“Hata nikifumba macho sasa nawakumbuka wote walioweka mkono katika safari yangu hata kwa ushauri tu.”~~~~Dina Marios

Katika safari ya maisha yetu kuna namna Mungu aliwatumia watu kutuvusha kutoka sehemu moja kwenda ingine. Pamoja na kupambana na kusherehekea mafanikio mbali mbali tuliyopata wapo watu walituvusha Au kutugusa kwa namna moja ama ingine. Kuanzia mwalimu alokufundisha kwa mara ya kwanza a e i o u...... binaadamu tunategemeana sana ili tuweze kufikia malengo yetu. Hata nikifumba macho sasa nawakumbuka wote walioweka mkono katika safari yangu hata kwa ushauri tu.

Hata wewe hapo ulipo najua unajua wapo waliokuamini hata wakati wewe mwenyewe hujiamini, waliokupa connection flani, waliokufundisha jambo flani, walikupokea kazini kwa mara ya kwanza wakakufundisha kazi, walikukutanisha na watu wakafungua milango ya mafanikio flani n.k

Japo kila siku tunajipa moyo kuwa tunaweza.....  tumefanikiwa......lakini wapo waliotusaidia pia tukaweza kufanikisha.........na pia sio wao ni Mungu aliwainua kwa ajili yako.

Good morning!

Leave a Reply