Hongera sana Rose M. Awiti na mumeo!

Hongera sana binamu yangu Rose M. Awiti kwa kufunga ndoa takatifu. Mwenyezi Mungu akujalie furaha, amani, afya njema, na akawe kiongozi wenu siku zote ili ndoa yenu idumu milele. Hongera sana. Kwafaida ya wasomaji wangu, Rose ni mtoto wa mjomba wangu. Baba yake ni mdogo wake mama yangu mzazi ambaye anamfuata mara ya 5 kuzaliwa. Wiki iliyopita siku ya Ijumaa alifunga ndoa na mpemba wake ??? na mimi sasa nina shemeji mpemba ?? safari hii nikienda Bongoland itabidi nifike Pemba ?? Mwenye shati la drafti ndio baba mzazi wa bibi harusi. Bibi harusi na shangazi yake mlezi-mama Igogo ambaye ni kama mama mlezi kwani yeye ndiye aliyesimama kama mama tangu mama yake mzazi bibi harusi afariki.

Bibi harusi na shangazi zake upande wa baba  Kwa mara nyingine, hongera sana binamu yangu. Mbarikiwe wote.

Leave a Reply