Dr. Shika kutambulishwa usikuwa wa 900 itapendeza!

Mara paa! Dr. Shika kwa celebrity! Jamani, it’s never too late to be you and achieve your dreams! Huwezi jua ni lini na kwa njia gani Mungu atakufungulia mlango wa kufikia malengo yako! Wewe fanya kazi zako kwa uwaminifu na kwa bidii mengine Mungu atakutimizia. Pia safari moja huwanzisha nyingine. Unaona hapa Dr. Shika alikwenda kwenye mnada wa kununua nyumba of his own dream japo mfukoni alikuwa “kachacha” lakini alithubutu. Mwenda bure si mkaa bure! Watanzania wangapi walikuwa wanamjua Dr. Shika lakini leo hii ndio the talk of the country! Katika umri huu kwa mazingira ya Africa haswa Tanzania sidhani kama hata yeye aliwahi kuwaza kua sentence yake moja tu “900 itapendeza”  itaweza badilisha maisha yake na kumuweka kuwa wa level nyingine kabisa! Leo hii ana mkurugenzi na kualikwa sehemu mbali mbali kuelezea maisha yake. Nani alijua kuwa maisha ya mtu kama Dr. Shika yanaweza yakawa kivutio na yahamasa kwa Watanzani?!  Somo hapa nikuwa wavumilivu katika safari za kufikia ndoto zetu kwani Mungu ndiye mpangaji na mtoaji wa vyote! Acha tamaa ya kutaka vitu kwa haraka! #900Itapendeza

Leave a Reply