CHADEMA HAINA HATI MILIKI YA KUWA UPINZANI PEKEE NCHINI. -Peter Sarungi

 Nilipokuwa natafakari maamuzi ya kwenda kugombea Spika wa bunge niligundua kuwa kama wewe ni mchezaji mzuri wa mpira wa miguu na unajiamini basi si lazima usajiliwe na timu kubwa kama Simba, Yanga ana Azam ili ucheze ligi kuu, kumbe unaweza kucheza ligi kuu hata kupitia Mbao Fc, Ndanda Fc, majimaji au hata Costal Union. Kinachotakiwa ni siku timu yako ikikutana na Simba ama Yanga hakikisha unafunga walau goli moja tu hata kama wao wataifunga timu yako kwa magoli 10. Hilo goli lako wataondoka nalo likiwa na jina lako. Hii ni bora zaidi kuliko kusajiliwa Simba ama Yanga halafu ukakaa benchi kwa sababu wachezaji ni wengi. Nchi yetu ni nchi ya demokrasia na nchi yenye kufunya siasa ya vyama vingi. Kuwepo kwa wingi wa vyama vya siasa ni moja ya tendo la demokrasia tunayo ikubali kila siku. Tanzania kuna vyama vya siasa zaidi ya 25 vyenye usajili wa kudumu vinavyo ruhusiwa kushiriki katika siasa zote za nchi. Ni kwa bahati mbaya Chama tawala hakijawahi kupoteza kushika dola huku vyama vya upinzani viki badilika badilika katika kuwa na wafuasi na nguvu za kisiasa hadi kupewa kijiti cha kuitwa chama kikuu cha upinzani. TLP, NCCR Mageuzi na CUF zimewahi kuwa na nguvu katika chaguzi zilizopita na kuwa chama kikuu cha upinzani wakati huo vyama kama Chadema Tanzania vilikuwa vipo chini sana na vilikuwa havijulikani kwa Watanzania walio wengi. 

Leo Bunge la Tanzania lina vyama 5 vyenye uwakilishi Bungeni huku CHADEMA kupitia muunganiko wa UKAWA wakiwa ni chama kikuu cha upinzani. Ukawa inabebwa na wabunge kutoka CUF, CDM na NCCR huku ACT ikiwa iko peke yake lakini katima kapu la upinzani ikiwa na haki zote kikatiba na hata kwa sheria za uchaguzi na za bunge.

Kumetokea taharuki kidogo juu ya nafasi za wabunge wa Afrika Mashariki hasa kwa upande wa vyama vya upinzani. Mnyukano ulikuwa ni kati ya UKAWA na ACT wazalendo juu ya nafasi 3 za upinzani. Mnyukano huo umeendelea hadi yalipo patikana maamuzi kutoka kwa Speaker juu ya mgawanyo.

Kilicho nisikitisha katika mnyukano huo wa hoja ni baadhi ya makada wa CDM kwa makusudi ama kwa kutojua kuhamisha mjadala wa kibunge na kuuweka kwa wananchi huku wakitoa lawama, matusi, kejeli na hata dharau kwa hoja iliyo tolewa na ACT kupitia mwakilishi wake Mh. Zitto Zuber Kabwe iliyotaka ACT wapate nafasi ya kugombea ubunge wa Afrika Mashariki. 

ZZK ametukanwa sana na baadhi ya makada wa mtandaoni wa CDM huku wakiamini wao ndio wapinzani pekee walio teuliwa na Mungu kuja kuwasemea watanzania. Mimi niwakumbushe tu makada wa CDM kwamba hata wao walikuwa kama mchicha kipindi CUF wakiwa Upinzani imara, Pia wakumbuke hata wao hawana HATI MILIKI ya kuwa UPINZANI pekee nchini. Wasikasirike, kubeza na kupinga wanapoona mbegu zingine za upinzani zinapo chepua kwa kasi, ipo siku mtahitaji ushirika wao ili kufikia malengo yenu.

By the way, inasemekana hata mgogoro wa CUF unawafurahisha sana CDM kuliko CCM, Maana wapo tayari na wamefungua milango kwaajili ya kuwasajili akina Seifu, Mtatiro na wengine pindi chama hicho kikifutwa kama alivyo sema Lissu kwenye mahojiano ya Azam… Daah kufa kufaana.

Msijisahau mkalewa kwa sifa na ubinafsi, ni kweli umoja ni nguvu lakini ni umoja wenye maslahi sawiha ulio Imara na wenye Nguvu.

Wasalam.

Leave a Reply