Hongera sana Rebeca Ngyumi! 2016 African Women Of The Year in Civil Society And Activism!

screenshot_2016-12-05-12-56-12-1

Hongera sana Rebeca kwa tuzo ulizopata! Wow! Wanawake Watanzania ndio watakao ubadilisha na kuondoa mfumo dume wa unyanyasji wanawake na watoto ndani ya Tanzania na Africa kwa ujumla! Umeonyesha ujasiri mkubwa sana, mfano mzuri mno kwetu sote! “Sina ambacho nitahathirika endapo serikali itasema hii sheria iendelee lakini nafikiri tunajukumu kama wana nchi kuhakikisha tunaweka mifumo mizuri ya sheria ambayo inalinda wana nchi wengine nasiyo tu sisi peke yetu”! Nimependa sana hayo maneno yako! Tatizo kubwa linalo sumbua Bara la Africa ni UBINAFSI! Tuondoe ubinafsi kuwa hilo halinihusu! Sikiliza nikwambie ee mwanamke mwenzangu; kama limemkuta mwanamke au msichana mwenzio basi hilo pia ni LAKO LINAKUHUSU SANA! Kwani laweza kutokea kwako wakati wowote ule au kwa vizazi vyako! Ngoja niseme ule msemo wa Mboni Masimba kuwa “Sauti ya mwanamke ni sauti ya jamii”!! Hivyo ondoa ubinafsi kwa faida ya taifa lako!screenshot_2016-12-05-12-55-33-1Kitu ambacho nimeshindwa kuelewa ni kwanini serikali ilikata rufaa?!! Baba yangu Dr. Magufuli hawa waliokata rufaa nao ni #JIPU tu wanahitaji kutumbuliwa kwakweli!!……….. Unajua hizi bangi za ukubwani ni shida sana, mie hapa ninakaribia kugonga 40 na ndoa bado naigopa kama gereza la Keko halafu eti watu wanapinga maamuzi ya Mahakama?! Kha! Natamani niwajue hawa watu, walikuwa Wanaume au Wanawake? Na nini haswa ilikuwa nia yao!screenshot_2016-12-04-13-19-13-1

Wanawake kwa pamoja tunaweza badilisha Africa lakini kumbuka kuwa siku zote mabadiliko huanza na wewe!!………Hongera sana Rebeca, well done! Very well deserved!!

 

Leave a Reply