file for Divorce bila kutaka! I truly feel sorry for her! Mungu amsaidie! Hata hivyo yeye si wakwanza kusimama bega kwa bega na mumewe katika scandal kubwa na za kufedhehesha namna hii! Wapo wanawake wengi wamefanya hivyo kama Hillary Clinton wakati mumewe anakesi ya kufanya mapenzi ndani ya moja ya office za WhiteHouse na secretary wake Monica Lewinsky!……… It’s hard to be a woman but it’s more harder to be a fully committed wife!! #StandByYourMan #GodHelpUs!

Alijisemeaga Oprah Winfrey kuwa labda hizo vows zingebadilishwa huwenda angefunga ndoa cause yeye haelewi wanaposema “katika shida na raha” what do they real mean?! 🙉🙉 Wenyewe wanasemaga hivi “if you can’t stand the heat better stay out of the ktchen” 😀😀😀 bora yeye kajisemea ukweli lol!………..Huko nyuma niliandika hivi 👉👉  TheBillCosbyTrial

 

Man-up and kill it with kindness!

Yess! Keep on moving Bosslady a.k.a the New C.E.O of the “Rich Gang” 😍😍 You Man-Up girl and em haters just kill them with kindness!!……………I just love this, do you guys see what I’m seeing?! The msg is on the shoes people!! While MEN are Manning-Up in 👞👟 “Flat” shoes  the Bosslady is Manning-Up in 👠 👢HighHeels baby 💪💪💪You Go Zari! Keep that Legacy going!! Tell them We Run this Planet, of course in HighHeels 😅😅 

Womanhood

“If you stop chasing meaningless friendships and relationships and look after and love yourself,you will enjoy your own company while the right people find their way to you🙏🏽❤️”~~~~May Charles Igogo

*****Very well said! Labda niongeze kwa kusema kuwa jinsi mtu (uwe mwanamke au mwanaume) unavyo zidi kujitambua na kujua thamani yako ule urafiki wa kama teenagers ni lazima u-cut off!! Sijui shoga yangu kutwa kuongozana kama matahira ni ujinga mtupu! If someone doesn’t add any value to you yani ukifika 33+ yani ni bora uwa drop off kwani mnapotezeana muda urafiki wenu hauna tija! Yani mimi hata rafiki anaye chukia kuona mwingine yupo happy au anafanikiwa huyo mie simtaki kabisa karibu yangu tutabaki story tu za hapa na pale tunapo kutana basi lakini ukaribu Nope! Kwani kama unachukia maendeleo na furaha ya mtu mwingine ambaye hajakukosea lolote basi hiyo nitosha kusema mimi will be next!………Hakuna kitu kizuri kama kujifunza ku-enjoy your own company kwani utakuwa na amani sana kuliko kuwa na marafiki chungumzima ambao hawakusaidii kwa lolote zaidi ya starehe!

Ujana ni ufunguo ~~~~Dina Marios

               UJANA NI UFUNGUO 

Hakikisha hupotezi funguo yako na unaitumia kufungua milango sahihi. Ukicheza na funguo yako ukaipoteza au ukachanganya usijue ufungue wapi, ukifika uzeeni ndio utajua. Sasa hivi ndio wakati wa kutengeneza maisha yako na sio uzeeni. Ukiharibu sasa hivi baadae itakuwa ngumu kuanza upya umri utakuwa umeenda.

Kijana wa leo ishi ukiwa na ndoto na maono. Sio woote Lila wengi wanaishi hawajitumi. Kijana umeshakuwa mkubwa uanze kujitegemea lakini bado unakaa nyumbani unagombania ugali na wadogo zako. Mtoto wake kiume umeshakuwa elimu unayo lakini hutaki kujishughulisha huna dira wala malengo. Watoto wa kike wamebeba uzuri kama ndio deal ya kuishi maana hana elimu, hana kazi, hana biashara, hana analolijua. Elimu anayo lakini maarifa hana ila uzuri ndio aloubeba na kuupa thamani. Hajui uzuri hufifia na kupotea je hapo baadae utaishije wakati uzuri haupo? Umbo zuri limekongoroka?

Wengi badala ya kusoma wamekimbilia mahusiano kuolewa ili iwe shortcut ya maisha………mume atamuhudumia.Ndoa zenyewe zimewafanya waishi kama Wajane ilhali waume zao hawajafa. Mateso, vilio na maumivu kila siku unalia wewe kama sio mjane kitu gani?? Simama usipoteze funguo yako……..kuwa na ndoto.

Kuwa na malengo na misimamo sasa hivi hakuna mwanaume anataka kuoa mwanamke mbugila mbugila. Huna mipango,huna maarifa wala mikakati. Unaamka saa tano hujui kupika wala kufua unajua vipindi vyote vya tv huna unachojishughulisha nacho, huna unalolijua upo upo tu. Kijana wa kiume huna ndoto zozote wala hujui unataka kuwa nani? baadae unataka uwe mume na baba wa familia kweli??? funguo yako unaijua kweli? unayo?

Kijana ishi kwa ujanja,uadilifu,kwa maarifa,kwa busara,kwa kujitambua na kwa tahadhari.
Dina Marios

“Let people get inspired by how you deal with your imperfections” ~~~~ShyRose Bhanji

“You don’t need to be perfect to inspire others. Let people get inspired by how you deal with your imperfections”………………… Maneno ya hekima haya toka kwa Dada wa Taifa! Maisha yako unayopitia au wewe mwenyewe jinsi ulivyo (your character) yawe mazuri au mabaya kwa namna moja ama nyingine lazima yatakuwa yanatoa mafunzo kwa wengine.  Huitaji kuwa mkamilifu kama “Malaika” ili kuwafanya wengine waone kuwa unafaa! Hakuna aliye mkamilifu hapa duniani na kama unafikiria wewe ni “Malaka” basi simama na uwe wakwanza kuturushia mawe sisi wadhambi!