Embu tucheke kidogo! Eti wewe waonaje kwa hili?

Juzi kati niliweka tangazo la msiba wa ndugu yangu  kwa hii blog , nikaambatanisha na picha ambazo tulipiga akiwa hai ambapo ilikuwa mara ya mwisho kuonana naye Tazama hapa ??  (Tanzia). Sasa kuna mtu ameweka comment akishangazwa na picha niliyotumia kwani tulikuwa tuna tabasamu. Anasema tunatangazaje kifo kwa furaha hivyo? Soma ??  Nimecheka kwani kwangu imekuwa kichekesho,nikahisi huyu dada lazima atakuwa Muhaya maana Wahaya akili zao wanazijua wenyewe, na hilo pozi wala uulizi katoka mkoa gani ?? …… Hivi kuna kanuni ya picha ipi itumike kutangaza msiba? Ukishaweka picha ya marehemu akiwa mwenyewe zile zingine sizinakua ni kumbukumbu mlizopiga!! Jamani, mimi ni Msabato na Mjaluo vile vile hivyo kuna vitu vingine haswa kwenye swala la misiba mtanisamehe. Kwani kuomboleza kupo tu lakini huwezi kuomboleza kama mpagani! Halafu, tujenge tamaduni za kuonyesha upendo wa dhati kwa wale ambao wanagusa maisha yetu wakati bado wako hai! Mambo ya kumlilia mtu na maneno mazuri akisha kufa ni upuuzi mtupu! Yani mimi kama umeshindwa kunipenda nikiwa hai, hata salamu hutujuliani gafla nikisha kufa eti wewe ndo unakuja na makelele yako kunililia?! No! Sitaki! Kaa kwako nitashukuru zaidi, kuliko kuja kunililia kinafiki! Kwanza kuliliwa na wanafiki inaweza ikawa kikwazo cha kuingia Mbinguni ?? just saying! Sipendi wanafiki haswa nikisha kufa nawaomba msije! Nionyeshe unanipenda na kunijali nikiwa hai! Nami nitafanya vivyo hivyo!

Leave a Reply