Kama “Boaz” angeambiwa achague mwanamke katika dunia ya leo…..!!

 Embu tucheke kidogo maana hii weekend ndefu hapa U.S.A kwasababu the Independence ya Marekani ni JumaNne!……… Basi kama ilivyo, nimekwenda kwa Instagram ya #Askcheyb nakukutana na hii topic ya wadada kuvaa nguo karibia na nusu uchi! Eti anasema kuwa kama “Boaz” wa kizazi kile cha kwanza angekua ndio anatafuta mke katika karne hii 21 ambapo wasichana wengi wanatembea nusu uchi kila siku mida yote; ingekuaje? Muandishi wa mada anasema wanawake wa namna hiyo wapo kwaajili ya “mburulaz”!  Labda nikukumbushe kuwa muandishi ni mtaalamu wa mambo ya mahusiano!~~~~~ embu jisomee mwenyewe ??

Could you imagine “Boaz” choosing some of these chicks who parade half naked on IG ALL  day everyday? Nah, them chicks are for “Dumbaz” ??” Sasa mimi nashindwa kuelewa kwani jambo kama hili lingeandikwa na “Muafrika” kutoka Africa nisinge shangaaa sana. Lakini huyu ni Mmarekani mweusi ambaye amezaliwa na kukulia hapa Marekani! Watu kutembea nusu uchi hapa Marekani nikitu cha kawaida sana. Sijui tatizo nikuweka hizo picha kwa Social media au ni nini! Kwamfano, mtu kama Oprah aliwahisema kuwa siku ukikutana na picha ya yeye amevaa “bikini” au swimsuit basi jua kuwa ni fake! Kwani hata siku mmoja haitokaa itokee yeye kuvaa hivyo kwa public! Lakini unakuta watu kama wakina Michelle Obama wao wapo free kuvaa swimsuit mbele za watu japo hukuti akizipost picha hizo kwa social media isipokuwa  ma-paparazzi huwa hawapitwi na jambo! ~~~~ Sijajua kwakweli inakuaje watu walio zaliwa kwenye mila na tamaduni sawa wakawa na mtazamo tofauti wa maadili ya mavazi! Embu tujikimbushe na hii topic hapa ?? KamaMkeRaisAnawezaVaa.    

SOMA MAONI YA WENGINE!

 

 

Leave a Reply