Joyce Kiria: Mange Kimambi wewe ni SUPER WOMAN katika dunia yako

Regrann from @joycekiriasuperwoman  -  NIWE MKWELI... @mangekimambi_ wewe ni SUPER WOMAN katika dunia yako... ukiamua lako unakomaaga, NAKUMBUKA WAKATI WA KAMPENI ULIVYOSIMAMA KIDETE, yaani kwa kweli niseme umetingisha nchi na MAANDAMANO yako.... Serikali ilivyokuongelea kwa nguvu tuu nikaogopaaaaaa ? kiukweli mimi nilikuwa na kiwewe cha hayo MAANDAMANO kuliko hata kihoro cha NDOA yangu? jana sijalala kabisa nawaza hayo maandamano itakuwaje, maana tuna majukumu ya kulea ati... lakini Yesu ni mkubwa sana Amen...Tz hatujafika hukoooo Anyway, mimi kama mpambanaji katika dunia yangu Nakupongeza kwa Nguvu uliyojijengea maana najua siyo kazi rahisi, ila pls nguvu hiyo isihatarishe Amani yetu bali itumie vizuri kujenga Taifa letu badala ya kubomoa ....kosoa unavyoweza lakini Amani yetu ni Bora zaidi tuilinde kwa garama yeyote... watanzania hatujafikia huko kwa maandamano jamani, tupaze sauti zetu lakini bila kutishia Amani yetu...

Again hongera kwa kuwa kinara  Super Woman, Mwanamke wa Nguvu, najua inahitaji UJASIRI mkubwa sana kuweza kufanya unachofanya, umefanikiwa kuteka mashabiki wengi sana kila kona unazungumzwa hata na wasio mitandaoni... kwangu mimi hiyo ni FURSA NZURI... ITUMIE VIZURI itangaze nchi na  AMANI yetu... Maandamano ya kitaifa siyo kabisa hatujafika huko pls... labda maandamano binafsi ya familia?

Nawashukuru watanzania wenzangu kwa kukupuuza na kutokwenda kuvunja Amani, maana kwa jinsi ulivyowasha moto sikuamini kama hakuna alieandamana leo? naimani watanzania bado tunaimani na Rais wetu na Taifa letu. 

Naimani serikali itatilia maanani changamoto unazoleta hadharani kwa niaba ya wengi, upinzani siyo dhami uwepo kuleta changamoto na serikali ifanyie kazi yale yenye Tija, watu wengi wanapitisha Changamoto kwako maana mwenye huo ujasiri ni mtihani, japo njia unayotumia wewe inaumiza sana kwa kweli, “matusi” woooiiiiiii hata kama ujumbe ndani yake upo lakini mijitusi yako inaondoa maana nzima kabisa ?? japo kwa wengine ndo kachumbari??

MIMI NASEMA NI SAWA KUKOSOA LAKINI KUSIHATARISHE AMANI YA NCHI YETU....  - #regrann

Leave a Reply