#FBF: DICOTA 2012

FB_IMG_1467387426171Ngoja nianze kwa kicheko jamani kwani najua wengi mtanicheka sana ??? hapo kwenye picha ni mimi na brother James Kitia back in 2012 in Chicago kwenye DICOTA. Jana niliweka post ya James  (soma hapa) hapa baada ya mwanangu kunionyesha hiyo story. Mwanangu alikuja kwangu akasema “umemuona rafiki yako?”…………yeye anajua my story na James ndo maana akasema “rafiki yako”! Sasa ngoja ni share nanyi hiyo story……..

Jamani mie na maneno yangu yote haya ESCALATOR / moving stairway / electrical stairs ni ugonjwa wangu mkubwa ??? Sipiti kwenye Escalators hata kwa dawa aaa.???  Yani hata kuzitizama naona kama nataka kuzimia ??

Sasa wakati nakuja U.S.A kwa mara ya kwanza kabisa, nilikuja kwa ndege ya British Airways- Business class. Sasa tulivyo fika Heathrow Airport ikabidi twende hotelini kulala mpaka kesho yake ndio tulikuwa tunaondoka. Humo kwenye ndege ndipo nilikutana na kaka yangu James Kitia. Yeye final destination yake ilikuwa Chicago, Illinois na mimi ilikuwa Berrien Springs, Michigan.

Sasa basi shuttle za kwenda hotelini zilikuwa underground ambapo ukitaka kufika in 5 minutes inabidi utembee na Escalators au la sivyo inabidi utembee kawaida bila escalators ambapo itakuchukua not less than an hour!…….Mjaluo Luo mimi mbona machozi yalinitoka?? ??? …….basi hapo ndipo my coolest brother, said to me “worry not my sister, nitakusaidia”  Talking about raising a gentleman?! Someone did his / her job right!! Kudos to James’s parents!

Yani sikumuomba James msaada, but he saw my desperation and offered his helping hand to me! James akasema subiri hapa kwanza, akapeleka our hand luggages first halafu akapanda tena juu kuja kunifuata! Akaniambia nimshike nakunisaidia kushuka. Japo kwa kilio kikubwa sana lakini tulifika chini salama??

Bahati mbaya tulikuwa tunakwenda hotel tofauti hivyo tulipanda shuttle tofauti. Na pia muda wetu wa kuondoka tuliondoka mida tofauti, hivyo hatukuonana tena. Lakini nilikuwa namuongelea sana kwa watu walio nizunguka including my daughter. Baada ya miaka mingi kupita kwa mara ya kwanza tukakutana Chicago nakupiga hiyo picha ?. Wakati nafanya malipo ya DICOTA yeye ndo alipokea simu yangu na kunisaidia basi tukakumbukana hapo.

James, najua nilishawahi kukushukuru kwa ukarimu wako. Lakini naomba tena leo nirudie kusema asante sana tena sana. Mungu aendelee kukubariki katika kila jema ulitendalo wewe na familia yako. ??

NOTE: Ugonjwa wangu na Escalators bado hupo pale pale hadi leo hii! It’s just my worst nightmare, sijui kama nitakuja fanikiwa kuzipanda ??

Leave a Reply