Jukwaa langu: Mahojiano yangu na Mange Kimambi

Regrann from @mutwiba – Katika kipindi cha JUKWAA LANGU Jumatatu hii ndani ya Kilimanjaro Studio, utaanza kwa kusikiliza mahojiano yangu na Mange Kimambi.

Kisha tujadiliane kuhusu “Diaspora Connect” / ama Diaspora Disconnect”

* Kwanini wapo Diaspora wanaoamini kwamba Diaspora ndio suluhisho la matatizo Tanzania?

* Kwanini wapo Diaspora wanaoamini kwamba Diaspora ndio tatizo Tanzania?

* Ni kweli kwamba walio nyumbani hawatuelewi ama ni kwamba kuna Diaspora wasiojielewa wanapoamini kwamba walio nyumbani hawajielewi?

****Haya ni kati ya maswali mengi tutakayoulizana hapa**** Pia tutapata mrejesho kuhusu Tanzania Day 2018 iliyokamilika Dallas. Kisha mgeni wangu ni Boniface Makulilo.

*Navy Veteran

*Fulbright Alumni

*Mwalimu

*Mwandishi

*Mshauri mtandaoni.

*Mmoja wa wakurugenzi katika NGO moja inayohudumu mataifa 18.

Ana mengi ya kujadili nasi katika saa la pili.

Si ya kukosa

Ni kipindi cha JUKWAA LANGU, Jumatatu hii (Aprili 30, 2018) na kila Jumatatu kuanzia saa 12 kamili jioni mpaka 2 kamili usiku kwa saa za Marekani Mashariki (6:00 – 8:00pm ET). Ni kupitia Facebook live (Mubelwa Bandio na Kwanza Production) ama Kwanza Radio kwenye TuneIn

http://tun.in/sfwyf ama piga simu 202-683-4570 *******************************

PRODUCER: Mubelwa Bandio – #regrann

Leave a Reply