Kagua ATM yako kabla ya kuweka card!

Kuna hivi vifaa vimeingia ambavyo mwizi wa kwenye ATM anaweza chomeka na kusoma maelezo ya siri ya card yako na kuchukua pesa bila wewe kujua. Nikifaa ambacho wanakiegesha kwa juu, hivyo kabla ya kuweka card yako kwa ATM  hakikisha umekagua kwa kuvuta kidogo ule "mdomo"ambao card yako inaingia ukiona inacheza basi jaribu kuvuta kwa nguvu kidogo ili ukichomoe. Pia jaribu  kujijengea tabia ya kukagua mazingira ya ATM kabla ya kufanya kitu chochote kwani kuna wezi wengine wanategesha camera kwa juu ambazo zinauwezo wa kusoma number zako za siri. .......Tazama video ?

Special thanks to Gloria kwa ku share nasi hii video ?

Leave a Reply