“Hii ni sababu mojawapo kwa nini ni lazima kuachia ya nyuma yapite”- Pastor Caleb Migombo

Umeshagundua kuwa ukiendelea kumchukia mtu, chochote kile walichokutendea kitaendelea kukuumiza maisha yako yote? Hasira zetu na chuki huzidi kutonesha vidonda vya majeraha ya huko nyuma (zamani).

Hii ni sababu mojawapo kwa nini ni lazima kuachia ya nyuma yapite na – kwa msaada wa Mungu – kufungulia hasira na chuki vitoke kabisa katika  maishani mwetu, na badala yake turuhusu Upendo wa Mungu kukaa ndani yetu. Kama tusipofanya hivyo, mioyo yetu itatiwa sumu na kujaa chuki na uchungu maisha yetu yote yaliyosalia, badala ya kuakisi upendo na rehema za Kristo.  

Kumbuka Yesu anasema: “ Wapendeni adui zenu na waombeeni wanaowaudhii” Mt 5:44. 

Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya. Waef. 4:31

Leave a Reply