Idriss Sultan: Unaweza ukawa loyal lakini usiwe blind!

Hii interview naona ilinipita ndio nimeiona leo!

Kwanza nianze kwa kusema hongera sana Idriss Sultan kwa kupata mkataba mzuri wa kuigiza nchini Marekani. Nakutakia mafanikio mema najua utatutoa kimaso maso!.......Unajua mimi nilionaga zile picha za jeshini nikajua kuwa ni mambo yako ya comedy! Kumbe ulienda JKT ??

TRUST: Interview yako nimeipenda sana. Hasa somo la kuwa "Loyal but not blind"!! Nafikiri wengi inatuchukua muda kuelewa hilo mpaka yatakapo kutokea zaidi ya mara moja ndio somo linaanza kuingia. Mimi nasema ukiona rafiki yako hapendi maendeleo ya wengine kaa naye mbali! Ukiona rafiki yako haguswi na upotevu au huaribifu wa mali zako au pesa zako hata kama ni Shilingi moja  achana naye kabisa! Ukiona rafiki ambaye siku zote anataka utumie njia ambayo itakughalimu zaidi achana naye! Ukiona rafiki yako ni rafiki wa karibu sana na watu wanaopinga maendeleo yako (mwenye tabia ya kuuma na kupuliza) muogope huyo rafiki! Ukiona rafiki ambaye pesa ni muhimu kwake kuliko UTU mkimbie haraka sana! Watu wanamna hiyo siku zote siyo waungwana, na wala hawana utu! BE LOYAL BUT NOT BLIND!! Somo zuri sana! BETRAYAL: Asikudanye mtu, betrayal hurts! Inauma sana kwani betrayal involves emotions which are your feelings! Hisia zako ndizo zinakufanya wewe jinsi ulivyo, hivyo mtu anapo kugeuka kwa kusudi la kukuangamiza au kusudi lolote haina tofauti na mtu anayekuchoma kisu bila ganzi! Ndio maana wenzetu wanasema "you stab me in my back"........ Naona wewe upo kama mimi ni ngumu sana kwangu kuwa na rafiki ambaye ameni betray! Don't get me wrong, nitakusamehe, tutasalimiana tukionana, hata kucheka naweza cheka nawe lakini urafiki na wewe ni MWIKO!  "When people show you who they are believe them" ~~~ Maya Angelou

KUTHUBUTU: Pole sana kwa changamoto ulizo pitia, na pia hongera sana kwa kuto kukata tamaa. Naamini wengi tutajifunza kutoka kwako japo wengine tu wakubwa zako. Maisha ni somo endelefu ambalo unaweza lipata toka kwa mtu yoyote bila kujali umri! You have inspired me!

WEMA: Masikini, ninesikitika sana kumbe Wema alikuwa mjamzito? Tena twins!! Dah! Pole yake sana. Mungu atampa wengine muda ukifika. Nimependa the way you talk about her you didn't trash her at all! 

LIFESTYLE: Jamani wanawake 30÷÷ eeh! Hivi huu UKIMWI unachagua ama?! Gosh!! What about magonjwa yazinaa yasiotibika hamyaogopi?! I hope you will well behave huko Hollywood maana huko ndiko kuna jehanam ya magonjwa ya zinaa!! ...........Otherwise, Congratulations! 

 

Leave a Reply