Hujafa hujaumbika: Mariah Carey amegundulika na Bipolar disorder

Wahenga walisema hujafa hujaumbika hawakukosea bali walitaka watu wajifunze kuishi kwa unyenyekevu bila kudharau wengine kwani kama bado hatujakuchimbia kaburi lako tegemea kupatwa na kitu chochote kila kibaya au kizuri! Just be humble! Kuna watu wengi ukiwaona utadhani wapo vyema kabisa kiafya na kiroho, kumbe ni wagonjwa kama siyo kiroho, basi kimwili, au kiakili! Tena humu kwenye social media ndio nirahisi sana kuwagundua ?? Wewe angalia sana watu wanaofanya vitu extreme just to get attention fanya kuwachunguza utagundua kuna shida mahala! Siyo tu wanao post matusi au picha za uchi, hapana! Hata wale ambao kutwa picha zao lazima ziwe na muonekano fulani "perfectly put together" the "divaish" behavior. Au mwingine kazi yake ni kupiga picha na viongozi wa siasa na "celebrates" tu haonyeshi maisha yake halisi zaidi ya hizo picha yani watu kama hawa wengi ni wagonjwa! Wengine ni waongo spare zake hakuna!!

Lakini  hakuna haja ya kumcheka mgonjwa japo saa nyingine katika hali ya kiubinadamu wengi tumejikuta tukifanya hivyo haswa kwa wale ambao wameumiza roho zetu! Kumbuka 'hujafa hujaumbika'! Wewe ona mtu kama Mariah Carey  uzuri na pesa zote alizo nazo bado amekutwa na huu ugonjwa! Bipolar siyo Ukichaa ila usipo tibiwa kwa muda mrefu unageuka kuwa kichaa kabisa. 

Mariah Carey aligundulika kuwa na huu ugonjwa mwaka 2011, ameficha kwa muda huo wote lakini sasa imefikia hali ambayo haufichiki tena. Kwa kuhofia kuwa ipo siku mtu angetoa hivyo siri kabla yeye hajasema imembidi sasa aende hadharani na kutangazia dunia kuwa yeye ni mgonjwa wa akili, hivyo dunia impokee na kumkubali jinsi alivyo!.....Kabla ya kuhukumu mtu jaribu kumjua kwa kiundani unaweza tena dhambi mbaya sana! #HujafaHujaumbika

Leave a Reply