JINSI YA KUJENGA JAMII DHAIFU NA BONGOLALA- Peter Sarungi

Nchi za Africa bado zitakuwa na kazi ngumu sana ya ki utawala katika kuunganisha jamii tatu katika nchi ambazo ni Wenye Nchi, Wana siasa na Wana Nchi ili kifikia maendeleo ya kweli. Kwa bahati mbaya kumekuwepo na udanganyifu mkubwa unao fanywa na Wana siasa walio pewa wajibu wa kuunganisha na kuleta mahusiano mazuri katika jamii hizi ili ziweze kufanya Kazi kwa ushirikiano hatimaye kuleta maendeleo ya nchi.

Wana Siasa wengi wa Africa wamevuruga nchi zao kupitia mifumo wanayoiweka katika kuongoza nchi. Wana nchi wengi bado hawajui athari za mifumo mbalimbali katika kuendesha maisha yao ya kila siku. Mifumo hii huanza kuathiri maisha ya wana nchi tangu wanapo zaliwa, ukuaji wao, kuelimika kwao, uchumi wao, afya zao, uhuru wao hadi uzee wao. Mifumo hii inaweza kuamua ni kwa kiasi gani wananchi waelimike, wapate afya nzuri, waajiriwe, wajitegemee, wapate uhuru na mengine mengi yakiwemo yanayohusu siasa. Ndio maana kuna msemo unasema ukiona wafuasi ni wabovu basi jua wametengenezwa na kiongozi wao na ukitaka kujua ubovu ama ubora wa nchi basi chunguza athari zinzowapata jamii husika kutokana na mifumo ya kuendesha nchi.

Watawala wengi wa Africa wamekuwa na uturatibu wa kutengeneza jamii dhaifu na masikini katika kuhoji, kushauri, kufikiri, wasi jitambua na wasio jua wanachokitaka. Watawala wamekuwa wakitengeneza jamii hizi ili kuendeleza malengo yao ya kutwala dola kupitia mifumo. Na kwa bahati mbaya mifumo hii imeweza kuwaathiri hadi wenye nchi na kujikuta wakitumikishwa na Wana Siasa, ndio maana utakuta kuna idadi kubwa ya wanajeshi walio ishia darasa la saba na kidato cha nne kuliko wale waliofika kidato cha sita na kuendelea. Wote hawa hujikuta wakitawaliwa na wana siasa kwa maagizo hata ya kutekeleza jambo kwa mnyonge kwa maana mfumo waliofundishwa na kuapa ni wa kutii bila kuuliza.

Watawala wengi wa Africa wameweza kupitisha na kuhalalisha mifumo ya kuzalisha jamii dhaifu na Bongolala kupitia njia tatu….fb_img_14819059905521. KUDHOOFISHA ELIMU KWA JAMII
Watawala wengi wa Africa wana amini kuwa kutawala jamii iliyo elimika kupitia Elimu bora ni ngumu sana na ina waweka katika riski kubwa ya kutawala milele, hivyo hulazimika kutengeneza jamii kubwa isiyokuwa na elimu ili kudhoofisha uelewa wao na uwezo wao wa kufikiri. Watawala hawa wana vuruga mfumo wa elimu kwa makusudi na kuweka mifumo dhaifu yenye kutoa nafasi ndogo ya wana nchi wachache kupata elimu hadi ngazi za juu na hata hao wanaopata nafasi hiyo hawapati Elimu inayostahili na kumkomboa karika utegemezi.

2. KUDHOOFISHA UCHUMI WA JAMII
Ni ukweli usio pingika kuwa Uchumi imara ni nguvu nzuri kwa jamii. Jamii yenye uchumi imara inaweza kuelimika kwa gharama yoyote ile ikiwa uchumi wao ni imara. Jamii yenye uchumi imara inaweza kuamua kufuatana na maslahi yao hata inaweza kupinga mifumo dhalimu ya nchi na hata kuwapinga watwala. Kwa kuhofia vikwazo hivyo, Viongozi wengi wa Africa wamekuwa wakidhoofisha uchumi wa jamii zao ili kuwafanya wanyonge wasioweza kuhoji ubaya ama uzuri wa watawala. Viongozi wengi wamekuwa wakikusanya pesa nyingi kupitia kodi na kujilimbikizia wao pamoja na utawala wao kama alivyofanya hayati Mobutu Seseko wa Congo. wanapenda sana kuona pesa nyingi zikiwa kwao kuliko kwa wana nchi na ndio maana hata sekta binafsi zina zorota katika kuchangia maendeleo ya jamii.

3. KUDHOOFISHA UHURU WA KUTOA MAONI
Watawala wengi wa Africa hawapendi kusikia maoni tofauti na waliyo nayo wao, hawapendi kusia ukweli walio uficha, hawapendi kupingwa kwa namna yoyote ile. Hivyo watawala hawa wataingiza sheria na taratibu za kuua uhuru wa kutoa maoni kinzani. Inaaminika kuwa kuna watu hata ukiwa dhoofika ki uchumi na ki elimu lakini bado wanaweza kiwa wajasiri wa kutoa maoni yao hata kama ni ya kupinga utawala bila kujali vikwazo walivyonavyo. Hivyo ili kuto ruhusu riski hiyo, watawala huweka mifumo ya sheria za kukandamiza Uhuru wa kutoa maoni na hata Uhuru wa kujieleza kwa jamii.

Peter Sarungi a.k.a The Next Speaker-Baba Pilato!
Peter Sarungi a.k.a The Next Speaker-Baba Pilato!

#MyTake
Africa kama ilivyo nchi ya kisadikika, ina safari ndefu sana ya kubadili mifumo ya nchi. Mabadiko hayo huletwa na jamii iliyovuka vikwazo vitatu hapo juu yaani lazima uwe vizuri kichwani, uwe vizuri mfukoni na uwe na njia nyingi tata za kutoa maoni yako. Kinyume na hapo itakugharimu wewe na familia yako.

Asanteni sana, ngoja niendelee kutunisha mfuko wangu ili itakapo hitajika kubadili mfumo nami niwemo.

Leave a Reply