Hongera sana Isaka na Sarah!

Mr and Mrs Isaka Alexander Olung’a Igogo

Hayawi hayawi sasa yamekuwa! Wamehalalishwa duniani na Mbinguni yakwamba wawili hawa ni mwili mmoja!

Sarah akila kiapo kitakatifu

Agano hili takatifu lilifanyika siku ya Jumosi tarehe 05 /08/2021 katika kanisa la viziwi lililopo huko Bunguruni, Dar es salaam. Tunawaombe baraka nyingi sana katika familia yao hii mpya walio ianzisha!

Bibi harusi

Bwanaharusi akihakikisha je kweli ni yeye?! Kabla ya kula kiapo, maana hukawii kubadilishiwa mke kama Jacob (Yakobo)! ? mjini mambo mengi jama! ?

Bwanaharusi amehakikisha na ameridhia! ?? Kama hujawahi sikia kisa cha Jacob (Yakobo) basi chukua Biblia yako na ufungue kitabu cha mwanzo sura 29 yote itakupa stori kamili!

Kwaufupi ni kwamba, Jacob baada ya kutumikia miaka saba kwa mzee Labani kama mahari ya kumuoa binti yake Rachel (Raheli), siku ya harusi akakuta amebadilishiwa mke anaye mpenda kwa dhati na kupewa Lea ambaye alikuwa ni dada wa Rachel (Raheli). Kwani kulingana na mila na desturi za kabila na ukoo wa mzee Labani ni kuwa mkubwa lazima aolewe kwanza ndipo mdogo anafuata. Kwa maana hiyo Jacob ilibidi atumikie miaka 7 mingine ili aweze kumpata Rachel. Kwa maana hiyo Jacob alitumikia miaka 14 kwa mzee Labani kama mahari ya kumuoa kipenzi cha roho yake! …… Sikilizeni wanawake wenzangu, kama mwanaume anakupenda basi hakuna gumu wala zito mbele ya macho yake! He will move mountains just to have you! Tena bila hiyana yoyote! Wanawake wazuri ni wengi sana lakini Mke ni mmoja tu ambaye kila mwanaume anajua hilo!

Maharusi na wapambe wao
Wasimamizi wao
Mchungaji aliye idhinisha ndoa hii

Sarah akisindikizwa na kaka yake aitwaye Alex ambaye ndiye aliyemlea toka wazazi wake wamefariki hadi leo hii anapokwenda kuanzisha nyumba yake mwenyewe. Kwa Sarah hamuoni Alex kama kaka bali ni baba yake mlezi na mke wa Alex ni mama yake mlezi, hao ndio wazazi wa Sarah.

Hapo juu ni baba mlezi wa Isaka ajulikanaye kama mzee O.O Igogo. Yeye ndio amemlea Isaka toka akiwa na miaka 5. Baba mzazi wa Isaka amefariki takribani miaka 7 iliyopita. Mzee 0tieno Igogo ni mdogo wake na marehemu mzee Alexander Igogo ambaye ndiyo Baba yake na Isaka.

Mama mlezi wa Isaka Mrs O.O Igogo akisalimia maharusi, nyuma yake ni mjukuu wake aitwaye Essy.

Mashangazi na mama wakubwa kwa wadogo upande wa bwanaharusi.

Baba mlezi akiwa na furaha nyingi usoni kwa kuongeza mtoto mwingine kwa familia.

Madada, mabinamu, na mashemeji wakiingia kwa shangwe!

Kutoka kulia, ni mdogo wa bwanaharusi aitwaye Blessing, akifuatiwa na mpwa (niece) wa bwanaharusi Essy, akifuatiwa na shemeji mkubwa Mrs. Vetto Igogo, na dada mkubwa (wapili kuzaliwa kwenye familia ya kina Isaka) Aphino Alexander Igogo (Mrs Ogoche).

Mdada mwenye nguo ya blue kutoka kushoto, huyo ndio kitinda mimba kwenye familia ya akina Isaka. Anaitwa Rhoda Alexander Igogo. Naye harusi yake ni mwishoni mwa mwezi huu. Wiki hii ni kitchen party yake.

Bibi harusi mtarajiwa Rhoda Alexander Igogo akiwa na maharusi Mr and Mrs Isaka Alexander Igogo.

Bibi harusi mtarajiwa, bi Rhoda akifurahia kaka kupata “jiko”!

Mama mlezi wa bwana harusi pamoja na baba msimamizi wa ndoa hii mzee Samuel Olung’a Igogo wakitoa nasaha zao.

Baba mlezi akitoa neno kwa niaba ya kamati!

Mama mlezi akiwa na maharusi

Maharusi wakikata keki!

Wapendwa, kwamahitaji yako ya Cake nzuri zenye ubora wake, juice fresh tamu, na Mc wa kitchen party, tafadhali husisite kumtafuta @isadoricakes_and_sassyjuice ndio habari ya taifa! ???

nnnnn

Maharusi wakifungua dancing floor kwa kucheza ziro-diatance music ?? asiye na wake akumbatie chupa ya soda! ???

Meza kuu upande wa bibi harusi

The Olung’as!

Hawa ni baba zake Isaka, wadogo kwa wakubwa. Kutoka kushoto ambaye kichwa tu ndio kimeonekana ni mzee Samuel Olung’a Igogo (baba mkubwa na msimamizi wa ndoa hii), akifuatiwa na mzee Charles Olung’a Igogo (baba mkubwa), akifuatiwa na mzee Otieno Olung’a Igogo (baba mdogo na mlezi wa Isaka), akifuatiwa na Genga Olung’a Igogo (baba mdogo)

Walianza na Mungu, wakamaliza na Mungu. Mama mdogo wa Bwanaharusi Mrs Emmanuel Agonda Sassi Igogo akitoa sala ya mwisho!

Mathayo 19:5 “akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja”!

Marko 10:9 “Basi, alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe” ….. I present to you Mr and Mrs Isaka Alexander Olung’a Igogo

Mc Rhevan mtu kati hapo

picha zote shukrani kwa Mc Rhevan studio. Ukitaka kuona picha za tukio nzima tembelea ????https://RHEVANSTUDIO2021.pixieset.com/isakaandsarahweddingphotos/

Leave a Reply