Happy Mother’s Day to all mothers around the world!

Mdogo wangu Magreth, mimi mwenyewe, na mama, March 2017, Segerea, Tz….nyumbani kwa mdogo wangu mzee William Igogo

Nawatakieni kheri ya siku ya wakina mama wa mama wote katika dunia hii! Mungu awabariki sana na azidi kutupa khekima ya kuwalea watoto wetu katika njia mpasayo! Wale ambao wanategemea kuwa mama, basi Mungu akawatangulie mjifungue salama. Nao wanao tamani kuitwa mama basi Mungu akawajaze mibaraka hiyo kulingana na mapenzi yake!………..Tunapokuwa tukifurahia Siku hii kuu duniani tusisahau kuwaombea wamama wote ambao watoto wao wamelala usingizi wa mauti! Mungu awaponye na awape sababu ya kuwapa nguvu ya kuendelea na maisha. Na wale wamama ambao watoto zao ni wagonjwa Mungu awaponye upesi. Nawale  ambao kwanamna moja ama nyingine watoto wao wapo kwenye matatizo yoyote yale basi Mungu akafungue njia, awapiganie na shetani asipate nafasi kamwe!

Mimi mwenyewe na mama yangu, December 2016, Dar, Tz…..makazi yetu ya zamani

Nawasii wamama wenzangu tuwalee watoto katika upendo wa dhati na hofu ya Mungu! Watoto ambao hawajalele katika upendo wanakuwa tatizo kubwa si tu kwenye familia zao bali hata kwa jamii husika. Kumfundisha  mtoto kuwa strong katika maisha haimaanishi kuwa unfundishe mtoto wako roho mbaya, ukatili, kuwa bully, muongo, mnafiki, mchonganishi n.k! Hapana! Kama ni mtoto wakike mleee kama ndio the next queen! Nakama ni mtoto wa kiume mfunze kuwa a gentleman! There are too many evil men in this world let us save the world by raising our children in a Godly loving manner! ……..Happy Mother’s Day to all mothers! ❤❤

Leave a Reply