Hawa wanaume wa hivi wapo kila sehemu! Niwakati sasa wakuwataja hadharani!

Wiki kama mbili zilizopita muingizaji wa kimataifa Lupita Nyong’o alikuwa ni mmoja wa wanawake waliojitokeza hadharani nakusema kuwa naye ni mmoja wa wanawake waliotaka kufanyiwa unyama na Weinstein Harvey! Wapendwa mambo haya yanatendeka sana hata kwenye jumuiya zetu siyo tu kwa celebrities peke yao! 

Actress Lupita Nyong’o

Kama wewe ni mtoto wa kike au wakiume ambaye umepitia hili tatizo la mtu kukuomba mapenzi ndio akusaidie au kwasababu amekusaidia naomba ujue kuwa hauko peke yako nawala usiiogope kusema hadharani. Ni muda sasa wakuwaumbua watu wote wenye hizi tabia. Hakuna mtu anatakiwa kufanyiwa unyama wa namna hii kwasababu yoyote ile!

Kuna wengine ni marafiki umemuamini rafiki yako kama hapo Lupita alivyofanya kumuamini rafiki halafu anakubadilikia!! Ni muda sasa wakuwasema hadharani!! Wasichana wengi wanateseka na hawa watu kwasababu wengi wa hawa watu ni wanaume ambao wamejijengea uwezo mkubwa wa kuaminiwa kwenye jamii kama huyo Weinstein Harvey! lakini hii ni karne ya 21 huna sababu yakuogopa tena kwani watu wengi kwenye jamii wamechoka na watu wenye hii tabia. Kama Joe Biden alivyo ongea hapa kwa hasira…..msikilize

Halafu hakuna kitu kinaniuma kama kuona wanawake ambao kwakujua kabisa wanaamua kutumika kuwakandamiza victims!! Hivi kama angekua ni mtoto wake au mdogo wake ungefanya au kusema hayo anayo yasema! Any kind of abuse hurts, itakuwa sexual abuse!?! So sad!

Wenye ujasiri wa kuongea hadharani ndio utapigwa vita kwa nguvu zote na kuzushiwa kila aina ya uwongo kama akina Alpha hapa! Lakini mimi siku hizi nimekubali kuchukiwa lakini nitasimama kwenye ukweli!! As a victim of abuse I can’t afford to see any woman going through the pain and suffering I went through!! #Silent is Complicity!!

Leave a Reply