Faraja Nyalandu: Nikifeli au nikiharibu shuleni hakuongea na mimi kwa ukali, aliongea na mimi kwa uchungu

Regrann from @farajanyalandu  -  Baba yangu alikuwa ni rafiki yangu. Mimi ni wale wanaoitwa daddy's girl. Ukilelewa huku una dhana ya kupenda na kupendwa inakujengea imani na ujasiri kwasababu unakua ukijua unastahili kutoa na kupokea. Una thamani. Unastahili. Nikifeli au nikiharibu shuleni hakuongea na mimi kwa ukali, aliongea na mimi kwa uchungu. Ilikuwa ni balance nzuri kwasababu nikikosea mama yangu aliongea kwa ukali. Kuna siku nilimpa report ya shule, baada ya kuizingatia kwa muda akisikitika, akaniambia anaomba report yangu. Kimoyo moyo nikasema uzee unamjia vibaya, ananiombaje report yangu wakati kaishika mkononi. Akaniambia anajua uwezo nilionao na ile report mbaya haiwezi kuwa yangu. Ni ule uchungu ulioniuma na kunifanya nisitake kumuumiza tena baba yangu. Hakuwahi kunichapa. Lakini nimekula sana vibao na mwiko wa kupikia kwa mama. Hofu pia ilinirudisha kwenye mstari. Nilitambua nikipewa haki inakuja na wajibu ninaotarajiwa kutimiza. Alinijengea nafasi ya kumwambia kila kitu, kizuri na kibaya. Na yeye aliniambia vingi, alivyokosea na alivyopatia, alivyoona vikipatiwa na kukosewa. Aliniambia yeye si mkamilifu na wala mimi si mkamilifu lakini natosha. Katika vyote alivyonipa, namshukuru kwa kuniwezesha kujiamini, kujitambua na kutaka kuwa bora. Hivi vitu haviuzwi dukani. Sina hakika kuna shule itavifundisha ipasavyo. Pengine hizi #weekendwisdom ni matokeo ya uhusiano wetu. Mwambie binti yako anatosha, jenga msingi imara asitokee mtu mwingine kumuaminisha vinginevyo. 

Happy Father's Day Fathers!  - #regrann

Leave a Reply